Udukuzi mpya umeingia Tanzania

Tzhacker 000

JF-Expert Member
Dec 11, 2017
658
686
Kwa Watanzania wote wanaoutumia simu za mkononi, hii ni kwa ajili yenu na naomba uwe makini uisome habari hii na kuielewa.

Huu ni wizi mpya wa kutumia teknolojia ambao umeingia mjini kwa kitaalamu wanauita “Swim Swap Fraud” na kuna baadhi ya watu katika eneo letu la Afrika Mashariki tayari wameshalizwa.

Jinsi unavyofanya kazi

1

Mtandao kwenye simu yako unapotea ghafla, unaona imeandika “No Signal au Zero Bars” halafu baada ya muda unaona simu inaingia.

2

Hiyo namba iliyokupigia simu unakupa huifahamu na inaweza kuwa ya mtandao wowote Tigo/Airtel/Halotel/TTCL/Vodacom na kadhalika kutegemea unatumia mtandao upi ambao muda huo sasa ndio unakuwa umekumbwa na hiyo shida ya kupotea potea kwa mtandao.

3

Huyo aliyepiga anatakuambia kwamba kuna tatizo la mtandao kwenye simu yako na wewe utakubali kwa sababu kweli kuna tatizo. Atakuelekeza kubonyeza 1 ili tatizo la mtandao kwenye simu yako liweze kutatuliwa.

Akikupa maelekezo hayo usifanye lolote, kata simu.

Kwa sabbat utakapobonyeza 1, mtandao wako utarudi ghafla na kisha kupotea (zero bars) na kwa kitendo hicho simu yako inakuwa imedukuliwa (hacked).

Wizi huu unaongezeaka siku baada ya siku na kama una fedha kwenye akaunti yako ya simu (Tigo Pesa, Airtel Money, etc) basi zote zinatolewa.

Baada ya tukio hilo wewe utaona tu simu yako shida ni kwamba haina network lakini tayari wakati huo line yako ya simu inakuwa swapped na taarifa zote kwenye line yako anakuwa nazo huyo aliyefanya tukio. Tatizo hapa ni kwamba hutapata taarifa zozote za kufanya kwa miamala ya aina yoyote kupitia simu yako kwa hiyo kwa wale wanaotumia USSD na Mobile Banking kuweni makini.

Wizi mwingine ambao umeshamiri sasa ni ule wa mut kukutumia meseji kama “Ile hela tuma kwenye lamba hii”, na wewe badala ya kucheki kwa makini unatuma. Jiridhishe wapi unatuma hela na kwa nini kwa sababu wengi wameshakuwa wahanga na hili si kosa la mitandao ya simu bali watumiaji. Teknolojia inaleta faida kubwa lakini pia inawapa wahalifu nafasi, tuwe makini na matumizi ya simu zetu.
Chanzo ni swahilitimes
 
Jana kuna Dada nilikuwa nachat nae.
nikamwambia ntakutumia hela.
ghafla ikaingia meseji namba mpya.
Hyo meseji Inasema.
Itume kwenye namba hii iyo pesa 0756833929.uwe makini Jina litakuja deus kutumwa.
Machale yakanicheza.nikampigia Yule Dada nikamuuliza una namba ngapi? Mbona kuna namba imeingilia chat yetu.?akasema sijui hiyo namba.
Nikawaza sana.nikasema wafanyakazi wa tigo wanaingilia meseji zetu na wanazisoma.
Alijuaje kama mimi nachat na mtu na ninataka nimtumie HELA?
 
Huu udukuzi unafanyika kwa watu walioko katika eneo moja kwa pigo au kuna kuwa na target (muhusika) anayedukuliwa nikiwa na maana kwamba, Mtu mmoja tu ndio simu yake itapoteza mtandao.?
 
Vipi huu wizi wa kutumia no yako au inayofanana na yako wakati huohuo na wewe unaitumia na hujui mtu mwingine anaitumia kuombea hela kwa watu walio kwenye contact zako maana imemkumba rafiki yangu ikabidi atujulishe

"Jamani wapendwa kwa yeyote atakaepokea message inayohusu kutuma hela kupitia namba yangu msitume mpaka mpate taarifa kutoka kwangu maana me nimepigiwa simu na mtu amenitukana kweli akafoward hyo msg na ukiangalia kweli no ni yangu sasa nawaomba tu maana utapeli huu umeingia na sijui huyo aliyetuma na hyo namba yake haipatikani."
 
Kna watu mnabisha Kuhusu utapeli Mnasema Mpaka iwatokee Itz Ok ngojeni Watu wanajipanga Na mikakati ya Kuja na Njia mpya Kila Siku sasa unapopewa taarifa Unapuuzia Endelea kupuuzia ukilizwa Cjui utaificha wapi hio aibu.
 
Mtandao utapoteaje kama uyo mtu yuko mbali na simu yako kuna vitu vingine naona kama havina logic ivi
 
Jana kuna Dada nilikuwa nachat nae.
nikamwambia ntakutumia hela.
ghafla ikaingia meseji namba mpya.
Hyo meseji Inasema.
Itume kwenye namba hii iyo pesa 0756833929.uwe makini Jina litakuja deus kutumwa.
Machale yakanicheza.nikampigia Yule Dada nikamuuliza una namba ngapi? Mbona kuna namba imeingilia chat yetu.?akasema sijui hiyo namba.
Nikawaza sana.nikasema wafanyakazi wa tigo wanaingilia meseji zetu na wanazisoma.
Alijuaje kama mimi nachat na mtu na ninataka nimtumie HELA?
Mkuu up right kabisa. Kuna wahuni kwwnye mitandao ya simu wanaingilia mawaailiano ya watu. Hiki ulichosema kiliwahi kunitokea. Kuna dogo nilikuwa nimtumie pesa, tukakubaliana nimtumie asubuhi ya siku inayofuata. Kufika asubuhi nikapokea sms ile peaa tuma kwenye ××××××× jina fulani.
Nikampigia yule dogo akasema ajatuma hiyo namba nitume kwenye namba yake.

Kwwnye makampuni ya simu kuna wahuni.
 
Kaaa hivo hivo sasa si shangai Mtu kumpinga Hadi mungu aliyetoa post yeye ni nani Usimpinge.
Mkuu Kitu gani kinachoweza kushusha bars za network yako kama sio Provider wako? Labda huyo mharifu afanye jamming ya signal kitu ambacho kitamtoa nae kwenye covarage hizi sms za kuforwadia kuna muda hazina logic kabisa huko fb ndio zimwjazana sijui share sijui vile ni Ujinga tu,
UTAPELI ULIOPO Ni huo wa tuma hela kwenye number hii probably kuna Wafanyakazi wa hizi kampuni hawako loyal ndio mana yanatokea mana mawasiliano yote wanayaona
 
Back
Top Bottom