Udaktari wa Vodafasta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udaktari wa Vodafasta

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by mangifera, Oct 16, 2011.

 1. m

  mangifera Member

  #1
  Oct 16, 2011
  Joined: Oct 15, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serikali kupitia wizara ya afya inaanzisha degree ya udaktari wa binadamu ya miaka mitatu. Hatua waliyofikia hadi sasa ni kuandaa mtaala(curiculum) na watu walikuwa morogoro wiki yote hii kwa ajili hiyo. Jamani wanajamii si wanataka kutumaliza? Iweje mtu asome miaka mitatu apewe dhamana ya miili na afya za wananchi wanyonge ilhali kwa kipindi hicho haimtoshi hata kuifahamu anatomia ya mwili?
  Au ni kwa kuwa wao hawatatibiwa na hawa Mavoda fasta maana hata juzi tu tulishuhudia mtu kapata upele kakimbizwa india fasta!!
   
 2. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Kaka hapa hatuna taifa yani tumewapa madaraka masela sasa unategemea mambo yapi? Mi sishangai kabisa na hizo taarifa maana kisicho wezekana kote duniani TANZANIA kinawezekana....we piga dili zako ukiumwa uende agakhan,indu-mandal na kcmc ila ukijichanganya uende temeke hospital basi andaa na sanda au jeneza.
   
 3. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  Nchi hii mambo yake ni ya hivi hivi!
   
 4. Pdraze

  Pdraze JF-Expert Member

  #4
  Oct 16, 2011
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kama hawa wa miaka mitano wanapasua kichwa badala ya mguu hao wa miaka mitatu itakuwaje..
   
 5. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,631
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  msicheke wanaJF! Wauguzi(NURSES) walikuwa wanasoma miaka minne sasa hivi ni miaka miwili, na tayari wameishaingia sokoni. Wanaua hao we acha tu,USHAURI:Kama unatamani uione kesho hakikisha una daktari wako binafsi vinginevyo hawa half cooked nurses and dr. Watakuua
   
 6. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #6
  Oct 16, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Mhh tanzania wameharibu mtaala wa sekondari sasa wameingia vyuoni!hayo ndiyo majibu mepesi mepesi ya kutatua tatizo la waalim na madaktari bila kuangalia kwa nini wanafunzi wanakimbia kozi hizo
   
 7. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #7
  Oct 16, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  kama ndio hivyo basi BBA, HR, BCOM degree watabadili na kuwa mwaka 1, wakati wenzetu wanaongeza miaka ya kusoma MD sisi tunapunguza
   
 8. C

  Cognitivist JF-Expert Member

  #8
  Oct 16, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 770
  Likes Received: 973
  Trophy Points: 180
  kinachoonekana kufanyika ni kuandaa madaktari wa kata kama walivyoandaa walimu bt then wao na watoto wao haooooo India kwa Apollo.
   
 9. Mr Suggestion

  Mr Suggestion JF-Expert Member

  #9
  Oct 16, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Sidhani kama taarifa hii itakuwa sahihi ngoja tuone, au wanataka kufanya miaka mitatu chuoni kisha miaka miwili ya intern!
   
 10. m

  mangifera Member

  #10
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 15, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  @Suggestion, hii si habari ya kupikwa kama ulivyozoea nyinginezo. Leo nimeonana na wataalam walotoka kutengeneza mitaala hiyo na ukweli unabaki ulivyo. Subiri kuuwawa kama huamini!
   
 11. N

  NIMIMI Senior Member

  #11
  Oct 17, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuna hospitali hata viwango hazina, yaani ni mfano halisi ile hospitali haina qualified Surgeon ni std VII leaver with an experience of working in the Surgeory Room, lakini amekua Surgeon haikutosha wameanzisha chuo cha Nursing ambacho wanaowapika wataalam hao wa afya zetu ni walewale wasiokuwa na sifa za kitaalamu. Na nilishaugua mara nyingi kila nikienda napigwa sindano za malaria pacpo mafanikio baada ya kwenda kwa mtaalam nikakutwa nina matatizo mengine tofauti. Hii sirikali inatumaliza, imejaribu kutuangamiza kwa kutumia vyandarua vya Bush wengi wamestuka na kutovitumia wameona wawapike wataalam(wauguzi) mbombo ngafu, kazi kweli kweli.
   
