Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 22,172
- 58,270
Huu ni bao unaoitwa Ouija, ni ubao uliochorwa herufi zilizochanganyikana na namba 0-9, kuna neno yes, hello na goodbye, unaitwa ubao unaoongea. Mtumiaji ataweka mikono yake hapo kisha kutamka neno Ouija, hapo tayari anakuwa ameunganishwa kufanya mawasiliano na roho za kuzimu.
Sayansi pamoja na dini zilipiga vita kuzuia matumizi ya vibao hivi vya kichawi zikisema kuwa badala ya kuwasiliana na wafu, roho za kishetani humuingia muwasilianaji na kuleta shida ya mwili wake kumilikiwa na roho wachafu kama ilivyowatokea wengi.
Inaelezwa kuwa uchawi huu wa vibao ulianza muda mrefu sana tangu miaka ya 1100 AD mpaka vikaja kupigwa vita visiwepo katika karne ya 19 baada ya kupotea na kuibuka upya. Kuna filamu nyingi zimefanywa kwa kuuzingatia uchawi huu wa ubao wa Ouija, mfano wa filamu hizo ni What Lies Beneath (2000).
Filamu nyingine ni ya I am Zozo ya mwaka 2012 , na Ouija ya mwaka 2014. Vibao hivi havipo tena miaka ya leo.