Udhalilishaji wa wanawake: Afisa ustawi wa jamii (w): Nimejisikia tu kutokuzungumza

BASHADA

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
513
148
Nimeangalia taarifa ya habari ya saa 2 usiku huu ITV, huko Tarime kuna mwanamke ameripotiwa kupigwa na mumewe mara kwa mara na hatimaye kufukuzwa na pamoja na watoto sita. Waandisi wa habari wakamfuata afisa ustawi wa wilaya ambaye alikataa kuzungumzia tatizo hilo, alipoambiwa kwa nini? Akajibu, "Nimejisikia tu kutokuzungumza" My take: Watu waliopewa dhamana na wananchi kutokutatua matatizo ya wananchi na wanapohojiwa hujibu kwa jeuri hii maana yake nini? Watanzania tukimbilie wapi ili kupata huduma?
 
Huyo afisa ustawi wa jamii siyo kichaa, atakuwa anafahamu anachokifanya. Tarime siyo ya kuendea kichwa kichwa.
 
Nimeangalia taarifa ya habari ya saa 2 usiku huu ITV, huko Tarime kuna mwanamke ameripotiwa kupigwa na mumewe mara kwa mara na hatimaye kufukuzwa na pamoja na watoto sita. Waandisi wa habari wakamfuata afisa ustawi wa wilaya ambaye alikataa kuzungumzia tatizo hilo, alipoambiwa kwa nini? Akajibu, "Nimejisikia tu kutokuzungumza" My take: Watu waliopewa dhamana na wananchi kutokutatua matatizo ya wananchi na wanapohojiwa hujibu kwa jeuri hii maana yake nini? Watanzania tukimbilie wapi ili kupata huduma?

Hili tatizo ni kubwa kuliko tunavyosikia, kuna wanaume wengine sijui mishipa ya huruma ilishakatika! Wao kazi yao ni kudhalisha tu baada ya hapo wanakimbia. Ningekua na mamlaka hawa watu ningewaweka kundi moja na wanaotuibia rasilimali zetu(mafisadi). Kumuachia mwanamke watoto sita ni mzigo mkubwa sana na matokeo yake ni kuhatarisha maisha ya watoto.
 
nin mashaka km huyu kweli ni afisa ustawi a jamii,inawezekana hao ndio wale wanaowekwa na magod father wao bila taaluma husika.halafu social workers wa kweli wanabaki hawana ajira ukizzingatia hata wizara ya afya na ustawi wa jamii haiwathamin maafisa utawi ndo maana huwezi kuona waziri kushiriki siku ya social workers duniani wala stahiki zao hata kutangaza ajira zao.ajira za mwisho zilitoka 2010 kkwa minajili ya kisiasa tu.bora taaluma ya ustawi iundiwe wizara yake ili iwe huru kusimamia taaluma.nawasilisha.
 
Hivi wanawake ndio pekee wanadahalilishwa?!! na ni Tarime tu au? manake ITV wanatangaza Tarime pekee kila uchao
 
Hata mimi nimeiona taarifa hiyo ikiruka hewani, si tu nimekerwa, lakini naamini huyu bwana anaunga mkono kilichomtokea mwanamama yule! Inawezekana mwanamume aliyemnyanyasa yule mama ni mdogo wake au ndugu yake wa karibu! Kwa maoni yangu huyu bwana hafai kushika ofisi nyeti kama ile!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom