Ufaransa watuunga mkono!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,987
Ufaransa yatoa Sh 100 mil kusaidia Kilosa

Fredy Azzah (mwananchi)

02_10_wnq0nx.jpg

UFARANSA kupitia ubalozi wake nchini, imetoa Sh100 milioni, kuwasaidia watu walioathiriwa na wa mafuriko wilayani Kilosa, Morogoro.

Akikabidhi msaada huo jana kwa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania, Balozi wa Ufaransa, nchini Jacques de Labriolle alisema, nchi yake imetoa msaada huo baada ya Chama cha Msalaba Mwekundu cha Ufaransa kuarifu kuwa mafuriko hayo yamesababisha maafa makubwa.

"Chama cha Msalaba Mwekundu cha Ufaransa kimetuambia kwamba hali katika Wilaya ya Kilosa ilikuwa mbaya sana, na kimetupa ushauri wa kuitikia ombi la msaada wa dharura lililotolewa na Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania," alisema Balozi Labriolle.

Balozi huyo alisema vifaa vitakavyo nunuliwa kwa kutumia fedha hizo kwa ajili ya wananchi waliokumbwa na maafa hayo ni pamoja na vyandarua, vyombo vya kupikia, dawa na mahema kwa familia ambazo hazina nyumba.

"Tunatumaini kuwa chama cha msalaba Mwekundu cha Tanzania. kitafanya kazi kwa karibu na mamlaka zilizo katika Wilaya ya Kilosa, ili kuhakikisha kuwa misaada inawafikia watu walioathirika zaidi, mimi mwenyewe natumaini kuwa nitakwenda Kilosa katika siku za karibuni na Waziri Mkulo kuona hali halisi," alisema Labriolle.

katibu Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania, Adam Kimbisa, aliyekabidhiwa msaada huo aliishukuu Ufaransa kwa msaada huo.

Hata hivyo Kimbisa aliwataka Watanzania, mashirika ya kimataifa, makapuni mbalimbali, mashirika ya ndani ya nchi na nchi marafiki kuendelea kutoa misaada kwa ajili ya wananchi wa Kilosa.

Maoni Yangu:
Kuchangia Red Cross ya Tanzania ndiyo njia ya uhakika zaidi ya kujiandaa kwa maafa kwa kujiandaa na majanga. Nawashukuru Ufaransa kwa kuona kile ambacho tulikiona wengine mapema zaidi. Inasikitisha hata hivyo bado taasisi zetu za ndani hazijaona umuhimu wa kuitikia wito huu. Nina uhakika wanasubiri janga litokee ndio waanze kuchangia tena.
 
At this very moment halafu sisi tumefisadi 25bn za kilimo kwanza wht a shame????
 
Nilipoona leo, sio tuu nikafarijika, bali nilihuzunika hawa waliokuwa wakoloni wetu hawajajoa hata senti tano!.

Asante Mfaransa.
 
Nilipoona leo, sio tuu nikafarijika, bali nilihuzunika hawa waliokuwa wakoloni wetu hawajajoa hata senti tano!.

Asante Mfaransa.
Ushawishi wa kwanini watoe hela hizo pengine haujafanyika.
 
yaani wakati mwingine najisikia aibu wakati mwingine najisikia matumaini; ila hiki tunachofanya leo hii mtaona kitakavyolipa huko mbeleni. Siku ambapo watawala watatamani Red Cross ingekuwa na uwezo zaidi!
 
Nilipoona leo, sio tuu nikafarijika, bali nilihuzunika hawa waliokuwa wakoloni wetu hawajajoa hata senti tano!.

Asante Mfaransa.

Sasa Pasco, hao waliokuwa mabwana zetu wako mbioni kuturudishia mabilioni tuliyoiba wakati wa kununua rada. Kwa nini waone huruma ya kutupa 100 mil./= (yaani dola elfu 90)?
 
Nilipoona leo, sio tuu nikafarijika, bali nilihuzunika hawa waliokuwa wakoloni wetu hawajajoa hata senti tano!.

Asante Mfaransa.

Sahihisho UK hawakuwa wakoloni wetu, ndio sababu walijenga sana Kenya ambao ndio walikuwa koloni lao.
 
Sahihisho UK hawakuwa wakoloni wetu, ndio sababu walijenga sana Kenya ambao ndio walikuwa koloni lao.

Kwa Kiswahili Waingereza walikuwa wakoloni wetu. I know that we were a protectorate, but that is in English.

Tunapoimba tulimng'oa mkoloni wewe unadhani tunakosea?
 
Kwa Kiswahili Waingereza walikuwa wakoloni wetu. I know that we were a protectorate, but that is in English.

Tunapoimba tulimng'oa mkoloni wewe unadhani tunakosea?

Ndio mnakosea kwa sababu mkoloni alikuwa mjerumani pengine mnapoimba mnachanganya wote.
 
Wachai,

Tunapoimba "tumewang'oa wakoloni" hatuwezi kuwa na maana ya kuwang'oa Wajerumani. Hatukuwang'oa Wajerumani; waling'olewa na Waingereza. Na sisi tukawang'oa hao wang'oaji.

Labda utupe 'definition" yako ya neno MKOLONI. Si lazima neno mkoloni litokane na neno COLONY. Narudia kusema kwamba kwa Kiswahili, colony, protectorate zote ni UKOLONI tu. Mngereza alikuwa mkoloni wetu. Hata yeye anajua hivyo.
 
Kudos to France....
 
Maoni Yangu:
Kuchangia Red Cross ya Tanzania ndiyo njia ya uhakika zaidi ya kujiandaa kwa maafa kwa kujiandaa na majanga. Nawashukuru Ufaransa kwa kuona kile ambacho tulikiona wengine mapema zaidi. Inasikitisha hata hivyo bado taasisi zetu za ndani hazijaona umuhimu wa kuitikia wito huu. Nina uhakika wanasubiri janga litokee ndio waanze kuchangia tena.

Msaada wa Sh100 milioni Tunasema Asante kwa Ndugu zetu Wafaransa lakini je Serikali yetu imefanya nini kwa hao Ndugu zetu waliopata mafuriko wilayani Kilosa? Au Serikali haikufanya kitu inategemea misaada toka kwa wafadhili? hilo ndilo Swali kubwa ninalo uliza kwa ndugu zangu wana JF Mnasemaje?
 
Back
Top Bottom