๐—Ÿ๐—ถ๐—ป๐—ฒ ๐—ฌ๐—ฎ๐—ธ๐—ผ ๐—ถ๐˜๐—ฎ๐—ณ๐˜‚๐—ป๐—ด๐˜„๐—ฎ

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
Line%20Yako%20kufungiwa_20230923_072141_0000.jpg


Tcra na makampuni mbalimbali ya simu nchini Tanzania wameleta mfumo wa watu kufungiwa line zao ikiwa hawajazitumia kwa muda.

Kumekua na tabia ya watu kusajili line mbalimbali Kisha kuziacha na kutozitumia kwa muda mrefu hatimaye Sasa suluhisho limepatikana toka Tcra na makampuni ya simu Tanzania.

Ikitokea umesajili au umesajiliwa line alafu ujatumia kwa muda kwa kipindi cha siku 90 sawa na miezi mitatu basi line Yako itafutiwa usajili na kupewa mtu mwingine.

View attachment 2759111

Ikiwa unahitaji line Yako unataka kuzuia kufungiwa Basi hakikisha umetoa Taarifa kwa watoa huduma wa mitandao Yako kama Tigo, vodacom, Airtel, halotel, Ttcl na Zantel ili kuzuia namba Yako kufungiwa au kupewa mtu mwingine.

Hakikisha umepiga namba hii 100 au fika Kwenye kituo Chochote Cha mtandao kilichopo karibu Yako ili kupata maelezo zaidi utaweza kuhifadhi namba Yako usiyotumia kwa kipindi Cha miezi 12 bila kufutiwa usajili.
 
Ndio kazi yao hawana kazi muhimu hao kausha damu yaan kazi kupandisha bando wameshindwa kudhibiti matapeli
 
Back
Top Bottom