Mkuu hivi vyuo ni vya umma. Duniani kote vyuo vya umma vifaa vya maabara na karakana ni first priority.viko well equiped.kwasababu ndo tanuru la kuzalisha watu wa kuendeleza nchi. China pamoja na kuwa na wanafunzi graduate>20mil na hakuna ada, maabara zinakilakitu.wamewekeza hapo kuliko kitu chochote. wanaamini ili washindane na ulaya na America lazima waandae wataalam waliopikika wakutosha.Hapa nyumbani ishu muhimu kama hiki cha Chuo kikuu tena ni ndo jicho la umma hakina vifaa Watu hawaoni ni Tatizo wao wanaingiza siasa tu ni aibu.watoto wanaosoma karibia 99% ni maskini wanaolipiwa na bodi hawachangii garama za karakana wala vifaa vya maabara.Safari zipi zilizoifanya FoE na sasa CoET idumae kwa miongo karibu minne tangu ianzishwe. Tusitafute majibu mepesi kwa maswali magumu. Hii ni issue siyo kwa serikali tu, hata kwa hivi vyuo vyenyewe. Kama tukiwategemea wanasiasa ndiyo watufanyie kila kitu, nakuhakikishia hatutafika popote. Ni lazima tufike mahali tuonyeshe kwamba bila wao tunaweza kujisimamia wenyewe ... na ninalazimika kuamini kwamba FoE (CoET) walizembea sana kuliona hili likitokea kwa sababu ya kutegemea misaada ya wafadhili kama Ujerumani, Sweden, Denmark, n.k. na hawakuwa na agenda ya je, hawa wafadhili wakisitisha huduma zao itakuwaje?
Ni lini serikali ilizuia vyuo kuwa na miradi ya kujiendesha kama siyo kukosa maarifa kwa waliopewa dhamana ya kusimamia na kuviongoza vyuo hivyo?
Wakati umefika sasa wa kubadilika kifikra ... tusiweke siasa katika kila kitu. Hizi siasa ndizo zinadumaza akili zetu. Kama tumelogwa vile!!
Tatizo ni kuwa tunadhani Chuo Kikuu ni glorified shule ya msingi! Tunasahau kuwa Chuo Kikuu ni kitovu cha utafiti na si mahali pa kufundishia peke yake. Badala ya kugeuza Chuo Kikuu kuwa mahali pa kutengenezea ujuzi (knowledge) sisi tumakimbilia kuwekeza kwenye department store uchwra na ukumbi wa harusi!
Mimi hata namna yalivyokuja maombi yenyewe yananitia wasi wasi. Bila kueleza nini hasa kinachokusudiwa kufanywa wanakimbilia kupanga viwango vya michango! Kwani tuko kwenye kikao cha harusi?
Amandla........
Shame upon us,How come chuo kiombe msaada kwa jinsi hii? jamani tutafika kweli?Wakati huohuo mnasisitiza watu wasome sayansi ili wawe mainjinia ,wataenda kusomea wapi?
Kibaya Companero hana mwingine zaidi ya Mpemba wakati mimi ninayo mizungu ya kumwaga. Ukimbana sana anaanza kukutajia akina Ibn Battuta na Tippu Tip
Kiongozi,Wakati wa kupata Uhuru nchi ilikuwa na wahandisi wawili tu. Tumewasomesha wengi tu baada ya Uhuru kwa kodi za Wananchi. Sasa mmekimbilia huko mnabeba maboksi kwa kutumia vifaa vya wahandisi wa Kizungu!
Kiongozi,
Hii dhana kwamba 'tumewasomesha' ni dhana muflis. Kujitapa kuwa umemsomesha mtu ni ulaghai na kutaka kuchukua credit yote bila kujali input za huyo msomeshwa, walimu wake na wengine wote walioweka juhudi ktk kumuelimisha mlengwa. It is just wrong.
Elezea maana ya dhana hiyo kabla ya kutoa madai yasiyoendana na maana husika! Kumbuka nilisema 'tumewasomesha kwa kodi za wananchi' hivyo dhana ya 'tumewasomesha' inajumuisha jamii nzima wakiwamo wao! Ebo!
COET inaomba, Maktaba wataomba, Laws wataomba, n.k., n.k.,
Nasema hivyo kwa sababu UD, hakuna idara iliyo na uzima. Nahisi mkuu wa COET kwa hapo lazima tuseme wazi yuko desperate.
Mfumo wa vyuo kwa sasa ni cost sharing. Kwa idadi ya wanafunzi waliopo COET, hawawezi kukosa zaidi ya shilingi milioni mia 2 kwa kila mwaka ili kuweka mazingira mazuri ya kufundishia, zikitokana na tutition fee.
Sasa tatizo liko wapi? Huyo VC anafahamu anachotakiwa kufanya? Naelewa kwa sasa huo ndo ugonjwa wa vyuo vyetu hapo Bongo. VCs wanaonekana kama stooge. Wanahangaika kupewa sifa na wanasiasa.
..................................................... Mimi hata namna yalivyokuja maombi yenyewe yananitia wasi wasi. Bila kueleza nini hasa kinachokusudiwa kufanywa wanakimbilia kupanga viwango vya michango! Kwani tuko kwenye kikao cha harusi?
Amandla........
Wakati wa kupata Uhuru nchi ilikuwa na wahandisi wawili tu. Tumewasomesha wengi tu baada ya Uhuru kwa kodi za Wananchi. Sasa mmekimbilia huko mnabeba maboksi kwa kutumia vifaa vya wahandisi wa Kizungu!
Hata hayo masomo mliyowasomesha mengi yameasisiwa na wazungu. Mikanuni, mifomyula, na mambo mengine mengi yanayofundishwa kwenye fani ya uhandisi, imevumbuliwa ulaya na mizungu. Hata hivyo vyeo sijui vya udokta au uprofesa na vyenyewe tumeiga toka kwa wazungu. Heck...hata uvaaji majoho kwenye mahafali tumeiga.