KERO Kuongezeka kwa gharama za maisha chuo cha UDSM (Direct cost)

KERO Kuongezeka kwa gharama za maisha chuo cha UDSM (Direct cost)

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Chuo kimepitisha waraka mpya unaoainisha kuongezeka kwa gharama za kuishi hostel, kulipia mitihani na mambo mengine hadi kufikia zaidi ya laki tano na hii ni njee ya ADA hivyo inatuthiri sisi wanafunzi tuliokuwa tunategemea BOOM ili kulipa ADA ambapo hatukupata asilimia mia moja lakini na muda huo kwa ajili ya malipo mengine ya chuoni ambayo ni nje ya Ada hivyo tunomba tatuzi

IMG-20261003-WA0005.jpg


Katiba kipindi ichi karibu na kufungua chuo gafla kumezuka maba
1380007.jpg
1380005.jpg
diliko makubwa kwenye direct cost,pia malazi hii imekuwa tabu na ngumu hata kuvumilika kwa sisi wanafunzi wenye hali za chini ikiwa imebak siku 23 kufungua chuo kwa nn hawajasm mapema
 
Gharam zinapanga 2 chuo kikuu cha dar es salaam udsm

Maneno ya rais
Waheshimiwa kiukweli ni seme hakuna hata mmoja aliyependa haya mabadiliko kutokea

Mabadiliko haya yalipitishwa tokea mwaka Jana na implementation yake ni mwaka huu

Ni masuala ambayo yamekubaliwa na serikali pamoja na chuo

Kitu kikubwa na sababu kubwa ni kwamba Gharama za maisha zimepanda sana kwa sasa so ilichuo kiweze kuendelea ..piah masuala ya direct cost na accomodations zikapandshwa

Ndugu zangu Mimi nimeingia serikali na kukuta hii ishapandishwa na vikao vyote VYA menejiment vimekwisha azimia ipande

Kwa sasa inafanyiwa implementation

Piah polen sana

Pole sana

Hili jamboa hata sisi tumeumia sana tena sana
Mabadiliko haya yamefanyiwa mapitio miaka mitatu nyuma

Na kupitishwa mwaka Jana , mwaka huu yakapitia Council nakupitishwa yaan approved mwez wa Tano na ni ruhusu ambayo chuo kimepewa kutoka serikalini kabisaa hivyo ni vitu vilivyopitishwa kwa mujibu wa sheria

Yako kwa mujibu wa sheria

Mimi nacho waomba wanafunzi wenzangu tuyapokee haya mabadiliko kwa sasa otherwise sisi huko mbele tutapeleka na sisi concern zetu kupitia Sheria husika

Sababu kubwa

Ila kwa sasa naomba tuyapokeeei

Mkutano wa 301 wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam uliidhinisha kupanda kwa kodi ya malazi katika mabweni na hosteli za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Viwango hivi vipya vya kodi vitaanza kutumika kuanzia mwaka wa masomo 2026/2027.
Baraza lilizingatia sababu mbalimbali zilizopelekea kuongezeka kwa viwango hivyo vya kodi, kama ifuatavyo:


i. Sera ya Malazi ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ya mwaka 2000, iliyofanyiwa mapitio mwaka 2022, inaelekeza kufanyika kwa mapitio ya gharama za malazi ili kukidhi gharama za uendeshaji na matengenezo.


ii. Viwango vya kodi vinavyotumika kwa sasa vilifanyiwa mapitio mara ya mwisho miaka 13 iliyopita, hivyo havilingani tena na gharama halisi za uendeshaji kutokana na mfumuko wa bei. Kwa sasa, gharama za uendeshaji wa mabweni ni takribani shilingi bilioni 5.4 kwa mwaka, wakati makusanyo ya kodi ni shilingi bilioni 2.25 pekee.

Hivyo, kuna hitaji la kuboresha miundombinu, kununua samani, pamoja na kuboresha vifaa mbalimbali.

Direct Costs ni gharama za huduma mbalimbali zinazolipwa moja kwa moja na mwanafunzi anapohitaji huduma husika kutoka chuoni. Ni muhimu kufahamu kuwa Direct Costs si fedha zinazolipwa wakati wa usajili pekee, bali zinajumuisha huduma mbalimbali za kitaaluma na za wanafunzi ambazo zinaweza kuhitajika katika kipindi chote cha masomo au baada ya kumaliza masomo.

. Gharama zinazolipwa wakati wa usajili
Kwa wanafunzi wa shahada ya awali, huduma zifuatazo hulipwa wakati wa usajili ili kukamilisha usajili:
1. Vitambulisho vya wanafunzi – 15,000
2. Gharama ya usajili – 10,000.
3. Huduma za TEHAMA na uboreshaji wa miundombinu yake – 20,000.
4. Huduma za Maktaba – 15,000.
5. Gharama za mitihani – 30,000.
6. Ada ya Michezo – 10,000.
7. Ada ya Jumuiya ya Wanafunzi (DARUS) – 5000
8. TCU Quality Assurence Fee – 20,000.
9. Bima ya afya (NHIF)– 50,400.
10. Gharama za kuhitimu na Convocation TZS 80,000.

Jumla ya direct cost hizi ni TZS 255,400/=

Kuhusu gharama za graduation 🎓
Kuanzia sasa, gharama za Graduation zitalipwa mara moja tu ndani ya miaka mitatu ya masomo, na ni lazima kwa kila mwanafunzi.

Na zitakuwa zinalipwa pale mtu anapoanza mwaka wa Kwanza wa masomo
Kwa sasa
1. Anayeingia Mwaka wa Kwanza, akishalipia hatolipa tena.
2. Anayeingia Mwaka wa Pili, akishalipia hatolipa tena.
3. Anayeingia Mwaka wa Tatu, akishalipia hatolipa tena.
NOTE Kwa kifupi: Malipo ni mara moja tu.kwa upande wa graduation charge
 
Hili jambo linaumiza sanaaa yaani Rais sijuw kiongozi anatoka huko aliko na kuwaambia hamna namna inabidi tukubaliane nayo tu na tuwashauri wengine wakubali tu huyo ni kiongozi kweli?

Mfano me mwaka wa pili au wa tatu au hata wa 4 nili apply chuo baada ya kupima gharama zoote nikaona hapa ntamudu sasa inakuwaje nishaingia tayari ndo mje mnibadilishie? Kwann kama ni mabadiliko wasifanye kwa freshers ili waone kama ni himilivu ile idadi ya wanafunzi itapanda au itashuka?

Kwann nije niathirike mm ambae wazazi wangu wanajua natakiwa nilipe 97 kama direct cost? Ntawaambia nn kuwa ni 255k?

Hata mm tu ambae sina akili timamu mwaki Msafi alishindwa hata kuuliza kaswali kadogo hako kwa faida ya zaidi ya watu elf 40 walio nyuma yake?
 
Tunataka press yakupinga hili jambo na kuomba chuo wagaili mara moja kama hoja za kupinga tutakusaidi⁩ imetokea juzi juzi Afrika kusima 2017 mbona mpka inafika 2018 zuma aligaili na kuleta elimu walau haikuwa bure ila ilikuwa nafuu
 
Unasema unaboreshaga hostel hali halisi tuione basi hata labda umeweka na tufeni vyumbani watu unakuta wana tule tufeni twao twa elfu 15 kukipigwa na upepo tu kameanguka au huwa wanaboresha kitu gani?
1380007.jpg
 
Wakuu shikamoni! Mmeongeza direct cost kutoka 97,400/= hadi 255,400/= sawa na ongezeko la zaidi ya 162%. Na gharama za hosteli mmepandisha kwa zaidi ya 50%.

Sikatai labda kweli gharama za uendeshaji na utoaji huduma kwa wanafunzi zinaweza kuendana na hicho kiwango kipya mlichotoa, ila nina swali naomba niwaulize

Mmegundua LINI kwamba huduma mnazotoa haziendani na kiwango tunacholipia?

A). kama ni zamani kwa nini hamkuchagua kuipandisha kidogokidogo kuliko kuipandisha hivi mara moja na kumuumiza mwanafunzi? Na pia ni kwanini taarifa isingetolewe mapema tukawa tunajua ili tujiandae? B)Kama mmegundua siku za hivi

karibuni.

kwanini msingesubiri mtushirikishe

kwanza kabla ya kufikia uamuzi huo? Kulikuwa na ulazima gani wa kuharakisha tunakuja kupata taarifa zimebaki siku chache tu kurejea chuo?. Tena ukizingatia kwenye direct cost kuna vipengele mmeviongeza ambavyo vingeweza kusubiri..? (Sports charges, Library Services charges, graduation charges, ICT Service charges) Vilikuwa na ulazima gani kuvin'gan'ganiza kabla taarifa ya onaezeko haiiawa communicated
 
Mm ningemshauri tu rais wenu vitu kama vitatu vya msingi ambavyo angeweza kusimama navyo kule kwenye vikao hata kama issue ingekuwa ngumu akasikilizwa

1. Angeomba hii issue itolewe before watu wajiandae nayo hata mwaka mmoja kabla wangesema hizi vitu labda zianze kutumia mwaka wa masomo ujao na uwe adopted na wale freshers wakaondoka nao mpaka mwisho yani hizi gharama zikawa zina base kwa wale wanafunzi wanaoingia kwa mara ya kwanza zisiwaguze hawa continuous ili mwanafunzi awe anakuja UDSM akiwa kashajitafakari kiuchumi kama anaweza
2. Angewaomba kama suala hili ni sensitive wangeongeza au wakawa wanachomeka kimoja kimoja kila mwaka sio vyote kwa pamoja kupunguza athari kwa wanafunzi kama umeongeza hostel za magu mwaka huu bei zingine zisalie vile vile mwakani ongeza na ya Mabibo na hizo gharama za ongezeko ziwe za wanafunzi wapya pekee.
3. Ambayo hii ingewachafua management kwa ujumla ni kukataa hizo vitu kabisa zisiwepo mpaka mm nitakapoondoka ila chini ya uongozi wangu kama mwakilishi wa wanafunzi hii kitu sitaki kuwa sehemu ya mchakato wako kuwaumiza wanafunzi walioniamini kusimamia changamoto zao afu niwe sehemu ya kuwaongezea changamoto tena📌
Haya ndiyo mawazo yangu makubwa matatu kama ningekuwa mwakigharama ningeuomba uongozi wa chuo ufanye
1380107.jpg
 
Kuna maswali Mhimu sana chuo kinatakiwa kiwajibu wanafunzi
1. Kwanza kinatakiwa kiwe wazi utaratibu kwa kulipo hizo direct cost na hostel huwezi nambia sehem kama Mabibo ambapo mtu unatumia 600 nauli jumla 1200kwa siku nauli unalipa 119k per semistet then hapo hapo hakuna Maji un
1380005.jpg
1379804.jpg
aoga chumvi hali kadharika kama magufuri sasa hii haiko sawa
2. ⁠kwa nini wajikite kwenye mkakati wa mda mrefu wa kuongeza hizo gharama wasitatue shida za wanafunzi kwanza huko hosteli kwamba haya mambo ni mageni kwao au hamnaaa na wanajua wanafunzi wengi wanatumia Boom na hela za ziada kujikimu kulipia mahitaji kama hayo mda mwingine hela haitoshi inakubidi usubili
 
Mmh, hili ni ongezeko kubwa sana la gharama - kutoka 97,400/= hadi 255,400/=, sawa na ongezeko la zaidi ya 100%.

Awali gharama za hosteli zilikuwa takribani Magufuli & ColCT 800-1,300/= na Mabibo 500-1,000/=. Ongezeko hili kwa wakati mmoja ni mzigo mkubwa kwa mwanafunzi ambaye pia anategemea boom hilo hilo kugharamia malazi, chakula, usafiri na mahitaji ya

masomo.

Ombi langu kwa Uongozi wa Chuo ni kulipitia upya ongezeko hili na kuzingatia uwezo halisi wa wanafunzi. Mhe. Selina Kingalame, tunaomba utufikishie kilio hiki. Pia tunaomba Wizara ya Elimu chini ya Prof. Adolf Mkenda, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba, Makamu wa Rais Mhe. Ndejembi, na mwisho Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, mtusaidie kulitazama suala hili kwa jicho la mwanafunzi.

Tunaomba suluhisho linalolinda ustawi wa mwanafunzi na kuhakikisha gharama za msingi hazizuii mwanafunzi

kusoma kwa amani.
1379804.jpg
 
Ni kweli Mkuu hili jambo limeathiri watu wengi sana na nitafurahi kama likichukuliwa hatua mapema zaidi

Maxence Melo JamiiCheck JamiiForums hebu mtusaidie katika hili mtupazie sauti katika social media akaunti zenu

Hawa watu hawajui hata kula na kipofu aisee yaani mwezi mmoja kabla ya vyuo kufunguliwa unatangaza kupanda kwa direct cost kutoka 97400 mpaka 255400 na mnapandisha mpaka gharama za malazi

Kwenye Direct Cost kuna huduma hapo zimeongezwa kiwiziwizi tu na nashangaa huko kote zimepitishwaje aisee
 
ELIMU NI HAKI YA MSINGI sana kwa vijana wa Tanzania, serikali inapoendelea kuweka juhudi ya kupambana na ujinga ifahamu kuwa moja ya sababu ya vijana kukosa elimu bora ni gharama kubwa ya elimu.

Ongezeko hili la "direct cost" ni pigo kubwa sana kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam. Huenda Chuo Kimetoa sababu za msingi kabisa za ongezeko, lakini kimetua Mzigo wake kwa kumbebesha Mzigo mwanafunzi asiye na uwezo wa kuubeba huo Mzigo.

Ni rai yangu kuwa, Mzigo huu pia, kama jinsi ulivyotuliwa na Chuo Kikuu, Serikali itachukua Jambo hili kwa uzito mkubwa sana na hali ya dharura (sense of emergency) na kuwatua wanafunzi mzigo Huu Kabla ya

vyuo kufunguliwa
1380005.jpg
a.
 
Itakuwa wanafunzi wengi saivi ni laini laini

Zamani migomo ilianzia sekondari, mtu akija hapo udsm anakuja kuendeleza tu 😅
Hali ni mbaya nyie hamjui tu. Imagine kabla ya ongezeko la bei, kuna wanafunzi walikua wanapata ID siku ya mtihani asubuhi, hapo ni baada ya kuchangiwa na wenzao, leo inapanda kwa kiasi hiki...unahisi maisha yatakuwaje?
 
Back
Top Bottom