IJUE Higher learning Student suport Fund..(HLSSF)

kakamukubwa

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
203
27
UTANGULIZI.
Website: www.hlssf.org; e- mail: info@hlssf.org
Contacts: +255 717 488
745/765 420 512. Telephone: +255-(0)
222183709. Fax: +255-
(0)222183710. HLSSF ni NGO ambayo
ilisajiriwa tarehe 30/10/2008
chini ya Wizara ya maendeleo
ya jamii,jinsia na
watoto.Ilipata usajiri namba
00NGO/00002621.

SWALI: Je, HLSSF inatoa huduma gani kwa ujumla? JIBU: HLSSF inatoa huduma zifuatazo kwa kifupi;

I. Inatoa mikopo kwa wanafunzi
wa elimu ya juu kwa ajili ya
kuwasaidia kulipa
karo,kununua chakula,kulipia
gharama za malazi,kununua
vitabu na kufanya utafiti pamoja na mafunzo kwa
vitendo.

II. Inawatafutia scholarship za
kusoma ndani na nje ya nchi
wanafunzi wote ambao
wanasifa za ufaulu stahili
kadiri ya masharti ya
wafadhili.

III. Inawatafutia kazi wahitimu
wote wa vyuo vikuu.Hii
inafanywa kwa
kuwakutanisha wahitimu na
waajiri kadiri ya fani zao.

IV. Inatoa fursa ya kuwasaidia
wahitimu wa vyuo na vijana
wengineo wanaotaka kujiajiri
katika fani za kisomi zaidi.Hii
itafanikiwa kwa kuanzishwa
kwa HLSSF ENTREPRENEURSHIP CLUBS kwenye vyuo
mbalimbali nchini ambapo
wanafunzi wanachama wa
HLSSF watakutanishwa
pamoja na kuweza kuandaa
michanganuo bora.Hii michanganuo itatafutiwa
mitaji na HLSSF ili kikundi
husika cha wanafunzi
waweze kuanzisha na
kuendesha rasmi biashara yao.

V. Kufanya utafiti juu ya
matatizo mbalimbali
yanayoikumba sekta ya elimu
nchini;pamoja na kutoa
mapendekezo kwa serikali juu
ya uboreshaji wa sera husika.

VI. Kuendesha workshops,events
na mafunzo mbalimbali
yanayolenga kuwapatia elimu pana zaidi wafanyabiashara
na wanafunzi juu ya maswala ya ujasiriamali, uongozi wa biashara, upatikanaji na
uboreshaji wa mitaji,risk
management,changamoto za soko huria n.k

II. Kutoa ushauri kwa wanafunzi
wa sekondari na vyuoni juu ya namna ya kufanya uchaguzi sahihi wa michepuo ya
kusoma pamoja na kozi
muafaka za kusoma kulingana na changamoto za ajira za sasa.

III. Kutoa msaada wa kufanya
maombi ya vyuo kwa njia ya
mtandao(TCU ONLINE
APPLICATIONS) pamoja na
kufanya maombi ya mkopo wa BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU (HESLB) kwa njia ya
mtandao (HESLB LOANS ONLINE APPLICATIONS).

SWALI: Je,Uanachama wa HLSSF unapatikanaje?
JIBU: Uanachama wa HLSSF unapatikana kwa kufanya
maombi ya uanachama.

Maombi haya
yanafanywa kwa kujaza fomu
za uanachama kulingana na
kundi lako husika;pia inabidi ulipe gharama ya uanachama
kadiri ya kundi lako husika.Pia
ambatanisha bank deposit slip
ya malipo yako pamoja na
fomu ya maombi iliyojazwa na
kubandikwa picha na kuituma kwenye sanduku la posta la
HLSSF au kuileta ofisini kwetu.

SWALI: Uanachama wa HLSSF uko wa aina ngapi?
JIBU: Uanachama wa HLSSF uko wa aina nne.Zifuatazo ni
aina za uanachama:

I. Uanachama wa mwanafunzi
wa sekondari.

II. Uanachama wa mwanafunzi
wa chuo kikuu

III. Uanachama wa mzazi/mlezi
wa mtoto aliye mwanafunzi.
IV. Uanachama wa taasisi isiyo ya
serikali,kampuni au chuo
kikuu.

SWALI: Ada za uanachama ziko vipi? Je, zinalipwa mara
ngapi? JIBU: Ada za uanachama ni kama ifuatavyo:

I. Ada ya uanachama wa
mwanafunzi wa sekondari na mwanafunzi wa chuo ni
Tsh.10,000.

II. Ada ya uanachama wa mzazi/
mlezi wa mtoto aliye
mwanafunzi ni Tsh.50,000.

III. Ada ya uanachama wa taasisi
isiyo ya serikali,kampuni au
chuo kikuu ni Tsh.100,000. ADA hizi zinalipwa mara moja
tu;pale ambapo mwanachama
anajiunga na HLSSF.

SWALI: Kuna michango ya mwanachama au la?Kama
ipo,Je ni ya aina gani? JIBU: Ndio kuna michango ya wanachama ya aina
mbili.Michango hii ni kama
ifuatavyo:

1.Michango ya mwisho wa
mwaka.Michango hii
inategemeana na aina ya
uanachama kama ifuatavyo: Mwanafunzi wa sekondari
atalipa Tsh.20,000. Mwanafunzi wa chuo atalipa
Tsh.30,000. Mzazi au mlezi wa wanafunzi
atalipa Tsh.80,000. Taasisi ya serikali,kampuni au
chuo kikuu kitalipa
Tsh.200,000. NB: Hii ndio michango itakayo
mtabulisha mwanachama
husika kuwa ni “active
member of HLSSF”.

2.Michango ya kila mwezi .Hii
ni michango itakayofanyika
kila mwezi kwa kiwango
kitachoafikiwa na
muhusika.Hii ni michango
itakayofanywa na wazazi au walezi wa wanafunzi wa
sekondari au chuo kwa lengo la kuwawezesha watoto wao kulipa gharama muhimu za chuo kwa miaka
ijayo.

Kulingana na makubaliano HLSSF
itamuongezea mwanachama
kiasi cha pesa kulingana na
michango yake ya kila mwezi
pamoja na mda wa kuchangia
pindi tu atakapo taka kupata pesa hizo kwa ajili ya kusomesha mwanae.

Mahesabuya kiasi cha nyongeza kitakavyo patikana ni kama
ifuatavyo
( ORDINARY ANNUITY REFERENCE): Ordinary annuity ni michango inayofanyika kila mwisho wamwezi.Kuna aina mbili zamahesabu;yale ya kutafuta thamani ya michango kwa
kipindi kijacho ambayo
imewekezwa kila mwisho wa mwezi.Kupitia haya mahesabu
ndo itawezekana kukokotoa
kiasi cha pesa kama ongezeko
la faida/support
atakayoongezewa
mwanachama kulingana na riba itakayokuwa imepangwa.

What Are Annuities? Annuities are essentially series
of fixed payments required
from you or paid to you at a
specified frequency over the
course of a fixed period of
time. The most common payment frequencies are
yearly (once a year), semi-
annually (twice a year),
quarterly (four times a year)
and monthly (once a month).
There are two basic types of annuities: ordinary annuities
and annuities due. Ordinary Annuity : Payments are required at the end of each
period. For example, straight
bonds usually pay coupon
payments at the end of every
six months until the bond's
maturity date. Annuity Due : Payments are required at the beginning of
each period. Rent is an
example of annuity due. You
are usually required to pay
rent when you first move in at
the beginning of the month, and then on the first of each
month thereafter. C = Cash flow per period
(michango ya kila mwezi)
i = interest rate (riba ya
mchango kwa mwezi)
n = number of payments (idadi
ya michango) FV ordinary annuity: thamani
ya pesa ya baadae ya annuity
due.Annuity due ni michango
ya pesa inayofanywa kila
mwanzo wa mwezi.Kanuni
iliyo hapo juu ndio inayotumika katika kupata
thamani ya baadae kwa
kipindi maalumu kijacho
inayofanywa kila mwanzo wa
mwezi. SWALI: Je,Mwanachama atapata faida gani kutoka
HLSSF? JIBU: Faida(Benefits) zinatofautiana kulingana na
aina ya uanachama na
viwango vya
michango.Makundi ya benefits
ni kama ifuatavyo: Mwanachama active;
mwanafunzi wa sekondari
atapewa kipaumbele katika
kupata mkopo wa masomo
kutoka HLSSF pindi aingiapo
chuo;pia atapata fursa ya kupewa scholarship ya kusoma
ndani na nje ya nchi. Mwanachama active;
mwanafunzi wa chuo
atapewa kipaumbele katika
kupata mkopo wa masomo
kutoka HLSSF, kupata fursa ya
kutafutiwa ajira;pamoja na support za kupata pesa za
mtaji kwa wale watakaotaka
kujiajiri. Mwanachama active; mzazi au
mlezi wa mtoto aliye
mwanafunzi atampa fursa
nzuri kwa mwanae kupata
msaada mkubwa wa kulipiwa
gharama za masomo ya chuo. Mwanachama active,kampuni/
taasisi isiyo ya serikali au chuo
kikuu atapata fursa ya
kufanya projects na HLSSF
pamoja na kuwa partner na
HLSSF katika mambo muhimu ya jamii kwa ujumla. SWALI:Kuna namna ngapi za uanachama? JIBU: Kuna aina mbili za uanachama.Uanachama wa
mtu aliye active na ule wa mtu
asiye active.Hivyo basi kuna
active members and passive
members.Active members ni
wale ambao wanalipa michango ya mwaka na
wanashiriki katika
mipango,vikao na shughuli
mbalimbali zilizopangwa kwa
ajili ya kufanikisha utekelezaji
wa malengo ya HLSSF.Passive member ni yule mwanachama
wa HLSSF ambaye bado halipi
pesa za michango ya mwisho
ya mwaka,hashiriki katika
shughuli maalumu atakazo
pangiwa na uongozi wa HLSSF. SWALI:Ni vigezo gani vinaangaliwa kwa ajili ya
kupewa mkopo? JIBU: Vigezo/Sifa hizi ni: Uwe raia wa Tanzania. Uwe mwanachama wa HLSSF. Uwe umefanya maombi ya
mkopo pamoja na
kuambatanisha nakala zote
zilizotajwa kwenye fomu. Bandika picha yako kwenye
fomu za uanachama na fomu
za mkopo. Lipa Sh.10,000 kwa ajili ya ada
ya uanachama;pia lipa
Sh.20,000 kwa ajili ya maombi
ya mkopo.Malipo yote
yafanyike kwenye akaunti
zilizotajwa kwenye fomu husika.Hakikisha
unaambatanisha original
deposit slip ya malipo yako
kwenye fomu husika. Mkopo utatolewa kwa wale tu
watakao kuwa na ushahidi wa
kwamba wamepata udahili
katika chuo chochote nchini
kinachotambulika kisheria
kwamba kinatoa elimu ya juu. Tuma maombi yako kwa njia
ya EMS au posta kwa: MKURUGENZI MKUU, HIGHER LEARNING STUDENTS
SUPPORTING FUND, UHURU STREET-KARIAKOO
AREA, P.O BOX 41866, DAR ES SALAAM. Hakikisha umejaza maelezo
yote muhimu yaliyoulizwa
kwenye fomu kwa kuwa
yatatumika kufanya tathmini
ya kupewa mkopo. Kipaumbele ni kuwapa mkopo
wale ambao hawatapewa
mkopo na bodi ya mkopo ya
serikali (HESLB). Wale wanaotaka kusoma
diploma,digrii ya kwanza
watapewa kipaumbele katika
mkopo huu. Wale wanaotaka kusoma
digrii ya pili,na PHD
watafanyiwa mpango wa
kupata scholarship za ndani na
nje ya nchi.Wachache
watapewa mkopo wa HLSSF. Wafanyakazi;hususani wa
serikali nao wanashauriwa
kuomba mkopo kwa kuwa
wao wanadhamana ya
mshahara kupitia salary slip. Kwa kipindi kijacho wale
watoto wa wanachama wa
HLSSF kupitia EDUCATION
INSURANCE SYTEM ya HLSSF
watapewa kipaumbele katika
kupata mkopo wa HLSSF kwa kuwa watakuwa
wanadhamana ya michango
yao ndani ya mfuko wa HLSSF. Kwa mwaka huu wa masomo
2012/2013; mwisho wa
maombi ya mkopo wa HLSSF ni
tarehe 30/10/2012. SWALI: Ofisi za HLSSF zinapatikana wapi? JIBU: Ofisi za HLSSF zinapatikana kwenye mtaa
wa UHURU karibu na makutano
ya barabara ya Lumumba na
Uhuru; jengo linatazamana
karibu na kituo cha
kujaza mafuta GAPCO. Jengo linaitwa CALIST TOWER, PLOT
NO 16, BLOCK 75, ghorofa ya TISA (9 th FLOOR). Office secretary wetu anaitwa
DEVOTHA KILEO; namba yake
ya simu ni +255 714 366 281.
Endapo hautamkuta ofisini
wasiliana nae kwa simu yake
ili aweze kuja kuwahudumia. Telephone: +255-(0) 222183709. Fax: +255-(0)222183710. SWALI:Mikopo itatolewa lini? JIBU:Mikopo itatolewa baada ya vyuo mbalimbali nchini
kutangaza wale waliopata
udahili katika vyuo husika.Pia
baada ya bodi ya mikopo ya
HESLB kutoa list ya wale
waliofanikiwa kupata mikopo kutoka katika bodi hiyo
(HESLB). SWALI:Je,maombi ya uanachama wa HLSSF yana
mwisho/deadline? JIBU: Maombi ya uanachama wa HLSSF hayana
mwisho;yanafanyika wakati
wowote wa kazi katika
kipindi chote cha mwaka. SWALI:Nini umuhimu wa uanachama wa mwanafunzi
wa sekondari ndani ya HLSSF? JIBU:Mwanafunzi wa sekondari anatakiwa kuwa
mwanachama wa HLSSF ili
aweze kutoa taarifa zake
mapema juu ya masomo yake
katika ngazi ya
sekondari.Taarifa hizi zitatumiwa na HLSSF ili
kuandaa mchakato wa
kutafuta scholarship kwa ajili
ya hawa wanafunzi pindi
wamalizapo kidato cha
sita.Pia itatoa fursa kwa hawa wanafunzi kuwa katika nafasi
nzuri ya kupata mkopo wa
HLSSF pamoja na kusaidiwa
katika kupewa ushauri wa
kozi za kusoma vyuo
vikuu,pamoja na kufanya maombi ya udahili TCU kwa
njia ya mtandao;pia kupata
msaada wa maelekezo juu ya
namna ya kuomba mkopo wa
HESLB kwa njia ya mtandao. SWALI: Fomu za uanachama na zile za maombi ya mkopo
zinapatikana wapi? JIBU: Fomu za mkopo na zile za uanachama zinapatikana
kwenye tovuti yetu ya www.hlssf.org. ziko kwenye homepage ya tovuti au
kwenye kipengele cha
admission au kile cha
download application form. SWALI:Wanafunzi walio vyuoni(continuing students)
wajaze fomu gani za maombi
ya mkopo? JIBU:Wanafunzi walio vyuoni wanatakiwa kujaza fomu
zilizoandikwa kwenye tovuti
yetu kama “HLSSF LOAN FORM
FOR MATURE ENTRY”. SWALI:Wanafunzi waliomaliza kidato cha sita na
wanajiandaa kuingia vyuoni
wanatakiwa kujaza fomu gani
za maombi ya mkopo? JIBU: Wanafunzi waliomaliza kidato cha sita na
wanajiandaa kuingia vyuoni
wanatakiwa kujaza fomu
zilizoandikwa kwenye
mtandao wetu kama
“APPLICATIONS OF LOANS FOR UNDERGRADUATE STUDIES OF
2012/2013. SWALI:Je,wanafunzi wanaoomba udahili kupitia
mature entry program;pamoja
na wale walioingia vyuoni
kupitia mature entry program
wajaze fomu gani? JIBU:Wanafunzi wanaoomba udahili kupitia mature entry
program pamoja na wale
walioingia vyuoni kupitia
mature entry program
wanatakiwa wajaze fomu za
maombi ya maombi ya mkopo inayoitwa kwenye tovuti yetu
“LOAN FORM FOR MATURE
ENTRY”. SWALI:Je,kuna riba kiasi gani inayotozwa kwenye mkopo
wa HLSSF? JIBU: HLSSF haitozi riba ya aina yoyote ila inatambua
ongezeko la thamani ya
mkopo wa HLSSF
itakayotokana na kushuka
kwa thamani ya pesa ya
Tanzania;shilling,mabadiliko ya kiuchumi pamoja na
changamoto la soko la fedha la
kimataifa.Hivyo
basi,kutakuwa na mahesabu
ya thamani ya mkopo
utakaorudishwa kama ifuatavyo: So, the following will be the
calculation for future value of
the loan for one who wants to obtain loan from
HLSSF. Future Value of Loan = Lo + Lo *r *t Whereby: t: number of years taken to repay the loan. r: annual estimated financial markets fluctuation rate. Lo: This is the amount of loan presently borrowed. Future value of loan: This is the value amount of loan to be repaid after t years period. For example: If a student receives a Tsh.2 million loan from HLSSF in the academic year 2012/2013; he/ she takes two years to start repaying the loan; while the estimated annual market fluctuation rate is 8%; then the following student will have to pay the following loan after two years. See the calculation below: Lo: Tsh.2,000,000. r: 8% t: 2 years Future Value of loan to be paid after 2 years is = 2,000,000 + 2,000,000*8%*2 = 2,000,000+ 4,000,000*0.08 = 2,000,000 + 320,000. = Tsh.2,320,000. For those who will receive HLSSF loan in the academic year 2012/2013. NOTE: We don’t have interest rates. We have just recognition of market Fluctuation cost as described above.So, just take into consideration of the formula above. Repayment of loan. The repayment of loan will be done on monthly basis. The calculation for the amount is as follows. Amount to be repaid = 10% * monthly basic salary. For example: Consider the example of the loan taken by a student in the above question. This student will start paying the loan after 2 years and the Future value of the loan to be repaid is already calculated as shown above.
 
