Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Ufaransa yatoa Sh 100 mil kusaidia Kilosa
Fredy Azzah (mwananchi)
UFARANSA kupitia ubalozi wake nchini, imetoa Sh100 milioni, kuwasaidia watu walioathiriwa na wa mafuriko wilayani Kilosa, Morogoro.
Akikabidhi msaada huo jana kwa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania, Balozi wa Ufaransa, nchini Jacques de Labriolle alisema, nchi yake imetoa msaada huo baada ya Chama cha Msalaba Mwekundu cha Ufaransa kuarifu kuwa mafuriko hayo yamesababisha maafa makubwa.
"Chama cha Msalaba Mwekundu cha Ufaransa kimetuambia kwamba hali katika Wilaya ya Kilosa ilikuwa mbaya sana, na kimetupa ushauri wa kuitikia ombi la msaada wa dharura lililotolewa na Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania," alisema Balozi Labriolle.
Balozi huyo alisema vifaa vitakavyo nunuliwa kwa kutumia fedha hizo kwa ajili ya wananchi waliokumbwa na maafa hayo ni pamoja na vyandarua, vyombo vya kupikia, dawa na mahema kwa familia ambazo hazina nyumba.
"Tunatumaini kuwa chama cha msalaba Mwekundu cha Tanzania. kitafanya kazi kwa karibu na mamlaka zilizo katika Wilaya ya Kilosa, ili kuhakikisha kuwa misaada inawafikia watu walioathirika zaidi, mimi mwenyewe natumaini kuwa nitakwenda Kilosa katika siku za karibuni na Waziri Mkulo kuona hali halisi," alisema Labriolle.
katibu Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania, Adam Kimbisa, aliyekabidhiwa msaada huo aliishukuu Ufaransa kwa msaada huo.
Hata hivyo Kimbisa aliwataka Watanzania, mashirika ya kimataifa, makapuni mbalimbali, mashirika ya ndani ya nchi na nchi marafiki kuendelea kutoa misaada kwa ajili ya wananchi wa Kilosa.
Maoni Yangu:
Kuchangia Red Cross ya Tanzania ndiyo njia ya uhakika zaidi ya kujiandaa kwa maafa kwa kujiandaa na majanga. Nawashukuru Ufaransa kwa kuona kile ambacho tulikiona wengine mapema zaidi. Inasikitisha hata hivyo bado taasisi zetu za ndani hazijaona umuhimu wa kuitikia wito huu. Nina uhakika wanasubiri janga litokee ndio waanze kuchangia tena.