 12. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,368
  Trophy Points: 280
  Muda unaokaa chuoni unaendana vipi na ubora wa elimu utakayopata?
   
 13. L

  Lwikunulo Senior Member

  #13
  Oct 17, 2011
  Joined: Jun 1, 2007
  Messages: 114
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35

  come on, ...are you serious? unadhani muda sio issue kabisa katika suala la elimu? ubora wa elimu unategemea vitu vingi ikiwemo vitendea kazi (vitabu vya kaida na ziada, reagents za maabara kwa pure science,nk), ubora wa walimu, ubora wa mazingira ya shule, muda ili kuweza ku-cover yale yote yanayotakiwa kufunzwa. Kama muda sio issue basi hata elimu ya sekondari (O'level) tuifanye kwa mwaka mmoja basi badala ya miaka minne ya sasa!
   
 14. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #14
  Oct 17, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Acheni uzandiki pale watu wanapotaka kuboresha nyie mnalialia, mbona RMA alipokuwa anaenda ku upgrade kuwa MA alikuwa anasoma miaka miwili badala ya mitatu kwa fresh from school? Hivi CO aliyemaliza mafunzo na kufanya kazi kwa miaka kadhaa bado anahitaji miaka 5 kama fresh from school?

  Angalieni pale Muhimbili college jinsi waliotoka kazini wanavyotesa kwa kufanya vizuri kimatokeo na si kudharau kila kitu mradi kinatoka ktk serikali ya Magamba
   
 15. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Mpaka huyu JK aondoke madarakani Tanzania itakuwa garasha in all fields, nyie subiri tu. Nani anatoa maamuzi ya kishenzi hayo. Yale yale ya mtu mmoja kuvuruga mitaala ya sekondari kuua fizikia, na chemia kuwa somo moja, kuua michezo-Mungai enzi hizo. TCU wako wapi
   
 16. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #16
  Oct 17, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,368
  Trophy Points: 280
  nayajua hayo yote, lakini katika hii mada sitaki kukurupuka na kuanza kuwalaumu walioamua hivyo. Tujiulize, kwanini wamepanga hivyo? Vipingamizi vyake hawavijui? Miaka mitatu kama kuna vifaa vya utendeaji kazi na walimu wazuri hamna shida. Cha msingi tusisitize utolewaji wa elimu bora. Maana mnaweza kukaa chuoni kwa miaka 12 lakini kama elimu mnayopewa ni duni bado utakuwa sio daktari bora.
   
 17. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  ninachofahamu na nilichokiona ni wale CO wakiingia mwaka wa 2/3 kusoma MD na ni sawa kwangu mimi kwakuwa wanauzoefu wa kazi, hapa hoja yetu ni hawa fresh from a-level
   
 18. Mr Suggestion

  Mr Suggestion JF-Expert Member

  #18
  Oct 17, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Ndio maana mkuu sitaki kukataa kwa kuwa huo mtaala sijauona hope jamaa wataongeza miaka ya intern kwa kuwa MD wengi wabovu kwenye practical so wanaepusha yale yaliyotokea kwa ndugu zangu pale Muhimbili wakati wa upauaji badala ya mguu wakampasua kichwa, Ngoja nisubiri mkuu
   
 19. Salanga

  Salanga JF-Expert Member

  #19
  Oct 18, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuna uwezekano mkubwa wanafanya mabadiliko mazuri.
  Lakini nina taarifa kuwa nchi kama Cuba baada ya mapinduzi yao walitengeneza madadk kwa miaka 4 tu kwa kuwa walikuwa na wataalamu wachache.

  Hata hivyo wanafunzi wa MD bongo wanakosa practicals hilo lipo wazi.Nafikiri wanaboresha zaidi mtaala na bila shaka wanaoandaa mtaala ni daktari.
  Lakin mtoa maada umeelza kidogo sana ndio maana kila mtu anaguess labda ni hivi labda vile ,ungeleta kitu kamili magreat thinkers tukakijadili .
   
Loading...