Udhalilishwaji wa waislam na vyombo vya dola

Mwanakijiji! mzee wetu Mohamed Said ameianza nakala yake kwa kuturudisha nyuma kidogo na habari ya yule Sheikh aliyerudishwa "kwao" Zanzibar halafu akaendelea kutupeleka mwaka 1964 wakati masheikh wengi waliwekwa kizuizini, hakutuacha hapo bali alitukumbusha mwaka 1993 ambapo kulizuka tafrani kati ya askari na Waislamu akamalizia tukio la Sheikh Kishki juzijuzi na Mufti wa Yemen halafu akaunganisha na lilomkuta yeye.
Huu ni mlolongo wa matukio baada ya matukio haiwezekani ulifananishe na tukio moja la Ulimboka au na jingine kama la Ulimboka pale na hapa......mwisho kauli yako imenishangaza sana kwani inaonekana kuihukumu Serikali kuwa na hatia ya utekwaji wa Ulimboka!
Mohamed said ametuletea udhalilishwaji wa Waislamu unaofanywa na vyombo vya dola, wakati ya Ulimboka ndio kwanza uchunguzi unaendelea!

Vyombo vya dola mwaka 2006 kama ilivyo leo vinaongozwa na Waislamu. Kwanini wasiseme ni waislamu serikalini wanawadhalilisha Waislamu wenzao? Mwaka 1964 waliowekwa kizuizini hawakuwa waislamu peke yao.
 
Pole sana Mohamed Said kama umejikuta matatani kutokana na utendaji mbovu wa vyombo vyetu vya usalama. Lakini inaonyesha vyombo vya usalama vimekua vinakufuatilia nyendo zako. Na inawezekana hata mwaliko wa Ibadan ilikua ni ktk kukuchunguza mambo yako ya udini! Inaonyesha ulimwaga nyongo ktk vikao rasmi na visivyo rasimi ukidhani wale jamaa ni wenzako!!! Mwisho ni kwanini umeleta hii stori ktk kipindi wafadhili wako Iran wakituhumiwa kupeperusha bendera yetu kukwepa vikwazo vya Marekani na EU?!
 
Ndugu mbona wewe mtata sana? Hulengi chochote zaidi yakupandikiza udini!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Mdini nani anaekasirika kwa kuwa Muislam kenda Iran au anekamatwa kwa kwenda Iran? Igeuze hii utapata picha kamili.
 
Hili nalo linahitaji uthibitisho? Ina maana wewe historia ya darasa la tano hukusoma? Mbona liko wazi kwamba walioendesha biashara ya utumwa Tanganyika ni waarabu, na kama ni waarabu, definitely ni Waislamu, sasa unataka ushahidi gani tena?
Je, unataka tum cross-examine shahidi wako ambaye ni historia ya darasa la tano?
Kwanza, hiyo historia ya darasa la tano imeandikwa na nani?
 
karibu sana MS, naona umerudi tena na hoja zako za kidini, karibu sana. Safari ile serikali ilikunyamazisha kwa kusema ukweli halisi kuhusu wapigania uhuru wa nchi hii kuwa sio waislam peke yao kama ulivyotaka kuwaaminisha wasiojua. Hilo limekufa naona sasa umekuja na lingine, FAHAMU TU KUWA KAMA SERIKALI IKIKUSHUKU KUWA WW NI TISHIO ITAKUPEKUA TU, NA HAIFANYI HIVYO KWA 7BU YA DINI YAKO BALI KUTIMIZA WAJIBU. ACHA MAWAZO MACHAFU YA UDINI
 
Pole sana Mohamed Said kama umejikuta matatani kutokana na utendaji mbovu wa vyombo vyetu vya usalama. Lakini inaonyesha vyombo vya usalama vimekua vinakufuatilia nyendo zako. Na inawezekana hata mwaliko wa Ibadan ilikua ni ktk kukuchunguza mambo yako ya udini! Inaonyesha ulimwaga nyongo ktk vikao rasmi na visivyo rasimi ukidhani wale jamaa ni wenzako!!! Mwisho ni kwanini umeleta hii stori ktk kipindi wafadhili wako Iran wakituhumiwa kupeperusha bendera yetu kukwepa vikwazo vya Marekani na EU?!

