dudus
JF-Expert Member
- Feb 28, 2011
- 24,960
- 57,059
... upepo wa kisulisuli ni upepo uvumao kwa ghafla, nguvu na kasi ukitimua vumbi na kutengeneza mfano wa silinda (cylinder) refu kwenda juu (hadi mita 50 au zaidi). Mara nyingi huvuma majira ya kiangazi kuelekea majira ya mvua. Kwa kawaida, huvuma sehemu za wazi zenye miti michache na vumbi hususan mashambani.Nashukuru ,,ila bado sijaelewa huo upepo ndo wa namna gani!!!!
Makabila mengi Tanzania wana mitazamo tofauti tofauti upepo huu unapoonekana. Kwanza, ni ishara kwamba majira ya mvua yamekaribia. Pili, kiimani utasikia "shetani" kapita, n.k. Kiingenreza hujulikana kama "whirlwind". Rejea picha; unaweza kuona uhusiano kati ya huo upepo na andiko hili: "Ikawa, hapo BWANA alipopenda kumpandisha Eliya mbinguni kwa upepo wa kisulisuli, Eliya alitoka Gilgali pamoja na Elisha."; 2 FAL 2:1