Uliyeleta hili umenikumbusha tukio moja pale bandarini. Nilienda kuchukua kabajaji kangu siku hiyo kalikotokea japan.Tuliingia kule ndani mnamo mida ya saa tatu asubuhi,pilikapilika za kule chini,na ukiritimba wa huyu anasign kakipande kadogo,unaenda kwa mtu mwingine,mara jengo jingine,tulimaliza hizo taratibu kama saa kumi na mbili jioni.
Tulipotoka kule chini,tukafika kuna ka kituo kengine karibu na getini,tukafanya Clearance hapo,ijapokua tulikua tunagombaniana sana. Sasa tulipomaliza hapo linafuata suala la kutoka getini, si yule mdada wa pale getini akatuambia system iko down.Aisee kumbuka nilikua sijala toka asubuhi,Nikamuuliza "kabla ya hii system milkua mnafanyaje?" Ooh,tulikua tunafanyamanually,Nikamwambia na hapa utafanya manually, kwa sababu najua kuna utaratibu huu, kila mahali panapokua na dharula lazima kuna alternative.
Akawa mbishi, watu wakaanza kuniunga mkono, na wengine wakaanza kuja kujaa. Kwani nilimuabia,wewe chukua details zote,system ikirudi uta update,alipoona wanachi wanabadilika ,si akatuhudumia.
Haya huwa ni mbo ambayo watumishi wengi wa umma huwa wanategea kazi,eti system hakuna hawafanyi kazi.Ni uvivu tu na kujenga mazingira ya rushwa.Mie huwa sivumilii upuuzi kama huo.