Uchaguzi 2020 UDASA yatoa tamko kwa vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu 2020 kuzingatia Kanuni, Sheria, Katiba

Mmemwambia nani, yule aliye fanya mkutano bila ya kuwa na ratiba na kibali cha tume pale kazuramimba, amekiuka mmekaa kimya mnamlenga nani
 
Hawa siku hizi hawawezi kuitisha mdahalo wowote pale Nkrumah wa kuionya na kuikosoa serikali. Wamegeuka kuwa wasomi-maslahi, au wasomi-tumbo. Chuo chao kimeacha kuwa chemchem ya fikra, wamebaki kuwa kama Lisekondari likubwa hivi!

Nashangaa kwenye tamko lao hawaongelei chochote kuhusu enguaengua za kimagumashi zinazofanywa na NEC ili kuibeba CCM

Na wala hawaongelei chochote kuhusu fairness ya vyombo vya habari kurusha taarifa za wagombea wote impartially.

Hao UDASA wakaandike machapisho ya kitaaluma maana chuo chao kina output ndogo ya machapisho ya kisomi, Waache kutumika!
 
Tumepokea tamko hili Naomba Upinzani wa Tanzania walisome kwa kutulia maana naona wanatoka nje ya reli mapema.
 
UDSM imekuwa jalala kweli kama alivyosema professor wao! Shame on them! NEC imepitisha wabunge 20 bila kupingwa wa ccm Tupu na chuo kimeshindwa kuwauliza maswali??? Shame on them!
 
UDASA/Kahangwa (w)angekuwa wa/mkweli (w)angesema haya (nimeyapakua huko Facebook)

"TAHADHARI: WADAU WA UCHAGUZI KUWENI MAKINI NA CHUKUENI TAHADHARI
Kuna kiashiria cha hatari huko tuendako. Ninawashauri wadau wa uchaguzi, hususan vyama vya Siasa kuwa makini na kuchukua tahadhari zote kuhakikisha hatari hii haitokei. Hii ni kwa maslahi mapana ya nchi yetu.

Hatari hii imefunikwa kwenye Kanuni ya Uchaguzi Na. 63 ya 2020. Kanuni hii imeghubika mambo mawili ya hatari sana.
Jambo la kwanza, ambalo hata Tundu Lissu, mgombea Urais wa Chadema nimesikia akilizungumzia na kulikazia kwenye mojawapo ya mikutano yake ya kampeini, linahusu Form Namba 20 Msimamizi wa kituo cha Kupiga Kura anakojaza matokeo ya kura zilizopigwa kituoni kwake.

Ninashauri vyama vyote vilichukue na kulibeba na kulivalia njuga suala hili hadi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iliondoshe kwa kulifanyia masahihisho katika kanuni husika.

Ukisoma kanuni hii katikati ya mistari utaona ujanja/njama za mpango wenye nia ovu uliofichika uliopo ndani ya Kanuni namba 63. Kanuni hii inasema kwamba mawakala wa vyama watapewa Form ya matokeo ya uchaguzi vituoni (namba 20) iwapo 'kutakuwa na nakala za kutosha'. Hili ni jambo lenye njama za hatari ndani yake. Form ambayo ikizalishwa nakala moja kwa photocopy gharama yake ni shillingi 25 na zikizalishwa nakala nyingi kwa kuchapishwa kwa wakati mmoja, nakala moja haiwezi kugharimu zaidi ya shillingi 3/- inawezaje kushindikana kuzalishwa nakala za kutosha wakati hiyo ndio shughuli kuu ya NEC? Ni vigumu kupata jibu sahihi la swali hili kutoka NEC au mtaalam wao aliyeandika kanuni hizi. Ni dhahiri kuna nia ovu ndani yake. Ninaamini kila anayesoma hapa na akiwa anaelewa mazingira ya siasa za uchaguzi ya hapa nchini ataweza kubaini au anaelewa moja kwa moja njama zilizofichika ndani ya Kanuni namba 63.

Wadau, hususan vyama vya Siasa, wanashauriwa kuendelea kushinikiza NEC hadi iondoe kadhia hii ya hatari kwenye Kanuni za Uchaguzi za 2020. Kanuni inatakiwa itamke bayana kuwa mawakala wote wanaotambuliwa na sheria kuwepo vituoni, ikiwa ni pamoja na mawakala wa watazamaji wa uchaguzi wa kujitegemea, watapatiwa nakala ya matokeo ya uchaguzi (Form namba 20).

Lazima kila kituo cha kupiga kura kuwe na nakala za Form namba 20 za kutosheleza mahitaji kwa kuwa hiyo ndio shughuli kuu ya uchaguzi, na, pengine, njia pekee ya kuliondoshea taifa letu balaa la visasi mara baada ya uchaguzi. Na ni lazima kila walaka (vyama/watazamaji wa uchaguzi) apewe nakala ya matokeo ya uchaguzi kutoka hapo hapo kituoni kwake.

