Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,222
- 10,730
Habari za jioni wapendwa naomba kuleta uzi huu kwa ajili ya kupeana maarifa kidogo yaliyopo katika jamii yetu. Karibuni.
Kama ni mfuatiliaji wa makala ninazozileta humu ndani basi ulishawahi kuona uzi wangu kuhusu ishu ya ubao unaoitwa Ouija Board. Nilieleza asili yake kinangananga pamoja na namna ya kuweza kucheza pia niliweka tahadhari kwani ubao huu unafungua milango yako ya fahamu kuweza kuruhusu shambulio lolote la kichawi au miujiza. Wakati naandika uzi huu sikuwa najua kama fikra za Ouija zinaeleweka baina ya wanajamii wa kitanzania na africa kwa ujumla. Shukrani kwa mchangiaji mmoja aliyenipa ushauri kuwa tusilete ufahamu kuu ya ubao huu maana ni kati ya vitu hatari sana mtu kutumia.
Lakini cha ajabu jana nilikutana na mtu akiwa na Ouija Board zaidi ya tatu akidai kuwa anaziuza kwa watu, kwa yeye mwenyewe amempiga (kuziona) kwa mtalii wa Kiitaliano. Yalikuwa ni maeneo ya Riverside kwa wanaoishi maeneo ya Dar es Salaam wanaweza kupafahamu. Nilimuuliza kuwa anajua taratibu zozote katika kuendesha zoezi la mawasiliano kati ya mtumiaji na pepo hilo. Akanijibu majibu ambayo yaliniweka katika wakati mgumu na kubaki kusema huyu jamaa anataka kuleta majanga ndani ya jamii ya Tanzania tu.
Kiukweli Nimeshangaa sana kuona ishu kama hizi zimefika Tanzania wakuu.
Nilihaidi kuwa nikikutana naye tena nampeleka polisi maana hajui maelezo muhimu wakati wa kutumia.
Nawasilisha uzi.
Sent using Jamii Forums mobile app