Tatizo ni Zenji Factor. Nadhani Zenji wanachangia 50% ya members wanaoingia kwenye CC. Hapo sijaweka wale ambao wanaingia huko kwa heshima ama kwa nyadhifa zao (viongozi wakuu wa Chama wa pande zote mbili, marais wastaafu na wazee wa chama kama akina Kawawa).
Ukishaweka hiyo Zenji factor automatically lazima utaishia kwenye conclusion ya Mwanakijiji.
Labda swali la kujiuliza ni kwanini Zenji inapewa nafasi sawa na Bara?
Kwani mada yako hapa sio udini?:
Na ukiongolea udini Tanzania, huongelei Ukristo na Uislamu?
Mwnkjj, utajutia hii thread, I tell you!
Wakati mnaendelea na mjadala, wajumbe wenyewe ndo hawa hapa:
1. Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete - Mwenyekiti
2. Ndugu Pius Msekwa - Makamu Mwenyekiti (Bara)
3. Ndugu Amani Abeid Amani Karume - Makamu Mwenyekiti(Zanzibar)
4. Ndugu Yussuf R. Makamba - Katibu Mkuu
5. Capt. (mst) George Huruma Mkuchika - Naibu Katibu Mkuu (Bara)
6. Ndugu Salehe Ramadhan Ferouz - Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)
7. Dr. Ali Mohamed Shein - Mjumbe
8. Ndugu Mizengo Kayanza Peter Pinda - Mjumbe
9. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha - Mjumbe
10. Alhaj Ali Hassan Mwinyi - Mjumbe
11. Ndugu Benjamin William Mkapa - Mjumbe
12. Mzee Rashid Mfaume Kawawa - Mjumbe
13. Dr. Salmin Amour - Mjumbe
14. Ndugu John Samwel Malecela - Mjumbe
15. Capt. (mst) John Zefania Chiligati - Mjumbe
16. Ndugu Amos Gabriel Makala - Mjumbe
17. Ndugu Bernard Kamilius Membe - Mjumbe
18. Ndugu Kidawa Hamid Saleh - Mjumbe
19. Ndugu Samwel John Sitta - Mjumbe
20. Ndugu Pandu Ameir Kificho - Mjumbe
21. Ndugu Anna Abdallah - Mjumbe
22. Ndugu Rostum Aziz - Mjumbe
23. Dr. Mohamed Gharib Bilal - Mjumbe
24. Ndugu Pindi Hazara Chana - Mjumbe
25. Ndugu Andrew Chenge - Mjumbe
26. Dr. Maua Abeid Daftari - Mjumbe
27. Ndugu Samia Suluhu Hassan - Mjumbe
28. Ndugu Mohamed Seif Khatib - Mjumbe
29. Ndugu Haji Omar Kheri - Mjumbe
30. Dr. Abdallah Omari Kigoda - Mjumbe
31. Ndugu Abdurahman Kinana - Mjumbe
32. Ndugu Anne Semamba Makinda - Mjumbe
33. Ndugu Fatuma Said Ali Mchumo - Mjumbe
34. Ndugu Zakia Hamdan Meghji - Mjumbe
35. Ndugu Omar Yussuf Mzee - Mjumbe
36. Ndugu Emmanuel John Nchimbi - Mjumbe
37. Ndugu Ali Ameir Mohamed - Mjumbe
38. Ndugu Yussuf Mohd Yussuf - Mjumbe
1. Katiba ya CCM inatoa nafasi ya upendeleo kwa wa Zenj kujazwa zaidi ya wabara ilhali wabara ndio wengi. Katiba ya Chadema haitoi nafasi kwa wachaga kujazwa kwenye nafasi mbalimbali kuliko makabila mengine.
2. Zanzibar kutokana na point hiyo hapo juu; wengi wao ni waislamu. Kwahiyo ukiwapa nafasi ya upendeleo utakuta wengi ni waislamu. Hii ni tofauti Chadema ambao ukiwapa nafasi ya kuteuwa wabunge huteua wanaohusiana au wachaga.
3. Sio CCM tu inailea Zanzibar bali hata serikali yetu ya Muungano inailea Zenj. Swali, kwanini tusiwe na serikali ya TATU?, kwanini kamkoa kamoja kadogo kuliko hata Wilaya ya Ilala in terms of population ina representatives kibao?, Bungeni, Chama chetu na tena wana ka baraza la wawakilishi linalowakilisha mikoa miwili tu?. Think of this.
Ni sahihi wewe ku side na akina Mbowe, lakini sio sahihi wewe ku spin mambo.
Ofcoz mada sio udini. Mada yake ni UKABILA, na inamuhusu Mbowe na Wangwe. Soma katikati ya mistari ndugu. Ndio maana kule sehumu ya hoja ya SAM nilikwambia unamwelewa mtu kimaandishi...................
Mgaya.
Utafiti wako ni finyu nakupa msaada labda upeo wako unaweza kutanuka.
1-Michael Tyson-muislam jina lake limekaa vipi?
2-Freddy Kanute mchezaji wa kimataifa ni muislam jina lake la kiislam?
3-Frank Riberry mchezaji wa Timu ya Taifa ya Ufaransa ni muislam jina lake linaweza kukusaidia kusema yuko dini gani?
4-Bondia Danny Williams ni muislam jina lake linakaa kidini gani?
5-Nicholas Anelka mchezaji wa Chelsea ni muislam jina lake linaelekea kuwa la kiislam?
6-Waziri Sophia Simba jina lake linaoekana kama muislam lakini ni mkristu,
7-DR.Batilda burian jina lake limekaa kidini ipi?
8-Ramadhan Mtoro Ongora ni mkristu muda wote kwa utafiti wako ungesema ni mtoto wa sheikh wa msikiti wa Mtoro,
9-Stephen Nemes masajage kipa wa Yanga na Taifa Stars ni muislam kwa jina utamjua?
10-Tariq Aziz aliyekuwa waziri wa karibu sana na Sadam Hussein ni mkristu wa kuzaliwa,kwa jina lake bila kuwa na utafiti utasema ni muslam(a) utasema ni mwarabu lazima awe muslam(b) jina lake utasema ni la kiislam kwa mujibu wa ubishi wako usio na hoja.
Umsimsahau Malcom X alikuwa kiongozi wa kiislam kwa jina utasemaje? nimekupa sample kidogo kama nisingekutajia watu hao dini gani katika hao 11 niliwataja ungeweza labda wawili tu.
...Kwa kadri hoja ya udini ilivyodhaifu ndivyo hivyohivyo hoja ya ukabila ilivyodhaifu.
...Lakini cha msingi hakuna mifano hai ya maamuzi ya CCM yenye sura ya udini, vivyohivyo hakuna mifano hai ya maamuzi ya chadema ya kikabila.
Mada sio udini vipi wakati ametumia analogy ya uwezekano wa udini ndani ya CCM ili aje kujenga hoja kuhusiana na ishu za ukabila ndani ya CHADEMA?
Mwisho wa siku anataka kurudi kwenye ishu ya ukabila lakini hapa ni analysis ya kuwepo au kutokuwepo na udini CCM. Sasa utasemaje mada sio udini hapa?
Tutegemee nini katika hii thread? Hotuba, ratiba?
Unategemea mchango wowote toka kwa wana jf?
Matazamo wangu: MKJJ anajaribu kutufanya kufikiri juu ya yale yaliojili katika CHADEMA na yaliopo katika vyama vingine. Ukiangalia kwa undani unaweza kwenda mbele zaidi na kusema mbona chama fulani kimejaa watu waliomaliza chuo fulani mwaka fulani, je, hili nalo tutaita uchuo au u-mwaka? Hvy nalazimika kuamini kuwa mtazamo wake ni zaidi ya kile kilichoandikwa.
Sio kweli.
Amelinganisha vitu tofauti. Udini CCM ni kweli hakuna lakini mazingira ya Uchaguzi wa wajumbe wa Kamati Kuu ni tofauti na wa CHADEMA. Wa CCM wako pre-determined. Katiba inasema kamati itakuwa na wajumbe wafuatao: Rais ya Jamhuri kutoka CCM. Huyo Rais hata akiwa ni m-Budha atakuwa mjumbe.
Uchaguzi wa Wabunge wa CHADEMA ni handpicked. Mwanakijiji ametengeneza a false comparison.