Ufahamu na kujiepusha na Jicho baya kwa watoto wadogo!!

displayname

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
1,950
1,039
Karibuni nyote katika mada hii inayokusudia kupata ufafanuzi na ufahamu juu ya JICHO BAYA katika maada hii najaribu tu kuchokoza wajuzi wa mambo kama akina Mshana Jr waje kutufahamisha na wengine;

Hoja ni JICHO ila ntaita jicho baya
kwa ufupi tu ni jicho ambalo mtu humtazama hasa mtoto kwa kumtamani au kumshitukia au kumshangaa aidha kwa uzuri wake, unene na sifa zake nyingie alizojaliwa na Muumba.

Tamaduni zetu zina mambo sana;

TANGA
Muku

Nilikuwa Tanga miaka fulani nikasikia habari ya "Muku" na kupigwa "zongo" hiyo muku ni watu huchanjia ili wawe na nguvu. Kwa jinsi nilivyosikia mtu aliyechanjiwa hiyo muku hapasi kukasirika hovyo ila ukimkasirisha na akikasirika na kuchuka hatua ya kukupiga hata kofi tu basi kuamka kwako kwa hitaji kudra za Muumba. (kwa wanaojua hili mtafafanua zaidi).

Zongo
Kwa mara ya kwanza nasikia neno zongo mkoani Tanga, utasikia wanasema amepigwa zongo hii ni kama uchawi fulani hivi ambao wanyekujua waje kutuelimisha kuufahamu na kujiepuisha nao. Hii inadalili zake pia mara kuuvimba tumbo nk. (Wenyekujua zaidi mtujuze).

ARUSHA
Jicho

Na sasa nimepata habari ya JICHO au macho, hii hali imeshamiri sana mkoani Arusha, kwa ndugu zetu wale wafugaji. Utasikia mtoto huyu anajicho kali sana inabidi akatengenezwe. Katika udadisi wangu mdogo, nimejifunza kwamba jicho au macho huwapata watoto weupe ikiwa ni watu aidha kwakujua au kutokujua wakimtazama mtoto kwa kumtamani, wivu au wakashtuka labda "dah mtoto mzuri huyu".
Hivyo mtoto hupatwa na hilo jicho na kuanza msumbua homa za mara kwa mara, kulia lia bila sababu na kadha wa kadha. Wanasema mtu akimshtukia mtoto basi ni sharti awahi kumshika sikio au kutema mate chini ili ule ubaya wa jicho lake la mshtuko limwepuke mtoto au mtu.

JICHO BAYA LIMPATAVYO MTOTO
Mtu aakimwona mtoto na kumshangaa aidha kwa uzuri wake au weupe wake basi au kwa kumtamani au wivu tu basi ubaya wa hayo macho humpata mtoto na kuanza mkusumbua.

DALILI ZA JICHO KWA MTOTO
Kwa na joto kali na katika vipimo hakuna ugonjwa, kushindwa kula, kukosa furaha, kulia na kuhangaika hasa nyakati za usiku, kutapika nk.

TIBA YA JICHO
Zipo njia kadhaa nimebaini ambazo hutumika kuwatibu au kupoza jicho kwa watoto, njia moja wapi ni maji, chumvi na magadi hapo kama umetoka tembea kwa mkusanyiko wa watu wengi na mtoto basi unapaswa kumwogesha mtoto na maji yenye chumvi na magadi. Husaidia kutoa jicho au kutuliza kama jicho kali.

Ila, kwa namna ya kutengeneza jicho hapo sasa wanasema ukisha mtengeneza mtoto wako wa kwanza basi sharti uwatengenezo wote hadi utakao wazaa hapo baadae (sijajua mahusiani yako hapo).'

Maombi, hii pia ukimwomba Mungu uponyaji wapatikana wa watoto au mtoto mwenye jicho baya.

KINGA YA JICHO
Hapa namna ya kumkinga na jicho huwa wanatumia mkaa au kumpaka mtoto usoni kama kwenye nyusi kama wanja vili hii wakiamini kwamba jicho baya humezwa na weusi kwa maana ya mkaa au kitu chochote cheusi (ndio maana pana baadhi ya wazazi huwafunga watoto hirizi wengine vitambaa vyeusi shingoni, kiunoni au mkononi ili machao ya watu wabaya badala ya kumshangaa mtoto yaishie kushangaa hirizi au kitambaa kwa mtoto).

Hii ndio maana utakuwa watoto wadogo huwa wanapakwa wanjaa au mkaa usoni ili wata wakimtazama wabakia kushaa ule wanja au mkaa nakuacha kumshanga mtoto hapo unakuwa umemlinda mtoto na hatari ya hayo macho ya watu.

Njia nyingi ni kukwepesha mtoto na macho ya watu, kwa mkufungia ndani tu au ikibidi kutembea nae nje basi utakuta mtu anamfunika mtoto gubigubi ili tu asionekane.
Kumwekea mtoto mkaa atembee nao.

Maji ya baraka na Maombi.

Kisa cha kujifunza
kuna mtu mmoja kila alipokuwa akija nyumbani kwangu na kuwaona mtoto wangu basi siku hiyo hakuna kulala mtoto analia tu, ila baada ya kugundua hivyo nikawa namwepusha mtoto na huyu mtu. Japo nilikuja kumwambia, ila wanasema pana watu wengine wanafahamu kuwa wana hayo macho mabaya na wengine hawafahamu.

MADHARA YA JICHO BAYA
Kuumwa, kukosa afya na husababisha kifo,

MJADAWA UPO WAZI KUJADILIWA
Binafsi na hitaji kujua zaidi haya mambo, je jicho ni uchawi? na mambo mengine kuhusu macho au jicho hasa kwa watoto nk.
Karibuni..
masai dada Mshana Jr Masai Kaskazini Masai Ladislaus Masai Msukuma Original na wengine wote wenyekujua haya mambo!!!

Marejeo
https://descubrir.online/sw/aprende-la-poderosa-oracion-contra-el-mal-de-ojo/
Tamaa kutoka jicho baya
Jinsi ya kujiondoa jicho baya?
 
Mkuu ulichokisema ni kweli tupu ntapata ku share story moja ilitokea maeneo ya uchagani huko miaka ya 80's

Aliishi bwana mmoja naye alikua na hicho unachoita macho basi huyo bwana akija kuangalia mtoto mchanga lazma huyo mtoto atafariki au akiangalia ndizi changa kabisa lazima itanyauka au kuvunjika

Mtoto wake wa kwanza na wapili walifariki mda mchache tu baada ya yeye kuja kuwaangalia na hapo ndio wazee wa mila wakagundua kua huyu jamaa ana hicho kitu ulichoita macho

Bas bhana mtoto wake wa tatu alipozaliwa kabla hawajamwonyesha mtoto halisi walichukua lile uwa la mgomba (lile linaning'inia kwenye ndizi) na kulifunga na baby show ikawa mithili ya katoto ka changa kamefunikwa bas wakamkabidhi jamaa kua huyu ndio mtoto wako jamaa kweli akampokea kumfunua ndio akakutana na lile uwa la mgomba kisha baada ya hapo ndipo wakamleta mtoto halisi na hiyo ndio ikawa pona ya kile kichanga ikafanyika hivyo kwa mtoto wa nne na wa tano pia.

Watu wenye macho ya aina hiyo hua wana uwezo wa kuathiri hata vyakula na vinywaji mfano pombe za kienyeji ndio maana kwa kule uchagani mtu akiwa ameanika chakula mfano ulezi,unga,nk kuna jani la mti fulani unaitwa mfifina hua wanaliweka juu yake inaaminika kua hilo jani lina uwezo wa ku deal na nguvu hasi kutoka kwenye macho ya watu

Pia wanapobeba vyakula mfano ndizi ,mihogo nk huliweka hilo jani kwa juu yake ili ku absolve negative energies kutoka kwenye macho ya watu na pia hata kutoka kwa washirikina hii pia kwa case ya pombe za kienyeji hasa mbege na dadii hilo jani linawekwa kwa mantiki hiyohiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
shukrani kwwa ufafaunuzi na kushare nguvu hasi ya macho...
 
ni kweli usemacho

mimi sikua najua hayo mambo ya macho ya husda nilipojifungua mtoto wangu mama alinambia nichukue mvuje niufunge kwenye kitambaa cheusi nimfunge nao mkononi

nilikua napingana naye sana tu nikimwambia mama tumuamini Mungu tu anatosha mama akanijibu ye kashatangulia kuliona jua kabla yangu nisiwe mbishi

honestly, nilikua namfunga ili mama asione nampuuza siku ambayo narudi kwangu ile kamba niliifungua nikaiweka kabatini katika kutembelea ndugu na majirani ile narudi kwangu jioni mtoto kila anyonya anatapika na kilio kama chote hatukulala ile siku ilibidi nimwamshe mama mtu mzima nimweleze akanijibu kama hivo nimpake wanja na kidoti juu ya paji la uso halaf niyaoshe maziwa yangu kwa jivu na magadi na nimfunge mvuje mkononi la mwisho nichane kitambaa ambacho nilikua natumia nikiwa kwenye ada yangu nimfunge nacho nikaona hi mizigo mwanangu yote ya nn akanambia nimfunge kiunoni ili isionekane nikafanya hivo na alinambia inasaidia husda au jicho baya au ile kumakiwa haimpat mtoto

kumakiwa n kule mtu humshangaa mtoto like khaaa kadogoo, au mtoto mweusi huyoo au mtoto mweupe kama mzunguu
 
Back
Top Bottom