Udhalilishwaji wa waislam na vyombo vya dola

Ikatokea umeanzisha thread yeyote hapa jamvini(hasa ya siasa au dini) alafu ukaona watu kama Mzee mwanakijiji,
Mkandara,Nguruvi3, Kiranga,Ogah,Chama wa G,mboto,Pasical,FJM, Mwita manyara,Mchambuzi,NazDaz na wale wote
wenye kufanana na hawa watu, ukakuta wameingia kwenye hiyo thread yako na wanaanza kutoa macoment basi ya
kupasa ujiandae kwa hoja na si viroja....yaani vinginevyo ni lazima ule chocho! chezea hao watu wewe. So binafsi
sishangai babu yangu Mohamedi saidi kuingia mitini! hata ingekuwa ni mimi lazima ningekula chocho....chezea hao watu wewe!
 
Hoja nyingine zinasikitisha kama si kushangaza! Kuna hawa wanaozungumzia mfumo kristo na ukiwauliza wananyooshea kidole baraza la Mitihani Tanzania. Hii ni kama ile simulizi ya Mwanakondooo na chui kwenye Ngano za Esopo.

Zamani watu hawa walikuwa vidole vyao wakivielekeza Ikulu; Mwalimu akatoka akamwachia mwenzao! Wakaanza kunyooshea vidole Wizara ya Elimu; akawekwa mwenzao! Na utawala huu wa awamu hii, nahisi rais akiogopa kuyaudhi makundi haya, amehakikisha wizara hiyo inashikwa na mwenye imani yao hao toka aingie na nina uhakika atamaliza wizara hii ikiendelea kushikiliwa na wenye imani hiyo hiyo. Sasa Ngebe za magenge yale zimehamia Baraza la mitihani!! Yaani rais mwenzao, Makamu wa rais mwenzao, waziri wa Elimu mwenzao, mkuu wa kitengo cha upelelezi (usalama wa taifa) mwenzao; lakini hawa watu bado wanauona mfumo kristo katika baraza la mitihani!!! Hawaishi kulalama kuwa baraza la mitihani linawahujumu, je huyu mkuu wa kitengo cha upelelezi ameshindwa kupandikiza watu wa usalama mle ndani ya baraza wakasambaratisha hiyo dhulma, na badala yake huwa anawapasha kwa siri tu kuwa wanabaguliwa?

Hiki ni kitovu cha unafiki na waseme kuwa nia yao si kupambana na mfumo wanouita mfumo kristo, ambao kikweli haupo. Nia yao ni kupambana na wasio na imani yao ili hatimaye wausimike mfumo wa imani yao ndani ya utawala!! Naam, siku zote watu hawa hujigamba kuwa imani yao ni mfumo kamili wa maisha ukihusisha na mambo ya utawala. Ikiwa nia yao ni kusimika mfumo wao wa imani katika utawala, basi waanzishe vyama vyao vya siasa visimame rasmi vikieleweka nia yake nini!! Hawa wanaotajwa tajwa ni visingizio tu, kama vile visingizio vya Chui dhidi ya mwanakondoo kwenye zile ngano za Esopo, nia yake ikiwa kumshambulia na kumla mwanakondoo.

Huyu msomi wetu Mohammed Saidi ni msemaji mkuu wa makundi yenye imani, fikra, misimamo na mwelekeo huu. Harakati zao zinakosa nguvu tu kwa kushindwa kuungwa mkono na wenye imani ya dini kama yao; ambao walio wengi wanaona dini kama dini na si chombo cha kutawala (kama vyama vya siasa). Ki-ukweli udhaifu wa hoja zao ndo tatizo kubwa ambalo linawafanya wengi wa wenye imani kama yao washindwe kuwaamini na kuwafuata. Mbinu zao zimebaki kwenye kutoa vitisho vya kishabiki kama tulivyoona wakitishia kugomea sensa!
 
ikatokea umeanzisha thread yeyote hapa jamvini(hasa ya siasa au dini) alafu ukaona watu kama mzee mwanakijiji,
mkandara,nguruvi3, kiranga,ogah,chama wa g,mboto,pasical,fjm, mwita manyara,mchambuzi,nazdaz na wale wote
wenye kufanana na hawa watu, ukakuta wameingia kwenye hiyo thread yako na wanaanza kutoa macoment basi ya
kupasa ujiandae kwa hoja na si viroja....yaani vinginevyo ni lazima ule chocho! Chezea hao watu wewe. So binafsi
sishangai babu yangu mohamedi saidi kuingia mitini! Hata ingekuwa ni mimi lazima ningekula chocho....chezea hao watu wewe!

hao uliowataja ndio coba wenyewe! Udhalimu wao kwa wislamu ni mkubwa hapa tanzania.
 
hiii hoja ngumu.......tumezoea kulalamika....kwa hivyo mnataka wote tufuate sheria zenu waislamu....
 
Sioni euledi wowote kwa huyu mzee zaidi ya kujenga chuki za kidini. Anaongelea "manyanyaso" ya watu kwa sababu ni waislamu, na wananyanyaswa na watawala. Kinachonifanya nimuone sio mweledi, anajadili kwa kuwahusisha watawala wanaonyanyasa waislamu na ukristo, simply because Nyerere alikuwa mkristo. Anashindwa kabisa kusema ni kwa nini "manyanyaso" haya yamekuwepo hata wakati ambao mtawala mkuu ni muislamu!!! Hivi wewe huoni katika hali kama hii kunakuwa na maswali mengi zaidi ya majibu. Mweledi yeyote anayeongelea suala la watu kunyanyaswa (na sometimes kuuawa) na watawala anatakiwa azingatie yafuatayo
- Sio wahanga wote ni wa dini moja
- Sio watawala wote walioamuru hayo ni wa dini moja
- Siasa na itikadi vimehusikaje
- Kufungamana na mataifa fulani ya nje kumehusikaje
- Mhanga wa manyanyaso alikuwaje tishio kwa watawala na/au taifa

Sio mtu anakuja na hoja dhaifu saaaana kuwa waliotendewa vibaya na watawala ni kwa sababu walikuwa waisalmu!!! wakati tunajua akina Oscar Kambona hawakuwa waislamu!!!

Heshima yako mkuu, nakuelewa sana unacho kisema labda nikili kwamba kosa nililo fanya ni kutosoma post yake in full. Baadae nilipo soma kwa kina ndio nikagundua kwamba kuna walakini fulani, kwa mfano: Anaposema kwamba kama angekuwa anatoka ziarani VATICAN hakuna mtu yeyote angemuhoji; Statement hiyo ilinishangaza SANA!!! alafu niliwahi kosoma somewhere akimsema marehemu Dk. Kyaruzi kana kwamba haukuwa mkweli kuhusu wadhifa alio kuwa nao kwenye chama cha TAA in terms ya mchango wake katika harakati zao! Si hilo tu hata ili la ku-conveniently avoid kutaja majina ya MaRaisi/Wakuu wa tahasisi za Serikali zinazo simamiwa na Waislaam wenzake zilizo husika katika matukio ya kuzuia fujo au maandamano yasio na kibali, badala yake kuilahumu Serikali wholesale! Siamini kama anashindwa kuwataja kwa bahati mbaya au ana kitu kingine moyoni MWAKE.
 
Why do Muslims like to complain, have you ever asked yourself these questions???

Where in the world is the beautiful and peaceful Muslim country that millions of people are trying to immigrate to?
Where in the world is that beautiful and peaceful Muslim culture that other nations so strongly admire?
Where in the world has the beautiful and peaceful religion of Islam created a society characterized by freedom, justice, and human rights for all that are godly?
Where in the world has the beautiful and peaceful religion of Islam produced economic prosperity and opportunity for the majority of its adherents?
 
jifunze ku summarize na wewe.... we unadhani tuna muda wa kusoma mahekaya marefu hivi..pole muislamu..
 
Heshima yako mkuu, nakuelewa sana unacho kisema labda nikili kwamba kosa nililo fanya ni kutosoma post yake in full. Baadae nilipo soma kwa kina ndio nikagundua kwamba kuna walakini fulani, kwa mfano: Anaposema kwamba kama angekuwa anatoka ziarani VATICAN hakuna mtu yeyote angemuhoji; Statement hiyo ilinishangaza SANA!!! alafu niliwahi kosoma somewhere akimsema marehemu Dk. Kyaruzi kana kwamba haukuwa mkweli kuhusu wadhifa alio kuwa nao kwenye chama cha TAA in terms ya mchango wake katika harakati zao! Si hilo tu hata ili la ku-conveniently avoid kutaja majina ya MaRaisi/Wakuu wa tahasisi za Serikali zinazo simamiwa na Waislaam wenzake zilizo husika katika matukio ya kuzuia fujo au maandamano yasio na kibali, badala yake kuilahumu Serikali wholesale! Siamini kama anashindwa kuwataja kwa bahati mbaya au ana kitu kingine moyoni MWAKE.

