Hembu tuangalie kwa sasa elimu,afya,ajira ni kundi lipi lipi lipo katika hali bora ukilinganisha na jingine?ni wazi kuwa waislam wapo nyuma katika mambo yote yaliyotajwa,mpaka mkapa kuwaonea huruma kuwa chuo walau kimoja morogoro.Hivyo udini kanisa unaolalamikia ni kejeli,kebehi,kuwasanifu waislam wajione wanafaidi na matunda ya uhuru walioupigania toka kwa muingereza na kumkaribisha nyerere kuongoza na baadae kuachwa solemba kwa kuundiwa chombo kisicho na tija kwao bakwata.
Bongolala, Unaweza kutuambia ni sehemu gani Tanzania ambako huduma za afya zinatolewa kwa Wakristo na watu wa imani nyingine kasoro Waislamu tu? Unaweza kutoa mifano ya shule ambazo zinabagua watu kwa dini? Unahitaji kupata taarifa sahihi kabla hujapandikiza mbegu za chuki kwa watu wengine dhidi ya ukristo.
Ajira zinategemeana na taaluma ya mtu. Mtu hawezi kuajiriwa kuwa pilot ama daktari kama hana taaluma hiyo. Taaluma hizo zinafundishwa vyuoni baada ya mtu kuwa na msingi wa elimu husika katika shule. Historia inatuambia elimu hizo zililetwa na wageni hapa kwetu. Walikuja waMissionary ambao ni waasisi wa dini unayoionea wivu ya Kikristo wakaeneza elimu ya dini pamoja na kujenga shule nyingi za mission ambazo zilikaribisha watu wa dini zote bila ubaguzi. Ndiyo maana utaona viongozi wengi wazee sasa waislamu watakuambia walisoma shule za mission.
Wakaja waarabu kufanya uchuuzi wa mali na binadamu (binadamu hao weusi walipofikishwa huko uarabuni inasemekana walikuwa wakihasiwa na baada ya utumwa kwisha waliuliwa maana hawakuwa na faida tena kwa mwarabu). Walichokifanya ni kile ambacho kilikuwa katika upeo wao wa kufikiri na kuelewa. Walianzisha madrasa (sijui yanaitwa hivyo) maalumu kwa elimu kwa waislamu. Wanachosomesha huko wewe unakielewa. Sasa wewe umesoma hadi mlango wa tatu kwenye shule hizo, ukagraduate, halafu leo unataka tukuajiri kama mchumi wa taifa! Inawezekana kweli? Acheni propaganda hizo na malalamiko yanayozidi kuwaonyesha ninyi ni watu wa aina gani. Wekezeni katika elimu sahihi ndipo mdai equality katika employment.
Unasema et waislamu wako nyuma kielimu. Kutokusoma kwenu ni tatizo la Wakristo? Kuna shule zenye ubaguzi wa kidini hapa zaidi ya shule za kiislamu? Ama unataka Wakrito wapite nyumba kwa nyumba wakiwafunga kamba waislamu na kuwakokota hadi shuleni? Badilisheni mtazamo. Msilaumu wa Kristo kwa mambo ambayo mmeyajenga wenyewe kwa imani yenu potofu ya kujibagua na kubagua wengine.
Hapa habari ni kwamba udini ulianza wakati wa Ally Hassan Mwinyi kwa sababu aliruhusu waislamu kutafuta equality kwa kuhujumu Ukristo. Ndiyo hoja. Na hadi sasa JK anataka kuingiza nchi katika vurugu za kidini kwa sababu hana uwezo wa KUADRESS MATATIZO HALISI YA WATZ.
WATANZANIA, TUKATAE CCM KUTUGAWA KWA MISINGI YA DINI. TUUNGANE PAMOJA NA KUDAI HAKI ZETU IKIWA NI PAMOJA NA KUWAJIBISHWA KWA MAFISADI, KATIBA MPYA, KUDHIBITI UBADHILIFU WA RASRIMALI ZETU. KATU TUSIKUBALI KUZUBAISHWA NA HILA ZA ANGENDA YA UDINI. UDINI AMBAO JK NA CCM YAO NDIO WAASISI WAKE . TUSIKUBALI KUGOMBANA KWA MISINGI YA UDINI PROPAGANDA ZA CCM NA KIKWETE.
TUSHIKAMANE KWA PAMOJA KUPINGANA NA HAWA WATAWALA NA MAMLUKI WANAOTAKA KUTUGONGANISHA KW A SUALA LA UDINI HUKU MAMBO Y A MUHIMU KAMA KUWAWAJIBISHA MAFISADI KINA LOWASA, ROSTAM, JK CHENGE NK, KUSIMAMIA MASLAHI YA WATZ KWA UAMINIFU NA UADILIFU, KUWAFICHUA WAHALIFU KAMA WAHUSIKA WA DOWANS NA DOWANS MWENYEWE ILI WAWAJIBISHWE, KUBORESHA ELIMU, KUONGEZA UZALISHAJI KATIKA SEKTA MBALIMBALI KATIKA KIPINDI HIKI CHA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI, NA MASUALA MBALI MBALI YA DEMOKRASIA NA UTAWALA BORA YAKIWA YAMEFUMBIWA MACHO.
SISI NI WATOTO WA MAMA MMOJA. TUSIKUBALI KUGOMBANA NA KUUANA ETI KWA SABABU YA DINI NA RASLIMALI. OIC WALA KADHI HATAONDOA UJINGA, UMASKINI, MARADHI NA MATATIZO TULIYONAYO WATANZANIA. TUONDOKANE NA UJINGA KWAMBA PENGINE NCHI IKIWA Y A KIISLAMU AMA IKISAJILI KADHI SHIDA ZITAISHA. HAKUNA!!.
JIBU NI KUBADILISHA MFUMO WA UNYONYAJI NA UTENDAJI MBOVU AMBAO UMEDUMU KWA MIAKA HAMSINI SASA HUKU SOTE TUKISHUHUDIA HALI YA NCHI IKIZIDI KUDIDIMIA SIKU HADI SIKU. TATIZO LA YOTE NI KUAMUA KULETA MABADILIKO HALISI. VIZAZI VYETU VITATUKUMBUKA. LA SIVYO TUTAISHIA KUUANA SISI WANYONGE NA SHIDA ZETU ZIKIONGEZEKA HUKU JK NA MAFISADI WENZAKE WANAOHUBIRI UDINI KUPOTOSHA ATTENTION, WAKILA KUKU KWA MIRIJA KATIKA MA MANSION YAO WALIOJIJENGEA NCHI ZA NJE.
NIMESEMA.