UDINI na MUSTAKABALI WA TAIFA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UDINI na MUSTAKABALI WA TAIFA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwananchi Mtanzania, Jul 4, 2012.

 1. Mwananchi Mtanzania

  Mwananchi Mtanzania Member

  #1
  Jul 4, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni wazi kwamba tunapotoka majumbani na kwenda kujitafutia riziki, au tukiwa na matatizo mbai mbali, tunapitia sehemu nyingi na tunasaidiwa na wengi. Tukipanda dala dala hatuuizi dereva ni dini gani, au kondakta ni dini gani. Hivyo hivyo tukienda kununua mchele dukani. Wala hatuulizi daktari au muuguzi anayetuhudumia ni dini gani. Kwa kifupi tuna marafiki, ndugu, jamaa na majirani ambao si azima wawe wana imani inayofanana na yetu. Nitashangaa nikimuona Bakari anamporomoshea matusi Yakobo kwenye mtandao, eti kwa sababu tu ya imani, wakati Bakari huyo huyo ana rafiki yake akiitwa Julius. Vivyo hivyo, nitashangaa nikimuona Yosefu akimkashifu Athumani, wakati Yosefu huyo huyo, kila siku hununua chakula au hufanya kazi kwa Abedi!!

  Leo naanza kuwashukia wenye hulka ya kupenda kutoa hoja kwa msukumo wa imani, bia kuangalia mustakabai wa taifa. Panapo majaaliwa, nitawashukia wenye ukabila;

  Wakati niko mdogo, nakumbuka ilikua ni jambo la kawaida sana kwa majirani wenye imani tofauti kuonyeshana upendo kwa njia kama ya kupelekeana mapishi wakati wa sikukuu mbali mbali za kiimani, bila kujali mwenye jina la kiarabu au a kizungu – au hata kama akiitwa Maganga, Masawe, Kimweri au Komba! Nilikua nikisikiliza Radio Tanzania wakati huo, viongozi wa dini walikua wakihubiri upendo. Kwa kweli, kipindi kile viongozi wa dini waikua si "wanasiasa"! Lakini siku hizi, sisi wananchi, vyombo vyetu vya habari na viongozi wa dini, naona kila kukicha tunajipeleka matatizoni wenyewe, tunabishania mambo ambayo wala hayastahili. Leo, kuingiza imani kwenye siasa limekua jambo ambalo watu hawaogopi. Kibaya zaidi, miongoni mwetu wapo wanaotumia mitandao ya kijamii kuporomosha matusi dhidi ya wenzao popote pale imani inapotajwa…. Japokua mimi sikusoma vitabu vingi vya imani, jambo moja ni wazi kwamba tunaambiwa tuhubiri upendo…. Uwe unaitwa Bakari, au John, Faruma au Suzana, habari ndio hiyo…. Tunasukumwa kuhubiri upendo, na si vinginevyo…..

  Cha ajabu sana, siku hizi akiinuka mwanasiasa akasema neno la kawaida tu "Kiongozi awe Mcha Mungu"; basi watu wataangalia aliyesema hivyo ana imani gani… halafu watu wenye imani ambayo si ya kwake, watamshambulia kwa kumuambia "mdini" – Ha! Tobaaaa! Yani maneno ya kiswahii tu "mcha mungu", ndio yanafanya watu waitwe wadini? Niliyaona haya wakati naperuzi mitandao katika siku tofauti tofauti kidogo, na nikakutana na matusi ambayo yalielekezwa kwa hotuba za Mzee Ruksa, pamoja na Mh. Sitta. Watu wote hawa, kwa siku tofauti, walitumia manono ya kawaida tu kwamba kiongozi awe "mcha mungu/muogopa mungu", lakini walihukumiwa kutokana na imani zao. Hili linadhihirisha wazi kwamba wengi wetu, katika makundi mawii makubwa tanzania, tumekua wahanga wa matusi kutokana na imani zetu… Inasikitisha sana.

