Mr.laravel
JF-Expert Member
- Oct 1, 2015
- 471
- 515
Mimi hua ni mfuatiliaji sana wa mambo hasa ya technology. UDSM kama chuo kinachoongoza Tanzania nilikua nategemea watakua mstari wa mbele kuendana na mabadiliko kwenye technology.
Nimepitia Syllabus yao ya hawa wanaoenda kusoma Computer Science/Engineering, yaani first year semester zote mbili Introduction to programming in Pascal.
Hivi nani dunia hii bado anatumia Pascal? Why learn a language ambayo hutokuja kuitumia mbeleni hata siku moja, hakuna industry inatumia Pascal siku hizi, na hakuna anayetafuta kujiajiri au kuajiri mtu mwenye experience na Pascal.
Miaka yote naona course outline haibadiliki, hawapangi kitu kipya, everything is old. Kuna languages nyingine nyingi nzuri zinazofaa kumpa mtu introduction into Programming, Python being one of them au angalau C japo watu wanalia "pointers, dynamic memory allocation" ila ni vitu vikielezwa vinazoeleka vizuri tu. No wonder serikali inalalamika daily kua watu vijana wanaomaliza Tanzania hasa engineering courses hawana uwezo wa kujiajiri.
Ni vizuri kuwapeleka speed wanafunzi kuanzia mwaka wa kwanza sio wanagusa vitu boring wanapoteza interest.
Aisee! yaani hatua ile ya Elimu mtu anafundishwa Pascal!
Ni hatari sana.
Watanzania watachelewa sana kuwa wataalamu katika ulimwengu wa "Programming".
Wakuu, kaa ukiamini kuwa hizi programming tunazofundishwa vyuoni ni kama basics, kwa hiyo tusilaumu sana mi chuo nilichosoma sikuwahi kufundishwa java lakini kwa mda wangu na jitihada zangu nimejufunza mwenyewe, programming language nyingi karibia zinafanana zinatofautiana vitu vichache katika mazingira ya ufundishaji, kwa hiyo tusiwalaumu sana
Siwalaumu sana, sema wajaribu ku-update tu some stuffs.. Watu kuanza kusoma kitu fulani mapema inaweza wasaidia sana hapo baadaye, na wengine wakianza na language boring zisizo na support wanaweza poteza interest kabisa kwenye progamming kabla hawajaonja utamu wake.
mpaka sasa nshawaelewa sasa kama mtu anataka kujifunza GUI based programming na sio CLI based ungeshauri aanze na Lugha gani lengo likiwa kwenye ktengeneza desktop applications maana Pascal mshai Dis sio strong
Ilikuwa lini hiyo?Why Pascal?
1. Pascal ndo language pekee iliyobuniwa kwa ajili ya KUFUNDISHIA.
Mwanafunzi anayejua ku-solve swali kwa dy/dx unamtafutia language useless kwa kigezo cha urahisi? By the way Python is far easier than old Pascal!2. Pascal is easy to learn. Sababu kubwa ni kwamba inatumia maneno ya kawaida ya kiingereza, mfano BEGIN, END , badala ya {,}. C, C+, C++, Java and the like are too symbolic to be understood by novices. Mfano, ipi rahic kueleweka kat ya BEGIN na { ?
Mwalimu, is this really a sound reason? Mwanafunzi ambaye hawezi hili, bora afanye kozi nyingine. Sayansi hataiweza kabisa. Labda akafanye Sayansikimu tu!3. Pascal is case-insensitive. Ni ngumu sana kumwelewesha novice kwamba variable "number" na "Number" na "NAMBA" zinarefer value tofauti kama ilivyo ktk C, Java na language nying.
4. Originally Pascal was structured(now there is object pascal). Structured programming ni rahic kujifunza kuliko object-oriented. I can bet 90% ya successful programmers wetu bongo wanafanya structured prog kwa kutumia OO prog language kama Java. This defeats the purpose of OO languages.
5. If u can program in Pascal then u can program in ANY LANGUAGE.
Mkuu twende mbele turudi nyuma, Pascal is a dead language..
Huo mfano wa app moja iliyoandikwa kwa Pascal doesn't make any difference, Ingeweza kuandikwa vizuri zaidi kwenye language kama C++. Wanaona uvivu kuiamisha tu sababu unaweza kuta codebase ishakua kubwa.
Pascal ilitumika miaka hiyo ya nyuma sana, siku hizi ukikuta industry inatafuta Pascal jua labda wana software ya zamani sana ambazo wanaona zitawacost sana kuziandika upya. Nenda google tafuta jobs uone kama utaona kampuni yoyote ya maana inatafuta mtu anayeandika Pascal. Hakuna hata moja..
UDSM hiyo choice ya language wamekosea, pitia vyuo vyote vikubwa duniani kama utaona kuna hata kimoja wanafundisha Pascal, kuanzia MIT, Harvard, Princeton, Caltech, wote utakuta ni Python au C. Wengine wanagusa Java, no one teaches Pascal nowadays. Hata internet kila kona wanasema its a dead language.
Maybe you should learn more programming iko wapi na inaelekea wapi, new features ni zipi na watu wanafanya nini before commenting. Ya nini kustick na language ambayo in the end you won't do anything significant with it, coz eventually utaiacha tu, kwanza haina support kwa hiyo ukiwa na tatizo utatafuta sana online kupata mtu ambaye angalau anaweza akajibu, pili utataka kuimplement a certain feature itabidi uandike from scratch from zero sababu hutopata library online ya kukufanyia wewe hiyo kazi. In the end hakuna kitu productive mtu anaweza fanya kwenye Pascal. Studying a language is more than just being able to code anything with it, its also about support utakayopata, kama utafanikiwa kutengeneza kitu cha maana, je utapata watu kirahisi kukusaidia kukuza codebase?
Facebook walijaribu kutengeneza Messenger service yao kwa language inaitwa "Erlang" ni very powerful language, hata Whatsapp ndo wanatumia, ila walikosa experts, wakahama language, wakatumia language iliyo na support kubwa. Sasa mtanzania ndo kwanza hata industry yetu iko very low, tuongeze shida tena kutumia languages zisizo na support, mwisho wa siku hakuna kitu tutaproduce
Python, PhP, ASP ni Scripting Languages. You might as well suggest we teach them using HTML!
Ilikuwa lini hiyo?
Kama ni hivyo si ungefundisha PHP basi? au hata C?
All in all, unaonekana kuwa outdated sana na hivyo kuzalisha Vijana wenye "kutu". Nakushauri ujitahidi ku update ufahamu wako. Nakushauri uwafundishe wanafunzi wako Python kwa kuanzia then kati ya C++, Java, C# au zingine kama hizo!
Natamani sana kujifunza IT hasa programming ingawa sina basic yoyote. Wapi naweza kupata hyo elimu kwa muda nje ya muda wa kazi??
Wanafunzi walewale wanaosoma Pascal mwaka wa kwanza, mwaka wa pili wanafundishwa OO Java. Hakuna sababu ya msingi ya kumfundisha lugha tofauti na Pascal kama hataelewa. Pia mim kama mwalim, sina mamlaka ya kuwabadilishia programming language, wala hakuna mwenye mamlaka mpaka pale syllabus inapobadilisha.
Pia, hakuna ushahidi kuwa ukiwafundisha wanafunzi programming kwa kutumia lugha tofauti na Pascal, basi watakuwa programmer wazuri zaidi.
Mwisho, naona wewe umesoma nje ya nchi. Kwahiyo, kama kawaida ya binadamu, unataka kuleta ligi za vyuo. Changu bora, chako kibovu. Mimi sina time na Ligi. Nimefundisha vyuo vikuu 4 tofauti, so naweza kusema am impartial-unlike you. Tambua kwamba vyuo vinaendana na mahitaji ya soko. Kama soko la Tanzania halihitaji Data mining tools hutaziona kwenye syllabus, same applies to machine learning etc.
Mkuu sisemi I am better than UDSM, ila still nimesoma chuo ambacho wamejipanga vizuri kuliko UDSM, I am simply sharing my experience ili wabadilike tusonge mbele, swala sio kufata mkumbo, kuna vitu UDSM wanapatia ila hili wanakosea. Nimesoma Computer Science & Engineering kwa hiyo najua vizuri courses zote zinahusiana na nini, na kuna very important courses ambazo UDSM ni cheche, tukiacha hilo swala la Pascal kwamba wako nyuma, turudi kwenye vitu kama Artificial intelligence, hakuna machine learning UDSM wakati dunia nzima iko huko sa hivi, any big tech company siku hizi wana machine learning algorithms kwenye backend zinahandle data, sio google, sio facebook sio quora, stackoverlow, apple etc, that way jamaa wanazidi kua on top of their competitors siku zote. Machine learning inafundishwa vyuo vingi tu duniani, tusiongelee sana marekani ila hata Asia vilevile. Hatuwezi kukaa tunabaki nyuma tunang'ang'ania mambo ya zamani na kusifia ati kisa jina UDSM, lile ni jina tu wanaweza kua top bongo ila tukija kwenye swala la world market kwenye technology hakuna wanachofanya. Course nyingine kama Computer architecture,kujua assembly code na deep down machine imetengenezwa vipi ni very important, sio tu kwa performance ila hata security, na bado ukitaka kuunda a fully programmable machine kama hujui low level kuna nini hutoweza.. We huoni bongo tunatengeneza vitu kwa kuunga parts tu, kusema tuweke our own programmable logic ni mziki, wachache sana wanaweza.
Hakuna kitu kama kila mtu kua mtaalamu wa part yake, sasa ya nini kua mtaalamu wa kitu ambacho hakina faida? Tunasoma ili iweje sasa? Ulimwengu wa software hauko hivo, ndio maana kuna kitu kinaitwa Open source, software siku zote lazima kue na ushirikiano, huwezi kaa mtu moja ukatengeneza microsoft word, its impossible. Sasa kama language unaijua mwenyewe utatengeneza nini cha maana. Mkuu em jaribu kujifunza programming kidogo ufike level ya kutrngeneza a very simple application alafu urudi utuambie kama hujabadilisha mawazo