Ufahamu na upeo wa baadhi ya wabunge na viongozi Chadema na ubabaishaji wa kisiasa

Ritz kuna wabunge au watu wamekatazwa kufika kwenye M4C?kwasababu ya wanakotoka?This is New to me?4 the benefit ya wanabodi unaweza kutuwekea hilo katazo hapa?na lilitolewa na nani na likiwa na lengo gani?failure tutajiridhisha kuwa upo kazini unatumika

Mbona lipo wazi mkuu bahati mbaya una uwezo wa kuhoji chochote ndani ya chama chako ukihoji unafukuzwa...hii dhana mtu akiwajibu kwa hoja mnakimbilia yupo kazini.
 
Acha uzushi chumvi ikizidi mno huharibu. Hivi wapi Lema alisema ataamuru Watu watupe simu chooni kwani wote tulikuwa tunafuatilia tukio hilo.

Sijui kwa nini ukiwa mfuasi wa Chadema unakuwa na upofu, kama huyu anakataa kabisa kama Lema akusema kuwa nitaamuru wananchi watupe line zao chooni.
 
Hao wameishiwa kisiasa, hawaana mwaanzo hawana nyuma, siasa zao majitaka watu wameshawashtukia hazina faida.

Wachumia tumbo tu hao hawana moja la faida kwa wananchi. Wanawachangisha wananchi kwa kutembeza kopo kwenye mikutano yao hallafu katibu mkuu anazikopa kujengea nyumba na kununulia fanicha za josephine. Source TUNTEMEKE

Zomba hilo lakuishiwa kama siyo kufilisika kisiasa,hoja na kifirsa ni jinamizi lilalolisumbua CCM na serikali yake hilo aliitaji degree kuligundua.wale mliokuwa mnajivunia kuwa ni wenu kwakuwa walikuwa hawajui wala awambiwi ukweli kuhusu maovu na udhaifu wenu sasa wamejua na wanendelea kujuzwa zaidi.mkienda sasaivi mpo watupu wanawajua ndani nje hakuna chakuwadanganya kazi mliyobakiwa nayo ni kukanusha na kujichekesha tu huku wananchi wakiwashangaa mlikuwa wapi siku zote.mnazidi kujiaribia pale mnapotumia vyombo vya dola kukandamiza haki zao za kuambiwa ukweli na kufumbuliwa macho juu ya yale wanayofanyiwa kinyume na matarajio yao.
Pilipili ipo mikononi mwako endelea kupakaza maeneo mengine
 
Last edited by a moderator:
Siwezi hata siku moja kukaa na kuanza kubishana na mtu mchache na kilaza Kama Ritz. Amefeli kila sehemu, kilichomfikisha hapo ni kubebwabebwa tu na ufisadi wa kutisha chini ya kivuli cha babake. Sijawahi hata siku moja kusoma point yoyote ya maana humu jf kutoka kwa huyo mtu. Anamasters ya kuungaunga tena kwa kubebwabebwa lakini bado anaupeo mdogo kuliko mtoto Wa form mtu.

Hata mbingu na ardhi zikutane kamwe hutoweza kujilinganisha na Mnyika kwa namna yoyote ile. Wewe na Mnyika kiupeo na kama mbingu na ardhi. Mpaka sasa sijampata mbunge yeyote mwenye uwezo Wa hali ya juu kwa upande Wa ccm kumlinganisha kwa namna yoyote ile na TL.

Ila mwisho wenu unakuja very soon, hapo mtakapokimbia hii nchi na ufisadi wenu Wa kutisha Kufanya nchi yetu Kama kitega uchumi cha familia yenu. ZOMBA hata sihangaiki naye kwani yeye ni mchumia tumbo na muendekeza njaa aliyekubali kuwa mtumwa Wa fikra na kuificha makalioni hiyo elimu aloipata huko ulaya mashariki. Shame on him.

Mkuu mie sipo JF kwa ajili ya kubishana nipo JF kutoa elimu ya uraia.
 
Hao wameishiwa kisiasa, hawaana mwaanzo hawana nyuma, siasa zao majitaka watu wameshawashtukia hazina faida.

Wachumia tumbo tu hao hawana moja la faida kwa wananchi. Wanawachangisha wananchi kwa kutembeza kopo kwenye mikutano yao hallafu katibu mkuu anazikopa kujengea nyumba na kununulia fanicha za josephine. Source TUNTEMEKE

Zomba hilo lakuishiwa kama siyo kufilisika kisiasa,hoja na kifirsa ni jinamizi lilalolisumbua CCM na serikali yake hilo aliitaji degree kuligundua.wale mliokuwa mnajivunia kuwa ni wenu kwakuwa walikuwa hawajui wala awambiwi ukweli kuhusu maovu na udhaifu wenu sasa wamejua na wanendelea kujuzwa zaidi.mkienda sasaivi mpo watupu wanawajua ndani nje hakuna chakuwadanganya kazi mliyobakiwa nayo ni kukanusha na kujichekesha tu huku wananchi wakiwashangaa mlikuwa wapi siku zote.mnazidi kujiaribia pale mnapotumia vyombo vya dola kukandamiza haki zao za kuambiwa ukweli na kufumbuliwa macho juu ya yale wanayofanyiwa kinyume na matarajio yao.
Pilipili ipo mikononi mwako endelea kupakaza maeneo mengine
 
Last edited by a moderator:
Acha uzushi chumvi ikizidi mno huharibu. Hivi wapi Lema alisema ataamuru Watu watupe simu chooni kwani wote tulikuwa tunafuatilia tukio hilo.

Sijui kwa nini ukiwa mfuasi wa Chadema unakuwa na upofu, kama huyu anakataa kabisa kama Lema akusema kuwa nitaamuru wananchi watupe line zao chooni.

Mkuu,

Kwa mtu kama Lema kutoa kauli kama hiyo sio kitu cha kushangaza. Inaonyesha hayo ndio maadili yake. Matusi,uzushi na uongo alioeneza wakati wa kampeni ya Ubunge kule Arusha dhidi ya Dr.Batilda ilitosha kwa jamii kumuona kuwa ni mtu asiyehitajika na asiyefaa kwenye uongozi hata wa kata. So CDM wanapoendelea kumtukuza mtu aliyekosa nidhamu na adabu kiasi hicho inatoa picha kuwa itikadi ya CDM sio amani na uadilifu. Bado Watanzania tunajigamba na kujidanganya eti "mtanzania wa siku hizi ameelimika,haogopi,anataka mabadiliko...". Mi napinga na naendelea kuamini kuwa bado watu wako kwenye ujinga wa hali ya juu,vinginevyo watu kama akina Lema walitakiwa wasisikilizwe na wapuuzwe kwa kila wasemalo. Jiulize kitu kimoja,watu wa Arusha mjini sasa hivi wanafaidika nini,kukaa miaka takriban mitatu bila mbunge kwa sababu ya Lema? Iliwashinda nini kuona kuwa matusi sio hoja na wakachagua mbunge mwingine!

Hao wengine akina Mnyika kuna mengi ya kuongea,lakini kwa ushauri wa bure,Mnyika angerudi shule kwenda kusoma,apate angalau degree moja apate exposure. Siasa za majukwaani za kujitafitia umaarufu,michango yake bungeni isiyo na mashiko,zinampoteza. Shule ni muhimu. Vyeo bila qualification havimjengi zaidi ya umaarufu wa mtaani.

Tundu Lissu,siasa za uchochezi ndio itikadi yake. Na mara nyingi,fuatilia,ukiona mwanasiasa ambaye akiongea lazima aongee kwa jazba,kunyanyua mikono na mabega kama anataka kupaa,kukunja sura,ogopa sana watu hawa,huwa ni waongo na wachochezi mfano wake hakuna.
 
Mbona lipo wazi mkuu bahati mbaya una uwezo wa kuhoji chochote ndani ya chama chako ukihoji unafukuzwa...hii dhana mtu akiwajibu kwa hoja mnakimbilia yupo kazini.

Ritz lete facts zenye evidence hapa tujadili siyo maneno ya kwenye vijiwe vya gahawa.hilo katazo lilitolewa na nani,wapi na lilikuwa linamlenga nani? Nani aliyefukuzwa kwa kuhoji ukweli?au umechanganya na CUF na NCCR?
 
tatizo ukipenda chongo utaita kengeza basi hili ndio tatizo la wanachama wa CHADEMA hata kama mbunge wao muelewa ni mdogo watamwagia sifa tele lkn ninachojua chadema wakiikamata nchi mwaka 2015 lazima nchi ibinuke jirekibisheni wana CHADEMA la sivyo .........
 
Mkuu,

Kwa mtu kama Lema kutoa kauli kama hiyo sio kitu cha kushangaza. Inaonyesha hayo ndio maadili yake. Matusi,uzushi na uongo alioeneza wakati wa kampeni ya Ubunge kule Arusha dhidi ya Dr.Batilda ilitosha kwa jamii kumuona kuwa ni mtu asiyehitajika na asiyefaa kwenye uongozi hata wa kata. So CDM wanapoendelea kumtukuza mtu aliyekosa nidhamu na adabu kiasi hicho inatoa picha kuwa itikadi ya CDM sio amani na uadilifu. Bado Watanzania tunajigamba na kujidanganya eti "mtanzania wa siku hizi ameelimika,haogopi,anataka mabadiliko...". Mi napinga na naendelea kuamini kuwa bado watu wako kwenye ujinga wa hali ya juu,vinginevyo watu kama akina Lema walitakiwa wasisikilizwe na wapuuzwe kwa kila wasemalo. Jiulize kitu kimoja,watu wa Arusha mjini sasa hivi wanafaidika nini,kukaa miaka takriban mitatu bila mbunge kwa sababu ya Lema? Iliwashinda nini kuona kuwa matusi sio hoja na wakachagua mbunge mwingine!

Hao wengine akina Mnyika kuna mengi ya kuongea,lakini kwa ushauri wa bure,Mnyika angerudi shule kwenda kusoma,apate angalau degree moja apate exposure. Siasa za majukwaani za kujitafitia umaarufu,michango yake bungeni isiyo na mashiko,zinampoteza. Shule ni muhimu. Vyeo bila qualification havimjengi zaidi ya umaarufu wa mtaani.

Tundu Lissu,siasa za uchochezi ndio itikadi yake. Na mara nyingi,fuatilia,ukiona mwanasiasa ambaye akiongea lazima aongee kwa jazba,kunyanyua mikono na mabega kama anataka kupaa,kukunja sura,ogopa sana watu hawa,huwa ni waongo na wachochezi mfano wake hakuna.

Uchambuzi wako juu ya Lema,Mnyika na Lissu unaonyesha ni jinsi gani wanavyowakosesha amani au walivyorushia mchanga kama siyo kuhatarisha vitumbua vyenu.kila mtu ana mapungufu yake ila haya wewe unayoyatoa ni majungu na si mapungufu.Kuhusu Mnyika kurudi chuo kwenda kupata degree sioni kama linamantinki elimu aliyonayo mnyika kama siyo degree na anaweza kuchambua hoja na kutoa michango yenye tija kwa wanyonge walio wengi japo inawaudhi wachache kama wewe uwezi kumlinganisha na Maprofesa wa chama chako Kapuya,Msolwa,Magembe,na wengine wengi.
Uwezo na michango ya lissu uwezi kuifananisha na werema hata kidogo na hilo limejidhiirisha mara nyingi sitaki kurudia kwenye mjadala wa katiba mpya na alifanya nini.
Wakati mwingine unaweza usimpende mtu lakini ukapenda mambo yake.
bahati mbaya sana wanaowachukua kina mnyika na lissu ni wale ambao wanaumizwa na michango yao ambao hata hivyo aikutarajiwa wawapende.wanaowapenda na kuwaunga mkono ni wengi ndiyo maana wapo hapo walipo pamoja na wewe kuwachukia
 
Lema kuropoka na kuongea maneno ya hovyo hovyo ndiko kulikomgharimu na kupoteza ubunge, wanaomtetea kwa ujinga wake ni wenye kuamini mkubwa hajambi.
 
tatizo ukipenda chongo utaita kengeza basi hili ndio tatizo la wanachama wa CHADEMA hata kama mbunge wao muelewa ni mdogo watamwagia sifa tele lkn ninachojua chadema wakiikamata nchi mwaka 2015 lazima nchi ibinuke jirekibisheni wana CHADEMA la sivyo .........

Kisavuli tunashukuru kama moyoni umeshagundua kuwa mwisho wenu ni 2015.hata zambia walikuwa na mawazo mgando kama yako kuwa Satta akichukua nchi itabinuka.Mnachojidanganya kuwa kwasababu CCM ndiyo inaongoza dola basi wanaojua wote wapo kwao chakushangaza pamoja na wao kuwa jack of all trade.Why are we stil poor for the past 50yrs?
 
Wanabodi.

Baadhi ya wabunge wa Chadema pamoja na viongozi wao wameonyesha ubabaishaji mkubwa kwenye maswala ya siasa.

John Myinka, aachane na siasa za vijiweni na zile za kwenye mitandao ya kijamii zinazomtukuza na kumuona shujaa akavimba kichwa, nchi yetu ina watu wenye upeo mkubwa wa maswala mbalimbali na kukaa kwao kimya anaporopoka, ni kwamba wanampuuza Mnyika amekuwa mtu wa kuropoka tu.

Tundu Lissu, huyu mwanasheria aliingia katika siasa akitokea kwenye NGO moja wa Wanasheria wa Mazingira, Lissu alidai ana mkanda wa video ambao unaonyesha wachimbaji wadogo wakifukiwa huko Bulyankulu alidandia hoja ya Augustine Lyatonga Mrema, kufanya mropanganda hiyo ambayo aliamini kuitumia kujipatia umaarufu kisiasa zaidi kuliko fani yake, leo hii ukumuuliza vipi ule mkanda video hana tena na ameishasahau.

Godbless Lema, sihitaji kuyasema sana kuyasema mambo yake nadhani wote mnafahamu na siasa zake za kusukumwa na jazba, jana nimebahatika kumuona kwenye Star Tv katika kuchangia Chadema, kauli ya Lema anayashambulia makampuni ya simu ambayo ni wawekezaji, Lema kwa akili yake anadhani hizo kamapuni ni wapinzani wa Chadema, Lema anaongea kwa jazba bila ushahidi wala ufahamu wa maswala ya mawasiliano, Lema anatoa amri mbele ya TV nyie makampani ya simu tafadhali nawaamuru wachieni line watu wachangie la sivyo kesho asubuhi nitaamuru wananchi wote watupe line zenu chooni, sababu Chadema ni chama cha wananchi.

Sometimes common sense must prevail na upumbavu ufichwe .Jaribu ku save space maana huu ***** wa nini sasa na una faida gani kuuleta hapa ?
 
Tundu Lissu naye ni kituko cha aina yake kama unafuatilia vikao vya bunge, kila anaposimama kuchangia kutokana na na kujiaminisha kuwa anajua kila kitu mara nyingi amekuwa akijikuta akiwa kichekesho, mbunge huyu ana hulka ile ile kama Mnyika, ambao wakisimama bungeni hudhania wanachosema au kuchangia ni kipya na wa6 kujiona visima vya mawazo mapya, ndio maana haishangazi kupewa taarifa na wenzao na wengine kuomba mwongozo spika.
Katika huu mwezi mtukufu wewe umefungaje? maana nilifikiri utaacha unafiki kwa mwezi huu,muda mrefu wewe umekuwa jaji mnafiki wa viongozi wa chadema na kuacha wa kwenu,nilidhani utapumzika katika kipindi hiki kitakatifu kumbe umepumzika kula kitimoto tu mambo mengine yapo paleplale. Vipi hujaongozana na mzee kumsindikiza Atta.
 
Lema, baada ya kuyafokea makampuni ya simu, akatoa kituko kingine akasema nikipata Chopa mbili CCM hawafiki siku ya Chrismas.
 
Mkuu,

Kwa mtu kama Lema kutoa kauli kama hiyo sio kitu cha kushangaza. Inaonyesha hayo ndio maadili yake. Matusi,uzushi na uongo alioeneza wakati wa kampeni ya Ubunge kule Arusha dhidi ya Dr.Batilda ilitosha kwa jamii kumuona kuwa ni mtu asiyehitajika na asiyefaa kwenye uongozi hata wa kata. So CDM wanapoendelea kumtukuza mtu aliyekosa nidhamu na adabu kiasi hicho inatoa picha kuwa itikadi ya CDM sio amani na uadilifu. Bado Watanzania tunajigamba na kujidanganya eti "mtanzania wa siku hizi ameelimika,haogopi,anataka mabadiliko...". Mi napinga na naendelea kuamini kuwa bado watu wako kwenye ujinga wa hali ya juu,vinginevyo watu kama akina Lema walitakiwa wasisikilizwe na wapuuzwe kwa kila wasemalo. Jiulize kitu kimoja,watu wa Arusha mjini sasa hivi wanafaidika nini,kukaa miaka takriban mitatu bila mbunge kwa sababu ya Lema? Iliwashinda nini kuona kuwa matusi sio hoja na wakachagua mbunge mwingine!

Hao wengine akina Mnyika kuna mengi ya kuongea,lakini kwa ushauri wa bure,Mnyika angerudi shule kwenda kusoma,apate angalau degree moja apate exposure. Siasa za majukwaani za kujitafitia umaarufu,michango yake bungeni isiyo na mashiko,zinampoteza. Shule ni muhimu. Vyeo bila qualification havimjengi zaidi ya umaarufu wa mtaani.

Tundu Lissu,siasa za uchochezi ndio itikadi yake. Na mara nyingi,fuatilia,ukiona mwanasiasa ambaye akiongea lazima aongee kwa jazba,kunyanyua mikono na mabega kama anataka kupaa,kukunja sura,ogopa sana watu hawa,huwa ni waongo na wachochezi mfano wake hakuna.

Mkuu wewe kweli MchukiaUonevu, tunashukuru kwa uchambuzi wako murua.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mie sipo JF kwa ajili ya kubishana nipo JF kutoa elimu ya uraia.
Mnafiki tu,elimu gani ya uraia unayotoa,wewe husitahili kutoa elimu tu,tulitegemea utachangia kwa mali wale watoto wa mtaani,wajane,wagonjwa nk, hatujakosa elimu ya uraia kiasi cha kuhitaji kutoka kwako.
Asubuhi njema.

Aaaah samahani nilitaka kusahau kukuuliza kuhusu kesi ya Lulu itatajwa lini tena,na kati ya mawakili wote wanaomtetea,hakuna aliyejitoa hadi sasa?
 
Nassari nae kijana mdogo ndio kwanza kaingia kwenye siasa juzi naye anaropoka eti nchi ni laini sana kama maini halafu wafuasi wa Chadema kina Sinta, Joketi, na baadhi ya mamiss wanashangilia.
 
Hii ndio hatari ya kujiingiza katika siasa bila kujua unachokitaka kukifanya ndio kunakosababisha udandiaji wa hoja, uzushi, madai yasiyo mashiko, Mnyika amekuwa mbunge wa mwogozo spika hivi kweli Mnyika anajua upungufu wake umelifikisha wapi Jimbo la Ubungo? Ni vyema Mnyika kabla ya kuwahukumu wenzake kwa kutoa kauli za kitoto angejipima kwanza je, amelifikisha wapi Jimbo lake.

ah! Ritz bana! bifu lako na Mnyika halijaisha tu? Sasa unataka tukusaidie vipi? Yaani imefika mahala kila mtu akisoma thread yako anaipuuza, ni mimi tu ndio bado sijakupuuza.
 
Ritz au kwa jina halisi Gabriel Athumani , mambo vipi kaka?

Naona unapromoti makala yako uliyoiandika leo kwenye gazeti la mzalendo na unachofanya ni kucopy na kupaste vipande vipande vya makala yako yenye kichwa cha habari "Sinema za Mnyika ,Tundu Lissu Bungeni" makala hiyo inamaneno na vifungu vinavyofanana na makala iliyochapishwa leo kwenye gazeti la mzalendo ukurasa wa tano.
 
Gabrile Athumani leo kwenye makala ya mzalendo kaandika nanukuu "kama ilivyo kwa watu makini sina budi kuwapongeza baadhi ya wabunge kutoka upinzani.hawa wameonyesha uwezo mkubwa wa kufanya kazi zao za kibunge kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kanuni za Bunge .......wabunge Freeman Mbowe, mbunge wa Hai (Chadema na kiongozi wa kambi rasmi ya Upinzani Bungeni);Zitto Kabwe ......Joseph Selasini......John Cheyo na Mrema"

kaendelea kuandika kwenye mzalendo ya leo jumapili uk.wa 5 "niseme kidogo kuhusu mbunge mwingine wa chadema , Tundu Lissu wa Singida Mashariki.Lissu kitaaluma ni mwanasheria .Aliingia katika siasa akitokea kwenye NGO moja ya wanasheria alikotokea kufahamika ......" Huyu ndio Gabriel Athuman .Ukija huku JF unakutana na mtu anaitwa Ritz anaandika kama mzalendo.....
 
Back
Top Bottom