Ufisadi wa CHADEMA Moshi: Ofisi zote Halmashauri ilikuwa zifungwe kwa wiki nzima!!!

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,882
13,170
Katika kile ambacho kingeushangaza umma wa kiTanzania, uongozi WOTE wa Halmashauri ya mji wa Moshi ilijipangia safari ya kwenda Kigali, Rwanda kwa ajili ya matembezi ya kusafisha macho na kuona usafi wa Jiji la Kigali.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Lawrence Gama, ameuwekea kauzibe mpango huo baada ya kuona gharama kubwa na ukosefu wa uwajibikaji kwa maana ya kusudio la kufunga Ofisi karibu zote za Halmashauri ya Moshi kwa wiki nzima au zaidi wakati wa matembezi hayo.

Safari hii ambayo ya ujumbe wa Halmashauri ya Moshi, ina mentality ya kishule shule kwa maana ya excursions, na ingewahusu Madiwani wote pamoja na Meya, wakuu wa Idara wote(pamoja nafikiri na Mkurugenzi), viongozi waandamizi wote kwenye halmashauri.

Jumla ya watu waliojipangia kwenda safari hiyo ni 57( Du! wanaiga wapi hii!!)
Na wote wangelipwa posho nono ya kufikia Tshs milioni 200 kwa hii wiki moja tu!!

Hii Halmashauri inaongoza na Meya Jafari Michael na ina uwingi wa maDiwani wa CHADEMA pengine kuliko halmashauri yoyote nchini.

Meya Jafari Michael(CHADEMA) amesikika Radio One asubuhi hii akilalama kuhusu kuingiliwa na Mkuu wa Mkoa kuhusu safari hiyo.
Ati alikuwa waende "kujifunza usafi" kutoka Kigali-sawa na kumfundisha ng'ombe kutengeneza maziwa!

Haya wana CDM changamoto kwenu na utawala bora, matumizi sahihi ya fedha za mlipa kodi, somo la ufisadi bado kitendawili hata kwa wateule wenu.
 
yaani mungu tuombe atupe pumzi tu,mpaka 2015 tutaona vioja kweli nchi hii.
 
kama ni kweli hawa madiwani ni mafisadi...hongera mkuu wa mkoa ila isiwemo hila ya kisiasa
 
Hata mimi nimeisikia.Kwakweli mabadiliko ya dhati ynahitajika.Ni suala la mfumo nadhani.
 
hiyo trip ilikuwa ni madiwani wa Chadema pekee ina maana hakuna madiwani wa CCM katika hiyo safari?. Unaonyesha kama vile una zile 'genetic' za umbea umbea za wana-ccm wote. Umeshawahi kufanya tathmini ya safari za Vasco Da Gama zimeigharimu kiasi gani nchi hii na kitu gani cha msingii anachoenda kufanya huko aendapo na zina manufaa gani kwa nchi?
 
hiyo trip ilikuwa ni madiwani wa Chadema pekee ina maana hakuna madiwani wa CCM katika hiyo safari?. Unaonyesha kama vile una zile 'genetic' za umbea umbea za wana-ccm wote. Umeshawahi kufanya tathmini ya safari za Vasco Da Gama zimeigharimu kiasi gani nchi hii na kitu gani cha msingii anachoenda kufanya huko aendapo na zina manufaa gani kwa nchi?

ucwe na mawazo chakavu kwan ccm ikiiba na nyie lazma muibe
 
Sitaki kuona mshabiki yeyote wa Chadema analeta unazi wake hapa. Hongera sana Mkuu wa Mkoa bwana Gama kwa kuzuia uhuni huu, Moshi ndio watu wanapaswa kwenda kujifunza usafi na si wao kwenda kujifunza usafi kwingine.

By the way jamani hivi usafi nao unafundishwa au ni kuagiza vifaa vya kufanyia usafi? huu ni uhuni na kamwe haukubaliki.
 
Suala si kutetea upuuzi huu. Haijalishi unafanywa na CCM, CHADEMA, CCM&CHADEMA, CUF&CCM. Huo ni upuuzi.

Madiwani wanatengeneza safari mbuzi ili kula hela. Na watendaja wanatumia kama hongo ili wakitoka huko wasiwe na chakusema.

Walipoingizwa chaka na CCM, kwanini hao madiwani wa CHADEMA wasigome?
 
ucwe na mawazo chakavu kwan ccm ikiiba na nyie lazma muibe
''nyie'' ndo akina nani?..................nilichokuwa namaanisha ni kwamba wizi wa aina yoyote hauna maana bila kujali chama gani maana mleta uzi kataja Chadema pekee. Asante kwa mawazo yako ambayo sio chakavu lakini yakukurupuka.
 
Habari hii kama ni ya kweli, Meya wangu Japhar unapotupeleka ni kubaya; CHADEMA chukueni hatua tunahtaj majibu
 
Ki ufupi ni kwamba, ni asilimia ndogo sana ya viongozi ambao ni wazalendo na waaminifu kazini, wengine wote ni wezi bila kujali wanatoka chama gani, hata hivyo asilimia ndogo hiyo ya wazalendo ikitokea wachache wao ni walioshika madaraka ya juu kabisa ya uongozi wizi unadhibitiwa vizuri na nchi inapata maendeleo. Tatizo la serikali ya CCM wako kinyume na wanafanya mambo kinyume chake...
 
ucwe na mawazo chakavu kwan ccm ikiiba na nyie lazma muibe

suala hapa ni makucliano kati ya madiwani wa ccm,cdm, wengine na wakuu wa idara zote juu ya hayo matumizi. Kama imepangwa na cdm tu wa ccm lazima wangesema ili kupiga kete ya kisiasa
 
Hata mimi nimeisikia.Kwakweli mabadiliko ya dhati ynahitajika.Ni suala la mfumo nadhani.


nawambia ndugu zangu ,ufisadi bwana cyo chama ni m2 ona sasa hapo meya chadema anakuwa fisadi lakini mkuu wa mkoa wa ccm kakataa ufisadi ,nashauri kwene ufisadi tusikiseme chama tumseme mhusika.
 
nawambia ndugu zangu ,ufisadi bwana cyo chama ni m2 ona sasa hapo meya chadema anakuwa fisadi lakini mkuu wa mkoa wa ccm kakataa ufisadi ,nashauri kwene ufisadi tusikiseme chama tumseme mhusika.

Tuna tatizo la mfumo wa CCM ndio tatizo kubwa, kwani unadhani kazi anayoifanya Mwakyembe sasa hivi hatupongezi au hatuioni? au kazi anayofanya Waziri wa nishati na madini unadhani hatuioni? tatizo ni hili dubwana CCM. nchi inatakiwa kufanyiwa overhaul ili tuanze upya.
 
Suala la ziara kama ni kwa manufaa ya Taifa na hasa manispaa yao ya Moshi mi sioni tatizo kwani fedha wanaweza kuchanga kutoka mifukoni mwao ikiwa ni wazalendo kwa Taifa lao.

Lakini badala ya kuishambulia Chadema peke yake, hivi DED, DC, Wakuu wa idara na madiwani wote pamoja na RC ni wa Chadema? Bado watendaji kazi wa ccm katika manispaa ya Moshi ni wengi, hivyo kama serikali imekubali na kuiweka kwenye bajeti kwa manufaa ya Manispaa ya Moshi sidhani kama kuna tatizo hapo labda wivu tu na propaganda. Lakini kama ni viongozi kujinufaisha ccm hamwezi kukwepa lawama maana serikali ni yenu, Chadema nafasi waliyonayo ni ya kuleta hoja na kuitetea lakini serikali inaweza kuipokea au kuikataa.

Ikiwa serikali imekubali hoja ya hovyo basi na yenyewe ni ya hovyo na siyo aliyeleta hoja.
 
Hawa CCM wana mbinu chafu sana na mkakati wa kuichafua cdm.wamefanikiwa mwanza sasa ni zamu ya moshi lengo ni kuipaka matope cdm. mwanza baada ya CHADEMA kuongoza jiji, CCM walianza kuropoka mapema kabla ya meya kuapishwa kuwa CHADEMA kamwe hawataweza kuongoza jiji. Na kweli tumeyaona kupitia kwa matata ambaye alipata kura 2 ktk kura za maoni CCM na kisha kutimkia chadema na kupata udiwani.

Mwanza ni jiji linaloongoza kwa usafi na mara nyingi tunaona makundi ya madiwani kutoka halmashauri mbali mbali Tz wakizulu M'za mbona hamjawahi kusema au kwa kua wa moshi ni CHADEMA. Mlizusha kuwa meya wa mwz ametolewa kwa sababu ya ufisadi, mlipobanwa mkasema ameshindwa kuongoza vikao
 
ufisadi ni ufisadi tu!,hamna wa cdm au cmm,na kwa sababu tunawategemea cdm ndio wawe mbadala wa ccm katika kuleta unafuu wa maisha kwa mtanzania thts why tunaona sio fair kung'ang'ania safari iyo!
 
Suala si kutetea upuuzi huu. Haijalishi unafanywa na CCM, CHADEMA, CCM&CHADEMA, CUF&CCM. Huo ni upuuzi.

Madiwani wanatengeneza safari mbuzi ili kula hela. Na watendaja wanatumia kama hongo ili wakitoka huko wasiwe na chakusema.

Walipoingizwa chaka na CCM, kwanini hao madiwani wa CHADEMA wasigome?
Ukweli usemwe! tusiangalie tu upenzi au ushabiki! hakuna wizi mzuri! kama ni kweli na mleta mada hajakoleza chumvi basi naiamini kamati kuu ya cdm! sina wasiwasi kuwa watashughulikiwa kwa kuwa si kama ccm ambao hakuna wa kumkemea mwenzie kuwa ni mchafu na hakuna alieoga! huwezi kumtuhumu mwenzio mchafu wkt wewe unanuka! asanteni nawakilisha
 
Back
Top Bottom