Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,946
- 51,094
Sijaelewa ni kwa nini Kila akikosolewa Samia Suluhu Hassan ndani ya chama chake ama kama Rais hoja kuwa ukosoaji huo unatokana na dini yake huibuka.
Hivi ni Rais gani wa nchi hii ambaye hajawahi kukosolewa. Jee walipokosolewa Nyerere,Mwinyi, Mkapa, Kikwete au Magufuli hao Marais walikuwa hawana dini?
Mwalimu Julius Nyerere alitaka kupinduliwa mara mbili wakati wa utawala wake (1964,1982). Jee waliotaka kumpindua walifanya hivyo kwa kuwa alikuwa ni Mkristo?
Mzee Ali Hassan Mwinyi aliitwa Kila aina ya majina ya kejeli na wapinzani wake. Jee hao waliomwita hayo majina walikuwa wanamwita hivyo kwa kuwa yeye ni Muislamu?
Alipoingia Benjamini Mkapa alifanya mambo mazuri na mabaya, lakini wakosoaji wake walimkosoa kwa kuwa ni Mkristo?
Alipokuja Jakaya Kikwete alifanya mambo mema na mabaya, lakini alikosolewa Kila Kona kwa mambo kadhaa wa kadhalika. Jee na yeye alikosolewa kwa kuwa ni Muislamu?
John Magufuli nadhani hakuna rais aliyekosolewa vikali na watanzania kama yeye. Jee alikosolewa kwa kuwa ni Mkristo?
Kwa nini Samia Suluhu Hassan akikosolewa inaibuka hoja kuwa Samia anakosolewa kwa kuwa ni muislam? Lengo la hoja hii ni nini?