Patriote
JF-Expert Member
- Jul 13, 2011
- 1,718
- 1,047
NAIBU Mkurugenzi wa Mifumo na Huduma katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Simon Jengo, amepandishwa kizimbani akikabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya ofisi katika ununuzi wa mashine 26 za kuharibu noti.
Kigogo huyo alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Jengo anyeakabiliwa pia na kesi nyingine katika Mahakama ya Wilaya Ilala, anatuhumiwa kughushi nyaraka kwa kampuni inayotengeneza noti za benki hiyo kwa lengo la kumdanganya mwajiri wake na kumsababishia hasara ya zaidi ya Sh 104 bilioni.Mwendesha Mashtaka wa Takukuru Ben Lincon, alidai mbele ya Hakimu Mkazi Rita Tarimo kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo kati ya Januari mwaa 2005 na Desemba mwaka 2008 katika makao makuu ya BoT.
Alidai kuwa mshtakiwa alimshauri vibaya Gavana wa BoT katika ununuzi wa mashine 26 za kuharibu noti pasipo kujali mahitaji halisi ya benki. Hata hivyo mshtakiwa alikana mashtaka na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika na kwamba hawana pingamizi na dhamana.
Hakimu Tarimo alitoa masharti ya dhamana ambapo mshtakiwa alitakiwa kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika watakaosaini dhamana ya maneno ya Sh 10 milioni kila mmoja.
Jengo alitimiza masharti hayo na kuachiwa kwa dhamana hadi kesi Februari 29 mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena.
Katika kesi iliyoko Mahakama ya Ilala, Jengo anashtakiwa na maofisa wengine watatu wa BoT akidaiwa kughushi nyaraka kwa kampuni inayotengeneza noti za benki hiyo kwa lengo la kumdanganya mwajiri wao. Washtakiwa wengine ni Kisima Mkango, Bosco Kimela na Ally Farjallah Bakari ambao kwa pamoja wanadaiwa kutenda makosa hayo jijini Dar es Salaam. 

Wanadaiwa kuwasilisha nyaraka kwa kampuni hiyo ili kuchapisha kiasi kikubwa cha noti tofauti na kilichoidhinishwa na mwajiri wao.

Katika mashtaka mengine wanadaiwa kuingia mkataba wa kuchapa noti kwa bei ya juu kinyume na makubaliano halali hivyo kuisababishia Serikali hasara ya Sh 104,158,536,146. 

Wanadaiwa pia kuupeleka mkataba huo kwa mamlaka zinazotengeneza noti ukionyesha bei ya uongo
Maoni yangu
Hapa hafungwi mtu uwendawazimu mtupu. Kumbukumbu zinaonyesha ukiiba pesa nyingi hapa Tanzania hufungwi, Ila ukidokoa ndo unafungwa miaka mingi kwa kuwa ni mpumbavu. Kosa limetendwa kati ya 2005 hadi 2008, Gavana muda huo alikuwa Balali, upelelezi hadi leo haujakamilika. Hapa hamna kitu. watu wazima tumeshaelewa. Hawa wamefikishwa mahakamani ili serikali ijipatie sifa kuwa ilishawahi kufikisha mafisadi papa mahakamani ila hakuna kufungwa mtu wala nini.
Source Mwananchi 31/01/2012