BASHADA
JF-Expert Member
- Jul 13, 2011
- 513
- 148
Nimeangalia taarifa ya habari ya saa 2 usiku huu ITV, huko Tarime kuna mwanamke ameripotiwa kupigwa na mumewe mara kwa mara na hatimaye kufukuzwa na pamoja na watoto sita. Waandisi wa habari wakamfuata afisa ustawi wa wilaya ambaye alikataa kuzungumzia tatizo hilo, alipoambiwa kwa nini? Akajibu, "Nimejisikia tu kutokuzungumza" My take: Watu waliopewa dhamana na wananchi kutokutatua matatizo ya wananchi na wanapohojiwa hujibu kwa jeuri hii maana yake nini? Watanzania tukimbilie wapi ili kupata huduma?