Udhaifu ni tusi?

leonaldo

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
2,585
3,179
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa kukijitokeza hali ya kutaharuki kwa chombo chetu cha bunge pale wananchi wanapotaja ama kuonyesha Udhaifu au madhaifu ya bunge letu,ipo mifano Mingi na nisingependa kuitaja yote ila Nina huu mmoja wa hivi karibuni nao ni kuhusu Muswada wa Sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii,nazikumbuka mbwembwe za wabunge ndani na nje ya bunge wakiimba pambio za kuisifu Sheria iliyokuwa mbele yao na baadae kuipitisha bila kujari Msiba na Kilio cha wahanga wa hiyo sheria. Juzi Sheria imepinduliwa na mwana mapinduzi aliuliza swali je sheria hii ingewahusu na nyinyi mngeipitisha? Jibu ni hapana.

Hii ni ushahidi tosha kuwa huwa hamvai viatu vyetu na sijui huwa mnavaa viatu vya nani! Vya serikali ai vyana vya siasa?

Kwa kifupi ni mala nyingi sana tumeshuhudia mkitenda mambo mengi yaliyobeba udhaifu ulio wazi.

Tukisema ni dhambi? Kumbukeni kuwa sisi ndio tumewatuma.
 
Bunge linatakiwa lifanye kazi kama walivyoagizwa na waliowapigia kura na wapiga kura ndio wanaolipima Bunge utendaji wake hivyo wakisema ni dhaifu au imara ni haki yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom