Ufafanuzi: Mimi Deo Kisandu ni Mnyamwezi(Msukuma) sio Msambaa

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,334
baba.jpg
mama.jpg

NB; Picha hizo mbili ni za wazazi wangu, Baba na Mama za nyuma kidogo.

Mimi Deo Kisandu, Nimekumbana na Maswali mengi juu ya kabila langu wengine wanasema Mimi Msambaa kwa kuwa niligombea ubunge jimbo LA Lushoto, Tanga mwaka 2010. Wengine wana dai Mimi Mchaga kwa kuwa nilikuwa CHADEMA.

UTHIBITISHO.

Mwaka 2009 nili dahiriwa kujiunga na Chuo Kikuu cha KKKT (Sekuco/Sekomu) cha Lushoto, nikitokea Mwamala Sekondari Nzega, Tabora, na nilipokuwa Chuo nilihamasisha mambo mengi sana maana tayari nilikuwa kwenye Harakati kwa miaka mingi. Niliweza pia kushosolaizi na wananchi na kuwa nao karibu na hivyo Viongozi wa CHADEMA wakati huo Mzee Zuberi(Mwenyeketi) na Abdalah Dhahabu(Katibu) waliniomba nigombee Ubunge jimbo LA Lushoto baada ya kuanzisha CHASO chuoni(CHADEMA Students Organization) na niliwakubalia.

Hata hivyo kuna eneo kipindi cha kampeni walinikataa wakitaka mgombea awe Msambaa mwenzao, nilijitahidi kutumia Katiba ya Nchi kuzima kelele hizo. Kuna mahali ilifika wananchi hawakutaka hata kutupokea hivyo viongozi wakapendekeza kuunda propaganda ambayo itatupa ushindi hivyo nilipopanda jukwaani, mwananchi mmoja aliuliza swali wewe ni kabila gani? Watu wote walicheka maana walijua fika Mimi ni Msukuma kutoka Shinyanga, hivyo nililazimika kupotosha ili tusipoteze kula nikasema "Mimi ni Msukuma lakini mama yangu ni Msambaa" watu walikaa kimya na kunung'una wakijua nimewazima maswali yao waliyoagizwa na propaganda wa CCM. Naomba kuthibitisha kuwa Mimi Wazazi wangu wote ni Wasukuma/Wanyamwezi na ni wakazi wilayani Kahama, mkoani Shinyanga. Mama yangu akiwa ni mtumishi wa Umma wa muda mrefu Hospitali ya wilaya ya Kahama(Nurse/storekeeper). Bi.Laurencia Maziku na baba yangu DJ wa miaka mingi Mr.Nalimi Kisandu.

Kuhusu kuwa Mchaga, Mzee wangu aliwahi kufanya kazi Arusha Mjini kama DJ kwa muda mrefu sana katika ujana wake. Na kitendo cha kujiunga CHADEMA watu wakazani Mimi ni Mchaga.

Unajua Nchi ni kubwa na hivyo tunatembea maeneo mengi na kujuana na watu wengi. Naomba kuwasilisha.

Sasa watu wanauliza kama ni Msukuma mbona Magufuli hakutaki hata kukusikia, ujue Siasa haina kabila na Mimi siwezi kuwa zezeta wakupelekeshwa kisa kabila. Naishi kulingana na maisha niliyo pitia.



Deogratius Nalimi Kisandu
30 Desemba 2017.
 
Mkuu Deo asante sana kwa taarifa. Mimi mwenyewe ni mtu wa Kahama ila kuna jamaa miaka ya nyuma alikuwa anafanya biashara ya kukoboa mpunga na kuuza mchele anaitwa PAULO KISANDU ni ndugu yako?
 
JF members we are dont like to read your personal post!

Kwa kuwa ukiposti, ili mtu aisome au kuiacha lazima asome walau title! nayo vile vile inachefua!
Embu badili mindset yako!

Sisi humu Jf hatukuamini sana juu afya yako ya akili kutokana na haya maudhui unayopost, na si kinyume cha sheria kwetu kuwa na mashaka na afya yako, ndo maana nimepata ujasiri kukwambia!!

Jaribu kujitadhimini upya!!
 
Back
Top Bottom