Udhalilishwaji wa waislam na vyombo vya dola

waislam tunaelewa fika kuwa tunafanywa daraja la pili katika nchi yetu wenyewe. waislam wote wanaelewa,huwezi amini kuanzia primary level to university level,makazini,mitaani mpka majumbani waislam wanaelewa kuwa kuna ubaguzi mkubwa wa kini. tumeongea na tunaongea sana lakini hayapatiwi ufumbuzi, na siku zote binadam haonewi mda wote! kama hakuna ufumbuzi naiona Biafra ya tanzania.
Mkuu,hapo penye rangi nyekundu, ebu fafanua ni kwa jinsi gani waislamu mnabaguliwa! Acha dhana ya jumlajumla ya ubaguzi unaohubiriwa na huyu mzee muovu Mohamed Said. Sema waziwazi wewe binafsi ulibaguliwaje kwa kuwa muislam.Nishule gani na university gani ulibaguliwa?
 
Jamani kila siku kulalamika tu, hakua mambo mengine.

Nimeishia pale kwenye kubomoa mabucha kitimoto aka mdudu nikaacha kusoma. Sasa nyie mnatia mchanga mboga halafu mnataka muangaliwe tu! Nyambaf! Chezea kichapo mpaka unaomba kubatizwa na maji ya bahari.
 
Taarifa hii si ya kweli ni upuuzi na kama vipi umeshindwa nini kututajia kwa majina?
Mi naamini kabisa kua ni ya kweli, sasa kama wao wanasoma kaswida tu na kupigania kuvaa kininja nani atawaweka katika sekta muhimu! Mtaendelea kusoma namba kila siku. Jiulize ni shule gani ya kiislam inatoa best students hapa bongo. Au necta inawachakachua?
 
Haaahaaa Sonara! Endeleeeni tu na mbio hizi. Maana mbio za sakafuni tunajua huishia ukingoni. Kamwe hakuna mtu atakayepata kitu asichofanyia kazi....kamwe hakuna mtu atakayevuna pale asipopanda. Who are you to violate the natural laws and principles that govern our universe?

Asante kwa kunijibia kwani kama nilivyo sema hapo juu kuhusu Hitler na kambarage na majibu yako yameowana na maelezo yangu Hitler alichokipanda kinaendea kushamiri na watu wanakivuna na kamabareage alivyovipanda ndivyo sasa nyie wafuasi wake mnaviendeleza na kuvivuna
 
Asante kwa kunijibia kwani kama nilivyo sema hapo juu kuhusu Hitler na kambarage na majibu yako yameowana na maelezo yangu Hitler alichokipanda kinaendea kushamiri na watu wanakivuna na kamabareage alivyovipanda ndivyo sasa nyie wafuasi wake mnaviendeleza na kuvivuna

Mfuasi wa nani? Chonde chonde hunijui hata nikoje na nafikiri nini. Kwahiyo unataka tuwe na mambo ya udini bila sababu ya msingi wowote? Unajua mimi nina marafiki wa ukweli wa dini tofauti na yangu. Sasa ukiniletea udini nikueleweje? Udini haupo...ila watu wachache wanaoshindwa na kashikashi za maisha ndio wanaoufagilia udini. Baki na dini yako na mimi na dini tuheshimiane, tushirikiane na kusaidiana. Tutafika mbali duniani na hatimaye mbinguni. Uovu utampeleka nani kwa Mwenyezi Mungu? Uongo na kulalamika lalamika kunasaidia nini?
 
Aisee mwandishi wa viroja..unatamani uwe kama yeye lakini ndiyo hivyo..umeishia na kujaaliwa kaundika vi-mistari miwili hapa JF period..

Mohammed ni kiwango kingine kwako.

Kwahilo umesema kweli, Kiwango cha uzushi, uzandi, fitina na uchochezi wa Mohamed Said hakuna anaye mfikia. Hana analoliweza zaidi ya kuzusha. Bahati mbaya amezowea kutoa mihadhara ya uchochezi na chuki kwa watu ambao hawamuulizi maswali. Akileta uchochezi wake hapa jamvini anakutana na wachambuzi wa mambo anapigwa maswali ambayo huwa hana majibu na kuishia kujisifu tu...... mara oh mimi nimetembea nchi nyingi........mara oh nimeandika paper nyingi........., mara oh.......kasome kitabu changu kuhusu..........na longolongo kibao! Tuta ishi kama watanzania wamoja na sio kama maadui kwa imani zetu! Mohamed Said na hila zake ameshashindwa kabisa.
 
Mzee moh'd said mimi nmezaliwa 1991 nadiriki kukuita kilaza, kwa hoja mufilisi.. Prove me wrong kwa kujibu hoja za nguruvi3 hapo juu. Na nakuomba acha hiyo tabia yako ya kutudhalilisha WAISLAMU mwisho wa siku unaufanya uislamu uonekane kama ni symbol ya UJINGA.
 
MS jibu hoja za Nguruvi3 sio unalalamika tu kwamba waislam wanaonewa ukiulizwa wanaonewa vipi unaanza siasa.....usomi wako hauwaasaadii waislam, umewafanya waislam wajione wanyonge na wanaoonewa mbele ya watanzania wenzao,
 
Another conspiracy in the making!!! Naomba nizungumzie hilo la SHEIKH NURDIN KISHKI NA UGENI WAKE KUTOKA YEMEN. Ikumbukwe kuwa kwa sasa Serikali inahaha kufunika wimbi la shutuma kutokana na yaliyomsibu Dr. Ulimboka. Kwahiyo, POLISI wameandaa CONSPIRACY ili kufunika kombe. Katika conspiracy hii, serikali kupitia jeshi la POLISI, imemwandaa SHEIKH NURDIN KISHKI ili ashiriki tukio ambalo limefanana na lile la kutekwa kwa Dr. Ulimboka. Baadaye ile kamati yao inayoongozwa na ACP AHMED MSANGI itakuja na conclusion kwamba waliomteka Dr. Ulimboka walikuwa ni majambzi na ndio hao hao waliomteka/waliomvamia SHEIKH NURDIN KISHKI NA UGENI WAKE!!!. Mkanda wa video hiyo utakuwa mtamu sababu kuna watu wataandaliwa maalum wajifanye wao ndio watuhumiwa na polisi itarusha kwenye vyombo vya habari jinsi walivyowahoji.......kiasi kwamba wenye akili ndogo wataamini ripoti ya POLISI!!!!Sheikh Nurdin Kishki akiwa na ugeni wa masheikh wenzake kutoka Yemen ndani yao akiwapo Mufti wa Yemen walivamiwa na askari waliokuwa wamevalia mavazi ya kiraia wakiwa njiani wakitokea Tanga na wakagaragazwa chini huku wakionyeshwa mitutu ya bunduki.
 
kama kawa mavuvuzela siku zote! waislamu wasifanywe watu wa
kuishi kwa kuonewa huruma kila sehemu! wekezeni kwenye elimu!
hamuwezi kulazimisha "akili ndogo kutawala akili kubwa"! hizi
wivu kama za wanawake walioko ndani ya mitara haziwafikishi popote!
msiongozwe kwa jazba, tafuteni busara!

Mohamed Said, kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho hawa ndugu zetu hutuogopa kwa majina tu ya Kiislaam. Hawana zaidi ya uoga, na uonevu wao wote lakini AlhamduliLllah Uislaam ndio dini inayokuwa kwa haraka kuliko dini nyingine yoyote duniani na hususan hukohuko Merekani, ushahidi huu hapa: Fastgrowing Islam winning converts in Western world - CNN
 
Duniani kuna watu wanafiki sana! yaani kila siku mtu analalamikia mfumo kristu....lakini mtu huyohuyo
kila siku kiguu na njia za kwenda Ulaya na America ambako huko ndiyo chimbuko hasa ya malalamiko
yake yote. Wee unajinasibu hapa oooh nilikuwa Germany nilikuwa USA mara oooh niliitwa na Chuo kikuu
cha Havard nk! sasa huko unafuata nini? hivi hujui kuwa hizo nchi na watu wake ndiyo waliyoleta hiyo
dini unayoichukia? Yale yale ya ndugu zetu wapemba....wanadai Watanzania bara ni makafiri lakini cha
ajabu wao ndiyo wamejazana Uingereza. Jamani tuache unafiki wa kufia hizi dini za kuletewa....Utaki unaacha
 
Mkuu Chamoto

Mkuu wangu kama humjui Mohamed Said utapata shida bure.Kifupi MS ana kale kaugonjwa ka udini hoja zake zote bila kumtaja Nyerere haoni raha.Haya tunakubali Nyerere mbaya lakini tunauliza pia vipi Mzee wa watu nahusika na upotoshaji wa vita ya maji maji.Mwaka 1995 hadi 2005 Rais wa JMT alikuwa Benjamin W Mkapa IGP alikuwa Omar Mahita muislam mwenzako aliyepanda cheo kwa kumrushia mabomu ya machozi kiongozi mkuu wa upinzani wakati huo Mheshimiwa A L Mrema.2005 hadi sasa 2012 Rais wa JMT ni J Kikwete na IGP Said Mwema muislamu mwenzako chini ya uongozi wake mtoto wa mfanyabiashara maaarufu Bwana Reginald Mengi alitaka kubambikiwa madawa ya kulevya uwanja wa ndege wa Dar sijamsikia Mengi akilalamika uovu uliokusudiwa kufanywa dhidi ya mwanae kwakuwa ni mkristo.Tatizo la Mohamed Said ni kusukuma kila jambo baya litakalomtokea kwamba limemtokea kwakuwa anaamini Uislam akienda Airport bahati mbaya akakosa ndege atadai mfumo kristo umesababisha,Mke wake akimwacha atasingizia kuna mkono wa Nyerere.Zikitokea fujo za kugombea uongozi na umiliki wa msikiti atadai Vatican inahusika.Mohamed Said inatosha tunakuomba uache hizo choko choko zako ambazo hazina mashiko wala haziwezi kulisaidia taifa liondokane na umasikini,maradhi,ujinga na ufisadi.

Nyerere kaondoka magogoni mwaka 1985 imeshapita miaka 27.Inashangaza unakamatwa uwanja wa ndege mwaka 2006 bado story yako haikamiliki bila kumtaja unakwepa nini kusema Jakaya Kikwete na IGP Mwema waIslamu wenzako wanatumiwa na wamerekani dhidi ya Uislam ?.



Mzee Mohamed Said naona kama umeamua kurudi kivingine kuleta ile historia yako yawapigania uhuru.

Nimeisoma vizuri hadithi yako ambayo imechukua kama 92% ya mada yako na nimeshangazwa katika matukio hayo ya kusikitisha yaliyokutokea mwaka 2006 hukuwahi kutaja raisi aliyekuwa madarakani kipindi hicho. Vivyo hivyo hukuwahi kutaja nani alikuwa madarakani mwaka 1993 wakati ndugu zetu waislam wanapigwa na mabomu ya machozi lakini hukusita kumtaja Nyerere mara mbili katika paragraph ya kwanza. Unawea kutueleza kinagaubaga kwanini hukuwataja?
 
Last edited by a moderator:
JUKWAA LA WAISLAMU LA KURATIBU MCHAKATO
WA MABADILIKO YA KATIBA TANZANIA
(JUWAKATA)
MUHIMU WA KWAISLAMU WOTE
1. JUWAKATA JUWAKATA ni Jukwaa la waislamu la Kuratibu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Tanzania. Chombo hiki kinaundwa na Jumuiya na Taasisi mbalimbali za Kiislamu sizizopungua 40. Chombo hiki kilizinduliwa rasmi katika kongamano kubwa lililohudhuriwa na kada mbalimbali za Masheikh, wanataaluma na viongozi wa Kiislamu lililofanyika Januari 6,2012 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam na kuhusisha vyombo mbalimbali vya habari. Makao makuu ya JUWAKATA ni Dar es Salaam. JUWAKATA lina mawasiliano ya karibu na Waislamu wa Tanzania visiwani kwa uratibu wa pamoja. Aidha azimio la mkutano mkuu wa Jumuiya na Taasisi za kiislamu, liipa JUWAKATA idhini ya kushirikiana na muislamu au mwananchi yeyote mwenye malengo ya kupatikana katiba yenye missing ya haki na uhuru pasina ubaguzi wa aina yoyote. 2. MAELEZO YA AWALI Nchi yetu imo katika mchakato wa mabadiliko ya katiba ya nchi. Wananchi wa Tanzania wanakabiliwa na jukumu moja la kuhakikisha katiba ijayo itakuwa kwa maslahi ya watanzania wote na yenye kuzingatia haki na usawa bila kujali kbila, rangi, dini wala jinsia. Tukio la kuundwa kwa katiba ya nchi ni miongoni mwa matukio makubwa kabisa katika nchi yoyote ile dunia. Ni kwa sababu hii, mivutano, ushindani, kupigana vikumbo, mizengwe na mahala pengine vita vya wenewe kwa wenyewe hutokea. Ni kwa kutambua ukweli huu, sisi waislamu wa Tanzania tayari tumekwisha ipatia ushauri serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na Tume ya kurekebisha katiba tahadahari y akuzingatiwa haki na uadilifu katika mchakato wote wa mabadiliko ya katiba ili katiba iwe ka faida ya wote wa mabadilliko ya katiba ili katiba iwe kwa faida ya wote na iwe msingi wa kudumisha amani iliyopo. 3. KATIBA YA NCHI NI NINI Katiba ya nchi ni makubaliano ya wananchi kuhusu haki na wajibu mbalimbali kati ya dola na raia na jinsi ya mgawanyo wa madaraka na rasilimali za taifa, mfumo wa utoaji haki na ulinzi na usalama wan chi. Kutokana na ainisho hili la ujumla, makubaliano haya ya katiba yanaweza kuwekwa katika maandiko au yasiwekwe. Hata hivyo nchi nyingi duniani zinaongozwa kwa katiba iliyoandikwa. Mara nyingi tumepata kasikia kwamba ‘katiba ndiyo sheria mama ya nchi’. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, sheria na kanuni mbalimbali zinazoongoza nchi chimbuko lake ni katiba. Katiba hujumuisha mambo makubwa ya kisheria ambayo huandikwa kwa mukhtasari. Kwa mfano kipengele kimoja kinachozuia ubaguzi, kinaweza kukusanya mambo lukuki yanayohusu ubaguzi wa rangi, jinsia, dini, ukabila umri, hadhi katika jamii nk. Kwa muktadha huo Bunge la nchi ndicho chombo kinachoundwa na katiba kwa unadhumuni ya kutunga sheria, kanuni mbalimbali ili kufafanua jinsi ya kutekeleza vipengele vya katiba huska. Sheria na kanuni ambazo hutungwa na bunge, ikiwa zitapingana na katiba ya nchi, sheria hizo huhesabika kuw ani batili (yaani ill and void). 4. Katiba zimegawanyika katika mfungu makubwa mawili. o Katia za kisekula na o Katiba ya Kiislamu. Katiba za kisekula zimebeba taswira kubwa mbili: (a) Katiba za kidikteta na (b)Katiba za kidemokarasia. Katiba za kidikteta ni zile ambazo wananchi hawana kauli juu mambo ya uendeshaji wan chi yao wala hawaruhusiwi kuchagua wawakilishi wao bali mamlaka na madaraka yote ya nci yako mikononi mwa mtu au tabaka la watu wachache. Katiba za kidemokrasia ni ile ambayo wananchi wanashirikishwa katika kuamua nchi yao iendeshwe namna gani na wanashiriki katika kuiendesha nchi kwa kuchagua wawakilishi wao. Katiba ya Kiislamu – Hii hutokana na Qur’n na snnah za Mtume (SWALALLAH ALAYHI WASALLAH) na Ijumaa ya wanazuoni. Wananchi hulazimika kutii na kutekeleza mipango na ibada nyingine kwa kadiri ya uwezo walio nao. Watawala wa Kiislamu huongoza na kutoa hukumu kwa kila jambo kwa kuzingatia mwongozo wa Allah (Subhaanahu Wataala) na Sunnah za Mtume (SWALALLAH ALAYHI WASLLAM). 5. MUUNDO NA VIPEGELE VYA KATIBA YA TANZANIA Muundo wa dola ya Tanzania kwa mujibu wa Katiba ya sasa ni wa ushirikishwaji wa wananchi katika uendeshaji wan chi kupitia wawakilishi ( wabunge, wajumbe wa baraza la wawakilishi na madiwani). Katiba ya Tanzania ina sehemu kuu kumi (10) na ibara (152) kuhusu mambo mbalimbali. Katika sehemu zake kumi (10) na ibara (vifungu) 152 katiba ina sehemu zinazoeleza misingi ya katiba, muundo wa dola, mipaka ya nchi, vyama vya siasa, sera ya nchi, haki za raia na wajibu wao, majukumu ya Serikali, bunge, Mahakama nk. Kwa ujumla kutokana na muundo huu wa katiba ya Tanzania, katiba iliyopo sasa inahesabika kuwa ni miongoni mwa ‘katiba za kidemokrasia’. 6. HATUA ZA MCHAKATO WA MABADILIKO YA KATIBA o Kupitishwa kwa Sheria yamabadiliko ya Katiba Hatua hii ilifikiwa mnamo mwezi wa Novemba, 2011 pale muswada wa Sheria Na. 8 ya mabadiliko ya katiba 2011 ulipopitishwa na Bunge. Kisha yalifuata marekebisho ambayo yalifanyika Januari, 2012. Sheria hii ya mabadiliko ya katiba, ndiyo inayomumika kuongoza mchakato huu. o Kuundwa Tume ya Katiba Tume ya kukusanya na kuratibu maoni ndicho chombo chenye dhima ya kushughulikia sehemu kubwa ya mchakato wa katiba mpya. Chombo hiki chenye wajumbe 30, Mwenyekiti na Makamu wake, kimeundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kushirikiana na rais wa Zanzibar April 6, 2012. Hatua hii imetanguliwa na ile ya bunge la Jamhuri ya Muungano kupitisha sheria ya mabadiliko ya katiba The Constitutional review Act iliyopitishwa Novemba 18, 2011. Tume ya Katiba itakuwa na sekretarieti yake ambayo ndiyo itakuwa mtekelezaji wa shughuli mbalimbali za tume kiufundi Ukusanyaji maoni kutoka kwa Wananchi Tume itaendesha, mikutano (mabaraza) ya hadhara ya ndani na nje, na hata kupokea maoni kwa njia ya maandishi kwa nchi nzima. Hii ndio kazi ya msingi ya tume mara baada ya kuundwa na kuapishwa wajumbe wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano.Baada ya kazi ya kukusanya maoni tume itaandaa rasimu ya katiba mpya itakayotokana na maoni iliyoyakusanya. o Rasimu yaKatiba mpya Baada ya kukusanya maoni na kuandaa rasimu ya katiba mpya iliyotokana na maoni yaliyotolewa, rasimu ya katiba mpya itachapishwa katika vyombo vya habari ili kutoa fursa kwa wananchi kuthibitisha maoni yao. Baada ya hatua hiyo rasimu ya katiba mpyaitakabidhiwa kwa Rais wa Muungano na Rais wa Zanzibar.

Rasimu ya katiba mpya kujadiliwa na Bunge maalum la katiba.Bunge hili litaundwa na wajumbe wafuatao.
i. Wabunge wote wa muungano
ii. Wajumbe wa baraa la wawakilishi Zanzibar
Na
iii. Wajumbe 166 kutoka:-

(a) Vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu
(b) Asasi za kijamii (NGO’s)
(c) Jumuiya za Dini
(d) Makundi ya wakulima
(e) Wafugani.
(f) Taasisi za elimu ya juu
(g) Wafanyakazi
(e) Makundi mengine yenye maslahi ya pamoja
(f) Makundi yenye mahitaji maalum.

Mwenyekiti wa tume ya katiba atasoma rasimu hiyo kwa mara ya kwanza ndani ya bunge maalum la katiba na kukabidhi jukumu hilo kwa Mwenyekiti wa bunge la katiba ili ijadiliwe na bunge hilo na hatimaye kuipitisha au kuirejesha ikafanyiwe marekebisho. Endapo Bunge maalumu la katiba litaipitisha rasimu ya katiba hatua itakayofuata ni kupigiwa kura ya maoni na watanzania wote.

o Kura ya maoni
Baada ya rasimu ya katiba kupitishwa na bunge la katiba itakuwa katiba iliyopendekezwa na itakabidhiwa kwa tume ya Taifa ya uchaguzi yaani NEC na tume ya uchaguzi Zanzibar ZEC kwa ajili ya kuandaa na kusimamia kura ya maoni, kwa kupiga kura ya NDIYO au HAPANA. Ikiwa rasimu hiyo itakubaliwa na wananchi wa bar kwa 50% na visiwani kwa 50% katiba mpya itakuwa imeundwa, na kwa matarajio ya serikali katiba hiyo itaanza kutumika Aprili 26, 2014.


7. KWA NINI WAISLAMU WNASHIRIKI KATIKA MCHAKATO WA KATIBA? Sababu kubwa ni wajibu wa waislamu kupigania haki ili kuwa na katiba nzuri inayolinda haki zetu. Kuwa na katiba inayolinda haki za waislamu kama sehemu ya watanzania ni njia bora zaidi ya hakikisho la haki katika mfumo w uendeshaji wan chi kama hii inayojiita ya kisekula. Kwa mfano, Katiba iliyopo imechangia kwa kiasi kikubwa kuwaathiri Waislamu kiimani, kiuchumi na kijamii. Waislamu tumekosa haki ya Mahakama ya Kadhi, haki ya kuwa na muwakilishi bungeni, haki ya kuwa na mfumo wetu wa elimu, haki ya kunufaika kwa misaada ya kishirika la kimataifa la waislamu OIC, haki ya usawa katika miliki ya ardhi, haki ya usawa katika uteuzi wa nagazi mbalimbali za uongozi wan chi, haki ya kuheshimiwa sheria za kiislamu n.k. Kutokana na udaifu w akikatiba uliopo, serikali kupitia amri ya Rais ilizifuta Mahakama za Kadhi mwka 1963 na ilipofika mwaka 1971 bunge lilipitisha sheria ya ndoa. Sheria hii inazidhalilisha sheria za Kiislamu kw akuhukumiwa na mahakama zisizo za kiislamu na pia kusimamiwa au kutafsiriwa na wasioziamini (wasiokuwa waislamu) na kusababisha kutolwea kwa taafsiri potofu. Mwaka 1992 serikali iliingia mkataba wa maridhiano na Makanisa (MoU) kugharamia shughuli za kijamii, kiafya na kielimu za Wakristo bila ya kuwasikiliza waislamu au kutupa fursa kama hiyo sisi waislamu nk. Aidha haki z amsingi za raia wakiwemo waislamu hutolewa na kuhakikishiwa (guarantee) na katiba. Kwa katiba iliyopo sasa haki hizi hazipatikana kwa uwazi, uhakika na kwa haki; na endapo mtu au serikali ikivunja haki hizo ni vigumu mno kuchukua hatua kwa mfano tokea mauaji ya Mwembechai, 1998 hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi ya wauaji. Kwa mantiki hiyo utaona wajibu wa kupigania mabadiliko ni MUHIMU SANA. Hofu yetu katika mchakato huu ni je, tume ya katiba itafanya uadilifu kwa wananchi wote bila kujali dini? Hofu hiyo si kigezo cha kuturudisha nyuma na kuwaacha wasiokuwa waislamu kuyasemea yanayowahusu waislamu. Hivyo bas waislamu lazima tushiriki kuhakikisha uadilifu, haki vinazingatiwa, waislamu wanasikilizwa na maoni yao yanazingatiwa. o Uislamu na katiba Mtume Muhammad (SWWALALLAH ALAYHI WASALLAM) aliandika waraka wa makubaliano ya namna ya kuishi kati ya waislamu na jamii mchanganyiko alipofika Madina. Makubaliano haya kwa lugha ya sasa yanaitwa katiba. Utaratibu huu ulimuwezesha Mtume (SWALALLAH ALAYHI WASALLAM) na waislamu kutekeleza Uislamu wao kwa uhuru na maelewano na jamii nyingine. o Mtazamo w aFiq-hi na mazingira yaliyopo Waislamu kwa nyakati tofauti ima watakuwa wanaishi katika dola ya Kiislamu (Daarul Islaami) ama dola kama ya Tanzania ambayo si ya kiislamu. Katika dola ya Kiislamu, sheria zote za nchi chimbuko lake ni Allah (Subhaanahu Wataala), na katika dola isiyokuwa ya kiislamu ni kinyume chake. Waislamu tunaishi katika nchi hizi (Daarul harb) na katiba zake zinatuathiri sana kwa njia moja ama nyingine. Kwa sababu hiyo tunalazimika kushiriki katika kuundwa kwake kwa lengo la kuondoa kabisa na ikibidi kupunguza madahara yake kwetu na kwa jamii na wala si kwa lengo la kuipa nguvu mifumo dhidi ya mwongozo wa Allah (Subhaanahu Wataala). Hapana shaka Fatwa ya jumuhuri ya wanazuoni wa iq-h ulimwenguni, Fatwa za Kamati ya Kudumu ya ataawa na Uchunguzi ya Saudia, Fatwa ya Chuo Kikuu cha Al Azhar, Sheikh Al Uthayminyn, Ibn Jibriin, Nassur ad-Dyn Al-Albany n.k zilizopitisha kuwa inajuzu kwa waislamu kushiriki katika mambo mbalimbali (kama siasa, chaguzi nk) katika nchi za kitwaaghuti wanazoishi, zimezingatia hekma ya Qur’an na mafundisho ya Mtume (SWALALLAH ALAYHI WASALLAM). o WAjibu kwa viongozi wa Kiislamu Kila jamii hutaraji maelekezo kutoka kwa viongozi wao. Kwa hiyo wajibu wa kwanza kwa kiongozi wa umma wa waislamu ni kujitambua kwamba waislamu wanamtegemea awaelekeze jinsi ya kushiriki wa namna itakayoleta tija kwao nakwa taifa kwa ujumla. Kiongozi pia anapaswa kuwa na ung’amuzi wa nini kinachoendelea katika kijiji, mtaa, mji, kata, tarafa, wilaya na Mkoa wake kuhusu mchakato wa katiba. 8. MAMBO YA KUPIGANIWA NA WAISLAMU KATIKA KATIBA MPYA Sehemu A. MASUALA YA MSINGI KWA WAISLAMU. i. UWEPO WA MWENYEZI MUNGU Hapa tunapendekeza katiba mpya itambuwe uwepo wa Mwenyezi Mungu Ibara ya 19 (1-3) inatoa uhuru wa imani na dini. Kwa kuwa katiba inatambua uwepo wa dini bas itambue pia uwepo wa Mwenyezi mungu isipokuwa tu kwamba kila mtu awe huru kuamini Mungu kwa mujibu wa imani yake. Ikumbukwe kuwa viapo mbalimbali hutolewa mahakamani, bungeni na serikalini kwa wabunge, majaji, mahakimu, watendaji wa serikali n.k. Basi ni busara na uungwana Mungu huyo anayemuomba kwa kusema “Ee Mungu nisaidie” uwepo wake utambuliwe katika katiba. ii. UBAGUZI WA KIDINI KWA SIKU ZA MAPUMZIKO UFUTWE Upendeleo wa kidini uondolewe. Mfano;- Siku za mapumziko Jumamosi na Jumapili ni siku za ibada kwa Wakristo. Hivyo ni vyema Ijumaa nayo iwe mapumziko walau nusu siku ili kuruhusu waislamu nao wawe huru kwa ibada hasa sala ya Ijumaa. Pia upendeleo wa kidini katika pato la taifa uondolewe. Kama MoU unayoitaka serikali kutoa pato la taifa na kuipa dini hiyo huku dini nyingine zikinyimwa haifai. Katiba mpya ni vyema ikapiga marufuku suala kama hilo kutendwa na serikali. iii. KATIBA ITAMBUE NA KUIREJESHA MAHAKAMA YA KADHI. Katiba mpya itambue na iweke utaratibu wa uwepo wa Mahakama ya Kadhi ambayo itaendeshwa na waislamu wenyewe kama moja ya Mahakama za nchi. Mashauri yote yanayohusu ndoa, talaka, mirathi, waqf, malezi ya watot, hibba (zawadi), wosia, biashara, bima kwa mujibu wa dini ya kiislamu yasikilizwe katika Mahakama ya Kadhi alimradi mhusika/wahusika ni waislamu. Pawekwe kipengele kinachozuia rufaa za Mahakama ya Kadhi kwenda kwenye mahakama za kawaida. Mahakama ya Kadhi iwe chombo chenye nguvu za dola na ipewe haki na uwezeshaji wa kifedha kutoka serilini ili kutekeleza majukumu yakekatika ueneshaji wa kesi. Ni dhahiri kuwa baadhi ya sheria za kiislamu ni sheria halali za nchi hii. Mfano sheria za ndoa na mirathi, seria hizi hazipati tafsiri sahihi kutokana na mamalaka zilizopewa jukumu la kuzisimamia kuendeshwa kinyume na misingi ya dini ya kiislau kwa asiyekuwa muislamu kuruhusiwa kutafsiri sheira za kiislamu. Hili pia linatokana na ujuzi finyu wa utambuzi matumizi ya hukumu za sheria hizi ambalo ni tatizo katika kusimamia haki zitokanazo na sheria za kiislamu. Kwetu sisi Waislamu kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria zakiislamu ni tendo la kiibada na kijamii, na vile vile kuhukumiwa nje ya misingi hiyo ni matendo yanayoingilia uhuru wetu wa kuabudu. Hivyo bas tunataka katiba mpya itambue na iweke utaratibu wa uwepo wa mahakama ya kadhi mahakama ambayo itaendeshwa kwa mujibu wa sheria za kiislamu katika mambo yahusuyo waislamu bila ya kuingliwa na chombo chochote. Hakika hili ni eneo muhimu na nyeti sana kwa uislau tunataka tume ya katiba isipuuzwe kwa namna yoyote hitajio hili kw alengo la kulinda amani na kuheshimu imani na uhuru wa kuabudu kwa waislamu. Ni pendekezo letu piakuwa rufaa za mahakama ya kadhi zishughulikiwe bila ya kuhusisha mahakama za kawaida. Tunataka mtu ambaye amefunga ndoa ya kiislamu au anaishi kama Muislamu ninamtambua kuwa ni Muislamu iwe ni kigezo cha shauri lake la mirathi na ndoa kupelekwa katika Mahakama ya Kadhi na siyo ridhaa ya warithi au maoni ya mtu mwingine. iv. ADHABU YA KIFO KWA MUUAJI IENDELEE KUTAMBULIKA KIKATIBA Yapo madai yanayotolewa kutaka adhabu ya kifo ifutwe kwa kuwa eti ni kinyume na haki za binadamu. Kuondolewa kwa adhabu ya kifo kutaleta hali ngumu kwa jamii na hasa wanyonge kwa sababu:- o Mauaji ya raia wasio na hatia yataongezeka sana. o Nchi zilizoondoa adhabu ya kifo kwa makosa ya mauaji, bado haikupunguza idadi ya wahalifu wa makosa ya mauaji. Mfano, Afrika ya kusini waliiondoa na sasa wanajadili kuirudisha. o Hoja ya wapinga adhabu ya kifo kuwa o Kosa la kuua linaumiza na linakwenda mbali sana zaidi ya kwa Yule alieyeuliwa ndugu yake hivyo basi muuaji akiendelea kuishi kwa kulishwa na serikali kwa kodi za waliouliwa ndugu yao kutachochea mauaji na visasi zaidi, tunaamini salama yake nay a jamii ni muuaji naye kuhukumiwa kuuwawa kuzuia raia kujichulia hatua mikononi mwao. o Hoja ya kwamba adhabu ya kifo haimpi muuaji nafasi ya kujirekebisha haina mantiki kwani adhabu si sehemu pekee ya kujirekebisha bali ni hukumu kwa matendo ya mtu na katazo (detterance) kwa wengine. o Pia hoja ya kwamba adhabu ya kifo inamdhalilisha mtuhumiwa nayo haina mantiki kwani hakuna adhabu ambayo inampa sifa mtuhumiwa; bali adhabu zote mfano kifungo, faini au viboko zinadhalilisha na dio maana zikaitwa adhabu na sio pongezi. v. KATIBA ITAMBUE HAKI YA WAISLAMU KUWA NA MFUMO WAO WA ELIMU. Nchi mbalimbali duniani zinaruhusu watu wa dini mbali mbali kuwa na mfumo wao wa elimu ili kutoa nafasi ya kufundisha watoto wao imani, mila na desturi zao alimradi wanaingiza na mitaala ya kiserikali. Afrika ya Kusini, Uingereza, India na hata Marekani hufanya hivyo. Waislamu tumeruhusiwa kuanzisha mashule yetu lakini yanadhibitiwa mitaala, vitabu, kanuni na sheria mbalimbali na Wizara ya elimu kiasi kwamba sisi ni waathirika wakubwa wa kufutiwa mitihani, kuhujumiwa hujuma mbali mbali pamoja na watoto wetu kuzuiwa kutekeleza dini yao katika shule na vyuo vya serikali. Mfano, sakata la wanafunzi wa Kiislamu ndanda Mokoani Mtwara kufukuzwa shule kwa kutekeleza uislamu wao. Katiba itamke wasi kuwa wananchi wana uhuru wa kuwa na mfumo wao wa elimu kwa mujibu wa dini yao. Tayari kuna shule na vyuo (academia) vinavyoenedshwa kwa mitaala ya Uingereza na hata kuendesha shule na vyuo kwa mitaala yao kama ilivyo kwa Vyuo vyao Vikuu? Kuendelea kulazimisha mfumo wa elimu wa pamoja ni kukiuka misingi ya haki za binadamu na uhuru wa mawazo (freedom of opinon). Sehemu B. HAKI ZA MSINGI ZA BINADAMU HAKI YA UHURU KAMILI WA IBADA NA UWAKILISHI KIDINI. a) Katiba itoe haki na uhuru kamili wakuabudu Katiba ya sasa inatoa uhuru wa kuamini na uchaguzi katika mambo ya dini (Ibara 19: 1-3) lakini haitoi uhuru wa kuabudu. Hii inafanya baadhi ya waumini kulalamika kwamba hawapati uhuru kamili wa kuabudu. Baadhi ya masuala yanayolalamikiwa ni pamoja nay a akina mama wa kiislamu jeshini, polisi, na baadhi ya masuala yanayolalamikiwa ni pamoja nay a akina mama wa kiislamu jeshini, polisi, na baadhi ya ofisi kutoruhusiwa kuvaa hajab, wanazuiliwa kuswali katika mashule, vyuoni na maeneo ya serikali nk. Katika uhuru wa ibada, sheria za kiislamu ziheshimiwe mfano mirathi, ndoa, talaka, waqf, biashara, bima n.k. zitambuliwe kikatiba kamasehemu ya ibada yetu. Hii itafanya mahakama ya kadhi iwe na maana kwani sheria zitakazotumika katika mahakama hizo zitakuwa zinatambuliwa na hivyo haitakuwa rahisi kuziondoa kama ilivyopata kutokea huko nyuma. Hili linajitokeza pale ibada hizi muhimu zinakandamizwa kwa vigezo vya haki za binadamu vya kimagharibi bila kuzingatia kwamba haki ya kuwa katika dini ni ya hiyari na kwamba mtu anaingia na kubaki katika dini akijua iko hivyo. b) UWAKILISHI WA KIDINI BUNGENI Katiba itamke uwepo wa viti maalum vya uwakilishi wa makundi ya dini hasa Waislamu na wakristo Bungeni. Bunge ndio mhimili wa dola unaowakilisha maoni na matakwa ya wananchi. Hali ilivyo hivi sasa yanapojitokeza mambo yanayowahusu waislamu na wanadini wangine bungeni maoni yao hayapati nafasi walakuzingatiwa. c) TUNATAKA UWAKILISHI WA KIDINI KATIKA BARAZA LA MADIWANI Katiba itamke kamatulivyopendekeza katika uwakilishi wa Waislamu na wakristo bungeni kwamba katika serikali za mitaa pia kuwe na uwakilishi kama huo. d) SHERIA YA UGAIDI IFUTWE Katiba mpya ipige marufuku sheria ya ugaidi ya mwka 2002 na utungwaji wa sheria kama hizo zinazopelekea kuvunjwa kwa haki za msingi za binadamu na ambazo utekelezaji wake unaleta manyanyaso na madhara makubwa kwa Waislamu kama ilivyo sasa nchini Tanzania. e) Haki za binadamu ziendane na maadili ya Dini nay a Kitanzania Tunataka katiba mpya isiruhusu mambo ya kishetani kama vile ulawiti, dnoa za jinsia moja, uto9aji wa mbimba, uhuru wa kupindukia wa motto dhidi ya wazazi wake na mfano wa hayo kuwa ni miongoni mwa haki za binadamu. Zipo kampeni zinazoshinikizwa na makundi yanayojiita watetezi wa haki za binadamu na hata baadhi ya nchi za nje kama vile Uingereza kutaka kushinikiza kuingizwa mambo hayo katika katiba mpya. f) Katiba mpya itoe ainisho sahihi la ndoa na familaia Kutokana na shinikizo la ushoga dhidi ya nchi yetu ni muhimu katiba iamke wazi maana ya ndoa. Katiba itamke hivi ‘ndoa ni baina ya mwanaume na wanawake au mwanaume na mwanamke. Ndoa kati ya watu wa jinsia moja zisiruhusiwe na iwe ni kosa la jinai iwapo watu wa jinsia moja watabainika kuoana au kuishi kama mke na mume ili kulinda maadili yetu. g) Nafasi mbali mbali za uteuzi serikalini na mashirika ya dini zizingatie uwiano wa kidini kati ya Wakristo na Waislamu. Katiba mpya iweke utaratibu kuwa nafasi zote za uteuzi serikalini na katika idara zake, uwakala wa asasi za serikali nk zizingatie uwiano ulio sawa baina ya dini za waislamu na wakristo, ili kuondoa manung’uniko kuwa kuna ubaguzi katika uteuzi wa nafasi za uongozzi serikalini. Hii itasiadia kuweka misingi ya usawa katika utumishi wa umma na kuondoa hisia za udini. Salama ya nchi hii kwa kiasi kikubwa inategemea kuaminiana na kuheshimiana baina ya dini hizi kuu mbili, hivyo basi uwiano katika uteuzi ukilindwa kikatiba itakuwa ni kujenga msingi imara wa amani, haki na kuaminiana. h) Urekebishwaji wa vifungu vya haki za binadamu ndani ya katiba. Pia tunapendekeza kuwepo taratibu makhsusi za urekebishaji wa vifungu vya haki za binaadamu katika katiba. Utaratibu wa sasa wa vifungu hivyo kurekebishwa kama vifungu vingine vya Katiba ni hatari kwa kuzingatia umuhimu na unyeti wa haki za binaadamu katika maisha yetu. Vifungu kama vile vinavyohusiana na haki ya kuishi, kuchagua na kuchaguliwa, kuabudu, kufanya kazi, kutokubaguliwa, uraia na kumiliki mali visibadilishwe mpaka iwepo ridhaa ya wananchi kwa njia ya kura (referendum). Haki nyingine za Katiba zisibadilishwe mpaka zaidi ya asilimia 75 ya wabunge kutoka pande zote za Muungano waridhie na pia iwepo haki ya wananchi wasioridhika na mabadiliko hayo kuyapinga katika Mahakama Kuu ya Katiba ndani ya siku tisini toka marekebisho hayo yalipofanyika. Muswada wowote wa kurekebisha kifungu chochote kinachohusu haki za binadamu lazima usambazwe kwa wananchi kutoa maoni yao ndani ya siku 90 kabla haujawomwa Bungeni. Ili kulindwa kwahaki zabinadamu na kuwepokwa uwazi tunapendekeza sheria zote kandamizi maarufu kama sheria 40 zilizoorodheshwa na tume ya jaji nyarali zifutwe. Adhabu ya kifo kwa makosa makubwa kama mauwaji ya makusudi iwepo katika katiba mpya na iwe ni moja kati ya mambo ambayo hayawezi kubadilishwa bila referandamu (kura yamaoni). i) Mahakama Kuu ya Katiba na haki za binadamu Tunataka katiba mpya iruhusu uwepo wa mahakama Kuu ya Katiba ambayo itapewa uwezo na nguvu za kisheria wa kutafsiri vipengele mbali mbali vya katiba na pia kubatilisha sheria yoyote itakayotungwa ambayo inapingana na katiba. Mahakama hii pia izuie marekebisho ya katiba yanayokinzana na misingi ya Katiba yenyewe. Na ili hili liwe na mantiki, Katiba itamke wazi kwamba baadhi ya vifungu vya Katiba kama vile vinavyohusu Muundo wa Dola, Muungano, haki za binadamu makhsusi zinazorekebishika kwa ridhaa ya wananchi ndio utakuwa msingi mkuu wa katiba na kawamba haiwezi kubadiliswa bila kuwa na ridhaa ya wananchi kupitia kura ya maoni (referendum). Pawepo na mahakama Kuu ya Katiba ambayo itakuwa na hadhi ya muungano na pia pawe na Mahakama ya rufaa ya Katiba ambayo pia itakuwa ya muungano. Mahakama Kuu ya Tanganyika na Mahakama kuu ya Zanzibar kamailivyo Mahakama ya Rufaa ya Tanganyika zisiwe sehemu ya Muungano. j) Mahakama za hakimu mkazi Mahakama za Hakimu Mkazi zifutwe na badala yake ziwepo Mahakama za wilaya ambazo zitaendeshwa na Mahakimu wa Daraja la Pili ambao watakuwa na uzoefu wa kuwa mahakimu wa mahakama za mwanzo kwa kipindi kisichopungua miaka mitano. Mfano wa sasa hivi wa kuwa na mahakama za wilaya na mahakama za hakimu mkazi ambazo zinaharibu mamlaka sawa hauna tija. Na pia mfumo wa kuwapa uhakimu mkazi wahitimu wa chuo wasiokuwa na uzoefu wowote unakwaza utoaji haki. Ni bora mahakumu kama hao wkanzia mahakama za mwanzo. k) Haki ya kumiliki Ardhi Haki y akumili Ardhi iwe ni haki ya raia.Mgeni anaweza kuruhusiwa kumiliki ardhi kwa kushirikiana na mzawa tu na kwa masharti kwamba hamilik zaidi ya asilimia 45 ya ardhi hiyo ya pamoja na kwamba umiliki wake uwe ni kwa ajili ya uwekezaji na si makazi. Pawepo na ukubwa maalumu wa ardhi mtu mmoja atakubaliwa kumiliki. Zaidi ya hapo raia awe na haki ya kukodisha ardhi anayoimiliki kwa muda usiozidi miaka kumi na tano. Hii inakusudia kuondoa uwezekano mtu mmoja au kikundi cha watu kumiliki na kuhodhi eneo kubwa la ardhi na kuacha jamii kubwa ya watanzania wakikosa haki ya kumiliki ardhi.. Ikumbukwe kuwa ardhi haiongezeki bali watu wanaongezeka. Mamlaka ya Raisi ya kutwaa ardhi kwa maslahi ya umma iweke wazi mambo yanayohesabika ni maslahi ya umma na itoe muda maalumu kwa mtu asiyeridhika kutaka rufaa dhidi ya uamuzi wa kutwaliwa ardhi yake katika Mahakama ya Ardhi. Katiba ielekeze Sheria za mipango miji zitenge maeneo ya dini (ibada) kwa kuanisha maeneo ya waislamu, wakristo na dini zingine kama vile majumba ya ibada, makaburi n.k na sio kutaja kiujumlajumla “eneo la kidini” kama ilivyo sasa. Kitendo cha kutaja kujumlajumla “eneo la Kidini” bila kuanisha dini gani kinafanya makundi ya dini moja kuhodhi maeneo makubwa kuliko makundi mengine na hivyo kusababisha manugu’niko. Sehemu C. MUUNDO W ASERIKALI NA MUUNGANO i. Tunapendekeza nchi yetu iwe na serikali tatu, yaani serikali ya Muungano, serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar Pendekezo hili linalenga kutrejesha katika dhamira ya uasisi wa Muungano kama unavyojidhihirisha katika hati ya Muungano ya 1964 ambao ulibainisha wazi kuwepo kwa muungano wan chi mbili n aserikali tatu. Hili pia linalenga kuondoa malalamiko ya mara kwa mara ya kila upande kuona unaburuzwa au kuonewa ndani ya mfumo wa serikali mbili tulionao hivi sasa. Vile vile litatibu kilio cha Watanzania kujiamulia mambo yao na kile cha watangayika kufuatiwa serikali yao. Mfumo wa sasa wa himaya tatu katika serikali mbili kuna matatizo mengi kiutendaji na kisiasa hasa katika himaya ya Tanganyika ndani ya serikali ya Jamhuri. Kwa mfano, nafasi kama ya Waziri Mkuu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali zinazua utata kama ni nafasi za muungano au Tanyanyika. Maana, hadhi ya Waziri Mkuu haitambuliki Zanzibar na kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Zanzibar nako kuna Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Pia wabunge wa Zanzibar katika bunge la Jamhuri ya Muungano chini ya mfumo huu wanpata nafasi ya kujadili na kutoa maamuzi juu ya masuala ya Wizara za Tanzania Bara kama vile Wizara ya elimu wakati wabunge wa Tanzania Bara hawana nafasi hiyo katika Wizara za Zanzibar. ii. Tunapendekeza Urais wa serikali ya muungano uwe ni wa kupokezana kwa Tanganyika na Zanzibar. Ili kuondoa manugu’niko kama tulivyoeleza hapo juu sisi waislamu tunaona kwamba umefika wakati sasa nafasi ya uongozi wa Rais wa serikali ya Muungano iwe ni ya kupkezana. Tunataka utaratibu huo sasa uwe rasmi kikatiba. iii. Mambo yaliongezwa katika orodha ya mambo ya Muungano yaliyopo katika hati ya Muungano yajadiliwe upya Masuala yatakayokubalika kuwa ya Muungano yasirekebishwe isipokuwa kwa ridhaa ya wananchi wa sehemu zote za Muungano kwa njia ya kura ya maoni (refere’ndum). Ili kulinda maslahi ya Zanzibar kutokana na idadi yao, kura zitazingatia uwiano wa sehemu mbili za Muungano na sio idadi ya watu. Katika masuala yanayoweza kukubalika kama masuala ya Muungano, Katiba ya Jamhuri ya Muunganoa na Katiba za Tanganyika na Zanzibara zitamke bayana kwamba iwapo kutakuwa na ukinzani wowote kati ya katiba ya Jamhuri na Katiba za Zanzibar na Tanganyika kuhusiana na masuala ya Muungano, katiba za nchi hizi zitakuwa batili kwa kiwango cha ukinzani kwenye vifungu husika.Hili litalinda uwezekano wa kuwepo migogoro inayotokana na moja kati ya nchi hizi kurekebisha katiba kwa namana inayoweza kuvuruga sura ya Muungano. Mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ya hivi karibuni yanaweza kutoa picha ya uwezekano huu. iv. MALIASILI NA MUUNGANO Kwa maoni yetu masuala ya madini na mafuta hayana sababu yoyote ya kuwa masuala ya Muungano. Ni bora yakabaki katika serikali husika ili kuondoa malalamiko kwamba sehemu moja ya muungano inataka kujinufaisha na maliasili zilizopo katika sehemu nyingine. Vi URAIS WA TANGANYIKA Tunapendekeza kwamba Uraisi wa Tanganyika uwe wa kupokezana kuzingatia makundi makubwa ya kijamii waislamu na wakristo. Kwa muda mrefu katika serikali ya Tanzania, has katika kipindi cha mfumo wa chama kimoja, kumekuwa na kanuni, japo hazikuandikwa, za kupokezana uraisi kati ya wailsamu na wakristo. Utaona kwamba Raisi w aPili Mwinyi ambaye ni muislamu. Mwingyi akarithiwa na Mkapa mambaye ni Mkristo naye akarithiwa na Kikwete ambaye ni Muislamu. Kwa mazingira yetu ambayo uwiano wa idadi kwubwa ya watanzania ni aidha waislamu ama wakristo na ukizingatia mvutano wa chini chini unaojitokeza kati ya wanadini hizi kuu mbili nchini kuhusiana na uwakilishi katika dola, ni busara kama mfumo huu aliotuachai mwalimu ukaendelezwa na ikibidi kulindwa kikatiba. Mfumo huu pia unaweza kuwa msingi wa kulinda umoja wetu na uvumilivu. Vii,. BARAZA LA MAWAZIRI NA UBUNGE Tunapendekeza Baraza la Mawaziri lisitokane na wabunge kama ilivyo sasa. Hii inatokana na ukweli kuwa mara kwa mara kumetokea mgongano wa kimaslahi kwa mawaziri kupleka miradi mingi ya maendeleo katika majimbo yao ili kujijengea uhalali wa kuchaguliwa tena. Vile vile pendekezo hili linalenga kutenganisha utendaji wa mihimili miwili ya serikali na bunge. Hailet maana nzuri wabunge kuwa sehemu ya serikali (executive) kwani ile dhana ya mgawanyo wa madaraka ambayo ni muhimu katika kuhakikisha utendaji na ufanisi haionekani kuleta tija inayotengemewa katika mfumo huu tulionao wa mawaziri kuwa sehemu ya bunge. viii. SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO Ili kutoa nafasi Aidha iwapo Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano atatoka upande mmoja wa Muungano bas swa katika pande zote za Muungano,ni bora nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iwe ya kupokezana kati ya Tanganyika na Zanziar. Naibu wake atoke upande wa pili. Katibu wa bunge pia iwapo atatoka upande mmoja wa Muungano naibu wake atoke upande wa pili wa Muungano. ix. SPIKA WA GUNGE LA TANGANYIKA Katika serikali ya Tanganyika kwa yale mambo ambayo si ya mungano tunapendekeza bunge la Tanganyika liwe na spika wake kwa kuzingatia uwiano kama tulivyopendekeza kwa nafasi ya urais wa Tangayika au uwepo utaratibu mwingine mallum unaofanana na huo. Nafasi ya katibu wa bunge pia iwe kama katibu ni wa dini moja basi naibu wake awe kutoka dini nyingine. x. WIZARA ZASERIKALI Ili kuleta ufanisi na kumpunguzia Raisi majukumu na madaraka, ni bora muundo na idadi ya Wizara zikatamkwa moja kwa moja ndani ya Katiba badala ya utaratibu wa sasa wa wizara na idadi yake kutegemea matamshi ya Raisi. xi. MAKAMU WA RAISI Tunapendekeza kama serikali ya Tanganyika itakuwepo, nafasi ya Makamu wa raisiwa Tanganyika isiwepo na badala yake pawepo na Raisin a Waziri Mkuu tu. Utaratibu wa sasa wa kuwa na mgombea mwenza ambaye anakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano uondolewe na badala yake kama Raisi anatoka Zanzibar Raisi wa Tanganyika awe kwa mnafasi yake ni Makamu wa Raisi wa jamhuri na kinyume chake. Ingawa kuna uwezekanao wa Raisi wa Muungano kutoka chama tofauti na chama cha Raisi wa upande wa muungano utakaostahili kutoa Makamu wa Raisi, mfumo huu ni mzzuri na wa lazima maana utakuwa umelinda maslahi na uwakilishi wa watu wengi katika upande wa Muungano unaohusika. Hilii pia itawzekana maana serikali ya Muungano itakuwa inahusika na masuala machache ya muungano wakati masuala mengi yakishughulikiwa na serikali zinazounda muungano. xii. MANAIBU WAZIRI Tungependekeza pia nafasi ya naibu Waziri kwa upande w serikali ya Tanganyika isiwepo maana inaongeza gharama bila sababu. Katibu Mkuu wa wizara anatosha. Kwa upande wa serikali ya Muungano, nafasi hiyo iwepo ili kuleta uwakilishi sawa kutoka pande mbili za muungano. Na pale Waziri akitoka upande mmoja wa muungano, naibu wake atoke upande wa pili wa muungano. xiii. SERA RASMI YA NCHI Tunapendekeza sera ya nchi yetu iwe nisera ya kujenga ustawi wa jamii yaani “welfare state policy” badala ya sera ya ujamaa ambayo kivitendo haipo tena. Pendekezo hili linazingatia ukweli kuwa sasa nchi yetu ni ya kibepari. Hivyo basi sisi waislamu tunaona kuwa ni heri sera ya nchi yetu iwe ni kuimarisha ustawi wa kijamii yaani ili kuifanya serikali iweze kuwajibika zaidi kwa wananachi kuwawekea ustawi wa maisha yao. xiv. BAADHI YA MSHARTI YA KUSAJILI VYAMA VYA SIASA YAONDLEWE Kwa kuwa kila mtu ana uhuru w akujiunga au kutojiunga na chama chochote cha siasa alimradi havunji seria,masharti yafuatayo ya uanzishwaji wa vyama vya siasa yaondolewe;- i. Sharti la kwamba chama cha siasa lazima kiwe na wanachama kwa Zanzibar na Bara liondolewe kwani linanyima uhuru na uchaguzi wa kujiunga na wengine kwani ridhaa ya mtu. ii. Sharti lakuwa na wanachama mikoa 10 bara na 2 Zanzibar liondolewe kani linaleta ulazima kwenye jambo ambalo kimsingi ni hiari. Chama kisicho na wanachama kiachwe kife chenyewe kwa kukosa wanachama.
iii. Vyama vya kidini viruhusiwe ili wananchi waamue wenyewe kwa sera za chama na katika sanduku la kura.hili linawezekana na kuna mifano hai kam avile Ujerumani, Australia, Uingereza, Cananda, DRC Congo, Denmark, Ufaransa, Italia, Rwanda, Ubeligiji, Afrika ya Kusini n.k kuna vyama vya kidini na wala hakuna matatizo yoyote.
xv. MAMLAKA YA RAISI Y APUNGUZWE Japo mamlaka ya kutosha kwa Raisi ni muhimu kwa maslahi ya umma ili kumuwezesha kutekeleza majukumu yake makubwa kama Mkuu w aNchi na Dola, ni bora, kwa lengo la utawala boara na kulinda zaidi maslahi ya umma, madaraka ya Raisi yakapunguzwa katika maeneo yafuatayo;- - Raisi asiwe na mamlaka ya kuweka watu vizuizini bila ya kufikishw amahakamani na Kuhukumiwa kwa kuthibitihswa shutuma dhidi yake. - Mamlaka ya Raisi ya kusamehe wafungwa yawe ni kwa mujibu wa vigezo maalumu vinavyotamkwa na sheria ya Bunge na iwe katika utaratibu ulio wazi. - Mamlaka ya Raisi ya kuunda idara mbalimbali za serikali pamoja na kteua wakurugenzi yatekelezwe kutokana na mapendekezo yatakayotolewa na Kamisheni ya Ajira na Idara za Serikaliitakyoundwa kw auwiano wa kimakundi ya kijamii. xvi VYOMBO VYA UTEKELEZAJI WA SHEIRA, UPELELEZI NA UENDESHAJI WA MASHITAKA a) Mkurugenzi wa mashtaka Mamlaka ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) yanahitaji Kupunguzwa ili kuleta ufanisi na uwazi zaidi katika mfumo wa utekelezaji wa sheria. Kwa maoni yetu, pale kesi ya jinai itakapoanzishwa na taasisi nyingine au mtu binafsi, DPP asiwe na uwezo wa kudihinisha kesi hiyo kwenda au kutokwenda mahakamani, kuondoa mashitaka mahakamani wala kuingilia isipokuwa tukama atatoa sababu za kisheria zitakazomridhisha hakimu aJaji anayesikiliza kesi kwamba kuna mwnendo unaowezakupelekea haki kutokutendeka. Katiba na sheria tulizonazo kwa sas zimetoamamlaka makubwa sana kwa Mkurugenzi wa Mahsitaka, kwani kwa mamlaka aliyonayo anao uwezo wa kuingilia au kufuta kesi yoyote iliyo mahakamani bila kulazimika kuto sababu yoyote na hakuna atakayemzuia kufanya hivyo. Hii imeleta maswhli na malalamiko mengi kuwa wapo watu wanaofaidika na mamlaka hayo makubwa ya DPP kutoweza kufikishwa Mahakamani kwa matendo yao. b) Taasisi ya kuzuia na kupambana narushwa (TAKUKURU) Tunapendekeza ofisi ya Kikosi cha Kuzuia na Kuondoa rushwa Tanzania (Takukuru) itamkwe ndani ya Katiba na iwe na mamlaka kamili na huru katika kusimamia sheria ya kuzuia rushwa bila kuingiliwa na ofisi ya DPP. Utaratibu wa sasa wa baadhi ya makosa kuhitaji ridhaa ya DPP kabla ya kupelekwa Mahakamani yanaleta matatizo kutekelezaji na yanapunguza uhuru wa Takukuru. Ni bora pia, ili kuondoa muingiliano, sheria ya Takukuru ijihusishe na makosa makhsusi ambayo hayatamkwi katika Sheria ya Makosa ya Jinai (Penal Code). Na lau baadhi ya makosa katika Penal Codeyanastahili kuwemo katika sheria ya Takukuru , sheria ya penal Code irekebishwe kuyahamishia makosa hayo katika sheria ya Takukuru. c) Ofisi y aMkurugezi na Mdhibiti Mkuu wa serikali CAG) Ili kuzuia ubadhilifu wa mali za umma ni bora ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali iwe na uwezo wa kutoa ushauri kwa mamlaka zinazohusika na mashitaka ya kushitakiwa au kumfungulia mashitaka yeyote atakayonekana kuwa na makosa kwenye taarifa hesabu za serikali. Na endapo vyombo husika vitakataa ushauri bila kuwa na sababu ya msingi kwa mtizamo wa Mkaguzi Mkuu, Sheria impe nguvu kulipeleka suala Mahakama Kuu ili iamue kam akuna haja ya kesi hiyo kufunguliwa. d) Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tunapendekeza utaratibu wa sasa wa Raisi kuunda tume ya Uchaguzi ubadilishwe badala yake iundwe na Chombo cha Kikatiba kitakachokuw akatika muundo unaozingatia uwiano wa maslahi ya kisiasa na kijamii. Hili litaondoa malalamiko kwamba Raisi anaunda Tume ya Uchaguzi kwa kuzingatia maslahi ya chama chake. e) Muundo w aTume ya Uchaguzi uwe wa kitaifa kuanzia chini hadi juu Muundo w atume kipande unawafanya viongozi wa Serikali wa Kuteuliwa na Raisi kuwa watendaji wa misimu wa Tume na hivyo kuzua malalamiko mengi kwamba haifanyi kazi kw auhuru. f) Matokeo ya Kura za Urais Katika iruhusumatokeo ya uchaguzi w aRaisi kupingwa katika Mahakama Kuu ya katiba.Ili kulinda usalama wan chi kesi hiyo itapaswa kufunguliwa ndani ya siku kumi na tano toka matokeo yalipotangazwa na kusikilizwa ndani ya siku thelathini. Mara baada ya kesi hiyo kufunguliwa, Katiba itamke kwamba Raisi aliyemaliza muda wake atakaimu nafasi ya Raisi ili kutoa nafasi kesi kusikilizwa kwa uhuru. Pia Katiba iamke wazi kwamba, kabla kesi hiyo haijafunguliwa, Mahakama Kuu ya katiba itafanya upembuzi wa ushahidi uliopo kuona kama kuna sababu zozote za msingi za kufunguliwa kwa kesi. Utaratibu kuwa uamuzi wa mwisho hata kama kuna malalamiko ya msingi yanazua wasiwasi kuw ahaki haitendeki. g) Mgombea Binafsi. Mgombea binafsi aruhusiwe katika nafasi zote isipokuwa nafasi ya Raisi. Mfumo wa sasa uanolazimisha mgombea kuwa na chama cha siasa unawanyima wananchi wasio na vyama vya siasa kushiriki katika uongozi wan chi wka kutumia haki yao yakuchagua na kuchaguliwa. Kwa upamde wa Raisi,mantiki ya kutaka wagomea wawe na vyama vya siasa ni kutoa nafasi ya kutosha kwa wananchi kutathimini sera vyama vyenye mgombea Urais ambazo ndizo zitakazotekelezwa na serikali itakayoundwa na Raisi atakayeshinda. Na pia kutoa nafasi kwa Tume ya Uhaguzi kutathimini sifa ya mgombea.Yawezekana mtu akajitokeza kuwa mgombea Uraisi na akawa na Sera inayopingana na Katiba na maadili ya nchi. Kuwa na chama cha siasa kutaifanya Tume kuchulia kwamba sera za mgombea ni kama zilivyo katika Katibana Sera ya chama chake. h) Mfumo wa serikali za majimbo urejeshwe Katiba isiwe na nafasi za Mkuu wa Mkoa, Wilaya na badala yake kuwe na uongozi wa majimbo na viongozi wa majimbo hayo watoke katika majimbo hayo na wapiigiwe kura na wananchi wa majimbo husika. i) Uhusiano na Jumuiya za Kimataifa Usiwe na Kibaguzi Katiba itamke kuwa Tanzania inaweza kujiunga au kuwa na uhusiano wa kibalozi, uanachama au vinginevyo na jumuiya yoyote yakimataifa pasi na kujali kama jumuiya hiyo ni ya kisiasa, kiuchumi, kijamii au za kidini alimradi kufanya hivyo itathibitika kuwa na maslahi kwa watanzania au sehemu ya watanzania. Ni kwa msingi huu waislamu w aTanzania tunataka Tanzania ijiunge na OIC kama ambavyo ina uhusiano wa kibalozo na Papa ambaye ni kiongozi wa Dola ya Kidini ya Vatican ya Kanisa katoliki. Kama hili la kujiunga na OIC haliwezekani, bas iwe pia Ubalozi wa Vatican nchini Tanzania usiwepo kwa sababu ni ubaguzi wa kidini. j) Mali za viongozi zihakikiwe kabla nabaada ya kutoa madarakani na CAG. Katiba iweke utaratibu maalum kwa mali za viongozi kuhakikiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa serikali (CAG) wakati wakuingia madarakani na wakati wakutoka badala ya tume ya Maadili ya Viongozi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba wajumbe wa tume ya Maadili wengi wao wanaweza wasiwe na ujuzi wa kutathimini na kuhakikisha mali hivyo atumike CAG. Na iwe ni kosa la kisheria kukaidi utaratibu huo. k) Rasilimali za maeneo husika ziwanufaishe wenyeji wa maeneo husika Katiba itamke kiwango ambacho wananchi wa maeneo yenye rasilimali kama vile gesi, madini n.k wanatakiwa wapatiwe kutoka kwa muwekezaji ili kuzuia kuhamisha mali kutoka eneo hilo kwenda kwingine au hata nje ya nchi bila wenyeji kunufaika. I) Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uwe wa Mkataba Katiba itamke kuwepo kwa Muungano wa mkataba na mambo yote ya Muungano yaliyoongezwa kutoka kwenye mkataba wa awali wa mwaka 1964 yapitiwe upya na pande zote husika. HITIMISHO Ndugu muislamu hii ni sehemu tu ya yale ya msingi kwa waislamu; yako mengine ambayo yanaweza kuongezwa wakati wa utoaji wa maoni, tafadhali muislam uwe huru kuyatoa mbele ya tume alimuradi hayapingani na maoni yetu ya msingi, vinginevyo pata ushauri zaidi toka kwa jukwaa la katiba la waislamu JUWAKATA;- Simu ya M/Kiti wa Jukwaa – 0785 955 859/0715955859 Simu ya Makamu M/Kiti wa Jukwaa – 0784 863539 Simu ya M/Kiti wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanznaia – 0689 378747 Simu ya Makamu Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu – 0715 631183 Sisi waislamu hatupaswi kutofautiana katika mambo ya msingi kwa ajili ya dini yetu. Tupo wanachama wa vyama mblimbali vya siasa, lakini tukiingia msikitini imamu wetu ni mmoja, hii ni fundisho kuwa sisi ni ummah mmoja. Tetea itikadi yako ya kisiasa alimuradi haipingani na dini yako. Itikadi ya kisiasa haipaswi kwenda kinyume na uislamu wako. Tafadhali jitambue na uutambue uislamu wako na uwe tayari kuutetea popote. Baaada ya maelekezo haya, tunamuomba kila muislamu sasa kujifunga kibwebwe na kusimama kutekeleza jukumu lake kwa uwezo wake wote. Nia zetu ni njema katika kushiriki mchakato wa mabadiliko ya katiba Tanzania na Allah (Subhaanahu Wataala) ni shahidi wa nia zetu. Tunashirki ili kuona kwamba katiba inazingatia matakwa yetu nay a wengine yasiyo na madhara kwetu na haitoi nafasi ya mtu yoyote kunyanyaswa. Ni wazi tutakapo simama na kudai haya tuliyoyasema tutasikia mengi kutoka kwa wale wote wasioutakia mema Uislam na waislamu.Wajibu wako wewe Muislamu kuitetea dini yako kwani kuna ujira mkubwa kesho mbele ya allah (SW). hautokuwa na udhuru wowote utakaposhindwa kusimama kuutetea uislamu wako kupitia mabadiliko ya katiba. Tumedhulumiwa kiasi cha kutosha ni wajibu wetu sasa TUSEME TUMECHOSHWA KUDHULUMIWA, TUNATAKA HAKE ZEETU NDANI YA KATIBA MPYA. TAFADHALI SASA TIMIZA WAJIBU WAKO Imeandikwa na: Jukwaa la Waislamu la Kuratibu Mabadiliko ya Katiba Tanzania (Juwakata) Dar es Salaam, Tanzania.



 
attachment.php


attachment.php


attachment.php
kama wakristomni wengi ni kwa nini wasijae kwenye ofisi za serikali?
 
Mohamed Said-KWELI WEWE KICHWA CHAKO KINA UTATA-MBONA UNAKUWA MUSILAM KAMA WENZAKO WA MIDDLE EAST-HAMUISHI KULALAMIKA-
TATIZO LA WANAOJIITA WAISLAM -TATIZO LINALOMHUSU YEYE BINAFSI ANACHUKULIA NI TATIZO LA WAISLAMU WOTE-ETU "TUNAONEWA"-HATA KAMA KAONEWA YEYE BASI ANAWEZA WINGI ILI KUTAFUTA SUPPORT YA MKUMBO WA WILDBEAST ILI WAWE WENGI-
MAMBO SI HIVYO KWA WALE WENYE TABIA NA MAWAZO MGANDO YA MTINDO HUO-
MBONA YULE MUISLAM SAFI ALIYEMPIGA KOF MHESHIMIWA MSTAAFU HAKUNA ANAYEONA KUWA ALITENDA KOSA NA HAMTAKI KUMSEMA KWA KUWA TU ALIKUWA NI MUISLAMU-KWA NINI MSILALAMILKE KUWA VIONGOZ WA KISLAM WANAONEWA/WANAPIGWA AU SERIKAL HAIWALINDI-
NDUGU ZANGU HII NI KARNE YA 21-HII NI 2012-HATUPO MIAKA YA ELFU MOJA NA USHEE ETI-BADILIKA
 
Mohamed Said amekimbia kujibu hoja.
Anachiosubiri mjadala uelekee kwingine kama baraza la mitihani,katiba, mahakama ya kadhi, Bakwata, Abdul Sykes nk.nk. ili arudi.

Mohamed, funga uzi kwasababu umeshindwa kusimama jamvini na kujibu hoja za wanajamvi.
Kama utarejea basi urejee kwa ufafanuzi na kujibu yatokanayo na mada yako siyo ' Pompous and grandiosity'
Binafsi nakukumbusha bandiko# 276
 
Mohamed Said amekimbia kujibu hoja.
Anachiosubiri mjadala uelekee kwingine kama baraza la mitihani,katiba, mahakama ya kadhi, Bakwata, Abdul Sykes nk.nk. ili arudi.

Mohamed, funga uzi kwasababu umeshindwa kusimama jamvini na kujibu hoja za wanajamvi.
Kama utarejea basi urejee kwa ufafanuzi na kujibu yatokanayo na mada yako siyo ' Pompous and grandiosity'
Binafsi nakukumbusha bandiko# 276
Wewe ndiye hasa uliyesababisha Mohamedi Saidi aikimbie Thread aliyoianzisha mwenyewe kutokana na mahoja yako
yanayofanana na ngumi za uso....chezea Nguruvi3 wewe!
 
Back
Top Bottom