lugamba2001
Member
- Aug 18, 2009
- 12
- 0
Habari za uhakika toka kwa raia wa India, aliyepata mkataba wa Kufundisha Sociology UDOM, zinasema kuwa raia wa India wapatao 50, wamepata mkataba wa kufundisha katika Chuo kikuu cha Dodoma, ambapo watalipwa dola za Kimarekani 3,000/ kwa mwezi. Mwandishi wa habari hii, alikutana na jamaa huyo katika chuo kikuu kimojawapo kilichopo, katika jiji la Hyderabad, India. Jamaa huyo aliyepata ajira Bongo, alionyesha hamu kubwa ya kutaka kuongea na mwandishi wa habari hii, baada kugundua ugumu wa nywele katika kichwa chake, kwa kuwa hapa India weusi si kigezo, Maana weusi hapa ni wengi kama vile Kariakoo. Alitaka kujua mwandishi, anatoka nchi gani. Baada ya kuambiwa anatoka Tanzania, alianza kutaka kujua mambo mengi, ikiwa ni pamoja na kuzungumzia ajira yake mpya UDOM. Alieleza kuwa, Interview ya kuwapata ilifanyika jijini Delhi, mwezi wa September, hivyo anajiandaa na safari ya kwenda Tanzania baada ya kufaulu interview hiyo. Baada ya kuona maswali yanakuwa mengi, akashtuka kidogo na kuanza kujidai ana haraka. Akawa hajatoa habari kamili ni lini atatua Bongo, na Mikataba waliyopata ni ya miaka mingapi! Hakuna aliyepatikana toka Serikali ya Tanzania wala UDOM kuthibitisha habari hii. Pateni uhakika toka UDOM au serikali ya Bongo, maana inaamini sana EE (External Expertriatism)