jamani kuweni makini na hii taasisi.
msikubali kutoa pesa zenu za form bila kuwatembelea hawa jamaa ofisini kwao kujidhihirishia wenyewe kuridhika na huduma wanayosema wanaitoa.
mimi binafsi sina imani nao na nnachokiona hapa ni kutumia panic ya wanafunzi wanaohaha kukosa mkopo ili kujipatia kipato. imagine 20000 x 1000 students ni kiasi gani wanakiingiza mfukoni,. then wanaingia mitini kama deci. ...wanasema wamepata usajili tangu 2008..jiulizeni walikuwa wapi siku zote...jamani kuweni makini nembo yenyewe tu ya kampuni inaonesha hawa watu hawako serious. iyo huduma kwa wateja ni ya ajabu.. me nahisi huu ni mradi wa watu .ndugu zangu wanafunzi lengo langu hapa sio kuwakatisha tamaa najua mnapitia katika hali gani ivi sasa baada ya kukosa mkopo..ila nawaomba tu kuweni makini kabla hamjachukua hatua
 
Hawa watu inabidi wajipange vzr kwa utapel coz ukijaribu kutress asasi wizara iliyosajiriwa hata kama hujaenda darasani inatia mashaka! Hilo jengo wanalodai wapo ni hotel ndo inaitwa calista tower hotel na ni ofisi gani ambayo haina nata sample ya foam yenyewe ya mkopo coz mimi nlifika hapo na nlimuomba huyo secretary wao foam akadai hata yeye hana pale ziko kwenye mtandao! pili nikamuuliza ofisi yenu mpaka sasa ina historia ya kusaidia wanafunzi wangap akananijibu hajui idadi kamili! ,tatu nikamuuliza je mnau shirikiano na Tcu na Helsb akahamaki kidogo na mwisho akasema kwa kiasi kidogo wanashirikiana basi mimi na jamaa zangu tukasepa mdogomdogo huku kila mtu akiwa na mtizamo tofauti. Hio ndo situation nliyoikuta na kuiona
 
Mkuu naungana na wewe cause wale jamaa ni wasanii. mi mwenyewe jana nilifika maeneo yale lakini kwa mazingira ya ile ofisi hakika ni changa la macho. Na mimi niliuliza wale walioomba mkopo mwanzoni mbona majina yao hayaonekani mtandaoni? wakanipa jibu ambalo sikulielewa kwa kweli na mbaya zaidi mpaka sasa wanapokea maombi ya mkopo na matokeo ya wanaomba sasa ni mwezi wa kumi na moja na vyuo vinafunguliwa mwezi wa kumi.

 
Mkuu naungana na wewe cause wale jamaa ni wasanii. mi mwenyewe jana nilifika maeneo yale lakini kwa mazingira ya ile ofisi hakika ni changa la macho. Na mimi niliuliza wale walioomba mkopo mwanzoni mbona majina yao hayaonekani mtandaoni? wakanipa jibu ambalo sikulielewa kwa kweli na mbaya zaidi mpaka sasa wanapokea maombi ya mkopo na matokeo ya wanaomba sasa ni mwezi wa kumi na moja na vyuo vinafunguliwa mwezi wa kumi.


walikujibuje mkuu?
 
Back
Top Bottom