Katambi: Madai ya kuibiwa Nyeti ni uzushi

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,282
Reaction score
3,955
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amesema uchunguzi uliofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama umebaini kuwa taharuki iliyozuka nchini ya watu kuibiwa sehemu zao za siri ni uzushi wenye nia ya kuvunja amani ya nchi.

Aidha, ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote wanaozusha taarifa za uongo katika mitandao ya kijamii ambazo ameeleza kuwa zinaweza kusababisha hatari ya kuvunja mshikamano na utulivu uliopo nchini.

Katambi ametoa kauli hiyo leo Aprili 6,2026, wakati akitoa salamu za pole kwa wafanyabiashara wa eneo la Mawasiliano, Ubungo mkoani Dar es Salaam, katika mkutano uliofanyika kati ya wafanyabiashara hao na Waziri Mkuu.

di​
 
FD71BC50-3D2A-48FF-94FB-956A9E78B19B.jpeg

Twende kazi..
 
Iwapo ningesikia ni matunda ya 2b ya content creators ningeelewa!
 
Amalizie kuwa waliotunga uzushi huu ni CCM ili kuwatoa wananchi kwenye mijadala ya Kupanda kwa bei ya mafuta, Reports za CAG na ripoti tarajiwa ya Tume ya Jaji Chande.
 
Hili suala la kuibiwa Nyeti naona vijana wenzangu wote hapa masikani wana kinga, mm pekee nimekaza Fuvu lakini Nyeti hazina confidence...😂
 
Back
Top Bottom