Udini ulianza kipindi cha Mwinyi - CCT

Udini ulianza kipindi cha Mwinyi - CCT

Status
Not open for further replies.
Udini haukuwepo wakati wa Nyrere, ulianza wakati wa Mwinyi, ukaondoka wakati wa Mkapa, ukarudi wakati JK, utaondoka wakati wa ................, halafu utarudi wakati wa..................


Nafikiri ungekuwa sahihi kusema kuwa Waislamu walinyamazishwa na kuonewa wakati wa Nyerere na wakati wa Mkapa alishindwa kuukataa ukweli kuwa Waislamu ni sehemu ya Taifa(tena ni wengi) na wakati huu wa Kikwete ameachia uhuru wa kusema hivyo kiasi chenu kulalamikia ile neema iliyozimwa baada ya kuondoka Nyerere.
 
Mwiba naona hujui tofauti ya dini na udini unachozungumza wewe ni mafundisho ya dini, tunachojadili hapa hatupingi dini ya mtu na mafundisho yake, dini zilikuwepo hata kabla ya Mwinyi tunachosema dini iwe na mipaka yake isingie sehemu isipotakiwa mafano serikalini dini iishie makanisani na misikitini ikitoka nje unakuwa udini, mfano wa ile mihadhara ya miaka 80s na 90s ile ilikuwa si dini ulikuwa mwanzo wa udini dini moja kutukana dini nyingine.

Mwenzangu inaonyesha hujui dini au labda huna dini! Hivyo utetenganisha vipi dini na Serikali wakati Serikali si majumba bali ni watu?? Nini udini kwenu?? Eti Jk kumchagua mtu mwenye kwenda msikitini? Hivyo nyini hamwendi kuabudu? Ingekuwa JK kaanzisha madrasa Ikulu au katowamsaada kwa waislamu watupu basui tungesema anafanya udini lakini eti kachagua Muhamedi badala ya John huku huyu Muhamedi anazo sifa za nafasi ile huwezi kusema ni mdini pia akimchakua Peter badala ya Juma wakati Peter ana sifa hatuwezi kusema kuwa ni mdini.
Kuhusu mihadhara ya dini mbonatunavumiliana kwa vyama na klabu ? Hivyo iwa[po mimi nikikwambia CHADEMA si chama ndio itakuwa si chama wakati wewe mwenyewe unajuwa kuwa ni chama???
 
Bwana mdogo kua uyaone, au kama unadhani umekua basi tembea uyaone. Hiyo Rwanda ulioishikia Bango hivi sasa inamwelekeo mzuri wa kiuchumi kuliko Tz ya ccm lakini Somalia tangu1990's hadi leo ni umwagaji damu na allahu akbar kwenda mbele!!. Vipi huko pakistan, Sudan, nigeria misri afighanstan nk? Kuna kanisa au sharia? Bwana mdogo kaa chini utafakari jibu utalipata, usikurupuke kuwakilisha hoja
Eti Wamarekani nao wanasema ALLAHUAKBAR kule AFGHANISTAN au unatujuvya kuwa wanaipinga hiyo???
 
Nini role ya maimam,mashekh na mamullah kwenye mauaji yanayoendelea Somalia, Iraq, Iran, Pakistan,Timor,Indonesia na Afghanistan au unadhani hatujui?

Nafikiri hujafanya utafiti na kujua vyanzo vya yanayoendelea huko! Anza na Somali ni Mmarekani. Pakistani ni ukabila, Timor hakuna uislamu wa hivyo bali ni kundi kuoneya wengine kama ilivyokuwa kwetu. Afghanistani kuna Wamarekani . Sasa nini role ya hao watu unaowataja wewe/
 
Kama kuna tofauti kati ya uislam na vurugu basi naomba nifahamishwe. Binafsi naona ni kitu hicho hicho tu. Tatizo la waislam ni kuhisi kuonewa. Dini gani inayoongoza kwa kuwa na vikundi lukuki vya kigaidi!!!!

KWA HESABU ZA HARAKAHARA, UKRISTO UNAONGOZA KWA KUWA NA VIKUNDI VINGI VYA KIGAIDI MFANO:
Irish Republican Army (IRA), Loyalist Volunteer Force (LVF), Orange Volunteers (OV), Real IRA (RIRA), Red Hand Defenders (RHD), Sendero Luminoso (Shining Path), Tupac Amaru Revolutionary Movement (MRTA), Alex Boncayao Brigade (ABB), Army for the Liberation of Rwanda (ALIR), a.k.a. Interahamwe, Revolutionary United Front (RUF), Basque Fatherland and Liberty (ETA), TAMIL TIGERS, Khmer Rouge, Manuel Rodriguez Patriotic Front CHILE (FPMR), National Liberation Army (ELN)-Colombia, United Self-Defense Forces/Group of Colombia (AUC-Autodefensas Unidas de Colombia), Zviadists (GEORGIA), : Revolutionary Nuclei (RN) a.k.a. Revolutionary Cells (GREECE), Revolutionary People's Struggle (ELA), (GREECE), Morzanist Patriotic Front (FPM) (HONDURAS), Kach and Kahane Chai (ISRAEL), Aum Supreme Truth (Aum) a.k.a. Aum Shinrikyo, Aleph (JAPAN), Japanese Red Army (JRA) a.k.a. Anti-Imperialist International Brigade (AIIB), BILA KUSAHAU SPLA(SUDAN),JOSEPH KONI OF UGANDA (LRA), NA KIKUNDI KILICHOCHOMA MOTO KANISA NA WAUMINI WAKE ZAIDI YA 1000 HUKO UGANDA!!!!

SOURCE: Terrorism - Terrorist Organizations NA PIA SOMA HAPA Joseph Kony - Wikipedia, the free encyclopedia HALAFU UTASHANGAA WAKRISTO WEUPE KUCHOMA KANISA LA WEUSI GONGA HAPA: 3 charged in connection with blaze at black church - The Boston Globe
 
Nimetembelea Rwanda hadi katika Jumba la makumbusho ya Genocide unachosema kuhusu kanisa sio cha ukweli walikuwa ni individuls wachache waliojawa ukabila ndani yake Uhutu na Utusi ndiyo walihusika tena wakati walipokuwa wanakimbia askari wa Interahamwe kujificha kanisani,ghasia zote zimechochewa na Shehe simkumbuki jina lake na walikuwa na kituo cha redio falsafa yao ikiwa chinja hao wakristo ili Kagame akute majeneza kisa wengi wao ni wakristo.picha zipo katika makumbusho hayo hauruhusiwi kupiga picha katika jumba hilo ukitaka kuona athari za Udini na Ukabila tembelea Jumba hilo nadhani utapata ukweli zaidi kuliko kusoma katika makala za uongo.
Kinachofanyika hapa TZ ni sawa na kuchezea kaa la moto,najua wakubwa wakitembelea Rwanda hawapati nafasi ya kufika katika makumbusho hayo hata wakifika ni kwa muda tuu.na ulinzi mkali.hauwezi kusoma historia ya Genocide ya Rwanda.Nilipata nafasi kupitia kila maelezo na kusoma hitoria yote na ilinichukua muda wa masaa 5 kuweza kumaliza yote nilifanya hivyo tena kwa roho ngumu kwani mengine yanasikitisha kama hauwezi kuvumilia huwezi kumaliza.HAYA YA UDINI NA UKABILA YASIKILIZIE KWA JIRANI YAKO YAKIKUFIKA NI MABAYA SANA TENA YA KUTISHA YASIYOELEZEKA
Na mimi pia nilitembela Rwanda na kuona sehemu zote lakini pengine wewe hukubahatika kupelekwa kwenye makanisa ambapo mauwaji yalifanywa na cha kuonyesha uongo wako zaidi ni kuwa tayari tumeshashuhudia kesi za Mapadre waliohusika ama Masshehe kwa Rwanda bado hatujawaona bali tuinawaona kule sehemu ambazo wageni wwanaingilia maamuzi ya wenyeji.
.
 
.

Mwalimu alikuwa na kipaji cha kushawishi na hakuna Rais aliyetokea kufikia karama/kipaji chake. kama mwalimu alipewa nafasi ya kuongoza kuomba uhuru basi ni kwa sababu ya uwezo wake na si kitu kingine.Nafikiri ni busara kutumia neno kuomba uhuru kwa waingereza kuliko kupigania. Tanzania haikupigana kwa damu kama ilivyo kwa baadhi ya nchi.

Baraza la kwanza la uhuru lilikuwa na waislamu wa kutosha mchanganyiko na wakristo. Baraza hili ndio lilikuwa kama moyo wa kuwaandaa watanzania kuanza maisha yao baada ya kupata uhuru. baada ya muda nyerere alinyang'anya shule za mission/seminari na binafsi nyingi zaidi zilikuwa za wakristo ili kila mtanzania apate kusoma kwani aliamini urithi bora kuliko wote ni elimu lakini pia alijua kwa sababu ya historia wakristo walikuwa wamewaacha mbali ndugu zao waislamu.Jambo hili ni kama dogo lakini kama falsafa hii ya nyerere ingeonekana kwetu sote mengine yote yasingejitokeza kuzungumzia uhalisia wa tofauti za maisha baina ya waislamu na wakristo hata hilo la kuomba uhuru lisingekuwa la mjadala.
Nilitegemea ungetueleza kwanini hili hali ya mgawanyiko mzuri wa Mawaziri ulikuwa kwa baraza la mwanzo tu???
 
ameruhusu uhuru wa kuzungumza ili waislamu wapate upenyo wa kuzungumza pumba zao za kigaidi (oic na kadhi).

kwa hilo tuko macho.

Wewe Jerusalem ndio pumba nambari wani, kwasababu hujui unalosema,, angalia hizo quote zako hapo.
 
Udini hauwezi kuwepo bila kuwepo kwa dini mbili tofauti zinazovutana. Kule Rwanda wakatoliki walikuwa kwenye vita vya udini na dini gani? sijawahi kusikia kwamba kule rwanda kulikuwa ni vita ya ukristo na uislamu.

Katika masuala ya vita watu wenye dini wanakuwa na makabila yao pia. vita ya rwanda ilikuwa ya kabila baina ya watusi na wahutu.
Kwa maana hiyo Udini upo Tanzania tangu Uhuru au sivyo? isipokuwa sasa ndio tunasema upo eti kina Muhamedi sasa wanapewa madaraka ambayo tulishaamuwa kuwa watum wa dini ya pili tu ndio haki yao???
 
Wakristo wengi wanaridhia kwa moyo mmoja kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi ndani ya taasisi za kiislamu kama moja ya imani yao.

Nimaamini wakristo wengi hawapingi ndugu zao waislamu kuwa na mahakama ya kadhi kwa sababu mahakama za dini ya kikristo zipo lakini ziko ndani ya kanisa hazihusiani na mahakama za kiraia. Mahakama hizi zinahusu maisha ya kila siku ya mkristo ikiwemo ndoa. Migogoro ya ndoa za kikristo inaanzia kwanza kanisani na kwa kuwa kanisa halivunji ndoa likishindwa wahusika wako huru kwenda mahakama ya kiraia lakini wakati huo hukumu ya kanisa inabaki palepale ndoa iliyounganishwa na Mungu (kitabu kitakatifu cha Mungu) binadamu haruhusiwi kuitenganisha.

Mkristo anaoa tena kwa mambo matatu, kifo cha mwanandoa mmoja, kichaa kwa mwandoa mmoja, uzinzi kwa mwanandoa mmoja japo hili linaombewa msamaha kwanza kama wanandoa watakubaliana.

