UFILIPINO : Kanisa Katoliki lamkosoa Duterte kwa mauaji ya walanguzi wa mihadarati

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
c4d4afcbd299855825916a70ab475ea1.jpg
Kanisa katoliki nchini Ufilipino, limetaja kampeni ya kukabiliana na walanguzi wa dawa za kulevya, inayoongozwa na Rais wa nchi hiyo, Rodrigo Duterte, kama ugaidi dhidi ya watu maskini

Kanisa hilo linasema kuwa, inafahamika bayana kuwa, kuna upendeleo mkubwa miongoni mwa wanaouawa

Kufikia sasa maelfu ya watu wameuawa katika juhudi hizo za Rais za kutaka kuangamiza magenge ya walanguzi na watumiaji wa mihadarati

Ujumbe wa kanisa hilo umesomwa kote nchini Ufilipino leo Jumapili

Tangazo hilo linakuja wiki moja tu baada ya Rais Rodrigo Duterte kuahirisha kampeni hiyo kutokana na ufisadi wa idara ya Polisi.

Chanzo: BBC /Swahili
 
Sio ugaidi dhidi ya maskini...

Ni mauaji dhidi ya wauzaji na watumiaji wa madawa ya kulevya...


Kama hawapendi wakatoliki wa kifilipino na wafalipino kwa ujumla wafe kwa mihadarati basi wangemkosoa Duterte kwa kutoa njia mbadala ya kudeal na wafilipino
 
Leo anaonekana kama anachokifanya ni ukiukwaji wa haki za binadamu,lakini siku moja taifa lake litakapokuwa free from Cocaine and the likes ndio watagundua kuwa yuko sahihi.Kuna wakati binadamu anahitaji kupitia hatua ya ukatili ili aweze kuwa na maisha bora.
 
Duniani bara la America ya kusini ndio kuna RC wengi kuliko sehemu yeyote au bara lolote duniani ikifatiwa na bara la AFRICA na ndo bara la pili kwa umasikini baada ya AFRICA na ndo bara ambalo biashara na wafanya biashara wakubwa wa madawa ya kulevya walitokea
 
Pamoja na mabalaa yote Dutetre kama kuna mtu atathubutu kuendelea na hiyo biashara hapo Ufilipino atakua ameamua kujiua mwenyewe.
 
Kabisa katoliki si ndio linahusika na hii biashara sasa wamekuja juu baada ya kuingiliwa na bwana duterte
 
Back
Top Bottom