UEFA yaipongeza Tanzania Kukuza Soka la Wanawake

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Shirikisho la Mpira barani Ulaya (UEFA,) limeipongeza Tanzania kupitia Taasisi isiyo ya kiserikali ya Karibu Tanzania Organization (KTO,) kwa jitihada zinafanywa katika kukuza soka la wanawake na wasichana katika ngazi mbalimbali za Elimu kwa kuanzia ngazi ya Elimu Msingi.

Hayo yameeelezwa na mtaalam wa michezo kutoka UEFA , Carine Nkoue aliyetembelea shule za Uhuru, Kibugumo na Gezaulole zilizopo jijini Dar es Salaam.

Kupitia taasisi ya UEFA Foundation For Children ambao ni mahususi kwa kuendeleza soka kwa watoto na vijana ambapo Tanzania kupitia Programu ya Mpira Fursa inayotolewa na KTO kupitia vyuo 54 vya Maendeleo ya Wananchi imekuwa mnufaika pekee wa Ukanda wa Afrika Mashariki.

Nkoue amesema, Tanzania inafanya kazi nzuri kupitia washirika wao wa KTO na amejionea namna mabinti wanavyojenga ujasiri kupitia soka la wanawake na wasichana.

Aidha, amesema UEFA itaendelea kusimamia na kushiriki katika miradi ya namna hiyo kuhakikisha soka hususani kwa watoto wa kike linakuwa zaidi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa KTO ,Maggid Mjengwa amesema kupitia programu ya Mpira Fursa inayotolewa katika vyuo 54 vya Maendeleo ya Wananchi imekuwa na matokeo chanya, kwa miaka minne ya utekelezaji wake umetoa wanawake wacheza soka, makocha wanawake pamoja na viongozi hali inayopelelea kukua kwa mpira wa miguu Tanzania.
 
Back
Top Bottom