Hakuna mahakama isiyotambuliwa na sheria za nchi na kwa kulijuwa hili Waislamu hawako tayari kufanyiwa janja. Waislamu wanataka mahakama ilyo ndani ya sheria mama ya Taifa. Kama si tatizo kwenu basi Katiba iwe wazi kuwa uamuzi wa Mahakama ya Kadhi kwa masuwala ya Kiislamu yawe ya mwisho bila kuingiliwa na mahakama nyengine. Unajuwa kwanini ? Kwa Waislamu maamuzi ya Mungu hayawezi kutenguliwa na mwanaadamu, wenzetu mnakubali kuwa mahakama ya kiraia yana uwezo zaidi kuliko mahakama zenu(kama zipo). Inabaki ni haki ya Muislamu kujiamulia namna ya kuabudu, na mnaposema aabudu namna fulani mtakuwa mnamnyima haki hiyo
 
Hivi Jamani issue ni kuanzishwa Mahakama ya Kadhi au ni kwamba kinachogomba ni mahakama hizo kuwa sehemu ya gharama za serikali. Nafikiri kama ni jambo la Imani ni haki ya waislamu kuanzisha mahakama ya kadhi na kama wanauwezo wa kuindesha kupitia sadaka zao na michango mingine hilo ni Jema lakini pale inapotakiwa Serikali kupitia kodi zetu kubeba gharama ya Mahakama ya Kadhi hapo ndiyo linapokuja tatizo. Ikumbukwe walipa kodi wengine ni Wapagani,wengine Waislamu na wengine Wakristu sasa iweje leo kwa nchi isiyokuwa na dini igharimie gharama za chombo cha imani ya dini kama mahakama ya kadhi? ili nini? kwa fedha kutoka wapi?

Nafikiri hoja siyo kuwa au kutokuwa na mahakama ya kadhi,you can go ahead na kuanzisha lakini jukumu la gharama mbaki nalo wenyewe wenye mahakama yenu full stop.

Serikali haiwezi kuepuka gharama katika kutekeleza haki za watu wake. Hivyo unataka kusema kuwa pale mashirika ya dini yalipopiga kelele kwa kukataliwa misam,aha ya kodi ulikuwa udini? Pesa nyingi zinapotea kwa kusamehe mashirika ya dini , hivyo tuanze kupangiana kiasi fulani kitumike kwa Waislamu(misamaha) na kiasi fulani kwa dini nyengine? Au hili hilijuwi kama ni gharama???
 
Mwenyekiti wa CCT, Askofu Peter Kitula amesema tatizo la udini lilianza mwaka 1986 na hakuna kiongozi wa serikali aliyejitokeza kulikemea badala yake Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilizidi kufanya makosa kwa kuingiza suala hilo katika Ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2005.

“Kuanzia miaka ya 1986 kulianza kujitokeza mihadhara ya kidini na kidhehebu katika jamii ambayo hatukuwa tumeizoea lakini jambo hili halikukemewa wala kuchukuliwa hatua za kisheria".
Ilani ya uchaguzi ya CCM 2005 ilitamka bayana kuwa suala la Mahakama ya Kadhi litashughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi, ikumbukwe kuwa mahakama ya kadhi ni jambo la kidini na kiibada katika dini ya kisilamu, jambo hili ni kinyume cha Katiba ya nchi na sheria ya vyama vya siasa hakuna aliyeona hatari yake na kwamba litakuwa chanzo cha udini ndani ya siasa za Tanzania, “alisema.

Kwa maneno ya Kitula umefika wakati sasa tuache unafiki tuanze kuwataja kwa majina yao wote wanaohusika kulipeleka taifa kusiko bila kumng'unya maneno, kwa kuanzia nitaanza na Mwenyekiti wa NEC anakotupeleka siko. Ni ukweli mchungu.


ASKOFU KAPOTOSHA UKWELI! KWANI ALIYEANZISHA UDINI TANZANIA NI MKOLONI MZUNGU MKRISTO!

SOURCE: http://www.igs.net/~kassim/nasaha/044/044-10.htm NA ZAIDI KUHUSU UDINI TANZANIA GONGA HAPA: http://www.igs.net/~kassim/an-nuur3/292/292-10.htm
 
Maaskofu waja juu Mahakama ya Kadhi Friday, 17 December 2010 09:22 *Wadai waanzishe kwa fedha zao
*Waionya Serikali


Na John Daniel

MAASKOFU wameitaka Serikali kuzika mara moja suala la Mahakama ya Kadhi na kuagiza Bunge kutojadili suala hilo kwa kuwa lina madhara kwa umoja na mshikamano wa Taifa.Wakizungumza Dar es Salaam jana, Maaskofu wa
Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) wamesema kwa mujibu wa Katiba, Serikali au Bunge kujadili Mahakama ya kadhi ni kosa.

“Tukiona mambo yanaenda visivyo na sisi tukakaa kimya tutakuwa tunafanana na hao wanaoharibu. Suala la Mahakama ya Kadhi ni la kidini na kamwe halipaswi kuihusisha Serikali au Bunge,” alisema Askofu Valentino Mokiwa wa Kanisa la Anglikana.

Askofu Mokiwa ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCT alisema kimsingi suala la Mahakama ya Kadhi inapaswa kuwa la dini husika na si kuihusiha Serikali kwa maana ya kutumia kodi za Watanzania kuishuhulikia.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCT, Askofu Peter Kitula, alisema Serikali ilifanya makosa kujiingiza katika suala hilo wakati Katiba imeweka wazi kuwa hiyo siyo kazi yake.

Naye mjumbe wa Tume ya CCT Askofu Askofu Owdenburg Mdegella, alisema nchi inatakiwa kuendeshwa kwa mfumo ulioweka kisheria mama na si vinginevyo.Maaskofu hao waliweka wazi kushtushwa na hali ya udini iliyojitokeza nchini hususan wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita na kuitaka Serikali kurekebisha makosa hayo.

Walisema Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alitambua hatari ya Serikali kujihusisha na siasa hivyo kutengansha suala hilo na uongozi wa nchi.
Walisema Serikali imekaa kimya wakati suala la udini likiachwa liendelee kushamiri katika jamii, lakini madhara yake ni makubwa zaidi.

Waliwataka wabunge pia kuwa makini na kutokubali kupokea malipo ya kodi za wananchi kwa kujadili masuala ya kidini.

Source: Maaskofu waja juu Mahakama ya Kadhi

Itabidi waunde kisiwa chao kwani kilichowapa wao jeuri ya kuionya Serikali na wengine wanaweza kuwanayo pia. Ni nini Utaifa, kujiona kuwa wao ndio wenye haki peke yao au vipi? Wabunge walichaguliwa na watu wa dini zote sifikiri kuwa CCT ndio mwisho wa busara yao hapa!
 
Ah ah ahaaaaah! hivi kweli unauhakika wa unachokiandika? Usifuate bila kutafakari kila unachokisikia kwenye masjid. Anyway mtatafuta visingizio vya kila aina ili kujikosha lakini hali halisi inaonyesha kila penye uislam vurugu, fujo, mauaji ni kama kazi. Jee unajua kuwa Saudi Arabia ilikuwa nchi ya kikristo, je unajua kuwa wakristo waliokataa kulazimishwa uislam saudi arabia zama hizo waliuwawa. je unajua kuwa baada ya miaka kadhaa mifupa yao ilichukuliwa na wakristo wa misri na kwenda kuzikwa huko kwa sababu saudi arabia sasa ikiwa nchi ya kiislam ilikuwa haramu kuwa na makaburi ya wakristo? Mtaifanya Tanzania nchi ya kiislam kupitia ccm, OIC na sharia courts (mahakama ya kadhi) lakini balaa kwa vizazi vijavyo ni kubwa, litawala wote waislam kwa wakristo, of course wakristo zaidi maana wao ndo first target na baadae waislam wasiowaislam zaidi.
Unanivunja mbavu yakhe!!! Historia hiyo umeisoma wapi iliyokwambia kuwa Saudia ilikuwa nchi ya ukiristo?? Ama kweli usilolijuwa usiku wa giza kwani kwa kauli yako unataka kuufanya ukiristo kua ni ukafiri. Saudia ilikuwa nchi ya makafiri wakiabudia masanamu sasa iwapo huo ndio ukiristo basi sijui wakristo wenzio watasemaje iwapo unawabandika dini isiyo?
 
