Ufisadi Bila Majibu: Rais Kikwete na Lowassa sasa jiuzuluni ndani ya siku 90 kupisha uchunguzi huru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi Bila Majibu: Rais Kikwete na Lowassa sasa jiuzuluni ndani ya siku 90 kupisha uchunguzi huru

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Uwezo Tunao, Nov 28, 2011.

 1. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  RAIS KIKWETE NA MJUMBE WA NEC CCM TAIFA EDWARD LOWASSA SASA NI WAKATI MWAFAKA MJIUZULU MARA MOJA KUPISHA UCHUNGUZI WA TUME HURU KUWATAKATISHENI MAJINA MBELE YA UMMA NA JUMUIYA YA KI-MATAIFA

  Kufuatia sakata la ufisadi juu ya ufisadi katika serikali hii ya awamu ya nne na viongozi kuzidi kutupiana mpira bila matokeo yoyote ya kubadilisha sura ya mambo, wananchi sasa tunasema kwa sauti kuu; Rais Kikwete na Lowassa mjiuzulu sasa hivi nyadhifa zote kupisha uchunguzi wa kujitegemea ili kutakasha majina yenu mbele ya umma.

  Wananchi tunayo haki ya kuhoji vitendo vyenu, tunayo haki ya kujua kwa kina kitu gani kinaendelea ndani ya uongozi wetu kiserikali na vyama vyao vinavyowafadhilini nyinyi kushika nyadhifa hizo.

  Ndio, nasema wananchi sasa tunataka majibu ya ki-uchunguzi juu ya Richmond, Dowans, Meremeta, IPTL na nyinginezo ili sote tupate kuanza upya katika ukurasa mpya kama taifa. Ndio,pale ambapo vyama vinavyowafadhilini kushika nyadhifa za umma zinaposhindwa kutolea maamuzi mambo nyeti na kero kubwa kama haya kwa taifa maana yake ni kwamba sasa maamuzi lazima yapatikane toka nje ya hicho chama fadhili.

  Na hiyo ndi sababu sasa umma wa Tanzania kwa ujumla wetu tumeamua kuwaombeni kupisha uchunguzi ufanyike haraka.

  Nasema hizi kelele mnazoendelea kutupigia makanisani, misikitini, na kwenye vikao vyenu vya maswahiba kuuziana chai wala hazitusaidi kupunguza ukali wa maisha ambamo vitendo vya rushwa vimetufikisha kama taifa hadi dakika hii.

  Kama hamnielewi bado nasema hivi, Jogoo akijinyea mwili mzima bandani hata siku moja kamwe hapati tu kutakata eti kwa kuzidisha sana kasi ya kuwika na kuwika kila mahala akitangaza utakatifu wake huo.

  Rais Kikwete, Lowassa na wengine wenye shutuma kama hizi za rushwa chonde mtusamehe na hizi siasa uchwara, Wa-Tanzania hivi sasa TUNADAI MAJIBU kwa haraka na kina zaidi. Endapo mlikua bado hamjui, uvumilivu wote sasa umeanza kutushinda na kweli Wa-Tanzania sasa tumechoka visivyo kifani na hizi 'bembeleza mwana' zenu hizi juu ya dhamira zenu kushughulikia rushwa nchini.

  Ni wazi tena mkumbuke ya kwamba mambo haya yote yamekua yakiendelea huku wananchi tukiendelea kuumia zaidi na zaidi kwa gharama ya maisha inaendelea kupanda ajabu, watoto kufa bila dawa hospitalini, vijana hatuna ajira, shughuli za ukulima mashambani yamekwama na haki kutoweka ofisi za umma kutokana vitendo vya rushwa mnazoshutumiwa nazo nyinyi hapo. Kwa nini muendelee kushikilia nyadhifa za umma wakati kila kona kuna kilio??

  Kwa kuwa hata na nyinyi hatupendi kamwe muonewe kutokana na vitendo vya rushwa ambavyo pengine hamkuzifanya, basi ndio maana tunawaelekezeni kwamba njia ya kistaarabu ni kujiweka kando na nyadhifa zote za umma hadi hivi sasa ili uchunguzi wa kina upite na baadaye historia ikawaamueni vizuri na kwa haki zaidi.

  Ndio, kufuatia sakata la ufisadi kila kona nchini bila ya wananchi kupewa majibu ya kuridhisha juu ya kila tukio, kupuuzwa kwetu sana, watu kurushiana mipira kusikoisha juu ya hili saratani linalorudisha nyuma maendeleo, na hata vikao rasmi vya baadhi ya vyama vikongwe nchini kushindwa kutolea jibu KERO HILI KUBWA KITAIFA, wananchi sasa tunasema Rais Kikwete na Waziri Mkuu uliyejiuzulu kwa kashfa hizi hizi za rusha sasa mjiuzulu nyadhifa zote kupisha uchunguzi wa kina juu ya mambo haya yote na kuweka wazi kodi zetu zilipo.

  Kwa kuhitimisha hoja yangu hii hapa, napenda kusema nafasi zote za umma watu huzishika kutokana na ridhaa na imani kubwa ambayo wananchi wanao kwa viongozi wao. Kwa kusema kweli hadi sasa wananchi hatuna imani kwenu tena mpaka siku tume huru itakapotupa sababu za kina za kutufanya kurejesha tena matumaini, heshima na imani kuendeleaa kutuongoza tena.

  Hebu fanyeni hima juu ya hili kabla taifa nzima hatujalazimika kutumia silaha yetu ya mwisho ya maandamano dhidi yenu mpaka kieleweke. Penye ustaarabu wananchi hatutosita kurudisha ustaarabu hata kama shutuma dhidi yako ni nyekundu kama damu, na kinyume chake pia ni kweli tena bila ajizi.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Nov 28, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,157
  Trophy Points: 280
  Sijafahamiana na Kikwete barabarani alisema Lowassa, akiwa ana maana kwamba Kikwete hana la kumfanya Lowassa
   
 3. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ushauri mwingine ni vichekesho kweli. Hivi mtu anategemea kuwa JK atamsikiliza na kujiuzulu.
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana kuona viongozi wa CCM wanavyogeuza janga la taifa kama hili la UFISADI kuwa ni jambo la kawaida kufanyia mzaha na kuingiza siasa za kichama ndani yake wakati taifa linaangamia kwa maendeleo duni bila ajira, bila dawa mi-hospitalini.

  Lakini ndio bado unasikia eti vikao vya NEC CCM vimeshindwa kulitolea uvivu ugonjwa huu na badala yake kuanza tena na hadithi za 'bembeleza mwana' na wananchi pia tuendelee tu kuwanyamazia huku wengine tayari wakionekana mashujaa na mashabiki wao katika rushwa?


   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Nov 28, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Jumatatu huwa ina mambo kweli kweli. Yaani mtu anaamka nazo then anakurupuka kupost vitu vya ajabu hapa JF. Bure kabisa hii.
   
 6. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #6
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nimekusoma FRUSTRATION yako sawa tu na mimi hapa Mwita25 kwa sababu tu wananchi tunadharauliwa sana na viongozi wetu, kutuchukulia misukule isioweza kuhoji kitu na vile vile viumbe tusio na haki ya kujua juu ya ubora wa utendaji wa serikali yetu na viongozi wake.

  Pia nimetambua unavyosumbuliwa sawa tu na mimi hapa kwamba eti mtu ukishakua tu rais basi kuwajibika kwako ni ndoto mpaka yakutokee yale ya Tunisia. Hapa nchini tusingependa tufike huko ndio watu wawajibike kutokana na shutuma nzito kama hizi dhidi yao!!

   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Nov 28, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Asiposikiliza na kujiulu atakuwa anawapa watu sababu kubwa ya kukikataa chama chake 2015
   
 8. Biera

  Biera JF-Expert Member

  #8
  Nov 28, 2011
  Joined: Dec 7, 2010
  Messages: 437
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Unaota ndoto za mchana wewe!
   
 9. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #9
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Watu walikokutania kusiwe sababu ya kutokutupa majibu juu yanayotosheleza juu ya shutuma hizi nzito za rushwa huku wengine wakionekana wazi wazi kushabikia UFISADI na hata baadhi ya mafisadi sasa kuanza kuonekana mashujaa!!!!!!!!!!!!

   
 10. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #10
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Biera, hoja hii huenda ikaonekana kama vile utani vile lakini ikitokea kwamba waheshimiwa hawa wawili hawatotii hili basi hapo ndipo sasa wananchi tutakua tumepata sababu za msingi na za dhati kabisa kuwakataa kabisa pamoja na chama chao cha CCM kokote kunakogombewa kiti chochote kuongoza ofisi yoyote ya umma.

  Nakwambia hili lisipotekelezwa basi adhabu ya mahakama ya waheshimiwa wananchi wapiga kura tutaupitisha na kupunguza viti vya ubunge CCM toka 250 hivi sasa mpake 78 nakuambia!!


   
 11. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #11
  Nov 28, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Don't urge with a fool people might not notice the difference, walio wengi tumekuelewa unazungumzia nini.
   
 12. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #12
  Nov 28, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Tatizo kubwa la Kikwete ni kutokuweza kutambua au kudharau public opinion juu ya mambo mbalimbali yanayolikabili taifa. Ni vizuri akitambua kuwa Urais kama cheo kinatokana na matakwa ya wapiga kura kuchagua mtu wanaedhani atawasaidia kutatua matatizo yao ya kimaendeleo.

  Wabunge nao huchaguliwa ili wawakilishe matakwa ya wananchi kwenye muhimili wao; hivyo basi maazimio yote yanayopitishwa na wabunge kama wawakilishi wa wananchi ni kauli ya wananchi ambao ndio waliomuweka Rais madarakani na hivyo anapaswa kuyaheshimu maamuzi hayo.

  Hatutegemei kuwa katika masuala ya kukosa uadilifu hapa nchini kama haya ya Jairo na Luhanjo, Kikwete atapata kigugumizi kuyashuhulikia kwa kufuata sheria za nchi; akitumia urafiki kama kigezo cha maamuzi yake itamuwia vigumu kiutawala kufanya maamuzi huko mbele yatakayowahusu watu ambao hawapo karibu nae na hiyo sio good governance!!
   
 13. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #13
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Yeyote anayepigania heshima ya UBINADAMU, HAKI NA UTU WA MTANZANIA, ndani au nje ya vikao vya CCM, hata ukiwa tu peke yako tu, ukae ukijua ya kwamba kamwe sauti zinazopinga UFISADI kwa wana CCM hazitokaa zimezwe na kwamba wala pumsi zenu hazitotoka bure bila ya Umma wa Tanzania kukuthibitishia kwamba tumekusikia.
   
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  KATIKA HILI LA MIKANGANYIKO JUU YA 'LA KUVUNDA LA EXECUTIVE CORRUPTION' CCM ITOKE VIPI: MOST URGENTLY EXERCISE RIGHT OF RECALL OF THE PRESIDENT ILI MPONE

  Chaguni ni kwa CCM hivi sasa kati ya kufa KI-LOFA KATIKA SIASA ZA NCHI HII kwa kumuona Kikwete ni wa maana zaidi kuliko chama chao na kwamba vile vile ni wa maana zaidi kuliko taifa letu la Tanzania au wajikomboe kwa ku-EXERCISE RIGHT OF RECALL OF THE PRESIDENT that is worst off diminishing their party's political fortunes and future.

  Laa sivyo, kama ambavyo tulivyowahi kuwaonya mapema zaidi huko nyuma - KILA KITU NI MDORORO MTINDO MMOJA mpaka CCM kugota kwenye aibu ya mwaka.

  Najua wengi hamtoamini haya ninayoyasema mpaka kuja kuyaona kwa macho na hatimaye kuyagusa kwa mikono ila wenye wenye upeo wa kuona mbali zaidi tayari wanazo taarifa hizi kibindoni.

  Watanzania Uwezo Tuna!!
   
