mopaozi
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 3,301
- 520
Dr slaa ameibua ufisadi ktk shule za msingi akihutubia katika mkutano wake mkoani Ruvuma jana alidai kuwa michango ya madawati inachangishwa kila mwaka kwa wanafunzi je ni lini madawati yatatosha wanafunzi wasichangishwe tena maana madarasa ni yale yale na madawati yanachangishwa kila mwaka ina maana madarasa hayo hayajai madawati kwa miaka yote hiyo! Nakubaliana naye kabisa kuna ufisadi shule za msingi ambao haujamulikwa kabisa na unawaumiza sana wanyonge wanaopeleka watoto wao.Pili kila baada ya miezi mitatu kila shule hupewa fungu la fedha za capitation ambazo hutakiwa kununulia vitabu,vifaa na matengenezo sasa tembelea shule ngapi zina library ya vitabu tangu zimeanzishwa zinapokea fedha hizo na wanadai vitabu vimenunuliwa Je kwa shule yenye miaka 10 iweje isiwe na library sasa kichekesho hata vitabu ukiuliza viko vichache na hata wanafunzi hawajui kama kuna vitabu vipo shuleni waazime wasome wizara inafanya kazi gani kuhakikisha vitabu vinanunuliwa mashuleni!!au ndo mkondo wa kuchakachua hela za vitabu!!!