Maggid ameeleza mtizamo wake binafsi nawe umetoa maoni na maeneo ambayo unaona yanasababisha JK asipate sifa za Maggid,hapa ndo raha ya mjadala.
.
Mkuu
Mig hapo umedadavua vyema kabisa na umenifurahisha sana ndugu yangu.. lakini ulichosema hapo chini ...
Binafsi kama nilivyochangia mwanzoni naafikiana na Mjengwa kuhusu udhaifu wa mfumo lakini nisaidie kuchangia katika uliyogusia.
Nakupongeza kwa kuafikiana na Mjengwa. Mimi sikuafikiana naye. Mimi na wewe tunatofautiana. Sisi ni watu wawili wenye mawazo huru lakini akili zetu zinahifadhi models tofauti inapofika wakati wa ku-analyse mambo mbalimbali.
Hoja uliyoichomeka juu ya udhaifu wa mfumo ni mjadala tofauti na mrefu. Kinachonishangaza mara kwa mara ni namna mijadala inayomhusu Mh Dr Kikwete kupindishwa na kuelekezwa kwa vitu au watu mbadala ili kumnusuru na kumsaidia kuepa lawama na laana za watu. Naona anawatumia vizuri sana watetezi wake. Kumbuka kuwa, tumekuwa tukisikia mara nyingi :
(1) Rais Kikwete ni kiongozi msikivu lakini wasaidizi wake ndio wanaomwangusha! Hapo amesafishwa kwa hoja dhaifu kabisa!
(2) Rais Kikwete sio dhaifu ila mfumo uliopo ni dhaifu na ameurithi toka awamu ya kwanza! Hapo tena ametakaswa!
(3) Rais Kikwete ndiyo kiongozi pekee aliyeweza kuchukuwa maamuzi magumu kuwafikisha katika vyombo vya sheria mafisadi! Hapo tena amekuwa hero na shupavu! Huu ni usanii tu...watu wanataka kuhadaa watoto waende kulala usingizi.
Mfumo huu anaotumia Mh Kikwete, ndio aliotumia Mkapa, ndio aliotumia Al~Hajj AH Mwinyi, ndio aliotumia Mwenyeheri JK Nyerere, je unadhani hawa nao walionesha udhaifu wa kiuongozi kama tunaouona kwa Col Kikwete? Fafanua ukizingatia matukio yafuatayo:
(i) Ndege ya kijeshi kutua nchini na kuondoka na wanyama hai bila kipingamizi chochote
(ii)Wezi wa pesa ya EPA kuombwa kurudisha pesa kwa hiari na bila kufikishwa mahakamani
(iii)Orodha ya wafanya biasha ya madawa ya kulevya kufikishwa kwa rais na yeye kukaa nayo miaka 7 bila hatua yoyote
(iv)Richmond: Kikwete.. "simjuwi mmiliki"...Lowasa: "Unakumbuka nilikupigia simu ...ili nisitishe mkataba lakini ukanizuwia.."
(v) Luhanjo, Jairo, etc
Kikwete ndiye Rais ambaye ameteua Majaji wengi kuliko Rais mwingine yoyote,je hapo amebomoa au amejenga mfumo wa mahakama?
Kuteua watumishi wa serikali na mahakama ni jukumu la rais kwa mujibu wa katiba iliyopo. Kuteua wengi au wachache ni hekima inayoongozwa na mahitaji ya taifa. Siyo hisani ama sadaka. Ni wajibu.
Lakini, je rais amefuata kanuni za uteuzi wa majaji hao wengi kupindukia? Je, falsafa yake katika kutenda hivyo ni nini? Ni kuboresha mahakama kweli? Je matokeo ya uteuzi huo yanaafiki hoja ya uboreshaji wa mahakama? Naomba ufafanue zaidi hoja yako mkuu
Kikwete ametoa uhuru mkubwa mno wa kutoa maoni,baba zangu aliwekwa rumande kwa kuhoji ujenzi wa shule na alichukuliwa kama mpinga maendeleo.BWM alitoka povu wakti wa kujadili report ya Jaji Kisanga na watu tukafikia hatua ya kumshauri Kisanga atangaze kujiuzulu kwani ulikuwa udhalilishaji wa wazi,unaikumbuka hiyo?
Je, huo uhuru mkubwa mno kama ulivyosema:
(1) Unatokana na hisani yake?
(2) Ni ishara ya utawala bora?
(3) umeleta maendeleo zaidi?
(4) Umeleta mazingira ya kuhishimiana zaidi na utengamano kama raia wa taifa moaj?
(5) umeleta manufaa gani? Mimi nilisema mwanzo kuwa uhuru huu ni ishara ya udhaifu wa ki-uongozi wa Col Kikwete. Hakuna uhuru usio na mipaka; yeye ameacha mipaka yote imevunjwa! Ameleta uhuru wa kutapakaa kwa majungu na fitna.. Kama siyo hivyo naomba urudi kufafanua zaidi hapo
Kuhusu baba zako kuwekwa rumande, nawapa pole sana. Je, ulikuwa na umri gani wakati wanawekwa ndani? Je, una hakika baba yako alihoji tu ujenzi wa shule? au kuna jambo la ziada alilofanya na hakutaka kukufahamisha, au wewe hutaki kutufahamisha? Hili naomba liwe kazi ya mahakama kuliamuwa. Ushahidi wa mtu mmoja hauwezi kutowa natural justice kwa pande zote zinazohusika. Kwahiyo hili mimi siwezi kulijadili...
Suala la Judge Kisanga na Mkapa ninalifahamu. Ni hoja nyingine, na inahitaji mjadala mwingine. Wala hoja hiyo siyo utetezi wa udhaifu wa Kikwete..
Katika utawala huu tumeona untouchables wakipanda karandinga la Polisi, member wa Saigon club (kaitafue hii) akisimama Kisutu Mahakamani.
Kwa wana CCM (mimi si mmoja wao) inabidi wamshukuru sana kwani anajua ku pre empty,angalia suala la katiba mpya.Tungekuwa na mhafidhina hii ingekuwa issue ambayo si ajabu damu ingeshamwagika na kwa mtindo huu CCM itaendelea kwa muda.
Nakiri ana mapungufu kama binadamu lakini mfumo una mapungufu zaidi.
Tuendelee kujadiliana
Haya maelezo yako ya mwisho, naomba nikuachie kama zawadi. Sitayagusa kwa sasa. Karibu sana mkuu
Mig