Udafisi: Mbinguni ni wapi endapo binadamu tukifa tunazikwa Ardhini?

Udafisi: Mbinguni ni wapi endapo binadamu tukifa tunazikwa Ardhini?

Ufahamu wako hapo ndo ulikofika! Maana nikikuuliza Mungu anaishi wapi utaniambia ni mbinguni, nikikwambia mbinguni umewahi kufika utaniambia hapana! Nikikuuliza shetani yupo utaniambia ndio nikikuuliza anaishi wapi utaniambia ni kuzimu je kuzimu ni wapi???? Mungu alipomuumba mwanadamu alimpa ukomo wa kufikiri na kuwaza, ndo maana mambo ukianza kujiuliza hayana majibu! Kwa hiyo amini kwamba Mungu yupo na kama Mungu yupo amini kwamba mbingu ni halisi na kuzimu ni halisi, kinachobaki ishi kwa imani ndipo utakapompendeza Mungu! Siri zote za wapi mwanadamu anaenda baada ya kifo zimeandikwa kwenye biblia, na kinachozikwa ni mwili tu lakini roho ambayo ndio uhalisi wa mtu huwa haipo toka huyo mtu alipokata pumzi siku ya kwanza! Na kwa nini mwili unaenda mavumbini biblia imeeleza!! Tatizo binadamu ni wabishi sana hamtaki kusoma biblia, hamtaki kuokoka na kumwamini Yesu!
Note: bila kumwamini Yesu amini kwamba utatupwa motoni na baada ya kifo unaenda kuzimu! Kuzimu na mbinguni ni sehemu ambazo zinafikika kupitia kifo tu! Bila kufa hizi sehemu huwezi kufika! Maana zinatambulikana kwa jinsi ya Rohoni!!
Yaani huwa na shangaa sana mnapo mchanganya Yesu na Mungu. Hivi ni vitu viwili tofauti, Mungu ni mkubwa kuliko Yesu.
 
Yaani huwa na shangaa sana mnapo mchanganya Yesu na Mungu. Hivi ni vitu viwili tofauti, Mungu ni mkubwa kuliko Yesu.
Ni kwa ufahamu wako ila Yesu ndiye huyo huyo Mungu! Sifa alizo nazo Mungu ndizo alizo nazo Yesu pia!!
 
Ukisikia mwili wa John umezikwa tambua aliyezikwa sio John chief ni mwili. John yupo.
Mwanadamu ana mwili na Roho. Mwili uliotengenezwa kwa udongo unarudi kwenye udongo. Roho haifi. Baada ya mwili kufa, Roho inarudi ilikotoka. Katika mbingu, kila kitu ni spirit, ndiyo maana mbingu hata kama ikiwa kwenye mazingira haya haya, huwezi kuiona ukiwa katika mwili. Mbingu huzungumzwa kama ni juu, kuonesha tu kuwa ni hadhi ya juu kuliko Dunia ya mwili, lakini siyo lazima iwe angani.
 
🙏🙏🙏 Hata kama sio conclusive and ultimate ila umeongea kwa ufahamu mkubwa wa kiroho hata iwe ni abstract kiasi gani ila shukrani sana
 
Je kuna John bila mwili wake?
Ndio mwili wa mwanadamu una maeneo matatu ndani yake. Nafsi, roho na mwili wa nyama. So wewe kuitwa John sio bahat mbaya mzee. Ulimwengu wa roho unafanyakaz katika ukamilifu. So ilishasetiwa utazaliwa utaitwa John nk.
 
Swali lako ni zito na la kina sana — linagusa masuala ya imani, mila, maandiko ya dini, na imani za kiroho kuhusu wapi binadamu huenda baada ya kufa, na kwa nini miili huzikwa ardhini. Hebu tuangalie kwa makini — tukiangazia Qur'an, Biblia, simulizi za kiroho, halafu tufunge na hitimisho lenye tafakari.
1. Qur'an Inasemaje?
Katika Uislamu, mtu akifa, mwili huzikwa ardhini kama sehemu ya kuurudisha kwa Muumba, kwa kuwa umetokana na ardhi. Maandiko ya Qur'an yanathibitisha hilo:

a) Mwanzo wa Binadamu:
“Kwa hakika Sisi tuliwaumba binadamu kwa udongo.”
(Surat As-Saffat 37:11)

b) Kurudi Ardhi Baada ya Kufa:
“Kutokana nayo (ardhi) Tumewaumba, na humo Tutawarudisha, na kutoka humo Tutawatoa tena mara nyingine.”
(Surat Ta-Ha 20:55)

c) Kaburini Kuna Maisha ya Barzakh:
“Mpaka watakapofikiwa na kifo, husema: Mola wangu! Nirudishe (duniani) ili nifanye mema…! Lakini hapana, hayo ni maneno tu anayosema. Na nyuma yao kuna kizuizi (Barzakh) mpaka siku ya kufufuliwa.”
(Surat Al-Mu’minun 23:99-100)

2. Biblia Inasemaje?
Katika Ukristo, pia kuna imani kwamba mwanadamu aliumbwa kwa mavumbi ya ardhi, na atairudia. Baada ya kufa, mwili huzikwa ardhini na roho hurudi kwa Mungu. Maandiko yanatoa msimamo huu:
a) Mwanzo wa Binadamu:
“Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.”
(Mwanzo 2:7)
b) Kurudi Mavumbini:
“Kwa jasho la uso wako utakula chakula mpaka utakaporudi ardhini, kwa maana katika hiyo umeumbwa; kwa kuwa u mavumbi, nawe mavumbini utarudi.”
(Mwanzo 3:19)
c) Wafu Wakingoja Ufufuo:
“Kwa maana mavumbi yatageuka kuwa mavumbi, na roho itarudi kwa Mungu aliyeitoa.”
(Mhubiri 12:7)
d) Ufufuo wa Mwisho:
“Wala mstaajabie hili; kwa sababu saa yaja ambayo wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake; nao watatoka.”
(Yohana 5:28-29)

3. Simulizi mbalimbali za kiroho
Katika mila za Kiafrika na simulizi za kiroho:

Watu huamini kuwa ardhi ni mama wa viumbe. Binadamu akifa, anarudi kwa Mama Ardhi, mahali pa asili, akingoja maisha yajayo.
Kuna simulizi za roho kutangatanga kama mtu hakuzikwa vizuri au hakuagwa kwa heshima.

Ndoto za wazee na masimulizi ya watu waliodai kufa na kurudi zinasema mara nyingi mtu hujikuta eneo la wazi au mlimani, au mahali penye mto — mahali pa mpito kabla ya kufika mwisho.

4. Hitimisho
Katika Qur'an na Biblia, kuna maelewano kwamba mwanadamu hutoka ardhini na huirudia baada ya kifo. Miili huzikwa ardhini kwa heshima na kama njia ya kurudisha alikotoka.
Roho, katika maandiko yote mawili, inaendelea kuwepo — ikiwa inangojea hukumu au maisha mengine.
Simulizi za kiroho na mila za Kiafrika nazo zinathibitisha umuhimu wa ardhi kama nyumba ya mwisho ya mwili na daraja la roho.

Kwa hiyo:
“Binadamu ni udongo ujao uhai kwa pumzi ya Mungu, arudipo mavumbini, roho irudi kwa Mungu aliyeiumba.”
 
Swali lako ni la msingi sana — linagusa imani ya mwanadamu kuhusu maisha ya baada ya kifo na wapi hasa mbingu ilipo kama binadamu huzikwa ardhini. Hebu tuchambue hili kwa kina kwa mtazamo wa Biblia, Qur'an, simulizi za Kiafrika, na hitimisho:

1. Biblia Inasemaje?
Biblia inafundisha kwamba baada ya kifo, mwili hurudi mavumbini lakini roho huenda kwa Mungu aliye mbinguni.
Mbinguni kwa mujibu wa Biblia ni mahali pa milele pa Mungu, malaika, na roho za wenye haki.

a) Mavumbi kurudi mavumbini:
“Kwa jasho la uso wako utakula chakula, mpaka utakaporudi ardhini, kwa maana katika hiyo umeumbwa; kwa kuwa u mavumbi, nawe mavumbini utarudi.”
(Mwanzo 3:19)

b) Roho kurudi kwa Mungu:
“Nayo roho itarudi kwa Mungu aliyeitoa.”
(Mhubiri 12:7)

c) Mbingu ni makao ya Mungu:
“Bwana amekwisha kuandaa kiti chake cha enzi mbinguni, Na ufalme wake unavitawala vitu vyote.”
(Zaburi 103:19)

d) Yesu alienda mbinguni:
“Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, alipaa kwenda mbinguni; akaketi mkono wa kuume wa Mungu.”
(Marko 16:19)
Kwa hiyo — mwili unabaki ardhini ukisubiri ufufuo, lakini roho huenda mbinguni au mahali pa kungoja hukumu.

2. Qur'an Inasemaje?
Katika Uislamu, mtu akifa, mwili huzikwa ardhini lakini roho huingia katika hali ya mpito inayoitwa Barzakh hadi siku ya Kiyama, ambapo itahukumiwa. Mbinguni (Jannah) ni makao ya mwisho ya waumini waliotenda mema.
a) Kurudi ardhini:
“Kutokana nayo (ardhi) Tumewaumba, na humo Tutawarudisha, na kutoka humo Tutawatoa tena mara nyingine.”
(Surat Ta-Ha 20:55)

b) Roho kwenda kwa Mola:
“Enyi nafsi iliyoridhika! Rudi kwa Mola wako hali ya kuwa unaridhika na umependelewa. Basi ingia katika kundi la waja wangu. Na ingia peponi mwangu.”
(Surat Al-Fajr 89:27-30)

c) Mbinguni ni wapi?
Qur'an haiwezi kueleza mbingu kwa nafasi ya kijiografia bali kama mahali pa neema, amani, na furaha isiyo na mfano.

3. Simulizi za Kiafrika Zinasemaje?
Katika mila nyingi za Kiafrika:
Binadamu huaminiwa kuwa na mwili na roho.
Mwili huzikwa ardhini arudie kwa mama ardhi.
Roho husafiri kwenda ulimwengu wa mababu au mahali pa mizimu, ambapo huishi kwa amani, na huweza kuwatembelea waliobaki duniani.
Wengine huamini mbingu ni mahali pa miungu na mizimu mitakatifu, lakini mara nyingi haijatajwa kwa maana ya kidini kama ilivyo katika Biblia na Qur'an.
Mfano wa methali:
“Mtu hufa dunia haisimami; roho huenda kwake Mungu, mwili hurudi ardhini.”

4. Hitimisho
Kwa msingi wa maandiko haya na simulizi:
Mwili wa binadamu huzikwa ardhini kwa sababu umetoka humo.

Roho ndiyo husafiri — kwenda mbinguni kwa Mungu (Biblia na Qur'an), Barzakh (Uislamu), au kwa ulimwengu wa mababu (mila za Kiafrika).

Mbinguni si sehemu ya kijiografia, bali ni ulimwengu wa kiroho wa utukufu na pumziko la milele.
Kwa hiyo:
“Binadamu hufa, mwili hubaki ardhini, roho huenda kwa Muumba mbinguni au sehemu ya kungoja, ikisubiri hukumu au kuungana na mababu, kulingana na imani ya mtu.”
 
Maneno yasiwe mengi ebu tuumize akili shusheni majibu tafadhari
Hakuna sehemu panaitwa mbinguni ni kauli tu za kwenye maandiko yaliyo andikwa na binadamu kama wewe ndio yanadai Kuna mbingu
Ukisikia mwili wa John umezikwa tambua aliyezikwa sio John chief ni mwili. John yupo.
Fanya kilichokuleta duniani. Kula kulala .mengine yaache kama yalivyo
Ufahamu wako hapo ndo ulikofika! Maana nikikuuliza Mungu anaishi wapi utaniambia ni mbinguni, nikikwambia mbinguni umewahi kufika utaniambia hapana! Nikikuuliza shetani yupo utaniambia ndio nikikuuliza anaishi wapi utaniambia ni kuzimu je kuzimu ni wapi???? Mungu alipomuumba mwanadamu alimpa ukomo wa kufikiri na kuwaza, ndo maana mambo ukianza kujiuliza hayana majibu! Kwa hiyo amini kwamba Mungu yupo na kama Mungu yupo amini kwamba mbingu ni halisi na kuzimu ni halisi, kinachobaki ishi kwa imani ndipo utakapompendeza Mungu! Siri zote za wapi mwanadamu anaenda baada ya kifo zimeandikwa kwenye biblia, na kinachozikwa ni mwili tu lakini roho ambayo ndio uhalisi wa mtu huwa haipo toka huyo mtu alipokata pumzi siku ya kwanza! Na kwa nini mwili unaenda mavumbini biblia imeeleza!! Tatizo binadamu ni wabishi sana hamtaki kusoma biblia, hamtaki kuokoka na kumwamini Yesu!
Note: bila kumwamini Yesu amini kwamba utatupwa motoni na baada ya kifo unaenda kuzimu! Kuzimu na mbinguni ni sehemu ambazo zinafikika kupitia kifo tu! Bila kufa hizi sehemu huwezi kufika! Maana zinatambulikana kwa jinsi ya Rohoni!!
Ninachojua tu kuwa tuna mtu aliyenauwezo MKUBWA ndio aliyetuanzisha sisi Kwa kujenga Kila kitu ila alipo ndio sipajui
Hiki ni kitendawili kinachoteguliwa na Geniuses tu.

Msio magenius mkojoe mlale.

Fuateni ushauri wa BICHWA KOMWE.

Cc: Lucas Mwashambwa Extrovert Lamomy raisi ajaye nchini NAMBA MOJA AJAYE NCHINI
Wakuu kesho nataka nimpige maswali mgumu yahusuyo dini hasa ya ukristo binti mmoja aitwaye Setfree ambaye kila dakika anaanzisha nyuzi zihusuzo imani mpaka modinyos wanalalamika kuwa Seva za JF zimezidiwa.

Sifanyi hivi kwa lengo baya bali kumshinda binti yule ili akimbilie kule Facebook then nyuzi za kiimani zipungue kidogo humu jukwaani.

Nitafungua Uzi wa kubishana naye kwa hoja nione atakeyeshinda.

Stay tuned!!

Siamini katika mbingu na mambo mengine yakinadharia yahusuyo roho na blabla nyengine za mizimu na wachawi..!!

Kama ambavyo ulikuwa hujitambui, haupo, si kitu si lolote kabla haujazaliwa ndivyo hivyohivyo ukifa unakuwa ktk hiyo zone ya si lolote, bila utambuzi.
Hakuna cha mbingu sijui ulipuliziwa pumzi ukaanza kuishi hizo ni longolongo za kitapeli tu watu wapitishe vitu vyao!, Dini na mafundisho yake yanatumika kutawala wengine na hao wanaotawala wanafaidika kifedha, wadhifa na heshima kwenye jamii lakini ni ulaghai ambao nakuapia karne zijazo ambapo ujinga huu utakapokuja kuondoka, basi vizazi vijavyo vitasoma jambo hili la dini kama jambo la "KIJINGA" ambalo limewahi kuwepo katika karne kadhaa!.

sawasawa na vile sisi tunavyosoma hivi sasa maswala ya utumwa athari zake n.k. Mpaka kuwashangaa akina mangungo walivyokuwa wanasaini mikataba ya hovyo nakuuza watu wake kwa vitu vya ajabu!.

So, ukifa hakuna chochote kinaendelea dhidi yako!. wewe ni ufahamu ukizima ndo umezima hakuna linalooendelea tena!.
Eti hauamini uchawi we jamaa bwana watu wanaigiza hadi kwenye movie inamaana umewazidi akili hao watu.
 
Wakuu kesho nataka nimpige maswali mgumu yahusuyo dini hasa ya ukristo binti mmoja aitwaye Setfree ambaye kila dakika anaanzisha nyuzi zihusuzo imani mpaka modinyos wanalalamika kuwa Seva za JF zimezidiwa.

Sifanyi hivi kwa lengo baya bali kumshinda binti yule ili akimbilie kule Facebook then nyuzi za kiimani zipungue kidogo humu jukwaani.

Nitafungua Uzi wa kubishana naye kwa hoja nione atakeyeshinda.

Stay tuned!!

😀😀
 
Eti hauamini uchawi we jamaa bwana watu wanaigiza hadi kwenye movie inamaana umewazidi akili hao watu.
Kwa hyo Mkuu una amini kuna dragon, unicorn santa claus na viumbe wengine wa ajabu wanatumiwa kwenye movie wapo kweli
 
Back
Top Bottom