UDOM inaniandikia application pending, natakiwa kulipia tena?

UDOM inaniandikia application pending, natakiwa kulipia tena?

hiram

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2013
Posts
266
Reaction score
393
Nilifanya online application UDOM na kulipia 30,000 kupitia tigo pesa (kutoka kwenye namba 0********6 kwenda namba +25565101101 muamala wa tarehe 24/07/2017 ) na waka confirm kwamba pesa imeingia hivi sasa nikiingia wananiandikia application pending payment kwamba bado sijalipia na natakiwa kulipia Tsh 10,000 tena. Ukiwapigia simu kwenye namba zao za customer support hawapokei, angalao basi wangeweka e-mail tuweze kuwasiliana nao.
 
Hiyo fedha hujalipa kwa mfumo wa udahili bali imeenda kwa mwenye hiyo namba,ukifuata hatua ulizoelekezwa kwenye dashboard utaona hatua zifuatazo hapo chini,uki click hatua inayofuata unaingiza namba yako ya tigo yenye fedha 10000tsh. Wakati huohuo utatumiwa code no. kwenye hiyo namba yako utaingiza hiyo code no. katika hatua inafuata na click next(katika hatua hii unatakiwa kuwa mwepesi kwani ndani ya dk. 3 code inaexpire) , itakuja muamala unaotaka kukatwa hiyo elfu 10000 chini kuna sehemu unaingiza namba ya siri yako ya tigo pesa halafu unaclick Confirm itatokea hatua ya mwisho hapo chini then unaendelea kujaza programes unazotaka.
IMG_20170731_005546_602.jpg
IMG_20170731_005644_854.jpg
IMG_20170731_011345.jpg
IMG_20170731_011212.jpg
IMG_20170731_011119.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
!
!
Aisee.... Hatari Sana. Ila ni chuo cha ubabaishaji sana kile. Uwekezaji mkubwa kama ule huku ukitegemea wanafunzi wa Loan board ni sawa na kufuga mbwa kwa kutegemea Mavi ya walevi.
 
hatua zi
Hiyo fedha hujalipa kwa mfumo wa udahili bali imeenda kwa mwenye hiyo namba,ukifuata hatua ulizoelekezwa kwenye dashboard utaona hatua zifuatazo hapo chini,uki click hatua inayofuata unaingiza namba yako ya tigo yenye fedha 10000tsh. Wakati huohuo utatumiwa code no. kwenye hiyo namba yako utaingiza hiyo code no. katika hatua inafuata na click next(katika hatua hii unatakiwa kuwa mwepesi kwani ndani ya dk. 3 code inaexpire) , itakuja muamala unaotaka kukatwa hiyo elfu 10000 chini kuna sehemu unaingiza namba ya siri yako ya tigo pesa halafu unaclick Confirm itatokea hatua ya mwisho hapo chini then unaendelea kujaza programes unazotaka. View attachment 554404View attachment 554407View attachment 554408View attachment 554410View attachment 554411

Sent using Jamii Forums mobile app
hatua hizo hizo ndizo nilizozifuata niliandika namba yangu ikakata yenyewe, ila nilifanya kipindi ambacho ada ni 30,000/= sasa baada ya ada kushushwa ile pesa niliyotuma inaonekana kama haijatumwa ikabidi niombe statement kutoka tigo pesa ndipo nikaipata hiyo namba ya simu,
 
Unapigaje simu weekend watu tumepumzika.

Piga siku za kazi uone kama hutasikilizwa

Sent using Jamii Forums mobile app
wakati nafanya usajili kulikuwa na tatizo la matokeo ya kidato cha nne 2014 nilipiga simu kutwa nzima sikubahatika kupokelewa mpaka tatizo likatatuliwa siku kadhaa baadae, na ilikuwa week days,
 
nil
Hiyo fedha hujalipa kwa mfumo wa udahili bali imeenda kwa mwenye hiyo namba,ukifuata hatua ulizoelekezwa kwenye dashboard utaona hatua zifuatazo hapo chini,uki click hatua inayofuata unaingiza namba yako ya tigo yenye fedha 10000tsh. Wakati huohuo utatumiwa code no. kwenye hiyo namba yako utaingiza hiyo code no. katika hatua inafuata na click next(katika hatua hii unatakiwa kuwa mwepesi kwani ndani ya dk. 3 code inaexpire) , itakuja muamala unaotaka kukatwa hiyo elfu 10000 chini kuna sehemu unaingiza namba ya siri yako ya tigo pesa halafu unaclick Confirm itatokea hatua ya mwisho hapo chini then unaendelea kujaza programes unazotaka. View attachment 554404View attachment 554407View attachment 554408View attachment 554410View attachment 554411