Wananchi wanashauriwa kuiandikia NEC kupitia WhatsApp, barua pepe na hata barua za kawaida kuitaka irekebishe dosari hili.
Lakini pia kuna jambo jingine la hatari zaidi lililofichika ndani ya kanuni namba 63.

Kwa makusudi kabisa kanuni namba 63 haitaji hata kidogo kuwa Msimamizi wa Kituo atabandika matokeo (Form namba 20) kura kwenye ubao wa matangazo nje ya Kituo cha kupiga kura mara. Ni vigumu kuamini kuwa hili ni kosa la kawaida au bahati mbaya. Hii itakuwa ni sehemu ya mtambo wa kushinda uchaguzi.

Tafsiri ya kutoainishwa kwa takwa hili la kisheria kwenye Kanuni # 63 ni kuhakikisha hakuna hata chembe moja ya ushahidi wa kura za wagombea itakayoachwa pahala popote nje ya udhibiti wa NEC, hususan kwenye vituo vya kipiga kura mara baada ya kura kuhesabiwa. Ukiangalia kimantiki, dhana nzima ya kisheria kuwa matokeo ya uchaguzi yanatangazwa vituoni, kutobandika matokeo ya uchaguzi kwenye mbao za matangazo nje ya vituo vya kupiga kura ni sawa na kutenda kinyume cha takwa la kisheria – kutotangaza matokeo ya uchaguzi kwenye vituo vya kupiga kura. Hata hivyo, umma utatangaziwa (bila ushahidi) kuwa matokeo ya uchaguzi ‘ambao kura zilihesabiwa na kutangazwa kwenye vituo vya kupiga kura’ kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi Sura 343, yanaonesha kuwa washindi ni akina fulani na fulani. Atakayebishia tamko hilo wakati huo atakuwa amechelewa kwa kuwa hatakuwa na ushahidi kuthibitisha anachoamini/anachotamka!

Tunahimiza wadau na wananchi kwa ujumla kuiandika NEC, kuikumbusha kuwa sheria inasema kuwa kura zikihesabiwa vituoni zinatakiwa kutangazwa kwa umma. Na kwamba njia ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi kwa umma ambayo imekuwa ilitumika kwa miaka 20 hadi sasa ni nakala ya matokeo hayo yaliyojazwa kwenye Form namba 20 na kisha kuthibitishwa kwa saini za msimamizi wa kituo pamoja na mawakala wa vyama vya siasa, ni kubandikwa kwa matokeo hayo kwenye mbao za matangazo nje ya vituo vha kupiga kura. Si vinginevyo!

Kwa ambao tumekuwa tukifuatilia mwenendo wa utendaji wa TUME, Serikali, vyombo vya usalama na vyombo vya habari (vingi vimetekwa walao kwa sasa), sasa tunaweza kuunganisha nukta kubaini sababu za matamko ya polisi ya mara kwa mara kusisitiza kuwa wananchi waondoke kwenye vituo vya kupiga kura mara baada ya kupiga kura. Kwamba wananchi wasiwepo karibu na vituo vya kupiga kura bali waende majumbani kwao kwa kuwa suala la ulinzi wa kura lipo mikononi mwa polisi siyo wapiga kura. Hii ni tofauti na kauli ya siku zote kuwa wananchi wema wawapelekee polisi taarifa za uhalifu!

Sasa tunaweza kubaini kuwa muda wa kutangaza matokeo na kubandikwa nje ya vituo ukifika hakutakuwa na pressure ya watu kutaka kupewa matokeo na wasimamizi wa uchaguzi watawaeleza mawakala wa vyama na waangalizi kuwa takwa la kubandika matokeo ya uchaguzi kwenye mbao za matangazo halipo kwenye kanuni. Mchezo utakuwa umekwisha!"
 
Mtu anasemaUDSM nijalala, hapo alipo unakuta alifight kupata admission hap akakosa na istoshe anashinikiza ndugu na jaamaa Waombe admission hpo. Tusiwe washika dau jmn
 
..hili tamko nimelipuuza.

..halijaigusa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

..vilevile halijawagusa viongozi wa Dini.
 
Nawapongeza mmetoa andiko zuri, wala msiogope hao wanaowakejeli maana hao wameshaandaliwa makao pindi pakitokea machafuko wataenda Ubelgiji kwa mabeberu wao kukaa. VITISHO na hamasa katika jamii havipaswi kuwa na uhai.
 
Acha kupotosha, na huo ni moja ya Uchochezi ambao unafanya. Lengo lako ni kuharibu Uchaguzi. Hili tunalujua ndio hasa Watu wa CHADEMA mnalitamani Sana maana mmetumwa na hao mabeberu kutafuta Kila aina ya chokochoko ili kusababisha vurugu hapa Tanzania.
 
Back
Top Bottom