Ahsante ndugu yangu.
Kuna mengi sikuyaeleza.

Mathalan mawasiliano yangu na "Jamaa pale Washington" na angalizo lao kwangu wakati naandika paper.
Haya sikupenda kuyasema kwa kuwa tulikuwa tukizungumza "in confidence"

Siyo walikuwa wananifatilia bali tulikuwa tukifatiliana.
Sasa ni rafiki zangu.

Walinipa na madarasa nisomeshe kwenye vyuo vyao.
Wenyewe wanasema hawana uadui wa kudumu wala urafiki wa kudumu.

Wao ni watu wa maslahi.

Hayo mengine ya "wafadhili wangu" yatatuharibia mjadala.
Epuka lugha hiyo haina maana.

Majuzi tu nilikuwa Ujerumani sasa na wao "wafadhili wangu?"
Au hujui kuwa hawa ni watu wa Martin Luther?

Jana nimepata mwaliko tena kutoka chuo humu humu Afrika na wao "wafadhili wangu?"
 
Vyombo vya dola mwaka 2006 kama ilivyo leo vinaongozwa na Waislamu. Kwanini wasiseme ni waislamu serikalini wanawadhalilisha Waislamu wenzao? Mwaka 1964 waliowekwa kizuizini hawakuwa waislamu peke yao.
Wakijiji sasa unazeeka vibaya! husikii siku zote kuwa ni MFUMO na wale wa Waislamu wapo pale kuutekeleza watake wasitake?
 
Hivi matatizo ya Tanzania ni uislam na ukristo eeh?
KUNDI- A;
JK-Islam, Pinda-Mkristo, CJ-Islam, AG-Mkristo, IGP-Islam, CDF-Mkristo, Judicial Administrator General-Islam, Speaker-Mkristo, mawaziri/manaibu changanyikeni; kadri ilivyompendeza raisi(Islam) wakuu wa mikoa/wilaya-changanyikeni;kadri ilivyompendeza Rais(Islam),makatibu wakuu-changanyikeni=kadri ilivyompendeza rais(islam), wabunge-changanyikeni;kadri ilivyowapendeza watanzania( huku ikidaiwa majority ya watanzania ni Islam). viongozi wa dini (maaskofu, mashekh, manabii, mitume, wazee wa upako, maimam nk)-changanyikeni;kadri inavyowapendeza waaminio.
hivi hamjagundua tu hilo ndio kundi linayoitafuna hii nchi?ndio waendesha ma VX/GX V8, ndio wajuao Iran,Mecca, Rome, America nk kukoje, ndio wanaofanya check up India SA na kwingineko?
KUNDI-B;
Makonda, madereva wa hiace, waalimu, manesi, wakulima na kila anaelala akiwa hoi-changanyikeni;kutegemea umezaliwa familia gani. ila unaweza toka mkono wa Mungu ukikufukia;eg Dimond, Late Kanumba nk au kwa kiasi gani unajua kujipendekeza au kuserve interests za kundi A hapo juu (inadaiwa hata Josephat Joseph alikua konda,source;thread moja humu JF).
Watanzania tuache ujinga, adui yetu ni hilo kundi A hapo juu na si vinginevyo. Na ndio wanatuchonganisha kikinuka, hao kina mleta mada wanasepa si unamsikia ujermani, usa, iran kokote ye anamarafiki, wa Vatcan wataenda, wa Saudia, Dubai wataenda mi nawewe tunaenda wapi?tatachinjana kama kuku. Ni kwa manufaa ya Rulling class tuendelee kupumbaa na huyu dini yangu, huyu chama changu, huyu kabila yangu wakijifanya wenzetu wakati wao k/koo wanalala kwe maghorofa mi nawewe tunalala shimoni.
 
Wakijiji sasa unazeeka vibaya! husikii siku zote kuwa ni MFUMO na wale wa Waislamu wapo pale kuutekeleza watake wasitake?

Ndivyo mnavyodanganyana kuwa JK hana say ktk uongozi wa nchi hii? nani kawateua hao vigogo wa nchi? acheni mawazo ya kitoto na kijinga
 
Ndugu Mohamed ni jukumu lako kufuatilia utolewe kwenye hiyo listi kama unaamini kwamba wewe huna ushirikiano na magaidi ama hata hisia zenye mwelekeo wa kigaidi.
 
Wee jamaa unaonekana ni mtu mzima na msomi lakini hoja zako ni za kitoto ile mbaya! Hivi wakati wa kipindi cha Nyerere ni watu wangapi waliokuwa detained kutokana na sababu mbalimbali? Au walioondoshwa na kurudishwa kwao; wazungu kwa waafrica? Tukianza kuwa na akili na mawazo mgando kama haya, basi hata wakinga watakuja na kichwa cha habari kinachosema udhalilishaji dhidi ya wakinga kwa kuwa tu Tuntemeke Sanga alinyanyaswa na Nyerere. Au wale watu wa Ukerewe watakuja na hoja kama hizo hizo kwa kuwa wengi wa walioko kule walipelekwa kama adhabu. Ni ufinyu wa fikra, kutolea mfano wa shehe aliyerudishwa Zanzibar kama mfano wa unyanyasaji dhidi ya uislamu.

Ninapata shida sana kukuelewa wewe binafsi na pia uwezo wako wa kuchambua mambo. Ni watu wangapi wamekatwa, achilia mbali uwanja wa ndege na kusingiziwa hizo kesi za madawa ya kulevya na hata mauaji? Ni kwa vipi kukamatwa kwako ukuhusishe na Uislamu? Nyie waislamu kama mtaendelea kuwa na akili finyu hivi hivi, mtaipeleka nchi vitani hii. Yaani wasomi wa elimu dunia kama wewe ambaye tulidhani muwe mmestaarabika, na nyie mnaendekeza ujinga uleule wa mafundisho ya madrasa. Kama na wakristo wangekuja na mafundisho ya kanisani na kutaka yaongoze nchi mnadhani kungekalika? Acheni fikra mbovu na finyu ya kuwazia udini kila wakati!

Jenga hoja kistaarabu nitajadili nawe na ninakuhakikishia utanufaika na maandishi yangu.
 
Mzee M. Said:

a. Wale waliokukamata uwanja wa ndege walihoji nini kuhusu Uislamu wake na harakati zako kama mtetezi wa haki za Waislamu?

b. Wale waliokukamata katika kukuhoji walihoji jambo lolote ulilolesema kwenye ule mkutano wa Iran?

c. Kuna yeyote aliyetoea kauli ya aina yoyote kuhusu shughulii zako kama Muislamu na alisema nini ambacho kilikukwaza?
 
Ivi kumbe adui wa muislam ni mkristo?mbona wachungaji wanakamatwa na madawa manaake wanapekuliwa..hata mtoto wa mengi alipekuliwa na ni mkristo
 
Hili la Utumwa zuri sana lakini kwanza itabidi tuanze na Transatlantic Slave Trade. Una ubavu tuanze kazi? Unajua kulikuwa na meli inayobeba watumwa kupeleka Marekani ikiitwa Jesus?
Mkuu, waarabu na wazungu wote walitumia dini kutufanya watumwa,so kama na wewe ni mwafrika utakuwa umenielewa.
 
Mzee M. Said:

a. Wale waliokukamata uwanja wa ndege walihoji nini kuhusu Uislamu wake na harakati zako kama mtetezi wa haki za Waislamu?

b. Wale waliokukamata katika kukuhoji walihoji jambo lolote ulilolesema kwenye ule mkutano wa Iran?

c. Kuna yeyote aliyetoea kauli ya aina yoyote kuhusu shughulii zako kama Muislamu na alisema nini ambacho kilikukwaza?

Hawakuwa watu wenye uwezo wa kunihoji.
Kilichokuwa kinatafutwa na kuwaridhisha Waamerika kuwaeleza kuwa "tunashughulika."
 
Afu huyo shehe aliyekuwa rafik yake nyerere ulitaka wawe marafik milele!hujui watu wanagombanaga..waliona hawaendan kla mtu akachukua hamsin zake.
 
Hawakuwa watu wenye uwezo wa kunihoji.
Kilichokuwa kinatafutwa na kuwaridhisha Waamerika kuwaeleza kuwa "tunashughulika."

Kwa hiyo tangu wakukamate hakuna yeyote aliyesema jambo lolote baya juu ya Uislamu, Waislamu au Mtume (SAW)? Wote walikutendea kwa staha na heshma?
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom