Udini ni nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udini ni nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ami, Sep 23, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Katika miaka ya karibuni, hasa mwishoni mwa utawala wa raisa wa awamu ya kwanza mwalimu Julius Kambarage Nyerere,hapa Tanzania pamekuwa na msamiati unaojulikana kama UDINI.
  1.Hivi hili neno kwa upana wa matumizi yake lina maana gani,na asili yake ni nini?

  2.Jee inawezekana kwa watu wenye dini kama vile waislamu na wakristo kufanya jambo lolote lile bila kuingiza dini?.

  3. Jee ni kweli kuingiza dini katika jambo lolote lile ni vibaya na hatari?.Au ni vyema kufanya hivyo ili dini ziendelee,kuepuka kuwa mapagani?

  4.Kwa vile msamiati huu hutumika Tanzania kama kiashirio cha uovu.Ni nani hasa wanapaswa kuutumia na kuugopa?.

  5.Ni nani wamekuwa wakiuutumia zaidi msamiati huu, na zipi zinaweza kuwa ndio sababu za kufanya hivyo?
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Sep 25, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ami,
  Mkuu wangu UDINI ni pale binadamu anapoingiza dharau na chuki isiyokuwa na sababu ila dini fulani na waumini wake kwa ku spread fear among others kuhusiana na imani au waumini hao. Udini pia ni pale mtu anapo practice discrimination against dini au waumini wa dini fulani kwa kuwatenga wao kiuchumi, kijamii na hata kimazingira kwa dharau au kuwaona chini (inferior) ya ustaarabu kulingana na tamaduni wa jamii hiyo.

  Kifupi chukulia dharau na chuki ya Ukabila, jinsia na hata Racism kwa jinsi unavyoelewa wewe kisha weka jina la Udini pale inapohusu moja kati ya hayo ndio unapata maana ya Udini.

  1. Asili yake imetokana na hisia au vitendo vya dharau na chuki isokuwa na sababu yoyote ya maana ila imani ya dini ya mhusika. Mara nyingi sababu huundwa kuhalalisha chuki au dharau ilojificha.

  2. Inawezekana kabisa Waislaam na Wakristu wakafanya mengi sana pasipo kuingiza Udini kwa sababu sote tumeumbwa tofauti na tunahitajiana kwa kila siku kama vile Mume anavyomhitaji mke, kama Mtanzania mweusi anavyomhitaji Mzungu, Mwarabu, au Mchina na wao wanavyowahitaji mataifa mengineyo..Kutambua tofauti zetu sio udini ila ni pale dharau na chuki inapoingia pasipo kuwepo na sababu ya msingi ila imani ya dini ya mtu.

  3. Sii vibaya kuingiza dini ktk jambo lolote kwa sababu hii ni imani ya kila mmoja wetu isipokuwa unapotumia dini isiwe kudharau au kuonyesha chuki ya dini au waumini wa dini nyingine..Kwa mfano huli nguruwe , ni jambo jema na ustaarabu kwako mhusika lakini usiwaambie wanaokula Nguruwe kuwa wao ni Makafir hali wewe mwenyewe pengine ni shoga! - haaa! haaa! haa!
  Ni vizuri zaidi kumfahamisha mwenzako madhara ya kula nguruwe badala ya kutumia dini kama sababu ya kupinga vitendo vyake hapa hataweza kuuona uharamu wa nguruwe isipokuwa Uharamu wa imani yake ya dini hata kama Ukristu umekataza kula nguruwe. Neno Kafir ni dharau na inajenga chuki..

  4. Mara nyingi katika mazungumzo ni vizuri sana kuepuka maneno ya dharau mbele ya wahusika kwa mfano sii vizuri kwa mzungu kumwita mtu mweusi "N" word lakini wao wanaweza kuitana hivyo, pia sii vizuri kwa mwanamme kumwita mwanamke "B" word lakini wao wakaitana hivyo na pia sii vizuri kumwita Shoga " F" pamoja na kwamba wao wanaweza itana hivyo. Mkristu anaweza kusema neno lolote la dharau kuhusiana na Ukristu kwa mkristu mwenzake sawa na Muislaam kwa Muislaam pasipo dharau na chuki kujitokeza lakini usitake kujiingiza kati ya hizi hasi na chanya kujaribu kusema unaloona sawa hali sii sawa kwa mwingine.

  5. Mara nyingi wenye kutumia msamiati huu ni wale wenye dharau na chuki ya waumini wengine. Iwe Mkristu au Muislaam inategemea na chanzo kisha mazingira. Yeyote anayeanza kuonyesha vitendo vya dharau au chuki kwa mwingine akitumia dini na hasa pale kundi moja ndio majority na mwenye nguvu ndio Udini hutumika kuonyesha dharau na chuiki zao..Wakati mwingine yule anayejibu pia mapigo kwa dharau na chuki vile vile huitwa mdini kwa sababu ameonyesha dharau na chuki yake kujibu mapigo kama vile wanajeshi vitani. Hawa wote ni askari in combat hawawezi kuitwa raia (civilian).

  Nadhani imetosha mkuu au bado?
   
 3. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mkandara hongera kwa definition yako ya udini.Naona umemweleza vizuri Julius Kambarage Nyerere na serikali zote zilizofuatia baada ya uhuru.

  Hapa ni pale uliposema... Udini pia ni pale mtu anapo practice discrimination against dini au waumini wa dini fulani kwa kuwatenga wao kiuchumi,...
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Sep 26, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ami,
  Mkuu wangu tuzungumze ukweli na sii hizi habari za kusikiliza midahalo ya watu wasiokuwa na shukran. Nyerere alifanya kipi haswa kwa tafsiri ya maneno haya - Udini pia ni pale mtu anapo practice discrimination against dini au waumini wa dini fulani kwa kuwatenga wao kiuchumi,...
  Nambie mkuu wangu...
   
 5. bona

  bona JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  udini ni hali ambayo member wa dini fulani kwa nafasi au uwezo wake anawasaidia au kuwapendelea member wa dini yake kupata kitu fulani unfairly! kuzungumzia au kutekeleza jambo fulani kwa kutumia dini nje ya condition tajwa hapo juu haina shida na ideally kila mtu angekua happy na msamiati wa udini usingeleta chuki!
  kutumia dini kwa mazingira tajwa hapo juu ndio inazua chuki dhidi ya member wa dini nyingine na kuhatarisha amani na umoja, na hali inazidi kua tete kwa nchi maskini kama zetu kwani maskini wengi wanapenda kujua sababu za umaskini wao kwa iyo jambo dogo watu wanalitumia kutoa frustration zao na linachukuliwa kwa uzito mkubwa na lina kua chanzo cha chuki pasipo maana yoyote!
   
 6. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,090
  Trophy Points: 280
  Udini ni ubaguzi au upendeleo kwa misingi ya dini.
   
 7. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2010
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Mkuu Mkandara, swadakta! Yaani hapa umemaliza na kutilia muhuri kabisa. Asante sana mkuu, majibu haya ndiyo sahihi kabisa, twende hivi tutafika. Niongeze neno moja tu, utu. Tukizingatia utu, ni rahisi sana kuzikubali tofauti za kiimani na kuziona kama mapambo ambayo Mwenyezi Mungu ameruhusu yawepo duniani. Mungu hakushindwa kuwaumba binadamu wanaoamini na kufuata kitu kimoja tu. Hebu tazama, katuumba sote tunafanana mengi kimsingi, mtoto akizaliwa leo Uchina anaanza kunyonya ziwa la mamake bila kufundishwa na yeyote, vivyo hivyo kwa mtoto wa kiafrika, kizungu, kihindi, kiarabu nk. Mungu angeweza kutuumba tuna dini tayari, ambayo tungefuata bila kuhubiriwa, lakini hakufanya hivyo! Mimi namini Mungu anaipenda hii diversity iliyopo, hasa ukizingatia kuwa dini zote zinahubiri wema tu. Asante mkuu.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...