Ufisadi wa CHADEMA Moshi: Ofisi zote Halmashauri ilikuwa zifungwe kwa wiki nzima!!!

Kama suala ni kuwa fair alitakiwa aje na mada yenye akili. Ulikuwa ni mpango wa halmashauri nzima ya Moshi yenye madiwani wa CDM, CCM na m1 wa TLP, vipi aseme wa CDM as if ni wao peke yao? Stupid!

Mi sio mshkaji wako, kawaite washkaji watoto wenzio facebook


wewe jamaa hivi unajua jinsi maamuzi yanavyofikiwa kwenye vikao vya halmashauri? mbona bado watu mnakuwa wajinga wajinga? ni jambo ambalo nilihisi limeshatokomezwa vichwani mwa watu wazima kumbe bado kuna mijitu inaujinga ujinga? mmeshasema CCM ni mafisadi, majambazi, wezi na majina mengine mnayotuita yanayofanana na hayo, je, kwa matumizi haya ya fedha ambapo madiwani wa chadema waliyapitisha, unahisi wao sio wafujaji wa mali ya umma? Mijitu mingine sijui ikoje kuandika upuuzi tu kwenye thread za watu, kwani lazima uchangie? inabidi ukapate elimu ya watu wazima ili angalau elimu ikukomboe.
 
Naipenda CHADEMA ila kwa hili sikubaliani nao. Safari kama hii anapaswa kwenda Afisa mipango miji pamoja na bwana/bibi afya then warudi kuwaelimisha wengine huko Moshi, wakiwamo hao madiwa. Tudumishe accauntability pamoja na ensure value for money.

unaakili sana na hii ndio michango tunayoitarajia kwa watu wenye weredi. Hatukatai mtu kukipenda chama chochote cha siasa, ila kama kuna madhambi uwe tayari kuyasemelea kwa lengo la kuboresha zaidi shughuli za chama, kuliko kuficha madhambi yao na kuona kila wanalofanya ni sahihi.
 
Dawa ni Kuvua Watu Magwanda kama Mwanza ili tuelewe kama CDM wako kihaki na hawatizami sura ya Mtu... kama kuna makosa iwe wazi hukumu za wazi ndio kutakifanya chama kiendelee kupendwa njia nyingine kama ni kuficha basi Watanzania tutakuwa tumelaaniwa na katu hakutakuja kutokea Changes hata tukifanya changes haitokuwa changes Yale yale... kama Hadithi ya Songoro
 
Lakin mkumbuke moshi na ccm kuchukua jimbo ni kitu kisichowezekan milele mnatakiwa mlijue kwanza ili
 
Hapa sasa tunataka Dr. Slaa aingilie kati mara moja maana ufisadi ni ufisadi tu hata kama ukifanywa na CHADEMA usifumbiwe macho.

Peleka watu wawili au watatu tu Kigali warudi watoe shule kwenye baraza la madiwani. Kwa jinsi hii naanza kupata mashaka na hivi vyama mbadala na umakini wao kwa sababu mpaka sasa hivi sijamsikia kiongozi wa juu wa CHADEMA kutoa tamko la kupinga hii kitu.

Ingekuwa wamefanya CCM daa ungemsikia slaa, mnyika, heche, mbowe na wengineo fasta wameshatoa tamko. Ila CHADEMA Moshi wawe makini maana naona kama watendaji wa manispaa wanawaingiza mkenge na kuwachonganisha na wananchi bila wao kujua, maana nikiangalia hii trip ya Rwanda plus kodi ya kuegesha magari stendi kuu mimi mmmh!
 
wewe jamaa hivi unajua jinsi maamuzi yanavyofikiwa kwenye vikao vya halmashauri? mbona bado watu mnakuwa wajinga wajinga? ni jambo ambalo nilihisi limeshatokomezwa vichwani mwa watu wazima kumbe bado kuna mijitu inaujinga ujinga? mmeshasema CCM ni mafisadi, majambazi, wezi na majina mengine mnayotuita yanayofanana na hayo, je, kwa matumizi haya ya fedha ambapo madiwani wa chadema waliyapitisha, unahisi wao sio wafujaji wa mali ya umma? Mijitu mingine sijui ikoje kuandika upuuzi tu kwenye thread za watu, kwani lazima uchangie? inabidi ukapate elimu ya watu wazima ili angalau elimu ikukomboe.

Kuwa mpole mkuu acha matusi, manispaa ya Moshi ina madiwani CDM, CCM na TLP lakini pia kuna watendaji wa serikali ya ccm kama DC, DED na wakuu wa idara. Hivi nani mwanzilishi wa hoja hii? Hoja hii ilipitaje kwenye kikao? Nani waliunga mkono na nani walipinga? Serikali iliyoridhia na kuipangia bajeti ni ya chama gani? Ikiwa hoja hii haina tija kwa Taifa na serikali imeikubali, je serikali hii inapaswa kuaminiwa na Watanzania?
 
Katika kile ambacho kingeushangaza umma wa kiTanzania, uongozi WOTE wa Halmashauri ya mji wa Moshi ilijipangia safari ya kwenda Kigali, Rwanda kwa ajili ya matembezi ya kusafisha macho na kuona usafi wa Jiji la Kigali.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Lawrence Gama, ameuwekea kauzibe mpango huo baada ya kuona gharama kubwa na ukosefu wa uwajibikaji kwa maana ya kusudio la kufunga Ofisi karibu zote za Halmashauri ya Moshi kwa wiki nzima au zaidi wakati wa matembezi hayo.

Safari hii ambayo ya ujumbe wa Halmashauri ya Moshi, ina mentality ya kishule shule kwa maana ya excursions, na ingewahusu Madiwani wote pamoja na Meya, wakuu wa Idara wote(pamoja nafikiri na Mkurugenzi), viongozi waandamizi wote kwenye halmashauri.

Jumla ya watu waliojipangia kwenda safari hiyo ni 57( Du! wanaiga wapi hii!!)
Na wote wangelipwa posho nono ya kufikia Tshs milioni 200 kwa hii wiki moja tu!!

Hii Halmashauri inaongoza na Meya Jafari Michael na ina uwingi wa maDiwani wa CHADEMA pengine kuliko halmashauri yoyote nchini.

Meya Jafari Michael(CHADEMA) amesikika Radio One asubuhi hii akilalama kuhusu kuingiliwa na Mkuu wa Mkoa kuhusu safari hiyo.
Ati alikuwa waende "kujifunza usafi" kutoka Kigali-sawa na kumfundisha ng'ombe kutengeneza maziwa!

Haya wana CDM changamoto kwenu na utawala bora, matumizi sahihi ya fedha za mlipa kodi, somo la ufisadi bado kitendawili hata kwa wateule wenu.


Kabla ya kuanza kuwalaumu tujikumbushe zile semina elekezi! Ni ofisi ngapi zilifungwa nchi nzima?
 
Ukiwa mpinzani kisha unatetea ufisadi (au kujiingiza katika ufisadi), basi unastahili kufungiwa jiwe kubwa na ukatoswe baharini.
 
mkuu wa mkoa wa kilmanjaro gama akihitimisha kikao cha waziri wa nishati na madini leo mjini moshi kilichohudhuriwa na wadau mbalimbali ameeleza kuwa aaingii akili kama kiongozi mkuu wa serikali mkoani kilimanjaro kwa madiwani wa halmashauri ya manispaa ya moshi kutaka anyamazie kuchotwa kwa shilingi milioni 174.9 za mafunzo kwa ajili ya kundi moja la madiwani na maofisa katika halmashauri kufanya ziara aliyoiita ya kitalii kwenda kigali rwanda kujifunza kufanya usafi.

rc huyo alifikia hatua hiyo baada ya mmoja ya madiwani kudai katika kikao hicho kwamba huo haukuwa ufsadi bali ulikuwa ni fedha zlizoidhinishwa katika bajeti ya halmashauri ya manispaa ya moshi kwa ajili ya mafunzo.

gama alisema kuwa fedha hizo zimeidhinishwa kwa mafunzo kwa kada na kasma tofauti tofauti na kwa bajeti ya mwaka nzima na siyo kwa kundi moja la watu kuchukuwa fedha zote za bajeti kwa safari ya kitalii ambayo haina tija kwa halmashauri hiyo.

profesa sospeter muhongo naye alipigilia msumari kwa kukejeli hatua hiyo akieleza kuwa hivi sasa shule za sekondari zinahitaji umeme wa solar ambao kufunga shule ya vyumba vinane ni shilingi milioni nne ambazo kwa kiasi hicho cha shiingi milioni 174.5 ni shule kibao.

alisema kuwa kupitia mabadiliko ya kodi za madini halmashauri ya nzega umezoa hundi ya dola milioni 1.5 ambayo kama wangeipata madiwani wa halmashauri ya manispaa ya moshi basi wangefanya safari za kwenda kujifunza mitindo ya usafi kuanzia uganda,kenya,burundi mpaka msumbiji.
 
Wanaelekea pazuri, kama wameanza kuzithamini hizi kodi zetu namna hii, hatua inayofuata iwe mishahara ya wabunge, magari ya serikali n.k
 
Safi sana Gama pambana na ufisadi hawa jamaa wanachosema kwenye majukwaa ni tofauti wanavyotenda wakiwa ofisini.
 
Safi sana Gama pambana na ufisadi hawa jamaa wanachosema kwenye majukwaa ni tofauti wanavyotenda wakiwa ofisini.

Na ccm wanachoifanyia tanesco wameigeuza na jina limekuwa kilonesco!!!!
 
mchanganuo halisi wa ufisadi huo katika halmashauri ya manispaa ya moshi ambayo ina jumla ya madiwani 29 ambapo kati ya hao cdm ni 24 ni huu hapa chini

GHARAMA HALISI KWA AJILI YA SAFARI YA MADIWANI NA WATAALAMU WA MANISPAA YA MOSHI KWENDA KIGALI-RWANDA-SEPTEMBA 2012


1. Outfit allowances 58 x 300,000/ = 17,400,000


2. Perdiem:

(a) Madiwani 29 x $420 x 1,600 x 3 = 58,464,000/=

(b) Wakuu wa idara 15 x $420 x 1,600 x 3 = 30,240,000/=

(c) Maofisa mbalimbali 14 x $ 365 x 1,600 x 3 = 24,528,000/=

Jumla ndogo Tshs = 113,232,000/=


3. Posho ya njiani kwa siku 2

(a) Madiwani na wakuu wa vitengo 40,000 x 2 x 14 x 2 = 7,040,000/=

(b) Maofisa Mbalimbali 35,500 x 2 x 14 x 2 = 3,640,000/=


4. Incidental allowance kwa madiwani na wakuu wa idara

Maofisa 20% x 117,704,000 = 22,646,400/=


5. Usafiri wa Basi = 11,000,000/=


Jumla kuu Tshs= 174,958,400/=

Angalizo: Katika orodha hii hawakuwekwa

(i). Mhe Mbunge Ndesamburo

(ii). Mkuregenzi wa Manispaa ya Moshi Mama Kinabo
 
Safi sana Gama pambana na ufisadi hawa jamaa wanachosema kwenye majukwaa ni tofauti wanavyotenda wakiwa ofisini.

ritz ee .......muulize huyo mkuu wa mkoa kama anafahamu capacity charge ya richmond ni 153 million per day au nawe hujui hilo?

yaani aptl wazalishe au wasizalishe hela inachotwa au shangingi moja tu la mkuu wa mkoa hio hela inatosha kwenda kgl

 
hivi jk na safari zake za kilasiku anatumia kiasi gani.......kwa siku moja tu nataka nijue gharama na faida zake alafu turudi kwa madiwani na sababu za wao kutaka kwenda kwenye mafunzo kama sio kujifunza.
 
Hawa CDMA wameonyesha mapema kabisa jinsi watakavyoifilisi hii nchi kama watabahatika kuingia madarakani[IKULU].Kitendo cha kupata Uongozi wa Manispaa ya Moshi wanataka kuifilisi kwa kutengeneza safari zisizokuwa na tija[PRODUCTIVITY]Wananchi kuweni macho na watu hawa.Kumbe ni mafisdi namba moja!Polepole tu,mpaka 2015 watakuwa wameshajulikana ni watu wa namna gapi.Hawa nadhani wako kimaslahi zaidi.
 
Back
Top Bottom