Udhaifu Wa JK: Tafsiri Yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udhaifu Wa JK: Tafsiri Yangu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Jun 24, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  " OUR President is important; but, he is not Tanzania. All of our people organaized together are Tanzania"- (Julius Nyerere, Julai 29, 1985)

  Ndugu zangu,
  Watanzania wengi hatuna mazoea ya kusoma, hata makala za magazetini ukiachilia mbali vitabu vya taarifa na hadithi. Ndio, tu wavivu wa kusoma.

  Kigong'onda ni aina ya ndege. Ndege huyu ana mdomo mrefu na anapenda sana kugongagonga mti kwa mdomo wake. Ndivyo anavyojipatia ridhiki yake.

  Lakini, kwa hulka yake ya kugong'onda kila kilicho mbele yake, basi, hata ukimwekea mti wa chuma porini, kigong'onda atahangaika nao mpaka damu zimtoke mdomoni. Ni hulka yake. Kiongozi hapaswi kuwa kama kigong'onda.

  Kuna hoja mezani juu ya udhaifu wa JK, imetokea Bungeni. Yumkini, kama mwanadamu, JK ana mapungufu na udhaifu wake, nani asiye na mapungufu na udhaifu? Lakini, tukimzungumzia JK kama taasisi ya ' Urais', namwona Rais anayejipambanua na waliomtangulia. Ni kwa kujitahidi kufanya yale yalo nafuu na yenye manufaa kwa nchi yetu kwenye mfumo dhaifu uliopo.

  Wanadamu tunapaswa kuhukumu dhamira ya mtu na si matokeo. Bado namwona JK kama kiongozi mwenye dhamira njema kwa nchi yetu. Nauona ujasiri ndani ya JK. Ni ujasiri wa kufanya yale ambayo, hata ndani ya chama chake hayakuwezekana kufanywa na Mwenyekiti wa chama huko nyuma. Na bila shaka, kuna wahafidhina ndani ya chama chake wanaomwona JK kuwa ni dhaifu kwa mantiki hiyo. Kuna wanaoamini, ndani ya CCM, kuwa Rais wa chama tawala anayekaa na kuongea na wapinzani Ikulu ni Rais dhaifu!

  Na hata haya tunayoyashuhudia sasa, yumkini ni matokeo ya dhamira njema ya JK. Naamini, kwa tunavyoenenda sasa, Tanzania atakayoiacha JK haiwezi tena kurudi kuwa kama ilivyokuwa kwa Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa. JK amepanua uhuru wa Watanzania kuchangia fikra zao bila hofu. Siku zote, hofu haijengi nchi.


  Maana, tumefika hapa kutokana na mfumo dhaifu unaozaa Serikali dhaifu, unaozaa Bunge dhaifu na unaopelekea pia kuzaa vyama dhaifu vya siasa ikiwamo chama tawala. Na chimbuko lake ni Katiba ya Nchi iliyo DHAIFU. Ndio, tatizo la nchi yetu ni tatizo la kimfumo.

  Ni tatizo lililoasisiwa tangu Awamu ya kwanza ya Urais. Angalia, Katiba yetu inampa nguvu nyingi sana Rais. Tuna bahati tu hajatokea Rais anayeamua kuzitumia ipasavyo nguvu hizo.

  Nimeona katuni ya ndugu yangu Masoud Kipanya kwenye gazeti la Mwananchi la jana, Juni 23, 2012. Kipanya alionyesha foleni ndefu ya wapiga kura Watanzania walio tayari kumpigia kura Rais Dikteta.

  Niliogopeshwa na michango ya maoni ya Watanzania juu ya katuni ile. Wengi walionekana kuikubali hali hiyo. Kuwa kwao kwa hali ilivyo sasa ni heri kutawaliwa na dikteta kuliko Rais dhaifu!

  Inasikitisha na inaogopesha kuona kuwa tumefika hapa. Naamini mimi na wengine wengi tuliokulia enzi za chama kimoja na Rais mmoja ambaye ni kila kitu, tusingependa kurudi huko tulikotoka. Nikayasoma jukwaa moja maoni ya Mtanzania Ludovic Mwijage aliyejaribu kuonyesha ubaya wa udikteta. Hapo chini nimeweka kitabu cha Mwijage kilicho kwenye maktaba yangu. Kwa mimi niliyesoma kitabu chake, ningeshangaa kama Mwijage angeunga mkono hoja ya kumwona JK dhaifu na kutamani Rais Dikteta.

  Ukweli, sisi wa ' Kizazi Cha Azimio' tuliwaona wazazi wetu wakiishi katika hali ya hofu na mashaka. Waliishia kunong'ona tu pale walipotaka kuishutumu Serikali na Rais aliye madarakani.

  Mjumbe wa nyumba kumi alikuwa ni mtu aliyeogopewa sana. Huyu alikuwa ni wakala wa Chama tawala na Serikali. Moja ya majukumu yake ilikuwa ni kuwatambua, katika nyumba zake kumi, wale wote waliokuwa na mitazamo tofauti na ya Serikali na Mkuu wa Nchi. Ni wale walioitwa ' Wapinga Maendeleo!'. Kuna waliosekwa rumande, kuna waliofungwa magerezani.

  Enzi zile viongozi watu wazima walisimama majukwaani na kusema; " We have a One Party Democracy!" Katika dunia hii hakuna ' One Party Democracy' bali ' One Party Dictatorship'. Hata kwenye nyumba mwanamme ukishaoa huwezi tena kutamka juu ya ' One Man Family!'- Na watoto wakiingia kwenye familia , nao pia wanatakiwa wawe na sauti.

  Afrika Rais anategemea sana wasaidizi wake katika kuifanya kazi yake. Hivyo, mfumo dhaifu huzaa wasaidizi dhaifu pia. Mfano, pale Bungeni hakukuwa na haja yoyote ya mbunge kutolewa nje kwa kutamka ' JK ni Dhaifu'.

  Badala yake, ilikuwa fursa kwa wasaidizi wa JK kujenga hoja za kubomoa hoja za mbunge huyo.
  Kumtoa Mbunge nje kumemsaidia zaidi kuwasilisha ujumbe wake na hata ukaaminiwa na wengi. Maana, swali la hata wasiofutilia vipindi vya Bunge ni ' Kwani huyo Mnyika amesema nini?" Ni yale yale ya Zitto Kabwe kutolewa Bungeni kwa hoja ya Buzwagi. Nakumbuka kumsikia Mzee Malecela akisimama Bungeni na kutamka, kuwa dawa ya kidole chenye kansa ni kukikata!

  Malecela na wengine katika CCM walisaidia, kwa kasi ya ajabu, kumtangaza na kumpa umaarufu Zitto Kabwe. Maana, wengi mitaani walitaka kukiona kidole hicho chenye kansa kinachokisumbua chama tawala na kikongwe hapa nchini, CCM.

  Na mpaka hii leo, CCM wanarudia makosa yale yale ya jana. Na kwanini wanarudia? Ni kwa baadhi ya watendaji, kuingiwa hofu na wimbi hili la mabadiliko, hivyo kutojiamini na hata kufanya yale wanayodhani yatamfurahisha aliyewateua, kumbe, wanamharibia, na wanazidi kukipaka matope chapa chao.

  Naam, tunaweza kuondokana na mfumo dhaifu kupitia Katiba mpya ijayo. Inawezekana.

  Maggid Mjengwa,
  Iringa.
  0788 111 765
  http://mjengwablog.com
   
 2. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,331
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Upinzani wapewe nchi yaishe.
   
 3. lm317

  lm317 JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Alisema haya!
  Mnyika.jpg
   
 4. c

  chayowa1981 JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 218
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  mheshimiwa mjengwa nimeipenda analysis yako the problem is someone may decide to say that the glass is half full or half empty meaning the same thing with diffetrent motive
   
 5. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,132
  Likes Received: 2,157
  Trophy Points: 280
 6. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,188
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Hongera Majid kwa uchambuzi wako murua.. Umeongea ukweli mtupu..
   
 7. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  Udhaifu wa jk ni udhaifu wa serikali- Tanzania daima.
   
 8. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Niruhusuni nipite hapa!
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Unataka Ukuu wa wilaya?
   
 10. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  "Nimemuua kwa dhamira njema" Hapa tukumu dhamira njema na sio matokeo ya kuua?


  Hapa ninakubaliana na wewe kabisa mfumo wetu ni dhaifu na ninakubaliana nawe pia kuwa Raisi wetu amefanya mengi kuliko watangulizi wake, likiwemo hili la "kutupa mdomo" wa kumkosoa. Tutakuwa wakosefu wa shukurani kama hatutalitambua hilo, angalau kulitambua tu. Lakini hilo halimfanyi asikosolewe. Yeye kama Mkuu wa Kaya, lazima alaumiwe kwa yale yanayotendwa na wasaidizi wake. Wengi tumekuwa tukimtetea kuwa yeye ni mtu imara lakini anaangushwa na wasaidizi wake, je kuendelea kuwang'ang'ania na hata kuwalinda tukuiteje?

  Bora kukosolewa ili ujirekebishe kuliko anayekusifu pale unapokosea.
   
 11. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  ni kweli mambo mengi ya kimaovu yanayofanywa na viongozi wa serikali tunayajua leo hii lakini tusingeyajuaga wakati wa mkapa...bt all in all i still think ana weaknesses zake nyingi tu. Ah tuvumilie tu hiyo miaka 3 iliyobaki
   
 12. B

  Bob G JF Bronze Member

  #12
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Katiba si suluhu ya UDHAIFU WETU, Tatizo la watanzania ni Ujinga wa Kuendelea kuikumbatia ccm na viongozi wake ambao muda wote wameshindwa kutofautisha Mtu mwovu na Mwadilifu, Tanzania Wahalifu wanaheshimika zaidi ya watu waadilifu, waadilifu wanasubiriwa wafe ndo tutambue Mchango wao, Nenda hata makazini waadilifu hawadumu kwenye kazi waangalie Mafisadi, wavivu, wezi, wambea, waongo, wazushi na wavivu wa kufikiri ndo wapo makazini. Katiba haitakua na maana kama katiba ya mwanzo haikuleta mabadiliko yaliyo kusudiwa.
   
 13. a

  admiral elect Member

  #13
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  <br>

  mnyika was right but not a hundred percent na nadhani alikuwa anaelekea huko wakamkatisha.ukweli ni kuwa tumefika hapa tulipo kwa sababu ya udhaifu na tamaa ya marais wetu (mwinyi,mkapa na kikwete),uzembe wa bunge letu,kwa sababu upuuzi wa ccm na zaidi kwa UOGA,UJINGA NA UNAFIKI WETU WANANCHI WA TANZANIA. ZAIDI KABISA MIMI BINAFSI NI WA KULAUMIWA SANA MAANA KAMA MTANZANIA SIJAFANYA LOLOTE KUBADILISHA HALI HII,SIJUI NITAWAELEZA NINI WATANZANIA WALIO WACHANGA NA WATAKAOZALIWA BAADAE.Hongera mnyika na lisu kwa kuanza kuwaambia watanzania ukweli hata kama hawajauzoea na hivyo ni mchungu kama shubiri ,maana tutaendelea kijidanganya wenyewe mpaka lini? je tutalalamika mpaka lini? je si wakati sasa wa kuchukua hatua za kubadilisha hali hii angalau kwa kuanza kuambiana ukweli?
   
 14. a

  admiral elect Member

  #14
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tukikiri kuwa mfumo wetu ni dhaifu tukubali kuwa na sisiwenye mfumo huo ndo wadhaifu no.1
   
 15. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #15
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,586
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Kama kawaida yako, a nice piece of work.Umenifurahisha mno.
  Kikwete kama binadamu ana madhaifu mengi lakini mfumo umetuumiza zaiadi.
  Tumepata uhuru zaidi hata kama palikuwa na force behind the scene lakini tunaiona Zimbabwe wanavyomaliza nchi ya kukataa kubadilika.
  Ni Raisi ambaye amepeleka pesa zaidi katika Halmashauri kuliko mwingine yoyote na nia ikiwa watu wapate maendeleo.
  Ana mapungufu lakini wa zamani hatuwezi kumsahau angalau tumeonja Uhuru na tuutumie vizuri kwa kuweka Utaifa mbele.
   
 16. a

  admiral elect Member

  #16
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tukikiri kuwa mfumo wetu ni dhaifu tukubali pia ukweli ulio wazi kuwa na sisi wenye mfumo huo ndo wadhaifu no.1.ndo maana hata mnyika alijijumlisha( bunge) kuwa ni zembe na lissu kuwa another silly season ya kujiongopea imekuja. mimi binafsi nakiri kuwa sio dhaifu tu bali ni ***** kwa kukubali mfumo dhaifu
   
 17. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #17
  Jun 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Ninakubaliana nawe kama ninavyokubaliana na Maggid - Katiba dhaifu iliyozaa mfumo dhaifu uliozaa (viongozi wa) serikali dhaifu, wabunge dhaifu, vyama dhaifu, na kama sitoudhi, hata Watanzania dhaifu kwa kukataa kwetu kuwa hatuko dhaifu.
   
 18. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #18
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Maggid bado uandishi wako uko biased...

  1. Unataka kuchora picture kuwa serikali ya awamu ya kwanza ilikuwa ya ki-dictator. Je, ni kweli hivyo ndivyo? Hizo ni harakati za kuunga mkono madai ya watu fulani fulani kwa sababu zao na zako pia. Hapa hujaeleza tatizo la nchi hii bado unazunguka kichaka ..

  2.Kipanya cha Masoud pia kilikuwa kinapotosha ukweli wa chaguo la wa-Tanzania. Sisi hatuchagui beina ya Dictator na Dhaifu. Tunataka kuchagua serikali na rais mwenye (a) Kuwajibika (b) Hekima (c) si fisadi (d) asiyejihusisha na mtandao wa mchwa na mafisadi wa ndani na nje. Kwahiyo kipanya cha Masoud na makala yako ni mambo ya kujifurahisha tu na kufurahisha baraza.

  3.Wewe kimsingi umeandika ili upate fursa ya kuramba viatu vya huyo rais dhaif Mh Dr Col (rt) JMKikwete. Umeokoteza sifa ambazo hata hivyo siyo sifa asilia. Mfano: Umesema kuwa Mh Dr Col (rt) Kikwete "amepanua uhuru wa wa-Tz kuchangia fikra zao bila hofu. Siku zote, hofu haijengi". Hapa unataka kudanganya watoto ili waende kulala. Mimi kwa mtazamo wa haraka naona hivi:

  (i) Kikwete ameongeza uhuru wa kuongea majungu katika taifa
  (ii) Kikwete ameongeza uhuru wa kuchafuana na kupakana matope
  (iii) Kikwete ameleta mitizamo ya kidini na nchi inakoelekea ni kubaya sana kama hali itaendelea kubaki hivi siku zote
  (iv) Kikwete wako ameleta ufisadi unaangamiza uchumi wa nchi na hawezi kuchukuwa hatua kudhibiti hali hiyo
  (v) Kikwete ameongeza idadi ya safari kuliko rais yeyote aliyemtangulia. Bahati mbaya safari zake hazijaleta kitu chochote cha maana kubwa kwa nchi hii zaidi ya wawekezaji wa Richmond, Symbion na Waporaji wa ardhi yetu nk. Mwisho UWT wamechoka na safari zake wameanza kuiba mabilioni ya safari ili kumkwamisha asisafiri tena
  (vi) Kikwete ameleta mtindo wa kutowa ahadi za uwongo kwa taifa hili
  (vii) Kikwete amedhoofisha (a) CCM (b) Muungano (c) Serikali (d) Mfumo wa sheria na mahakama, na (e) Bunge

  Kumtetea kiongozi wa jinsi hii janga kwa taifa na ufupi wa mawazo. Nimekusaidia kidogo tu...
   
 19. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #19
  Jun 24, 2012
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Majid you're too paradoxical.

  Nlichobold na ku-underline kinanitatiza. Zaidi ya uhuru wa kujieleza hakuna dhamira nyingine JK aliyonayo katika Tanzania. Hebu zitaje dhamira hizo na alichaofanya. Njoo na dhamira hizo na viasharia / mafanikio serikali yake iliyofikia.

  Umesema vizuri kabisa kwamba tatizo ni la kimfumo.. ambalo limefanya tukawa na Rais dhaifu JK. Sasa JK kama Rais na U-Rais kama taasisi na JK yuko kwenye ngwe ya pili ya U-Rais ame-address vipi tatizo hili la kimfumo. Majid unatuambia kwamba JK anajua tatizo lililopo ni la kimfumo, na U-Rais kama Taasisi na yeye kama Raisi anamamlaka na uwezo wa kubadilisha mfumo. Ni mwaka wake wa saba madarakani ameshindwa / hataki kubadili mfumo ili tumuone ana dhamira ya kweli halafu unasema JK si dhaifu?

  Makala yako iliyopita kwenye Raia Mwema (kama sijakosea) ulitoa mfano wa Socrates miaka hiyo alipotembea na kurunzi mchana akiwa ameiwasha. Alipoulizwa akasema KUNA WATU JAPO JAPO WAPO KWENYE MWANGA LAKINI HAWAONI. Funguka my brother.

  Tanzania ni yetu sote Majid.... Tuna na dhamira ya kweli kwa Tanzania yetu.... unafikra za Kimapinduzi Majid.... Naamini huzioni fikra hizo kwa JK and his co-pilot members members.
   
 20. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #20
  Jun 24, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,526
  Likes Received: 1,313
  Trophy Points: 280
  a very hypocritical journalist.....ndio sababu wewe huwezi kupata safu kwenye gazeti kama Raia Mwema....because you are a hypocrite.....Seems kuna kitu unatafta toka kwa watawala....you are a very very desperate journalist...very sorry for you...ungekuwa unarudi kujibu michango ya watu humu ningekuonyesha how hypocritical you are....lakini kwa vile hutarudi kujibu michango ya watu humu...i'm just sorry for you....
   
Loading...