Siku zote mkuu mi nasema haya malalamiko ya 'waislamu' hayatolewi na waislamu sio kwa masuala ya waislamu. Mtaani na maofisini huku tunaishi na waislamu, tena waislamu kweli kweli. Ukijadiliana na muislamu ana kwa ana, hakuna aliye na malalamiko ya aina hii.
Huu ni mchezo tunachezewa na watu wachache wenye ela na mafisadi. Wametumia vizuri sana mbinu ya wagawe uwatawale. Wamefadhili watu kwa hoja za 'kutetea' uislamu. Wamefadhili uanzishwaji wa redio za 'kiislamu'. Wanafadhili makongamano yenye mlengo wa kuchochea chuki baina ya waislamu na watu wengine. Wana mtandao mkubwa wa 'masheikh' Tanzania nzima ambao baadhi wanajijua na baadhi hawajui kuwa wanatumiwa.
Lengo lao kubwa ni kuhakikisha kuwa serikali inayofuata inabaki mikononi mwao. Kwa bahati mbaya watanzania wengi bado hawajaligundua hili, lakini wakiligundua, itakuwa too late!!!
 
Why do Muslims like to complain, have you ever asked yourself these questions???

Where in the world is the beautiful and peaceful Muslim country that millions of people are trying to immigrate to?
Where in the world is that beautiful and peaceful Muslim culture that other nations so strongly admire?
Where in the world has the beautiful and peaceful religion of Islam created a society characterized by freedom, justice, and human rights for all that are godly?
Where in the world has the beautiful and peaceful religion of Islam produced economic prosperity and opportunity for the majority of its adherents?

Mkuu usikubali kutekwa na wapumbavu wachache wanaotugawa. Sio culture, wala jiographia inayotutofautisha tusio waislamu na waislamu. Waislamu ni sawa na wewe, wana upendo kama wewe, wana akili kama wewe, ni wastaarabu kama wewe, na uislamu ni upendo. Kitu ambacho tunapaswa kujua ni kuwa kuna watu wachache kwa maslahi yao binafsi wanautumia uislamu kuwagawa watanzania, na hata watu wa mataifa mengine.
 
Mkuu usikubali kutekwa na wapumbavu wachache wanaotugawa. Sio culture, wala jiographia inayotutofautisha tusio waislamu na waislamu. Waislamu ni sawa na wewe, wana upendo kama wewe, wana akili kama wewe, ni wastaarabu kama wewe, na uislamu ni upendo. Kitu ambacho tunapaswa kujua ni kuwa kuna watu wachache kwa maslahi yao binafsi wanautumia uislamu kuwagawa watanzania, na hata watu wa mataifa mengine.

well said chief, but take it from me, these people love to complain a lot, find time to have a talk with them, very few posses the qualities you have pointed out, but the majority are headache. Just use your commonsense how was this religion spread??? Then we can be on the same page. Allllll the bessssst
 
Duh mpaka leo Mohamed Said hajatia uso kwenye huu uzi kweli nimeamini JF ina vichwa vya ukweli.Pole mzee wa Gerezani umekimbia uzi wako mwenyewe ha ha ha ha siku nyingine jipange vizuri.
 
Shukran sheikh kwa ujasiri wako wa kuitetea dini ya kiislam kwa hali na mali INSHA ALLAH MUUGU akupe ujasiri zaidi ya hapo AAAMMMMMMMMMMMMMIIINNNNN
 
tatizo sio uislamu bali matamshi uliyoyatoa nakuhakikishia hata kama ungekuwa mkristo kwa matamshi yale wakubwa hawa akina bush na blair wasingekuacha salama. mbona dr. ulimboka alipigwa akabakiza kufa je ni muislamu. mbona mwandishi Daudi Mwangosi amepigwa na kuuawa je alikuwa muislamu, acha kutugombanisha ss watanzania hatuna udini bali wenye udini ni ccm ebu angalia safu yao ya uongozi
 
Hivi mambo yako binafsi kwa nini mnakimbilia kwenye UISLAM?
Kwa nini mnapenda kulalama tu, na kuhusisha UISLAM na tuhuma zako binafsi?
Kwa kuwa wewe ni muislamu, basi hakuna halal kukushuku?
Kwa vile we muislamu, serikali ikuogope kuwa huwezi kufanya JINAI?
Mnachofanya kinazidi kudhalilisha DINI yenu, ingawa mnaona mko sawa!
 
UDHALILISHWAJI WA WAISLAM NA VYOMBO VYA DOLA VYA TANZANIA

Utangulizi

Sheikh wa kwanza kudhalilishwa na serikali ya Tanzania alikuwa Mufti wa Tanzania kwa wakati ule Sheikh Hassan bin Amir ambae kwa amri iliyotolewa na Julius Nyerere alikamatwa nyumbani kwake usiku wa manane akiwa kavaa khanga tu na akachukuliwa hivyo hivyo hadi uwanja wa ndege na kurejeshwa “kwao” Zanzibar. Kisa cha yeye kufukuzwa Bara ni kirefu na kwa sasa hapa si mahali pake kueleza. Nimekiweka kisa cha Sheikh Hassan bin Amir mwanzo kwa kuwa kina nafasi ya pekee katika historia ya Waislam na mapambano yao na serikali toka uhuru upatikane mwaka 1961. Lakini mwaka wa 1964 masheikh wengi waliwekwa kizuizini kwa amri ya Nyerere hiki nacho ni kisa kingine kinachohitaji wakati maalum kuhadithiwa. Baada ya haya ndipo kwa mara ya kwanza moto wa makumbi ukajitokeza juu na Waislam wakapambana na serikali katika mitaa ya Dar es Salaam mwaka 1993 na mabomu ya machozi na risasi zikapigwa. Haya ndiyo yalikuwa maandamano ya kwanza kufanywa na Waislam baada ya uhuru. Hili lilikuwa sakata la kuvunjwa mabucha ya nguruwe. Damu ya Waislam ilimwagika. Masheikh kumi na moja wa Wilaya ya Kinondoni walikamatwa pasi na adabu usiku wa manane majumbani mwao, wakapigwa pingu na kutupwa katika malendrova ya polisi kama majambazi. Lakini haya yote si kitu tokeo lililotokea siku ya Jumatano tarehe 4 Julai lilifurtu ada. Sheikh Nurdin Kishki akiwa na ugeni wa masheikh wenzake kutoka Yemen ndani yao akiwapo Mufti wa Yemen walivamiwa na askari waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia wakiwa njiani wakitokea Tanga na wakagaragazwa chini huku wakionyeshwa mitutu ya bunduki. Hii ilikuwa habari kubwa lakini vyombo vyote vya habari kama ilivyo ada kwa mambo yanayowahusu Waislam vyombo vyote muhimu vilipuuza stori hii.

Baada ya utangulizi huu naeleza kisa kilichonifika mikononi mwa vyombo vya dola miaka sita iliyopita:

Mkasa Wangu wa Kukamatwa Uwanja wa Ndege wa Mwl. Nyerere, Dar es Salaam Mwaka 2006

Mohamed Said

“Mwaka 2006 Radio Tehran walipendekeza jina langu rehekwa Wizara ya Mambo ya Nje Iran wanialike katika hawli ya Imam Khomeni. Sababu ya ya mie kualikwa ni kuwa mara kwa mara nilikuwa nikifanya mahojiano na Radio Tehran Idhaa ya Kiswahili kuhusu siasa za Tanzania hususan wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 na ikatokea kuwa yale mahojiano yangu yakawa yanapendwa na wasikizaji wa Afrika ya Mashariki na Kati na sehemu za Emirati. Nilkwenda Iran na waalikwa walikuwa kutoka dunia nzima na wa kila aina, waandishi, wahadhiri wa vyuo vikuu, wasomi wa kawaida, mawaziri wa serikali kutoka nchi tofauti na watu wengine wengi. Msafara wetu wa wageni kwenda mahali ulikuwa ni msururu wa mabasi zaidi ya kumi yakisindikizwa na kimulimuli cha polisi. Kutoka Tanzania nilikuwapo mimi pamoja na waandishi kutoka Daily News na Kituo Cha TV cha Channel Ten. Nikiwa Tehran niliingia studio za Radio Tehran Idhaa ya Kiswahili na tukafanya mahojiano na mtangazaji wao mashuuri Abdulfataa Mussa na wenzake na vilevile kurekodi vipindi vingi kuhusu hali ya Waislam Tanzania.

Mambo yalianza wakati sasa narudi Dar es Salaam na ndege ya Emirates iliyokuwa inatua usiku. Inaelekea maofisa wa pasi pale uwanjani walikuwa na taarifa zangu mapema na walikuwa wakinisubiri kwa hamu kubwa kwani nilipotoa pasi yangu kwa afisa wa pasi hapo ndipo shughuli za kunishughulikia zilipoaanza. Mimi sikuwa na hili wala lile. Nikawa namuona yule dada aliyekuwa kwenye kile kizimba akikukurika na pasi yangu akiitia katika mashine na kuitoa mara kadhaa. Fikra iliyonijia kwa haraka ilikuwa mashine ni mbovu na harakati zile zilikuwa ni kurekebisha mitambo. Kumbe sivyo wahusika nadhani walikuwa wanahakikisha kuwa mimi ndiyo huyo waliokuwa wakimwinda na kumsubiri na sasa kapatikana, kaingia mwenyewe kwenye mtego na kanasa. Yule afisa wa pasi akanambia nikae pembeni natakiwa kwa mahojiano na watu wa usalama. Hofu haikuwa imeniingia kwa kuwa nilikuwa natambua kuwa harakati dhidi ya ugaidi zilikuwa zimepamba moto na labda nilitakiwa kwa mahojiano mafupi kutaka kujua nyendo zangu. Sikujua wala kutarajia kuwa mshtuko mkubwa ulikuwa unanisubiri.

Nilichukuliwa hadi kwenye chumba kimoja na hapo niliwakuta maofisa wa usalama watatu wakanikaribisha kwa taadhima kisha wakanambia kuwa niko chini ya ulinzi kwa kuwa zimewafikia taarifa zangu kuwa mimi nasafirisha mihadarati. Mpaka hapa sikuwa na hofu bado ilinijia picha kuwa yawezekana wamefananisha majina. Niliwaambia huenda Mohamed Said muuza madawa ya kulevya siyo mimi niliye mbele yao. Wakaniambia kwa kujiamini kabisa kuwa taarifa zao ni madhubuti muuza unga ni mimi na wamekuwa wakinifuatilia siku nyingi. Hapo ndipo walipotoa pasi yangu na kuniomba niitambue kama hiyo pasi ni yangu au la. Niliwajibu kuwa hakika hiyo ndiyo pasi yangu khasa. Wakaniamuru sasa tutoke twende nikachukue mizigo yangu ili wafanye upekuzi wa mihadarati katika mizigo niliyotokanayo Tehran. Hapo ndipo nilipojuwa kuwa niko katika lindi kubwa la matatizo na ubongo wangu ukaanza kufanya kazi kwa haraka huku nikosoma dua kumuomba Allah ulinzi wake kwani kwa hakika nilijua kama ni njama zimekamilika na leo imefika siku yangu. Nikajiuliza itakuwaje watakapotoa madawa kwenye mizigo yangu. Nikaanza kufikiri vichwa vya habari vya magazeti yatakavyopambwa na habari zangu. Ikanijia yakini kuwa watu wa usalama wameniwekea madawa ya kulevya katika mizigo yangu ili waniangamize na maadui zangu wapumzike na shari yangu.

Nilimgeukia yule ofisa mkuu aliyekuwa ananihoji nikamwambia kuwa sitokubali kugusa mizigo yangu bila kuwapo mashahidi isijekuwa mizigo yangu ishawekewa hayo madawa ya kulevya kwani nilikotoka mizigo ilikuwa imekaguliwa na ilikuwa salama. Hoja yangu kubwa kwao ilikuwa kupata uhakika kutoka kwao kuwa wananijua vizuri kiasi cha kuthibitisha kuwa kweli mie ni msafirishaji wa madawa ya kulevya. Jibu nililopewa ni kuwa wao wanafanya kazi kutokana na taarifa zilizowafikia. Wakasema, “Sisi tunazo taarifa zako kamili kuwa wewe ni msafirisha madawa ya kulevya.” Nikawauiza, “Baada ya kupata taarifa hizo zangu nyie mmechunguza kutafuta ukweli?” Wakasema, “Ndiyo maana leo tumekukamata.” Nikawaambia, “Si kweli kama kwa sababu mie nafahamika Dar es Salaam takriban kwingi maana ndio nilikozaliwa na kukulia. Hapo Kariakoo ukiwaambia watu kuwa Mohamed ni “Mzungu wa Unga” kila mtu atacheka maana huo kwao ndugu zangu ni mzaha mbaya.” Walitaka kujua nilkwenda kufanya nini Iran. Niliwaambia nilialikwa na serikali ya huko kuhudhuria mkutano. Wakataka kujua vipi nilipata mwaliko. Nikawajibu kuwa hilo swali sina jibu labda waiulize serikali ya Iran. Nikawaeleza kuwa mbona siku zote napita hapo uwanjani nikenda sehemu tofauti duniani kwa mialiko na kutoa mada sijakamatwa kimezidi nini katika hii safari ya Iran? Niliwaeleza kuwa miezi michache iliyopita nilikuwa Chuo Kikuu Cha Ibadan kwa mwaliko tena mkutano umefadhiliwa na serikali ya Amerika na wamenipa na tiketi toka Dar es Salaam hadi Lagos na kuniweka hoteli na kunilipa fedha. “Mbona hamkunikamata wakati ule?” Ikawa swali na jibu swali. Nikafungua mlango mwingine nikawaambia, “Nakuapieni nyie msingethubutu kumkamata Mkristo anaetoka Vatican mkutanoni. Lakini kwa kuwa mie ni Muislam sina wa kunitetea. Nchi hii nani atakuuliza kwa kumnyanyanyasa Muislam?” Walishtuka na wakawa wanyonge sana wakasema si kweli kuwa naponzwa na dini yangu.

Baada ya kukurukakara nyingi na mabishano makubwa kuhusu mie kukubali kufanyiwa upekuzi wa mizigo yangu alikuja binti mmoja katika wao na yeye akanihakikishia kuwa wao ni serikali na sio wahuni. Hawathubutu kuniwekea dawa katika mizigo yangu hivyo akanisihi sana kwa upole nikubali ili wajitoe wasiwasi na wataniachia endapo hakuna kitu. Niliomba apatikane shahidi wa kushuhudia mizigo yangu kabla ya kufanyiwa upekuzi lakini hakuna mtu aliyekubali kuchukua dhima ile katika maofisa waliokuwa kazini pale uwanja wa ndege usiku ule. Upekuzi ukafanyika hadi mwilini. Hakuna kitu. Wakanipela katika choo maalum cha kutolea madawa kwa njia ya haja kubwa. Nikakataa kujisaidia pale. Ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kuona choo kama kile. Choo chenyewe ni cha aluminium. Tofauti na vyoo vya pale ambavyo siku zote ni vichafu, hiki kilikuwa kisafi sana kiasi mtu unaweza hata kutengewa chakula na akala bila ya kuhisi kinyaa.

Nilitegemea wataweka ahadi yao kuwa ikiwa hawatakuta madawa ya kulevya katika mizigo yangu watanirejeshea uhuru wangu wataniachia niende nyumbani. Haikuwa hivyo. Wakanirudisha ofisini kwao. Sasa wakaacha madawa ya kulevya wakahamia katika vitabu na “audio cassette” nilzokuwa nimepewa kama zawadi kule Tehran wakaniluliza kwa nini naingiza vitu vile khasa kanda za Khomeni na vitabu vyake nchini. Nikawauliza, “Kwani kanda na vitabu vya Khomeni haviruhusiwi kuingizwa Tanzania? Maana mimi hata nyumbani kwangu hii leo mkifika nina vitabu vya Khomeni na wanafalsafa wengine kama Karl Marx ambao nimesomeshwa pale Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.” Sasa hapo ikaja kejeli. “Ala wewe mtu wa Kariakoo lakini umefika hadi Chuo Kikuu!” Sikujibu kitu. Awali waliponitia mbarani waliniuliza kwetu na nikawaeleza kuwa nimezaliwa Kariakoo.

Hawakunipa jibu kuhusu kuingiza vitabu na cassette za Khomeni. Ikawa sasa kama vile wameishiwa maswali. Nikaona kuwa sasa ni zamu yangu nami kuwapiga maswali. Yule aliekuwa akinihoji nikamwambia, “Mimi wewe nakufahamu vizuri sana kwa sababu ukicheza mpira Simba Sports Club na mie ni mpenzi wa club hiyo toka utoto wangu wakati huo ikiitwa Sunderland na mmoja wa baba zangu alikuwa mchezaji marufu wa club hiyo katika miaka ya 1950 akafiikia hadi kucheza Kombe la Gossage.” Nilihisi amepata mfadhaiko kidogo akanambia,“Unanifananisha yule aliekuwa akicheza Simba ni ndugu yangu.” Alikuwa anasema uongo lakini mie nikamkubalia. Hapo nikajua kuwa nishampata sasa hana nguvu tena ya kuuliza maswali. Kusema uongo ni dalili ya kujihami. Nikamrushia kombora lingine, “Sasa tuhuma za madawa ya kulevya zimekwisha tuko katika kwa nini naingiza vitabu vya Khomeni nchini?” Akanijibu kinyonge, “Tumeridhika huna madawa.” Kufika hapa tukawa tumemaliza mahojiano.

Wakati huo sasa ni usiku wa manane na nishapeleka SMS kwa sahib yangu mmoja bingwa wa mambo ya mtandao wa kompyuta kumjulisha kuwa nimekamatwa uwanja wa ndege kwa tuhuma za uongo za kuvusha mihadarati na yeye ile kuipata tu ule ujumbe wangu akaifahamisha dunia kuwa nimekamatwa uwanja wa ndege nikitokea mkutanoni Iran na nimebambikiziwa tuhuma za kuingiza nchini mihadarati. Waliponitia mbaroni tu walinionya kuhusu kutumia simu yangu ya mkononi lakini bahati nzuri hawakuninya’ganya. Aliyenipa onyo hili alikuwa mkuu wa kituo cha polisi cha uwanja wa ndege. Huyu rafiki yangu akawa kanisaidia sana maana hadi kumekucha wapenzi wangu wote ndani na nje ya nchi pamoja na vyombo vya habari vinavyonifahamu walikuwa na taarifa za kukamatwa kwangu. (Kwa kipindi takriban miaka ishirini nyuma kwa nyakati fofauti nimekuwa nikifanya mahojiano na radio zote muhimu kama, BBC, VOA, Sauti ya Ujerumani, Sauti ya Iran nk.).

Nikawaomba wale watu wa Usalama waniachie basi nende zangu kulala nyumbani nirudi hapo kesho asubuhi kwa kuwa sikuwa nimebeba madawa ya kulevya. Wakaniambia, “Itabidi tukulaze hapa hadi asubuhi wakubwa wetu watupe amri ya kukuachia. Maana amri ya kukukakamata wewe imetoka juu.”
clip_image001.gif
Sasa hapo ikawa nimelipata jingine. Kumbe wauza unga hawakamatwi hadi amri itoke juu. Sasa kama amri haikutoka ndiyo muuza unga atapita aingize sumu zake mitaani? Hili likazidi kunidhihirishia kuwa kukamatwa kwangu hakukuwa na uhusiano wowote na vita dhidi ya mihadarati bali ni vita vile vile vikongwe dhidi ya Uislam.

Nikawa pale usiku kucha. Sasa wakati niko pale wakidhani nimelala. Wakawa wenyewe kwa wenyewe wanazungumza kuhusu hii ‘operation’ neno walilotumia ni kuwa 'leo tume-dial wrong number.' Wakawa wanasema, “Huyu bwana mbona hakuelekea kama muuza unga tena huyu mtu bwana kasoma kweli kweli” Wanadhani mie nimelala kumbe ni macho nawasikiliza. (Vipi utalala katikati ya michongoma?). We umeona jinsi alivyokuwa akijibu na kuchambua mambo.” Hilo ndilo likawa gumzo lao wakinisifia kwa ufasaha na mantiki lakini wakizungumza kwa sauti ya chini kabisa. Hapa ikanidhihirikia kuwa hawa vijana walikuwa wanatimiza wajibu wao wa kazi tu lakini kiini khasa cha kukamatwa kwangu hawakuwa wanakifahamu.


Walionikamata walikuwa vijana kama wanne na wote walijitambulisha kwa majina ya Kiislam. Nilijua ni waongo kwa kuwa Muislam anonekana katika uso na katika matumizi ya lugha. Lakini yule mchezaji wa Simba ni Muislam na yeye ndiye aliekuwa mkubwa pale akiongoza ile shughuli yote tena kwa kujidai na kujifaharisha sana. Kisa kile kile cha mtumwa anelimishwa na yule anefanya kazi za ndani nyumbani kwa bwana. Ila kitu kimoja lazima nikiri. Wale vijana walikaa na mimi kwa wema na hawakunibughudhi hata kidogo. Hata nilipokuwa nakwenda msalani kijana alienisindikiza alinitaka radhi akasema, ”Nakusindikiza kwa sababu ni sheria lakini sisi tunakustahi kwa hiyo utuwie radhi kwa kukufuta hadi msalani.”

Asubuhi wakubwa wakaja kazini lakini hakuna alienikabili. Walikuwa wakinichungulia kutoka mlangoni kama simba ndani ya kizimba kwenye zoo, nami nikawa najifanya siwaoni. Ndipo akaja mkubwa mmoja tena akaniita kwa jina langu na kwa heshima na bashasha sana, "Bwana Mohamed tuwie radhi sana pamekuwa na makosa kidogo tuwie radhi sasa hivi tutakuruhusu uende nyumbani. ” Akatoka nje akawa akipiga simu. Kisha akarudi ndani akaamrisha nibebewe mizigo yangu na gari la polisi linirudishe nyumbani. Kistaarabu kabisa nikakataa gari ile huku nikifanya maskhara kuwa naogopa gari ya polisi asijepiga simu akasema mrudisheni huyo mtuhumiwa. Ofisi nzima ikacheka. Hapo ndipo wale wakamataji wangu wa usiku wakabeba mizigo yangu nami nafuata nyuma tunatoka nje ya uwanja.
clip_image001.gif


Kilichobaki sasa ni kueleza sababu ya mimi kukamatwa. Mwaka wa 2006 Chuo Kikuu cha Ibadan, Nigeria kilifanya kongamano la kimataifa hapo chuoni kwao kuzungumza kuhusu Ugaidi katika Afrika ya Mashariki na Maendeleo ya Afrika (Conference on Islam, Terrorism and African Development). Mimi ninlitoa mada iliyokuwa na anuani hii: Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience. Katika mada hii nilijikita mahsusi katika kuisema Marekani kwa udhalimu wao duniani. Nikaeleza kuwa huo udhalimu wao ndiyo unaopelekea wao kuchukiwa dunia nzima. Hapa ningependa kufahamisha kuwa mkutano huu wafadhili wakubwa walikuwa Iran na Marekani. Saudi Arabia ilikataa kuchangia mkutano ule. Wakati nasema maneno haya ya kuwakanyaga wenyewe Waamerika wapo hapo mkutanoni.

Baada ya kuwalani Waamerika sasa nikaigeukia serikali ya Tanzania na kuishutumu vikali kwa kupitisha Sheria ya Ugaidi. Hapa nikaeleza kuwa Waamerika wasione kuwa Tanzania imepitisha sheria hiyo ya ugaidi kwa haraka kwa sababu Tanzania ina tatizo na ugaidi. Nikaeleza kuwa sheria hiyo imepitishwa kwa sababu Bunge la Tanzania limehodhiwa na Kanisa na kupitishwa kwa sheria hiyo hakuna uhusiano wowote na ugaidi ila Wakristo wamepata fursa ya bure ya kupambana na Uislam wakitumia serikali ya Marekani kama upawa wao wa kuopolea chinyango ya moto kwenye chungu kinachotokota. Nikauchekesha mkutano kwa kuwaambia kuwa Wamarekani wamefanywa wajinga na Kanisa kwa kuchonganishwa na Waislam wa Tanzania ambao hawana ugomvi nao asilani. Baada ya kusema hayo nikahitimisha kwa kueleza nguvu ya Waislam Tanzania, kwanza kwa wingi wao na kisha kwa historia yao iliyotukuka iliyodumu takriban miaka mia wakipambana na ukoloni wa Wajerumani kwa silaha (1905 1907), kisha ukoloni wa Waingereza (1929 1961) na kuhitimisha kwa kuleta uhuru na kuanzia 1961 hadi sasa wanapambana na nguvu ya kanisa katika kupiga vita Uislam.

Kufikia hapa ukumbi ukawa umepata joto. Wanigeria wamesimama kutaka niwaeleze vipi Waislam watakuwa wamepigania uhuru kisha wako wengi nchini wanaruhusu wao kufanywa raia daraja la pili. Wakashangazwa kuwa hata historia ya mashujaa Waislam waliopigana Maji Maji na kunyongwa na wakoloni na mashujaa walipigania uhuru wa Tanganyika hawatajwi katika historia ya ukombozi. Nilitoa majibu kadri Allah alivyoniwezesha. Nakumbuka kitu kimoja walichosema wale ndugu zetu Wahausa. Walisema hali hiyo iliyoko kwenu haiwezekani kutokea Nigeria kwa kuwa hiyo itakuwa na sawa na kutangaza vita. Kisha wakanihakikishia kuwa sheria hiyo ya ugaidi haitapitishwa Nigeria hata siku moja.

Wapashaji habari wangu wakajanieleza baadae ni hili hitimisho langu ndilo lililosababisha Wamarekani kuleta taarifa Dar es Salaam kutaka taarifa zangu za “ugaidi” ikawa sasa sababu imeptikana ya mimi kushughulikiwa na vyombo vya dola. Ndipo ikatengenezwa hadithi ya kuku jike na ng’ombe dume (cock and bull story) kuwa Mohamed Said ni Mzungu wa unga kwa hiyo akamatwe.

Mkasa huu ulinifika miaka sita iliyopita lakini hadi leo kovu la mkasa ule limebaki katika pasi yangu. Sielewi pasi yangu inaonyesha nini inapotiwa katika compyuta baada ya mkasa huu kwani kama mara tatu husimamishwa kwa muda na kuombwa nitoe maelezo ya ziada kuhusu niendako kila nisafiripo nje ya Tanzania. Nimeshuhudia hali hii Uwanja wa Ndege Amsterdam na Detroit, Marekani. Berlin, Ujerumani niliambiwa mzigo wangu umepotea lakini hata kabla sijatoka uwanjani nikatafutwa na kukabidhiwa mzigo wangu na kwa hili sikuwa peke yangu nilikuwa na mwenzangu, jamaa wa Kiarabu kutoka Misri. Sijui kama mizigo yetu ilikuwa imebakishwa nyuma kwa upekuzi zaidi. Amsterdam, Uholanzi baada ya kupita sehemu zote muhimu za upekuzi wakati naelekea kituo cha mwisho niingie kwenye ndege inayoelekea Detroit, Marekani nikachopolewa kutoka kwenye mstari na nikawekwa pembeni peke yangu kwa usaili wa ziada. New York kadi yangu ya benki ilikataa kutoa fedha kwa siku nzima hadi siku ya pili. Nilikujafahamishwa baadae kuwa “system” ilikuwa inanichunguza kwanza. Ilikuwa siku ya pili baada ya kuonana na maofisa wa benki ndipo kadi yangu ikaanza kutoa fedha. Geneva, Uswisi kadi yangu ilikataa kutoa fedha katika mgahawa. Sikujua kama ni yale yale au haya yalikuwa mengine. Lakini pasi hii afisa wa uhamiaji wa Tanzania alipoiingiza kwenye compyuta yake alimwita mwenzake kuja kutazama kisha wakawa wanacheka. Waliona nini kwenye pasi yangu Allah ndiye ajuaye.”

M
Inahusikaje na sheria hii?! Kuna jukwaa la masuala ya dini.
 
Shukran sheikh kwa ujasiri wako wa kuitetea dini ya kiislam kwa hali na mali INSHA ALLAH MUUGU akupe ujasiri zaidi ya hapo AAAMMMMMMMMMMMMMIIINNNNN

Hivi hapo ww umeona anatetea dini??? acha kushabikia wapuuzi
 
Back
Top Bottom