UDOM yatwaa ubingwa wa Cyber Premier League (CPL) 2026

University of Dodoma (UDOM)

Public Institution
Joined
Feb 24, 2024
Posts
50
Reaction score
55
4d110ec5-163d-4dab-aa42-2bc605cd3012.jpeg

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimeibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya kitaifa ya usalama wa mtandao ya Cyber Premier League (CPL), baada ya timu yake ya wanafunzi watano, S4LV4T0R3, kuonyesha umahiri mkubwa na kuibuka kidedea miongoni mwa timu 76 kutoka vyuo mbalimbali nchini Tanzania.

Fainali za mashindano hayo zimefanyika leo, tarehe 11 Aprili 2026, katika Ukumbi wa CRDB uliopo jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Wanu Hafidh Ameir.

Mashindano ya Cyber Premier League (CPL) ni jukwaa la kipekee linalolenga kupima na kukuza ujuzi wa usalama wa mtandao kupitia mfumo wa ushindani unaofanana na ligi ya michezo, ambapo washiriki hutumia akili, mikakati na ushirikiano wa timu kutatua changamoto halisi za kiusalama mtandaoni.

Timu ya UDOM iliyoshinda iliundwa na wanafunzi watano ambao ni Martine George, Festo Ndunguru, Almas Ashraf, Amani Nsemwa na Erick Sanga. Ushindi wao umeiwezesha timu hiyo kujinyakulia zawadi mbalimbali zikiwemo fursa ya kufadhiliwa safari ya kwenda Dubai kuhudhuria Kongamano la Kimataifa la Usalama wa Mtandao, pamoja na vocha za kupata vyeti vya kitaaluma vya usalama wa mtandao vinavyotambulika kimataifa.

Ushindi huo ni hatua muhimu kwa Chuo Kikuu cha Dodoma katika kuendeleza ubora wa taaluma ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, hususan katika eneo la usalama wa mtandao, na unadhihirisha uwezo wa vijana wa Kitanzania katika kukabiliana na changamoto za kidijitali duniani.
 
View attachment 3571237

Haya tumewasikia ma mahackers
 
Washincanishe na wenzao wa Africa Sasa? Zamani kulikuwepo na mashindano ya ZAIN inter university challenge , ilikuwa ni aibu kwa vyuo vya bongo. Kila swali utasikia Pass , pass😃😃
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom