Ndugu yangu Nderingosha,
Mosi, mimi nina safu kwenye Raia Mwema tangu toleo namba moja. Pili, inashangaza kuwa unaongelea Raia Mwema wakati husomi Raia Mwema. Na haya unayosema hapa huenda umesukumwa na chuki binafsi. Ni tatizo lako.
Maggid
Well said, well done Mkuu Maggid, mimi nimesoma post yako na mapendekezo yako ya kujenga wala sioni kama kuna kitu umekosea au eti
"unajipendekeza!!" wakati mwingine ni vigumu kuelewa kama watu wanatatizwa/kasirishwa na
mfumo au wana chuki
binafsi tu na
muhusika, kwa nini hawataki kuzungumzia vitu +ve ambavyo JK ame-contribute katika awamu yake; nakubali naye ni binadamu kama sisi tulivyo, ana mapungufu yake lakini tusiya-blow out of proportion as if awamu za viongozi walio pita ilikuwa ni holly.
Waingereza usema kama huna jambo jema la kuzungumza kuhusu binadamu mwenzako, basi ni kheri ukae kimya au umseme kwa kumpa ushauri ajirudi.
Mimi natoa RAI kwa Watanzania wenzangu, tunacho takiwa kufanya ni kumpa moyo JK na kumshauri kwa nia njema na siyo kutumia hira na kuanza kukuza kuza mambo mengine ili dunia imuone kama ni liability kwetu, sio vizuri kujaribu kumkatisha tamaa. Hivi tujiulize ni kiongozi gani aliwahi kumfikisha mahakamani Mawaziri au katibu mkuu, kutema rafiki yake wa karibu, kukubari mawaziri wajihuzuru - kwani unafikili angekataa nani angemlazimisha?
Katiba yetu imempa mamlaka ya kuwa Dikteita wa kutupwa kuliko alivyo kuwa STALIN, lakini mimi sijawahi kuona Jakaya anatumia rungu yake HIYO kutoka ndani ya katiba, kwani unafikili anaogopa RAIA?
Mwisho nisema hii tabia iliyo jengeka ya kuwaona watu ambao wanatoa maoni tofauti kuhusu JK, wana hukumiwa kwamba wanajipendekeza kwake sio tabia nzuri hata kidogo - kila mmoja wetu analitakia mema TAIFA letu, haya mambo kwa mfano: yakumpa Jakaya a tall order ya kuwavurumisha watu mahakani/kuwafunga kwa kutumia hisia tu bila ushahidi litavuruga nchi na hakuna ambae atasalimika.
Juzi hapa niliona watu wanazungumzia mambo ya EPA kwa hisia kali wanasema kwa nini JK anawasamehe walio kubari kulipa DENI? Mambo ya ajabu kabisa: Hivi mtu ukikopa fedha mwisho wa siku anapashwa afanye nini hata ukimfikisha kwenye vyombo vya sheria - atahambiwa arudishe fedha alizo kopa, basi! Akishindwa ndio anafungwa au anafilisiwa, je hawa walio kopa hela kutoka EPA
(bila kujali mbinu walizo tumia kukopa) si majina yao yanajulikana?
Sasa JK alikosea nini kusema rudisheni hizo pesa la sivyo? Lakini watu wenye agenda zao watataka dunia imuone JK ndiye muhusika namba moja!!! Je wakini Maranda walifikishwa mahakamani kuhusiana na jambo gani? Nani kasema mkono wa sheria utahishia kwa watuhumiwa hao peke yao, mambo mengine tuwe na subira.