 15. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #15
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Chombo cha juu kabisa cha maamuzi ki-chama pindi kinaposhindwa kutoa maamuzi juu ya KERO LA TAIFA LA UFISADI, je kitu gani kinatakiwa kifuate kwa wahusika?
   
 16. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #16
  Nov 28, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Miluzi mingi haiwezi kumuua mbwa lakini wakati mwingine humchanganya asikudhuru, so keep on whistling.
   
 17. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #17
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Katika hoja hii hapa, wahusika wakaifanyie kazi au la wala si kazi ya mtoa hoja kuhangaishwa nayo kwa sana, ni kwamba Wa-Tanzania tunatafuta kuweka KUMBUKUMBU SAWA NA HISTORIA IJE ITUAMUE HIVO.

  Kwamba hatukuwanyamazi Rais Kikwete na Lowassa kwa kipindi ambapo madai mazito ya ubadhirifu wa kodi za umma ulipotendeka chini ya uangalizi wao na ndani ya uwezo wao kuuzuia ubadhirifu huo kwa kutumia mamlaka na madaraka tuliowakasimu kwenye nyadhifa hizo za umma.
   
 18. Possibles

  Possibles JF-Expert Member

  #18
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 1,361
  Likes Received: 558
  Trophy Points: 280
  Kete hii ya kisiasa ya hawa mabwana wakubwa itatuumiza kwa kuwa nia yao ni kuhakikisha wa-tz hatujadili mambo ya msingi yanayokabili taifa hili.Instead twawajadili wao.l
   
 19. n

  nyuki dume JF-Expert Member

  #19
  Nov 28, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 438
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tatizo la Wabongo maneno mengi kuliko vitendo hasa watu Dsm, wamikoani hawana maneno mengi wawo wanasubiri chaguzi ndio wanaonyesha kwa vitendo,
   
 20. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #20
  Nov 28, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  TATIZO LA CCM HIVI SASA NI MADAI YA UKWAPWAJI WA RAIS KIKWETE MWENYEWE NA KULE KUONEKANA KUSHINDIKANA CHA KUMFANYA WAKATI KILA KONA ANAHISI DOLA YATOSHA KUMKINGA VYA KUTOSHA

  Tatizo la CCM wala si la kiitikada kama Daktari Bana anavyajaribu kuwaaminisha, nasema tatizo la CCM wala si makundi kama ambavyo Mzee Mkama anavyojaribu kupaka mafuta mgongo wa chupa.

  Ndio nasema hiviiii, tatizo la CCM wala si swala la kiu ya urais na usemi kwamba eti watu wnapigania kumbo kufa na kupona juu ya hilo nakataa kata kata kwa kuwa najua fika kwamba tatizo la CCM hivi sasa ni uporaji wa mali ya umma unaofanya na uongozi wa juu kabisa katika nchi yetu hivyo watu wachache tu mle ndani HUZIDIANA MGAO na kuanza kununiana mwisho wa siku majambazi kuchinjana wenyewe kwa wenyewe hata kabla yetu sisi wenye mali kuwagusa.

  Lakini kwa kuwa sisi siku zote ni wale mafundi wa kutibu goti kwa dawa maumivu ya kichwa kama ambavyo wafanyavyo Muhimbili kwetu kila uchao, tutaendelea kujizungusha weeeee bila tija yoyote mwisho kuibuka tu na maneno ya kifedhuli kwamba eti hatuna ushahidi na ufisadi ndani ya chama chetu; bure kabisa na wala hamna kitu pale!!

  Tiba pekee ya kukifanya CCM ipone ni NEC wa chama hicho kujikamua kupata ule ujasiri wa Marehemu Mwalimu Nyerere na kuutumia ujasiri huo KUMUITA NYUMBANI RAIS KIKWETE, kama ambavyo ANC ilivyofanya kwa Mbeki kule bondeni, ili huyu baba akapishe uchunguzi wa kina (Public Inquest) kufanyika juu ya madai mbali mbali ya rushwa dhidi ya yake mwenyewe na uongozi wake.
   
Loading...