UDSM: Miaka 50 iliyopita na ijayo - mtazamo wangu

MPIGA ZEZE

JF-Expert Member
May 16, 2011
2,539
2,296
Kwa mtazamo wangu, UDSM katika miaka 50 ya uhai wake - kwa makusudi au kwa bahati mbaya - imezalisha generation ya wasomi na watawala/wanasiasa wenye fikira na vitendo vya KIFISADI. Haya ndio matunda tunayovuna na 'kujivunia' baada ya miaka 50 ya uhuru. Hili linajidhihirisha katika mkusanyiko (tulihabarishwa kwenye picha magezetini) wa wageni rasmi, waheshimiwa waliokuwa wamekaa viti vya mbele na wenyeji wao katika ukumbi wa Nkrumah wakati wa kilele cha sherehe za chuo hiki kutimiza miaka 50. Tukubali kwamba miaka 50 imekuwa hasara!! Hata hivyo asasi hii bado inaweza kubadilishwa ama kufanyiwa mageuzi na kuwa chimbuko la generation ya wasomi na watawala wenye fikra na matendo ya KIUADILIFU katika miaka 50 ijayo. Katika nchi zilizopiga hatua kiuchumi na kijamii duniani, vyuo vikuu ndivyo 'viwanda' vya kufyatua UBUNIFU na UADILIFU. Tanzania bila UFISADI inawezekana na 'wasomi' wanaoweza kuongoza harakati hizi.:lol:
 
Back
Top Bottom