UDOM moto wawaka!!

Mawenzi

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
1,251
345
Jana kulikuwa na mkutano kati ya uongozi wa UDOM na mawaziri wa Elimu na Mambo ya Ndani. Mkutano uliendelea hadi saa nane usiku wa kuamkia leo. Na leo asubuhi kulikuwa na msafara wa wote waliokutana usiku kutoka UDOM kwenda mjini, labda kwenda kum-brief Waziri Mkuu.

Na Waziri Mkuu amekubali kukutana na wanafunzi wote wiki ijayo. Amewataka waorodheshe shida/madai yao yote.

Haya ni matokeo mazuri sana kwa UDOM kwani viongozi wake wanajifanya miungu watu. wanachojali ni maslahi yao binafsi tu.

Ujio wa Waziri wa Mamboya Ndani inawezekana ni kutokana na unyama uliofanywa na polisi kwa amri ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma
 
Naomba mambo yawe shwari kwenye chuo chetu kikuu cha kata!!!

wanaJF 2navyozidi kuwasiliti na kuwatenga vijana wenzetu wa UDOM as kila student wa UDOM ni msaliti/ccm,kumbe ni vilaza wachache 2
 
moto upi kaka?
hiki chuo cha kata
sio siri kweli kina utata
miundombinu ni kwenye kuta
kwa rangi zinazomeremeta
wahadhiri ni wa ukata
digrii moja yaani voda fasta
mi naeleza sio nasuta
misimamo yao ya kusitasita
nawasii watakuja juta
migomo waachieni majita
udsm sua kweli ni mafaita
 
UDSM acheni kujisifia mimi nimemaliza udsm miaka michache iliyopi wakati huo kweli kulikua na migomo ya kueleweka ikiongoza na akina waitara mwita, mwita magesa, mtatiro na wengine. Lakini baada ya hapo UDSM wamenywea hasa chini ya uongozi wa prof. Mukandara ambaye amewaweka kiganjani. UDSM hawana ujasiri tena na hata hiyo DARUSO haina sauti tena imeshapunguziwa madaraka. Ndio maana sasa hivi wanafunzi wote wanasajili upya kila semister na kupewa vitambulisho vipya kila semester tofauti na ilivyokua miaka 3 iliyopita ambapo wanafunzi walisajiliwa walipofika mwaka wa kwanza tu na kupewa vitambulisho walivyotakiwa kuvitumia hadi watakapohitimu chuo. Tunajua pia hakuna mwanafunzi wa UDSM anayesajiliwa bila kulipa asilimia anayotakiwa kulipia kwenye tuition fee. Kwa mambo yote haya mbona wana UDSM hawajagoma? Jibu ni simple tu, mkandala amewadhibiti. Hivyo sisi wana udsm tusibaki kujisifia bali tuwaunge mkono wana udom kwa move nzuri waliyoifanya hasa ikizingatiwa kua chuo chao ni kipya na hakikua na uzoefu wa mambo ya migomo. Tuache kufuata mkumbo na kuwalaumu eti wao ni wana ccm, mara tuseme walimchangia JK mil. 1, mara walilaani walkout ya wabunge wa chadema.... Hizi zote ni propaganda za kisiasa zinazoendesha na ccm kusababisha "divide and rule"
 
Jana kulikuwa na mkutano kati ya uongozi wa UDOM na mawaziri wa Elimu na Mambo ya Ndani. Mkutano uliendelea hadi saa nane usiku wa kuamkia leo. Na leo asubuhi kulikuwa na msafara wa wote waliokutana usiku kutoka UDOM kwenda mjini, labda kwenda kum-brief Waziri Mkuu.

Na Waziri Mkuu amekubali kukutana na wanafunzi wote wiki ijayo. Amewataka waorodheshe shida/madai yao yote.

Haya ni matokeo mazuri sana kwa UDOM kwani viongozi wake wanajifanya miungu watu. wanachojali ni maslahi yao binafsi tu.

Ujio wa Waziri wa Mamboya Ndani inawezekana ni kutokana na unyama uliofanywa na polisi kwa amri ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma
Hawa UDOM si ndio vijana wa CCM nambari wani,walimchangia hata Mkwere kwa ajili ya kuchukua fomu za kugombea Uraisi,sasa wanaandamani nini waache wanywe maji ya kijani
 
wana ccm wa udom ni vilaza wachache 2,baadhi ni majembe ye2 ndugu zanguni,ila hta hvyo hicho ni chuo kikuu cha kata,so nacho ni kichanga. . . .
 
moto upi kaka?
hiki chuo cha kata
sio siri kweli kina utata
miundombinu ni kwenye kuta
kwa rangi zinazomeremeta
wahadhiri ni wa ukata
digrii moja yaani voda fasta
mi naeleza sio nasuta
misimamo yao ya kusitasita
nawasii watakuja juta
migomo waachieni majita
udsm sua kweli ni mafaita

kaazi kweli kweli
 
Back
Top Bottom