  Labda niulize hivi: Mfano itokee mawaziri wote ni kina Juma Rashidi na Bakari, lakini kina Yohana, Yosefu na Samsoni wanapata hakisawa. Au, itokee kwamba baraza lote a Mawaziri ni kina Antony, George and Martin, lakini kina Idrisa, Ismai na Mustafa wote wanapata haki sawa – kwa nini baadhi yetu wataaamika eti „"hakukua na uwakilishi sawa wa kidini" wakati kazi inayofanyika siyo ya kiimani? Wapo wenzetu ambao, bila kujali ni awamu ipi ya uongozi (nitasemea sana kuanzia ya pili, tatu na nne kwa sababu walau mambo mengi nina ushahidi nayo) wapo wenzetu ambao pale Rais anapoteua watu, basi walikua wanaangalia ana jina la kiarabu ama kizungu. Cha kushangaza, hakuna anayeridhishwa katika hawa, pale ambapo majina ya asili anayoyataka yeye yamekua yamepungua.. basi haraka haraka, hapa watu walikua wanaanza kusema… Rais fulani Mdini… Ukweli ni kwamba, katika Marais wetu wote wanne, kila mmoja amerushiwa makombora haya – au jina hili la "udini"! Jambo la kuangalia hapa ni kwamba, kama una kereka tu kwa sababu waziri au mkurugenzi hana imani inayofanana na wewe, lakini huna uthibitisho kwamba aliwahi kuto kutenda haki kwa mtu mwingine mwenye imani tofauti na ya kwake, basi wewe ndiye utakua una udini… bila kujali unaitwa Rashidi au Samsoni! Je, ni sababu ipi haswa inayokufanya uangalie viongozi wenye majina yanayofanana na ya imani yako? Yawezekana basi kumbe ni wewe, na wala siye anayeteua, mwenye katatizo ka "udini"! Je, unafanya nini kupambana na hilo tatizo lako?

  Na huu mtindo wa kusema eti chama fulani ni cha waislamu na kingine ni cha wakristo sijui umeibukia wapi! Je, viongozi wetu wa dini wanafanya juhudi gani kuwaambia waumini wao kwamba wako huru kujiunga na chama chochote? Viongozi wa vyama vya siasa wako tayari kuwakataa hadharani wapiga kura ambao watataka kuwachagua kutokana na imani tu?

  Mwaka 1992 Ulipoingia mfumo wa vyama vingi, Bwana James Mapalala na Wenzie walianzisha chama cha CUF. Baadae, Maalim Seif aliingia. Kutokana na historia ya Zanzibar, na kama sikosei iliyopelekea vugu vugu la kisiasa kua tete Zanzibar miaka ya 1980, na labda hata historia ya nyuma ya hapo, ni wazi kua Maalim Seif alipata ufuasi mkubwa kutoka Pemba. Kutokana na Mazingira ya zanzibar, haikushangaza kwamba wafuasi wengi wa mwanzo walikua ni waumini wa Kiisam. Hata kwa huku bara, wafuasi wengi wa mwanzo walikua ni wale wenye asili ya kipemba. So, this was more of a historica fact. Kama kulikua kuna wauminii wa kiislamu waliofikiri kwamba CUF ni kwa ajili ya Uislam, walifanya makosa makubwa kuchanganya dini na siasa. CUF na NCCR vilikua na nguvu kubwa kwenye uchaguzi wa Mwaka 1995. Cuf waiwahi kufanikiwa kuwa na wabunge wawili bara, Bw. Wilfred Lwakatare (Bukoba Mjini), na (Bw. Frank Magoba, Kigamboni).

  Kuanzia 2005, CHADEMA kimekua ni chama kinachokua kwa kasi. Labda kutokana na Mgombea urais wake wa 2010, baadhi ya watu walikihusisha chama hiki na ukatoliki. Yawezekana wapo baadhi ya watu, kama iivyokua kwa CUF mwaka 1995, walitaka kuamini hivyo... au waliamini hivyo... au walitaka iwe hivyo. Hawa nao hawakua sahihi hata kidogo.

  Swali la kujiuliza hapa, kwa nini tuhuma hizi za udini zisielekwzwe kwenye vyama vidogo ila zielekwzwe kwenye vyama vikubwa tu? Je, kama CUF ingekua ni ya kidini, Je, Mchungaji Christopher Mtikila angekubali kufanya nacho kampeni ya pamoja (nafikiri ama 2000 au 2005, kwa ajii ya hoja ya serikali 3)? Je, Kama CHADEM kilikua ni kwa ajii ya wakristo, vipi kiliibuka nafasi ya pii kwenye jimbo la Uzini Zanzibar, mbele ya chama kikuu cha upinzani CUF? Kwa nini iwe CHADEMA na CUF. Kwa nini si kwa CCM, UDP, TLP, NCCR, nk.?

  Jambo jingine ambalo linaudhi au linatia uchungu zaidi, ni tabia ya baadhi ya viongozi wa dini, kwa hii style yao mpya ya kujibizana wao kwa wao bila kujali madhara wanayosababisha kwa wananchi. Sijui ni kwa kiasi gani wanatathmini kauli zao, au kero wanazosababisha kwa wananchi ambao tuna imani tofauti. Nina wasi wasi kwamba watu wamesahau kua imani ni suala zito, na hivyo ni vizuri kuchunguza kila kauli tunazotoa. Tatizo si tu kutumia haki ya kikatiba ya kutoa maoni… la hasha. Ukweli wa mambo ni kwamba kutokana na utofauti wa imani, yapo mambo ambayo hayawezi kukubalika kote kote. Hivyo basi, lugha inayotumika, au sababu zinazotumika, lazima zifikiriwe kwa kina kabla ya kwenda gazetini. Kinachoniudhi ni kwamba viongozi hawa husema eti wanatoa maoni kwa serikali, lakini ukweli halisi ni kwamba wanajibizana wao kwa wao… Nafikiri tunakumbuka zile story za Waraka na Muongozo….. kipindi kileee….. Jambo linalotia wasi wasi ni kwamba, wakati kiongozi wa upande mmoja yuko tayari kulalamika au kukemea kiongozi wa upande mwingine kwa maneno ya kukwaza, ni mara chache viongozi wa makundi husika, huwakumbusha wenzao kwamba wana uwajibu wa kuhakikisha hawawakwazi wenzao…. Kwa kweli ni nadra sana (mimi sina kumbu kumbu nzuri haswa) kusikia ama Sheikh anamuambia Sheikh; au Askofu anamuambia Askofu kwamba lugha inayotumika kwenda upande wa pili si nzuri… Na kama haya yakisemwa, basi hua inakua ni kitu cha mara moja moja…! Bahati mbaya, zaidi, msukumo kutoka kwa sisi waumini, tuwe tunaitwa kina Bakari au kina Yohana umekua ni mdogo… Kwa kweli, sijawahi sikia Tanzania kwamba waumini wamewaonya viongozi wao kuacha kutoa kauli zenye utata… hapa nafikiri na sisi tuna tatizo. Kwa hiyo kinachotokea: Viongozi wa dini wakichefuana, na sisi wananchi tunachefuana… Hivi tumesahau kwamba viongozi wetu wa dini sio miungu, na hivyo tunaweza kuwakosoa, haswa kwenye mambo ya kaizari ambayo wao hayawahusu?

  Ila jambo ambalo Limenikera kuliko mengi, ni hii tabia ya siku hizi ya kuanza kulinganisha… kwamba eti kwama wao wana taasisi fulani, na sisi tunataka hii… au mbona sisi hatuna hii, basi na wao wasiwe nayo… hii ni hatari… hatari sana….!! Wala haihitaji utafiti kugundua kwamba Uislamu na Ukristo vina misingi tofauti, japokua kote kote tunasoma kuhusiana na akina Musa, Yusufu, Daudi, Nuhu na wengine…. After All, Yesu si ndie Issa? (any way, sitaki kuingia sana huko, kwani dhumuni si kusema nani yu sahihi, kwani kila mtu hilo analo moyoni mwake… na ni kweli hakuna mwenye dini mbii)…. Turudi tu kwenye mada kwamba Uislam na Ukristo vina historia na taasisi tofauti. Kwa hiyo ni jambo la ajabu kuona viongozi wa kiimani kuanza kulazimisha… eti: "kama wao wana vatikani, na sisi tuwe na…"; au "sisi hatuna kadhi, na hivyo wao.. wasiwenayo…". Iweje leo Waislam wawachagulie wakristo taasisi wanazozihitaji wao, au Wakristo wawachagulie waislam taasisi zao, au namna ya kuziendesha? Nani amewaambia kwamba unaweza ukafananisha matakwa ya dini ambazo zina historia na misingi tofauti?

  Nashangazwa kuona baadhi ya Masheikh wakijadili Vatikan, au baadhi ya Maaskofu wakijadili Kadhi, kwa sababu wanajadili mambo ambayo yako nje ya mipaka yao…. Je, sisi waumini tunawakumbusha kwamba wanatoka nje ya utaratibu? Au tunawakumbatia kwa sababu ni "wenzetu"? Hivi Juma ana uhakika gani kwamba akienda kumkata panga Joni, familia yake (Juma) itabaki salama? Na Yesaya ana uhakika gani kwamba akienda kuchoma nyumba ya Hamisi, famiia yake (Yesaya) itabaki salama?

  Hatari zaidi ni hili la siku hizi la kia kiongozi wa dini kudai eti "kwa sababu waumini wake nao ni waipa kodi, basi serikai ifanye vile wanavyotaka…" Hii si sawa! Hivi, kila mtu leo akitaka kodi itumike kutokana na matakwa ya imani yake, je, ile dhana ya "serikali haina dini" tuna isahau? Si hivyo tu, kwani ni mambo mangapi ya kiserikali yanafanyika ambayo yako kinyume na imani zetu? Tumeyagundua siku hizi? Na mbona tusikatae ulinzi wa polisi au kutumia bara bara kwa sababu si kila kinachokusanywa na kodi ya serikali kinaweza kuwa "halali" kutokana na imani zetu? Hapa ndipo iitupasa sisi waumini tuwaambie viongozi wetu kwamba masuala ya kodi au sheria ni ya kaizari, kwa hivyo wasithubutu kuongelea hayo. Yapaswa tuwaambie viongozi kwamba tunapoingia kwenye Ibada, hua tunachokifanya ni kumuabudu mungu, na humalizia Ibada zetu kwa kusema Amen. Iweje tunakua tunashughuika kutoleana macho wakati tutake tusitake Tanzania ni ya kwetu wote na wala hakuna mwenye haki kumzidi mwenzie?

  Watanzania wenzangu, tuwaambie Viongozi wetu wa dini washughulike na yanayowahusu. Mradi hakuna anayemzuia mwenzake kufanya ibada, basi na anayetaka taasisi yake na aipate, mradi tu iwe inamuhusu yeye! Sioni haja ya kutoleana macho wakati kama tungezaiwa Brazil, au Dubai au Uchina, tungekua tunaongelea mitazamo tofauti.

  Naomba kuwaasa Watanzania, tuache mashaka na kutokuaminiana. Bakari usimuangalie Joni ukahisi anakuhujumu, na Joni usimuangalie Bakari ukadhani ni Al-Kaida au Al-Shabab. Haya mashaka tunayokua nayo, na huu mtindo wa kia mmoja kutaka kumchunguza mwenzie ana abudu vipi, au kutaka kunyima mwenzie uhuru wake wa kuabudu, au kulazimisha tu kuwa na kitu Fulani kwa sababu mwingine anacho, and vice versa; ndio vinasababisha "misimamo mikali". Kwa bahati mbaya, unapoingia katika msimamo mkali, wala huwezi kujijua. Ni muhimu kugundua hatari hiyo ya misimamo mikali, na hakuna upande ambao utasema kwamba katika dunia hii haujawahi kuona wenzao wenye msimamo mkali… Tuliyaona Ireland (Protestants vs Catholics), Tunayaona Uganda (Joseph Koni na azma yake ya amri kumi), Tunayaona ya Al-Shabab na Uamsho!

  Navuta kasi kwa ajili ya kuwavaa "wakabila"!!
   
 2. fige

  fige JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2012
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  well said Mkuu
   
 3. M

  Makupa JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  bila kuficha mimi ni mwana ccm hai, ila sio siri swala la ukabila n udini linachochewa sana na Nape, Mukama na Wasira .Hii dhambi ik siku itawarudi. Tuliamini kabisa kuwa chama kilipata katibu mkuu msomi
  kumbe ni bure kabisa.
   
 4. Hayajamani

  Hayajamani JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2012
  Joined: Jul 2, 2012
  Messages: 883
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kweli kabisa, tatizo hilo lipo sana, hata ccm 2010 hata kabla kampeni hazijanza wana dini fulani kwenye sherehe na mikusanyiko mbalimbali walikuwa wanahimiza waumini wao wasiwe wajinga na kuhakikisha wanamchagua mtu wao. Baadaye kampeni zilipoanza mambo hayo yakajitokeza kwenye vyama vingine tena pamoja na madhehebu. Jamani hii ni dhambi ambayo italeta madhara makubwa.

  Ukizingatia hizo tunazoita dini zetu!! zimeletewa na wageni. Basi walioamua kufuata wageni wa Kiarabu sawa na walioamua kufuta wageni Wakizungu sawa tu. Pia dini hizohizo zimebagua na kudharau mila, tamaduni na desturi zetu, leo hii ukienda/kuhamia dhebu fulani lazima uwe na jina lingine la nyongeza kama vile John au Abdallah! Yametoka wapi haya jamani! Waafrika tumejisahau kabisa na kutukuza utamaduni wa wageni. Kuna mambo ya kufuata/kuiga kwa kiasi lakini mengine kama hayo yaliotajwa ni kufuru tupu. Laiti hao waasisi wa dini wangetokea Tanzania basi hata kwenye vitabu/katiba hizo zingeandikwa ugali, mapera, na hata matunda ya porini kama masasati au mashindwe n.k. Lakini sababu zimetokea kwenye utamaduni mwingine tumekuwa tunatukuza vyakula vyao na kuviita eti vitakatifu kama vile wali, tende, zabibu, mkate n.k. Upuuzi mtupu huu. Kuhusu mavazi, hatusemi tubaki uchi au nusu uchi kama mababu zetu sehemu fulani fulani lakini tubadilike kiasi na twende na jiografia. Tusiwe watumwa wa kutukuza mavazi ya wageni kule dini zilikoibukia. Hapa maeneo mengi hatufugi mbuzi (wanyama) na hivyo hatuhitaji kuwa na fimbo/bakora kila wakati, ni kwa baadhi ya maeneo tu fulani (pia ni tamaduni), hakuna jangwa lenye upepo wenye vumbi na kutufanmya tuvae mavazi fulani yanayoendana na hali hiyo. Wala hatuna baridi kali ili kuhitaji kuwa na suti/tai kila wakati au tuonekani rasmi. TUMEKUWA WATUMWA WA MAWAZO JAMANI!. Na mijitu mingine ndio inajifanya kama vile waanzilishi wa dini hizo ni wajomba zao na kutumia itikadi hizo (za kigeni) kama silaha za kubagua, kutukana, kunyanyasa hata kuuwa wengine.

  JAMANI TUPENDANE
   
 5. rugumye

  rugumye JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Waasisi wa udini nchini ni CCM kwani katika uchaguzi wa kwama 2005 waliweka kwenye ilan yao ya uchaguzi kuwa watahakikisha mahakama ya kadhi inarudhishwa, lengo lilikuwa kupata kura za waisilamu, bila kungalia madhara yake hapo baadae. wakati CCM wanafanya hivyo walikiuka katiba ya nchi ibara ya 18. inayosema kuwa haitakuwa halali kwa chama chochote cha siasa kupigania au kuweka katika ilan zake kupigania maslahi ya dini fulani na chama kitakachofanya hivyo kitafutiwa usajili, katiba ikaongeza kuwa kazi ya kutangaza dini itakuwa ni binafsi, serekali haitahusika katika maswala ya dini. Je CCM ilifutwa kwa kukiuka katiba ya nchi? tusimtafute mchawi, MCHAWI ni CCM.
   
 6. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Awamu zote kumekuwako shutuma kwa viongozi kwamba ni wadini. Ila tukiangalia hali ya sasa tuhuma za udini kwa kiongozi wetu mkuu hazikwepeki na ni za wazi! Yeye ndiye mpandikizaji na yumkini amefauru sana katika azma yake. Sasa hatimaye medani za kimataifa zinaanza kusuta na Tanzania itaingia kwenye mgogoro wa vikwazo kimataifa kwa sababu za udini wa kiongozi wetu. MUNGU INUSURU NCHI HII!
   
 7. d

  dostum JF-Expert Member

  #7
  Jul 4, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 215
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  naweza kusema ni WARAKA BORA KWA MUDA WOTE na unaofaa kuwa mwongozo kwa viongozi wetu na hasa viongozi wanaojitayarisha.

  unapaswa kuwa kiongozi na kama ni URAIS nitakupa kura yangu.


  HAKI SAWA KWA WOTE
   
 8. Democracy999

  Democracy999 JF-Expert Member

  #8
  Jul 4, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 947
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ondoa majina yote yenye asili ya mataifa mengine, ili kurudisha udugu wetu africa
   
 9. A

  Aman Ng'oma Verified User

  #9
  Jul 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 930
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 60
  Waromani katoliki ndio wanaongoza kwa udini Tanzania na ndio wanaoivuruga nchi yetu kwa kushirikiana na mawakala wake waliowapa ilani yao ya uchaguzi chadema,kusudi eti nchi isitawalike thubutu,padre hawezi kuingia ikulu akavae joho arudi kanisani.
   
 10. M

  Mathy laut nyami Member

  #10
  Jul 4, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Fernando lugo a roman catholic bishop who was a president of uruguay now compare tz and uruguay dont be a fool mr.Kichwa mbovu dini is nothing in leadership
   
 11. Mwananchi Mtanzania

  Mwananchi Mtanzania Member

  #11
  Jul 4, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna ubaya ikiwa Sheikh au Askofu ataingia Ikulu, mradi tu kiongozi chake ni Katiba, Uadilifu, Kutenda Haki. Full stop. Iwapo utampenda kiongozi kwa sababu tu ya dini, then wewe ni Mdini. How do you work to stop that?

   
 12. rugumye

  rugumye JF-Expert Member

  #12
  Jul 5, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  NOTHING BURNISH NEGATIVE FEELING MORE QUICKLY THAN POSITIVE ACTION. hivi wewe iliye andika kuwa RC wanaongoza kwa udini ulienda shule? na km ulienda umeelimika kweli? huyo Dr Slaa anapoibua mijadala km ile ya EPA na Mengine hivi faida na kwa wa RC? Zito Kabwe au Prof Lipumba (Muslim) wanapo simama kutetea maslahi ya TZ wanawapigania waislamu? huu ni umaskini wa mawazo. CCM waliahidi kuwapa mahama ya kadhi waislamu je wamefanya hivyo? km siyo kutaka kuleta fujo na kuwagawa wananchi ni nini? Ndugu yangu mswahili unapigania dini katika uongozi wa nchi, tafakari.
   
 13. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #13
  Jul 5, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Hii thread imeanzishwa kuwalenga watu aina yako!
   
 14. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #14
  Jul 5, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  we mwehu tena kichwa mbovu kama id yako toa udini wako hapa mtoa mada anaupinga wewe unauendeleza badili tabia yako huyo shekhe dhaifu ndio anafaaa?
   
 15. m

  mob JF-Expert Member

  #15
  Jul 5, 2012
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 509
  Trophy Points: 280
  mbona hili swala liko tu bara kwa nini hamsini upande wa pili
   
Loading...