Uwezo Tunao
JF-Expert Member
- Nov 14, 2010
- 6,942
- 1,190
- Thread starter
- #321
... Makinda naye bana, eti sitogombea 2015 wakati anajua fika KURA ZA CHUKI zinavyokisubiri hiki chama cha MAFISADI wasiovulika gamba ifikapo mwaka huo.
Well, simlaumu sana mama yetu lakini anawakilisha mawazo ya kizazi kilichopita chenye uvivu wa kujituma na kumtumikia kafiri bora mkono uende kinywani....
Ni kizazi ambacho hakina matumizi makubwa ya kichwa.... hakiwezi hata kuset priorities za taifa..... ni kizazi cha hunters and gatherers...... hakijafikia hata stage kuitwa horticultural societies.........
1. Kizazi hiki huona bora kiue kiwanda cha kiatu ili kinunue viatu vya ulaya.....
2. kizazi hiki huona bora kiue ginerry na vyama vya ushirika ili products zikawe processed ulaya.....
3. Kizazi hiki hudhani kuwa kutembelea 4 wd za gharama kutainua uchumi kuliko kujenga barabara bora....
4. Kizazi hiki hupenda kwenda kupumzika ulaya na si kuendeleza mambo mazuri ili kipimzikie nyumbani....
5. Kizazi hiki hupenda sana dili za muda mfupi mfupi hata kama zina gharama kwa taifa...
6. Kizazi hiki hakioni umuhimu wa huduma ya reli kuwa bora na umuhimu wa huduma hii kuwa chini ya state.....
7. Kizazi hiki ni hopeless.... ni hopeless kuliko kile cha chifu mwangunga kwani kimeenda shule lakini mambo yao kama kinavuta bangi mbichi......
NOTE: it is high time tulijipanga kwenye forum zetu kuwa tupigane mshahara wa mbunge uwe as high as the university professor....ili ONLY COMMITED PEOPLE TO GET IN PALE MJENGONI.........
Kwa heshima na taadhima NINAWAOMBA WABUNGE WOTE WAZEE WAFUNGASHE NA WAIGE MFANO WA MAMA MAKINDA (ambaye kwa kauli hii nimemuheshimu sana)....
Pia nawaomba wale wabunge vijana wanaofikiri kwa kutumia masaburi pia waunge bogi.....
lets leave the brilliant DOT COMs produce the new cadre to save our sunking Tanzania....
such that hakutakuwa na KULOGANA tena kwa ajili ya hii position......
kiasi kwamba B**** letu limekuwa kambi la wachawi.....
mAMA YETU KASOMA ALAMA ZA NYAKATI...she is brilliant!
Mungu mbariki Makinda...
Mungu ibariki Tanzania...
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwa makini na kuchukua hatua za haraka kurejesha amani kabla Watanzania hawajaishiwa uvumilivu na utawala wa serikali yake ...
kwakua mheshimiwa umekua unatufariji mara kwa mara hasa kwenye misiba iwe ya raia ua viongozi bila kuja kujali itikadi za vyama vyetu.tunakuomba uwakumbuke na wananchi wa songea hasa ukizingatia kuwa jeshi letu la polis limekiri udhaifu kwa kutumia nguvu nyingi bila sababu za msingi kwa kuuwa raia wasiokua na hatia
JK Aongoza Kamati Kuu Ikulu Leo February 27, 2012
Source: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Kampeni ya kupunguza umri wa urais haina uhusiano na mimi kutaka kugombea urais 2015 « Zitto na Demokrasia
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Kampeni ya kupunguza umri wa urais haina uhusiano na mimi kutaka kugombea urais 2015
KABWE ZUBERI ZITTO, MPKIGOMA KASKAZINI TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARIKampeni ya kupunguza umri wa urais haina uhusiano na mimi kutaka kugombea urais 2015
Baadhi ya vyombo vya habari vimehusisha kauli yangu ya kutaka kupunguza umri wa kugombea urais na mimi ‘kuutaka urais'.
Mimi nikiwa mwanachama na kiongozi wa chama chama changu cha CHADEMA naelewa na kuziheshimu taratibu na kanuni tulizojiwekea za kuomba nafasi mbalimbali za uongozi, ikiwemo nafasi ya urais.
Nafasi ya uongozi ndani ya CHADEMA haiombwi kwenye warsha. Iwapo chama changu, wakati muafaka ukifika na kutokana na matakwa ya jamii, kikiona nipewe jukumu lolote sitasita kutekeleza wajibu huo niwe au nisiwe mgombea.
Kwa hivyo, nilichozungumza jana ni kutoa maoni yangu kwamba muda umefika kwa Taifa letu kupunguza umri wa kugombea urais. Maoni yangu haya yanatokana na ukweli kwamba hakuna sababu zozote za kisayansi zinazomfanya mtu aliye chini ya umri wa miaka 40 akose sifa za kuwa Rais.
Msimamo huu nimekuwa nao tangu zamani nikisoma shule na haujawahi kubadilika. Hakuna mahala popote katika maoni yangu niliyotoa jana niliposema kwamba nataka umri wa urais upunguzwe ili nipate fursa ya kugombea nafasi ya urais. Pia siwezi kutaka katiba iandikwe kwa ajili yangu.
Vilevile kamwe isionekane kwamba matakwa ya muda mrefu ya vijana ya kutaka umri wa kugombea Urais kupunguzwa yanalenga kunipa fursa mimi kwani mimi ni binaadamu naweza nisiwe na sifa za kuwa Rais lakini kukawa na vijana wengine wengi wenye umri chini ya miaka 40 wenye Uwezo na Uzalendo wa kutosha kushika usukani wa nchi yetu.
Ni maoni yangu kwamba tupate mabadiliko ya vizazi katika uongozi wa nchi yetu ili kukabili changamoto za sasa zinazokabili Taifa letu.
Tunapojiandaa kutoa maoni kuhusu Katiba Mpya ni vizuri vyombo vya habari vikajikita kutoa taarifa bila kuweka tafsiri au kuwatafasiria maoni ambayo wananchi na viongozi watakuwa wanayatoa kuhusu maudhui ya Katiba Mpya.
Dar es Salaam29 Februari 2012