Ndugu yangu wewe ni muungwana, na muungwana yeyote ni vitendo, unaonekana hautawaliwi na jazba na ni mtu unaependa maelewano,lakini hapo kwenye RED si sawa mimi ni mtu makini sana, lakini kama ungefuatilia vizuri mimi nilichokiandika ni kwamba mimi na wewe mawazo yetu ni mamoja, mtu niliyemjibu, nimejibu na reply with quote, kwa sababu nia yake si njema na watu kama yeye ni chukizo kwa mwenyezi mungu, yeye hoja yake anataka kupotosha kwamba kanisa ndio lilihusika na GENOCIDE ya Rwanda kwamba sasa kanisa lote dunia nzima halifai, je wewe unaweza kumuunga mkono mtu mwenye akili mgando kama huyo?
ndio maana nimejaribu kuonesha mifano mingi kwamba hawa magaidi mambo wanayofanya je ni haki kusema uislamu ni dini ya kigaidi? hapa jibu lake si kweli.
mbona hawamtaji kibwetele wa uganda aliyedanganya waumini wake kwamba ni mwisho wa dunia, halafu akawafungia kanisani kwake na akawapiga kiberiti wote, je hapo utahusisha ukristo na mafundisho ya shetani?
mimi sio mfia dini na siamini kama dini itanipeleka katika ufalme wa mungu bali naamini ni matendo yangu ndio yatakayokuwa jugdement yangu kwa mungu wangu.
watu wote wanaoshabikia udini ni wapuuzi tu, tena wajinga wajinga tu.
Pengine ulikurupuka na hukufahamu vipi uhusiano wa Kanisa na Rwanda ulikuja. Ulikuja ili kuonyesha chokochoko hizi za CCT zinafanana na zile za Rwanda. Kule Rwanda ukabila ulijificha ndani ya kanisa na ukazua balaa kwa kutumia udhaifu wa binaadamu na imani na CCT wanachofanya ni kuchonganisha Waislamu na Wakristo na mifano tunayo humu ambapo Wakiristo wanalani hili. Lazima tukubali kuwa viongozi wa dini kuzungumzia makinzano si busara kwani kwa bahati mbaya tuna dini tofauti Tanzania.
 
visingizio tu, lakini ukweli ni kwamba uislam ulianza kwa vita na umwagaji damu, hata mtume wake alipigana na kuua na kuteka nyara, je hujui kuwa jambia lake lilijulikana kwa jina la "zulfikar" yaani "vunja shingo au uti wa mgongo". Mtoto wa nyoka ni nyoka, uislam umezaliwa kwa vurugu, umeenea kwa vurugu na utafanya vurugu hadi kiama itakapojulikana muuaji ni nani na mwokozi ni yupi. Unasema kuingiliwa na nchi za magharibu, je unajua ni kiasi gani iran inapandikiza ushia nchi mbalimbali au hela kiasi gani saud arabia inatumia kueneza uslam africa, europe, america nk, unajua nani anasponsor misikiti inayoota kama uyoga duniani kote hivi sasa? je unajua nani ana sponsor al qaida, taliban, al shabab kama siyo saud arabia, je unajua northern nigeria nani ana sponsor fujo za kuua wakristo na kuchoma makanisa? unasema nchi za magharibi kuingilia nchi zingine? tafadhali elekeza pia darubini yako mashariki ili upate picha kamili.
Kama hufahamu mungu akusamehe la unafanya makusudi kwa chuki basi chuki zako haziwezi kuondowa ukweli. Hebu nani kakwambia kuwa Uislamu uliletwa kwa vita? Waislamu na huyo kiongozi wao alihama Makka huku akikimbizwa ili auliwe na uislamu ulikulia Madina ambako vita ilipganwa pale ambapo maaduwi waliwafuata Waislamu> Cha ajabu kipi hapa duniani na kupigana vita ili kuleta haki? sisi Watanzania si tulipigana na vita mbalimbali hadi tukapata uhuru jee ina maana kuwa sisi ni watu wa vita??
Kuhusu kueneza dini ivyo wewe katika historia yako wazee wako walikuwa wakiabudu nini? huo ukiristo ulianzia Mzizima? Na nani mwenye haki dunia hii ya kueneza imani yake na nani hana haki?
Ya Nigeria ni matokeo ya mambo kama haya ya CCT na kuhusu mauwaji Marekani anaendelea kuuwa Iraq na Afghanistan au nae ni Muislamu???
 
Kama kuna tofauti kati ya uislam na vurugu basi naomba nifahamishwe. Binafsi naona ni kitu hicho hicho tu. Tatizo la waislam ni kuhisi kuonewa. Dini gani inayoongoza kwa kuwa na vikundi lukuki vya kigaidi!!!!

Pengine ungejiuliza hili vurugu kwanini ndani yake kuna waliowatakatifu?? Hivyo ukibishana na mjinga unakuwa nani??/
 
TANZANIA TUNAYO LESENI YA KUJENGA KITUO KA BIASHARA NA JUMBA LA IBADA KWA PAMOJA?

Nakubaliana kabisa nawewe ndugu katika madai haya mazito!!!

Na kwa mtindo huo huo Mzee Mwinyi alivyopandikiza MBEGU TUSIOIFAHAMU VEMA Tanzania hizi chuki za KIDINI nchini na sasa Mhe Kikwete kulitekeleza kwa kasi ya ajabu, ni jukumu lao kulizima moto huu haraka kwa kitisha MJADALA WA KITAIFA kuandika upya KATIBA.

Hivi kweli nyinyi MLIWAHI KUONA KATIKA NCHI gani ambapo mfanyabishara anapoenda kuomba leseni ya kujenga kituo chake cha biashara na HAPO HAPO anaambatanishiwa na leseni ya kujijengea mle mle JUMBA LA IBADA??? Hata nyinyi wataalam wa maswala ya ardhi yetu hii ya Tanzania, ni sahihi kweli kufanya hivyo.

Naomba JIBU KWA MHE KIKWETE mwenyewe, ambaye ndiye niliyempa au kukasimu haki zote na madara ndani ya KATIBA ya sasa kumiliki kwa niaba yangu ardhi ya Tanzania na vitu vyote vilivyomo chini na juu ya ardhi hiyo, AKANIRIDHISHE BILA ya kubakiwa na maswali zaidi kichwani kwamba kile kiwanja mkono wa kushoto Njia Panda ya Ubungo unapotokea Mikoani ni (i) KIWANYA CHA BIASHARA au (ii) KIWANJA CHA JUMBA LA IBADA (ambalo naliheshimu sana bila kujali ni wa imani gani) au (iii) ni KIWANJA CHA MATUMIZI YOTE MAWILI KWA PAPOJA.

Na kule Al-Jazeera ukielekea Mbeya je??? Na Pale Mombo vipi nako??? Tukirudi tena pale njia panda Ubungo pale naona Supermarket, Naona Kituo cha Mafuta cha OILCOM na vile vile kwenye ubavu wa kuelekea Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, kuliko na wataalam wengi zaidi juu ya masuala ya ardhi na matumizi yake sahihi nchini mwetu, naona MSIKITI. Mpaka hapo, ninapopita au kusubiri daladala (usafiri wangu wa kudumu) huwa najikuta na mijadala isioisha ndani kwa ndani.

Na nikikumbuka wakati ule mtambo wa gesi Ubungo uliponusurika kulipuka au ujambazi wa mara kwa mara pale, wakati mwingine huwa nakijikuta nikihoji mantiki ya mwanataaluma yeyote aliyefanikisha miradi kama hii. Je, nchini kote tutegemee sura za aina hii ngapi zilizopo na zinazoendelea???

Kama jibu ni namba tatu hapo juu kama ambavyo inavyoonekana kiukweli pale, je mheshimiwa ulikua unatumia sheria zetu hizi hizi katika kusimamia matumizi sahihi ya ya rasilmali ardhi ya taifa letu???

Na kama huu ndio mtindo wa kisasa, je nao wenzetu wenye asili ya Ki-Asia wakajijengee mijumba yao ya ibada sehemu zao za biashara???

