Ufisadi Bila Majibu: Rais Kikwete na Lowassa sasa jiuzuluni ndani ya siku 90 kupisha uchunguzi huru


NEC CCM PINDI WANAPOKAA NA BARAZA LA MAWAZIRI KAZI ISIWE NI YA KUREFUSHA LISTI YA WATANZANIA GANI WAFE KWA KUWA HAKUNA KITU 'AMANI' KWA NCHA YA UPANGA HAPA

Taarifa hizi tunazo tayari kwa zaidi ya wiki sasa.


Hata hivyo maswali ya msingi sana ya kujiuliza ni kwamba je huu mpango wa mauaji wa hivi sasa watu wazito kama vile Askofu Mkuu Mwadhama Polycarp Pengo, Samuel Sitta, Ruaichi na wengine kibao tu ambao yote yanatarajiwa kutekelezwa KWA FAIDA NA MANUFAA YA NANI Tanzania hii eti kwa kisingizio kwao wao kuwa chanzo Kikwete na CCM kushindwa kutawala?????????

Naam, kunabainishwa kwamba kuwa orodha inakwenda ikiongezeka kila uchao huko kwa madalali wa mauaji nchini, hata hivyo listi nzima nayo iko mezani. Suala la Dr Mwakyembe na waraka wa siri juu ya mikasa yake ndio kabisaa taabu tupu huko ndani maswali yakiulizwa bila majibu eti SIKU ANAPOAGA DUNIA Tanzania itakuaje??

Lakini hata hivyo, hata kabla ya hawa MADALALI YA MAUAJI Tanzania hawaja piga hata hatua moja kwa ajili ya kutetea uchuro wote huu dhidi ya umma nchini, ni vema yeyote mwenye kujali akawauliza kwamba je NYUMA YA KISOGO CHAO NA KILE CHA MATAJIRI WANAOAGIZA MAUAJI HAYA KUTEKELEZWA wao wanaona kitu gani hapo hadi sasa??

Hakuna amani hapa kwa ncha ya upanga kwa mtu yeyote kudiriki kutetea UCHURO mbele ya uso we umma wa Tanzania.

Swala la Dr Mwakyembe sasa limeongezeka 'ugumu' zaidi tena kupita maeleza huko ndani jikoni.


Wakuu lisemwalo lipo na kama halipo linakuja,hawa watu siwafahamu kwa kuwaona uso kwa uso.

Kuna taarifa kutoka jikoni kuwa hawa watu wanasababisha nchi isitawalike,kwa fununu tu ni kwamba hawa watu watauwawa kwa wakati tofauti,namjua Samweli Sita ni Waziri na Mbunge hao wengine siwajui.

Naomba yeyote aliye karibu nao awape hizo,mambo sio mazuri kabisa system nzima imeharibika,okoa maisha yako!

source mimi na mtu wangu wa jikoni!
 
Ni ajabu sana pindi GIZA inapojiweka bize mno kupigana vita na MWANGA ndni ya nchi hii!!!!!!!!!!
 
Inakua vipi Benki Kuu ya Dunia idese mawazo yaliojadiliwa humu JF kiundani zaidi mnamo 2011 na kutumia mawazo hayo hayo kuishauri serikali hii ya CCM yenye sikio zito sana na huku sisi hapa serikali hii hii ikawa imegoma kutusikiliza tangu hapo mwaka jana??????

Au ushauri mpaka utoke nje ya nchi mpaka taifa tunadhalilika kama vile hatuna watu wenye mawazo mazuri ki-uchumi hapa nchini?????

Jana; Taarifa ya Habari Radio One saa 2 na saa 4 usiku, Radio 1 walitoa Habari WB imeishauri Serikali ya Tz kubana matumizi na kuweka vipaumbele.

Ukweli ni kwamba nilijisikia aibu sana kwamba hadi wafadhili wetu, wanaotudai mamilioni ya dola (ingawa kihalisia wao wangefanya biashara kwa kuzidi kutukopesha) wanaiona Serikali yetu imejaa ubadhirifu kwa matumizi makubwa yasiyo ya lazima na kushindwa kuweka na kuzingatia vipau mbele.

Kama tungekuwa na viongozi wenye haya, ushauri huo wa WB ni udhalilishaji.
 
Hivi mnajua Lowasa alisoma nini chuo Kikuu? Ngoja nikumegee alisoma kucheza ngoma (Paukwa). Ni kichekesho kwa hiyo yeye ni mwigzaji wakati wote. Wote na rafiki yake they have never ever been serious. Muulize kamanda mkubwa kabisa wa JWTZ kabla ya Mwamunyange.
 
Hapo kwenye RED, Mkuu hili nilikua silifahamu hata kidogo kwamba ndio mchepuo wa huyu Baba Richmond.

Hivi mnajua Lowasa alisoma nini chuo Kikuu? Ngoja nikumegee alisoma kucheza ngoma (Paukwa).

Ni kichekesho kwa hiyo yeye ni mwigzaji wakati wote. Wote na rafiki yake they have never ever been serious. Muulize kamanda mkubwa kabisa wa JWTZ kabla ya Mwamunyange.
 
MAAGIZO YA VIJANA WA TANZANIA KWA KAMANDA LEMA:
KWA KUSHIRIKIANA NA
'WASHIRI-CHADEMA' NENDA ARUMERU MASHARIKI KUWAFIKISHIA SALAAM ZA KUPIGANIA KUREJESHWA KWA 'HAKI, HESHIMA NA UTU WA KILA MTANZANIA'


Hakika Vijana wote nchini Tanzania nawapeni HEKO SANAAAAAAAAAAAAAAAA kwa kumfanya kijana mwenzetu Mhe Kamanda Gobless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini, kwa kumfanya huyu mwenzetu awe ni mtu wa kukinyima usingizi kila kiongozi wa MAGAMBA pamoja na maafisa wa serikali ma-kada kama Yohana Tendwa.

Kimsingi, huyu kijana mwezetu wala hatumheshimu kwa kitu pesa alizo nazo mfukoni maana kiukweli fedha bado hana; na wala vijana hatujachagua kumheshimu huyu kijana mwenzetu kwa kuwa na cheo tu cha ki-bunge maana wapo wengi tu wenye vyeo vikubwa zaidi ya hiyo tena wanaolipwa
Tshs 20,000,000/- na miposho zaidi juu (Kafulila et al).

Naam, nasema Machalii wote Tanzania hatujachagua kumheshimu na kumpa ufuasi uliotukuka Kamanda Lema shauri ya usomi wowote maana kama ni usomi tu tunao Ma-Profesa kibao nchini lakini wanajificha mbele ya dhuluma tunaofanyiwa wanyonge wa nchi hii huku wao wakiendelea kuvuta kuku kwa mrija hata bila ya kujali vijana wa nchi hii hali yetu ikoe.

Hakika, kuna kitu cha kipekee mno kile kinachomfanya Kamanda Lema nyota yake ang'ae mpaka kuwatikisa Ma-Washiri CCM huko AruMeru, kila alichonacho huyu kijana mwenzetu ambacho Mamilionea wenye fedha za kukwapua kama Lowassa hawana.

Ndio, nasema kuna kitu kikubwa sana chenye upekee kinachomfanya wanyonge wa nchi hii wamkubali Kamanda Lema na kumkataa Msomi kama Dokta Bana anayeonekana kuwa ni mfano hai wa wasomi wanaokubaliana na wadhulumishi wa nchi hii kwa kila kitu ilmradi tu mkono uende kinywani mwakwe.

Wala sio siri tena kwamba kwetu sisi vijana kumtii kule huyu kijana mwenzetu maneno yake na kumpuuza Waziri Ngeleja yoooote haya yanatokana na kitu kidogo sana lakini chenye upekee mno katika uhai na mustakabali mzima wa taifa letu leo na kesho.

Ni kweli, kwake huyu Kamanda Lema kwamba vijana tunatambua kitu lulu, kuaminika, kutegemeka na thamani kubwa iliomo ndani ya KILE ANACHOSIMAMIA NA KUIAMINI KWANIABA NA FAIDA YA WANYONGE kutufariji wakati wote wa shida na dhuluma zisizoisha kote nchini

Kwake yeye Kamanda Lema, bila kitu KUJIKWEZA, vijana wenzake tunatambua dhahabu ya ajabu mno katika ule ujasiri wake wa kutete Maslahi ya Umma kwa kuzingatia misingi ya ile falsafa ya KUREJESHWA KWA HESHMA, HAKI NA UTU WA MTANZANIA.

Hadi hapo sasa, Kamanda Lema, kwa maagizo yetu sisi vijana wa nchi hii tunaodhulumiwa sana, tunaoporwa sana rasilmali zetu na vile vile kila mara KUPOKONYWA HAKI ZETU ZA KUJICHAGULIA VIONGOZI TUNAOWAPENDA SISI WENYEWE, hivi sasa tunakuagiza kupitia chama chetu makini CHADEMA uongozi timu ya kukata na shoka kwenda AruMeru Mashariki kusaidiana na Wapiganaji wenzetu wakazi wa pale kuendesha kampeni ya kufa mtu, chumba hadi chumba hadi kiongozi wa kweli wa wananchi kupatikana bila rushwa!!

Kazi iendelee na utetezi wa haki za sisi wanyonge iwe mbeeeeeeeeele kama tai!!
 
'WASHIRI-CHADEMA' NA SISI VIJANA SASA 'KUPIGA KURA KWA FUJO' KUMUUMBUA SHETANI YA MAGAMBA NA MBUYU WAKE UFISADI NCHINI

Kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu atutiae nguvu, vijana sasa 'tunapiga kura kwa fujo' kuumbua shetani, kuandika upya na vizuri historia pale AruMeru Mashariki hivi karibuni.

Nasema vijana wa nchi hii tunategemea kufanya hivi huku tukiongozwa na kazi murua wa Kamanda Lema kwa kushirikiana kwa karibu sana na
'Washiri-CHADEMA' ili kumuumbua huyu naibu mpya wa kujitolea kwa Nape, Ndg Yohane Tenwa.

Azma yetu hii mpya inatokana na ukweli kwamba hata siku moja 'Washiri-CCM' hawajawahi kuteuliwa na Wameru ili wawe wazungumzaji wa 'Washiri-CHADEMA' kupitia kwa Afisa Mwandamizi mpya na Kada wa chama hicho kwa cheo kipya cha Naibu Afisa wa Itikadi na Uenezi CCM, Bw Yohane Tendwa.

Jamani kwa propaganda hii ya tendwa inaonesha kabisa ni msaidizi wa nape na wanafanya kazi moja au nyie mnaonaje?

Ni naibu wake siyo kaimu. Alikuwa underground sasa katokea kumsaidia bosi wake.

 
Mzee Tendwa kama ni siasa safi ni siasa safi kwa sana lakini kukijitokeza propaganda kwa kujificha hapo kwenye ofisi yetu hiyo ya umma wote wa Tanzania sasa hadi hapo ndio usipime.

Machalii wote AruMeru Mashariki ndio kama hivi tunakuja jinsi tulivyo tunagonga vija Dar mpaka Meru mpaka 'Washiri CCM' nao wapate kucheka wao wenyewe na roho zao.
 
Kumbe Botswana kwa wakati huu kuna mnuso wa KI-CHAMA lakini wengine tunatumia rasilmali za KI-SERIKALI kwenda huko kucheza na Makirikiri!!!!!!!!!

World Bank, wenzenu huku Tanzania ndio kama hivo tumeshaanza kujibania matumizi na kujiwekea vipaumbe muhimu zaidi kitaifa. Asanteni sana kwa ushauri wenu murua!


attachment.php


Laana unayo wewe usiyeheshimu wakubwa wako! kila jambo lina ngazi zake za utekelezaji! Haiwezekani kila jambo rais aingilie kati utafikili hakuna watendaji.

Ushauri mwingine ni vichekesho kweli. Hivi mtu anategemea kuwa JK atamsikiliza na kujiuzulu.
 
Mwambie ajiuzuru mzee wako cheo cha ubaba kwako kwa kuwa ameshindwa kukulea vizuri huna heshima na kumbuka heshima huwa inaanza ndani ya familia,unaleta siasa zako hapa hivi tu kama humpendi Raisi ni wewe na familia yako kwa sababu zenu binafsi usitusemee eti watanzania wamechoka sema ivi wewe na familia yako mmechoka kwa sababu zenu binafsi lakini sisi tuliomchagua tunataka aendelee mmeona vyama vyenu vya ukabila,ukanda,undugu na udini vimeshindwa kuingia ikulu kwa njia ya demokrasia mnataka kuhamasisha watu muingie kwa vurugu kaeni mkijua mbinu zenu watanzania wamezijua na hawako tayari wewe itisha maandamano utatokea wewe na mkeo wala si umma wa watanzania mmedoda imekula kwenu shabashi!
 
Tarati, taratibu mkuu!!!!!!!!

Hebu kwanza pokea hii hanjifu nyeupo, kajipanguse nayo povu mdomoni, ukajiachie japo kinafasi kumeza mafundo mawili au matatu hivi ya mate ndipo urudi sasa tukajadiliane HOJA KWA HOJA.

Lakini kwa sasa kwa mtaji wa hii kukurukakara za mfa maji wala hakutojulikana kati yetu wawili KICHAA HALISI ni yupi hasa.

Siku njema.


Mwambie ajiuzuru mzee wako cheo cha ubaba kwako kwa kuwa ameshindwa kukulea vizuri huna heshima na kumbuka heshima huwa inaanza ndani ya familia,unaleta siasa zako hapa hivi tu.

Kama humpendi Raisi ni wewe na familia yako kwa sababu zenu binafsi usitusemee eti watanzania wamechoka sema ivi wewe na familia yako mmechoka kwa sababu zenu binafsi lakini sisi tuliomchagua tunataka aendelee.

Mmeona vyama vyenu vya ukabila,ukanda,undugu na udini vimeshindwa kuingia ikulu kwa njia ya demokrasia mnataka kuhamasisha watu muingie kwa vurugu.

Kaeni mkijua mbinu zenu watanzania wamezijua na hawako tayari wewe itisha maandamano utatokea wewe na mkeo wala si umma wa watanzania mmedoda imekula kwenu shabashi!
 
IGP Saed Mwema, mauaji ya wananchi Songea tunahitaji kuona hatua zaidi ya kuomba tu msamaha kitendo hicho bado kuendelea hata leo.
 
Waachie ngazi wenyewe waje watu wengine wenye moyo wa kuongoza tena kwa faida ya walalahoi wote nchini.

Chombo cha juu kabisa cha maamuzi ki-chama pindi kinaposhindwa kutoa maamuzi juu ya KERO LA TAIFA LA UFISADI, je kitu gani kinatakiwa kifuate kwa wahusika?
 
Katika hoja hii hapa, wahusika wakaifanyie kazi au la wala si kazi ya mtoa hoja kuhangaishwa nayo kwa sana, ni kwamba Wa-Tanzania tunatafuta kuweka KUMBUKUMBU SAWA NA HISTORIA IJE ITUAMUE HIVO.

Kwamba hatukuwanyamazi Rais Kikwete na Lowassa kwa kipindi ambapo madai mazito ya ubadhirifu wa kodi za umma ulipotendeka chini ya uangalizi wao na ndani ya uwezo wao kuuzuia ubadhirifu huo kwa kutumia mamlaka na madaraka tuliowakasimu kwenye nyadhifa hizo za umma.
Tukubaliane kuikomboa nchi kwa kumsaidia Rais wetu kwa kumwambia wanaomuharibia sifa zake au wanaomkwamisha katika utawala wake. kwa kutaja Ufisadi unaofanyika katika maeneo yetu yanayotuzunguka mfano maofisini mwetu. Tunawafahamu wale wote anaokula kodi ya Mtanzania bila aibu.

Watanzania tusimulaumu sana Rais JK maana hana uwezo wa kuona kila kona ya Tanzania na ndani ya ofisini mwetu, ni jukumu letu kukemea haya matukio ya UFISADI (Mafisadi tunawajua sana na jinsi wanavyoitafuna Taifa)

 
Back
Top Bottom