Ufafanuzi tafadhali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufafanuzi tafadhali

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Gurta, Apr 20, 2011.

 1. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  1. Simu yangu imeibiwa
  2. Nimeibiwa simu yangu.
  3. Simu yangu imeibwa.
   
 2. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,136
  Likes Received: 3,328
  Trophy Points: 280
  1 & 2 yote majibu.
   
 3. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,963
  Likes Received: 23,843
  Trophy Points: 280
  Namba mbili....Bingo!
   
 4. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  1 na 3 yana maana moja.
   
 5. msadapadasi

  msadapadasi JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 504
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Sentensi zote tatu zina maana inayo lingana kimaana katika hali ya mazoea, na utofauti wake upo katika maumbo (mofolojia) au mpangilio wa maneno pekee, hata hivyo sentensi namba 1, ina utata kwa msomaji au msikilizaji kwa maana kwamba inaweza maanisha simu ilikuwa na kitu fulani inachokimiliki, ie. yaweza kuwa ni programau au vyovyote na imeibiwa (imetolewa) kutoka katika simu hiyo. Hivyo simu ndiyo iliyoingia hasara kwa kuibiwa kifaa au programu yake iliyokuwa ikimiliki. Hivyo basi, kwa mtazamo wangu sentensi hii hutumika kimazoea zaidi na si kwa kuzingatia utaalamu na mintalafu ya lugha, hususani lugha ya kiswahili.
  Hivyo kwa maelezo hayo ni dhahiri kuwa sentensi #2 n#3 ndizo tungo sahihi zaidi kuelezea tukio la wewe kuibiwa simu yako, na hiyo #1, hutumika katika hali ya mazoea ya kutumia lugha, na inamakosa kimantiki na kisarufi.
  MAOMBA KUWASILISHA....
   
 6. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  # 1 wakati uliopita lakini si jana wala juzi "kama dakika 5-10"
  #2 tukio limetokea sasa hivi
  #3 tukio limitokea jana ama zaidi ya jana

  P.S ni maoni yangu ......
   
 7. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  big up! excellent! bravo! n many mo .....100%
   
 8. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2011
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,642
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  uko sawa sawia...ulichonena hapa ni sahihi sina cha kuongezea
   
 9. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #9
  Apr 25, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  #1. Kuna kitu kilicho ibwa toka kwenye simu. Labda imeibiwa line au memory card ama credit! Hebu badili neno "Simu" kuwa "kaka, dada, mjomba, mpangaji, mtoto nk kisha weka "a" kwenye "i" ya kitenzi 'imeibiwa'
  #2 & 3 Ina maana wewe ndo ulio ibiwa simu.
   
Loading...