Je, tukitaka sasa kuwe usawa wa aina hii ambapo hata Marehemu PROFESA Kigoma Malima (apumzike kwa amani) aliwahi kuasisi kwa kujijengea MSIKITI katika ofisi ya serikali pale Wizara ya Fedha sasa na kila mtu akijengee tu mijumba yao ya ibada ama mashuleni, ofisini, kwenye biashara zao HATIMA YAKE ITAKUJAKUA NI NINI. Mwisho wa siku tunatafuta nini hasa na MKAKATI KAMA HUU kwa taifa letu??? Hivi kweli jamani????
Kwa kukujibu moja tu nililolifahamu na kukuuliza, iwapo Dini ya Kighoma inamlazimu aswali akiwa wakati wa kazi na akaamuwa kujiwekea kasehemu ndani ya ofisi yake kuswali badala ya kuweka sehemu ya kuweka pombe za kukaribisha wageni utasema kajenga msikiti? Na jee huo msikiti alioujenga ulivunjwa au upo mpaka sasa? Si lazima unijibu ikiwa lugha yako ndio hiyo hapo juu!
 
Mimi ninaamini kabisa kwamba UISLAMU kama ulivyo UKRISTO wetu hauna ugomvi na mtu isipokua ni baadhi tu ya watu wachache wenye agenda binafsi ndio wanaoupotosha kwa kukumbatia vijivurugu vya hapa na pale tu.

Hata hivyo turudi kwenye hoja ya msingi hapa, tuachane na yajitokezao ndani ya mjadala.
 
Mwenyekiti wa CCT, Askofu Peter Kitula amesema tatizo la udini lilianza mwaka 1986 na hakuna kiongozi wa serikali aliyejitokeza kulikemea badala yake Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilizidi kufanya makosa kwa kuingiza suala hilo katika Ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2005.

"Kuanzia miaka ya 1986 kulianza kujitokeza mihadhara ya kidini na kidhehebu katika jamii ambayo hatukuwa tumeizoea lakini jambo hili halikukemewa wala kuchukuliwa hatua za kisheria".

Ilani ya uchaguzi ya CCM 2005 ilitamka bayana kuwa suala la Mahakama ya Kadhi litashughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi, ikumbukwe kuwa mahakama ya kadhi ni jambo la kidini na kiibada katika dini ya kisilamu, jambo hili ni kinyume cha Katiba ya nchi na sheria ya vyama vya siasa hakuna aliyeona hatari yake na kwamba litakuwa chanzo cha udini ndani ya siasa za Tanzania, "alisema.

Kwa maneno ya Kitula umefika wakati sasa tuache unafiki tuanze kuwataja kwa majina yao wote wanaohusika kulipeleka taifa kusiko bila kumng'unya maneno, kwa kuanzia nitaanza na Mwenyekiti wa NEC anakotupeleka siko. Ni ukweli mchungu.

- You know what, hawa viongozi wa dini kama huyu Askofu Kitula mimi ningekua Rais wa taifa hili ningeanza kumuweka Detention kwa kuhatarisha Usalama Wa Taifa, na ningemuacha huko kwa muda mrefu sana kwa sababu his act here ndio udini wenyewe hasa, I mean ameongea maneno mengi lakini hakuna substance wala common sense, na for sure uwezo wake wa kufikiri ni mdogo sana,

- Ungekuwa mkubwa angeelewa kwamba hakuna kesi ya Murder au Rape itakayosikilizwa huko kwenye Kadhi, sasa why waste his time even mentioning it? Mhakama ya Kadhi itapunguza au kuongeza nini kwenye hili taifa? Sasa badala ya kuonyesha nini madhara ya kuwa na Mahakama ya Kadhi as far as udini is concerned kwa hili taifa, yeye anaweka hoja ya Mahakama ya Kadhi halafu anaiacha hewani halafu some of us Great Thinkers bila hata kufikiri wala kutfakari tunarukia right on it bila hata kuchambua kilichosemwa na ambacho hakikusemwa, it is simply PATHETIC!

- Ya Kaizeri wangemuachia Kaizeri, wao waendelee na ya Imani! ndio maana kwenye Constitution kunatakiwa kuwepo na kipengele cha Separation of Church and power, kwa sababu huyu Askofu has no clue what is politics!, so somebody needs to tell this man to shut up!

William.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom