Udsm direct cost ni kubwaaa

Udsm direct cost ni kubwaaa

1juma2

Member
Joined
Aug 27, 2025
Posts
13
Reaction score
17
Good morning UDSoL family hope wote ni wazima na tumeamka salama. ⚖️⚖️

Naomba nitoe ufafanuzi kwenye suala la ongezeko la Direct Cost na msimamo wetu kama UDSoL. Binafsi taarifa ya ongezeko hilo tumeiona jana kama ambavyo kila mmoja wetu ameona kwenye makundi mbalimbali ya whatsapp na social medias zingine. Lakini vile vile gharama hizo zimechapishwa kwenye UDSM Admission Year Book. Ya 2027/2027.
Lakini changamoto iliyopo ni kwamba hakuna taarifa rasmi ya chuo kutoka utawala ambayo tunaweza kuitolea tamko na kuchukua hatua dhidi yake.
Hivyo uongozi wa UDSoL haukubaliani na ongezeko hilo kwa namna yoyote ile kwani zimekuwa ghafla sana na ongezeko ni kubwa sana ambapo wanafunzi wengi hatutaweza kumudu gharama hizo.
Hivyo basi kwa sasa tuwe watuliwa kwani uongozi unafwatilia hili ikiwemo kukaa vikao na Wenyeviti na Makatibu wa Colleges, Schools na Institute zote za Mlimani Campus ili kuja na tamko moja la wapi tuanzie.
N.B Hakuna kiongozi yeyote yule aliye ridhishwa na ongezeko hili lakini tunaendelea kufwatilia kwa kina zaidi na kufwata njia za kisheria kutatua hili.
Niwatikie utekelezaji mwema wa majukumu yetu ya kila siku.

Regards.
Mbwana Ally Awadhi.
UDSoL Chairperson.
1382272.png
1382197.jpg
 
Back
Top Bottom