Sent using Jamii Forums mobile app
ipewa code number kila kitu kama wewe
 
Jamani nauliza aliyefanikiwa kuapply SUA maana mimi inanikatalia. Nimewapigia simu wanadai computer ninayotumia haiko vizuri! Nikawajibu kuwa sijatumia moja bali nimejaribu na zingine, wakasema ni logout kisha ni login. Nikawaambia nimefanya hivyo wakakata simu. Aliyefanikiwa tafadhali anijuze jinsi alivyofanya.
 
[emoji95][emoji95]TAARIFA[emoji95][emoji95][emoji95] Nimefanya mawasiliano na Admission Office kuhusu tatzo la wale wote ambao Status za Applications zao ziko pending. Wameniambia kuwa Swala hilo linashughulkiwa lakin haimaanishi kuwa applications hazijafika. Wamesema application hzo znakuwa tayar zshawafkia. Isipokuwa swala la kuondoa hyo pending ndo inashughulkiwa. Kwahyo wanawaondoa hofu wale wote ambao status zao znasoma pending kuwa applications zao zmeshapokelewa na swala la neno pending kuondoka linashughulikiwa. Asanten na pole kwa usumbufu. Karibuni UDOM, WE EMBRACE THE KNOWLEDGE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilifanya online application UDOM na kulipia 30,000 kupitia tigo pesa (kutoka kwenye namba 0********6 kwenda namba +25565101101 muamala wa tarehe 24/07/2017 ) na waka confirm kwamba pesa imeingia hivi sasa nikiingia wananiandikia application pending payment kwamba bado sijalipia na natakiwa kulipia Tsh 10,000 tena. Ukiwapigia simu kwenye namba zao za customer support hawapokei, angalao basi wangeweka e-mail tuweze kuwasiliana nao.
Pole kjana mwenzangu kumbe wahanga tuko wangi ,hata mm nili- apply trh 25/7 nikalipia 30000 but mpaka now iko pendng na ukiwapgia simu wanasema nisubir itakubali yaaan niaamua nije nilipe tena maana sina jins

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitu cha ajabu sana ni kupenda kukimbia ilihali unaichukia miguu.

Nimejaribu kufuatilia nilichokiona ni kuwa wanafunzi wanalalamika sana mitandaoni kuhusu kadhia za kuomba vyuo mwaka huu. Si UDOM tu, ni vyuo vyote vilivyokimbilia katika "online application system".

Miaka fulani nyuma utaratibu ulikuwa hivi (kuomba moja kwa moja vyuoni, hakukuwa na uombaji kupitia TCU), lakini kwa kuwa ilikuwa ni hardcopies (unatafuta form, unajaza na kutuma posta) haya malalamiko hayakuwapo. Hatupingi "Online Application system" maana ndiyo ukuaji wa teknolojia, la hasha, ila namna hivi vyuo vimeshindwa kutoa taarifa kuhusu malalamiko ya waombaji ndiyo imekuwa kizungumkuti!

Watu wanalalamika simu hazipokelewi, kero ya kuchwa nzima toka systems za maombi zifunguliwe! Hivi walishindwa hata kutengeneza pages (katika mitandao ya kijamii) kujibu malalamiko haya, kama simu zimewashida. Ajabu ni kuwa malalamiko ni yaleyale (anachokiulizia leo muombaji A ndicho hikohiko atauliza B), hata hayagharimu muda mrefu kuyajibu.

Yaani unaanzisha "Online Application System" wakati wewe mwenyewe hutaki kuwa "Online" lol!!
 
Yale yale-leo 01/08/2017 mwanangu amekula application pending payment. 10000 ikaliwa akaona ajaribu tena kumi nyingine ikaliwa. Sasa hapa tunarepoti UDOM au TIGO?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom